Ndachuwa
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 6,269
- 4,579
Kufuatia hali ya kutokuaminiana katika uendeshaji wa shuhuli za kisiasa ikiwemo chaguzi mbalimbali hapa nchini Tanzania, napendekeza badala ya kuitisha uchaguzi mkuu 2020 iundwe serikali ya umoja wa kitaifa itakayoshirikisha vyama vyote vyenye wabunge ili kufanya yafuatayo:-
(i) Pesa yote ya uchaguzi ielekezwe kugharamia na kusimamia mchakato wa katiba mpya itakayoweka mifumo ya uwajibikaji wa kitaasisi katika uendeshaji wa serikali na ugawanyaji wa madaraka
(ii) Kuweka mifumo thabiti na shirikishi ya uendeshaji wa serikali ikiwemo mchakato shirikishi wa kuwapata viongozi wakuu wa serikali na taasisi zake
(iii) Kuunda tume huru ya uchaguzi ambayo itaonekana kutoa haki sawa kwa washindani wote
(iv) Kuweka misingi ya kufanya uchaguzi mkuu wa 2025 chini ya tume huru ya uchaguzi.