Pendekezo : Nguo za Askari wa usalama barabarani zisiwe na mifuko

Pendekezo : Nguo za Askari wa usalama barabarani zisiwe na mifuko

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,420
Reaction score
17,735
Hawa jamaa ni jasiri sana linapokuja suala la kuchukua takrima.

Japo wapo wachache waaminifu ila kwa siku hizi mbili jana na leo nimewaona wakiwa makini barabarani kukagua ila konda na dereva nawasikia tu wanatajiana viwango vya kuwapa kila gari linaposimamishwa.

Kupunguza rushwa (sio kuondoa maana niliwahi kumuona mmoja posta mpya rushwa zake anatunza kwa fundi viatu) wasiwe na nguo zenye mifuko.

Pamoja na yote, nawapongeza kikosi fulani cha traffic huwa wanatembea wengi kwenye kama Noah na wakati mwingine zile land cruiser zenye viti nyuma.

Hawa wakisimama sehemu hata tsh 0 hawachukui ni kuandikiwa kila kosa. hakuna mjadala wala rushwa. sijui Kwa nini ila kama bado wanaendelea vile Wabarikiwe sana..
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ila 30,000/- usawa huu ni kurudishana nyuma, bora tuendelee tu kuwapigia polish viatu vyao.

Sent from my DUB-LX1 using Tapatalk
 
Kwamba unaagiza watu watoe 30 na kudai risiti si ndio?
 
Kuna kipindi nliwahi kumsikia Rais anasema kwamba Askari polisi wapewe rotations waingie kwenye Utrafiki kwa muda ili wapate "za kubrashia viatu"
 
Unataka utoe efu 30 badala ya efu 5 mkuu na kosa ni lako....
Mkuu kuwa serious kidogo efu 30 inaefu tano 6 ujue....

Sie wabongo 98% wote karibia vipato vyetu tumemiksi na magumashi watu hawaezi acha toa efu 5 wakiombwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwka juzi kuna pahala niliona jamaa wa kirikuu walikua na kosa ikabd wawape kuku pale pale jamaa walikua wamebeba kuku
Ukiwekwa idara ya traffic ni sawa na kupewa ulaji. Utabadilisha mboga kila siku, watoto watasoma na nyumba utajenga.

Ukipokea taarifa za kupandishwa cheo utoke hapo unaweza kuzimia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka utoe efu 30 badala ya efu 5 mkuu na kosa ni lako....
Mkuu kuwa serious kidogo efu 30 inaefu tano 6 ujue....

Sie wabongo 98% wote karibia vipato vyetu tumemiksi na magumashi watu hawaezi acha toa efu 5 wakiombwa

Sent using Jamii Forums mobile app
kumbe Shida sio traffic.
wenda faini ni kubwa
au sisi wabongo ni wapenzi wa rushwa na ujanjaujanja kuliko traffic .
 
Back
Top Bottom