Pendekezo : Nguo za Askari wa usalama barabarani zisiwe na mifuko

Pendekezo : Nguo za Askari wa usalama barabarani zisiwe na mifuko

nenda depo na wewe.. wivu tuu....
tuvae nguo bila mifuko vipi?..
vaa mwenyewe nguo ka' pazia.......halafu uone..
 
Hawa jamaa ni jasiri sana linapokuja suala la kuchukua takrima.

Japo wapo wachache waaminifu ila kwa siku hizi mbili jana na leo nimewaona wakiwa makini barabarani kukagua ila konda na dereva nawasikia tu wanatajiana viwango vya kuwapa kila gari linaposimamishwa.

Kupunguza rushwa (sio kuondoa maana niliwahi kumuona mmoja posta mpya rushwa zake anatunza kwa fundi viatu) wasiwe na nguo zenye mifuko.

Pamoja na yote, nawapongeza kikosi fulani cha traffic huwa wanatembea wengi kwenye kama Noah na wakati mwingine zile land cruiser zenye viti nyuma.

Hawa wakisimama sehemu hata tsh 0 hawachukui ni kuandikiwa kila kosa. hakuna mjadala wala rushwa. sijui Kwa nini ila kama bado wanaendelea vile Wabarikiwe sana..
wavae kanzu isiyo na mifuko au overall

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora waendelee kuwekewa mifuko, binafsi nimewahi kuona traffic ananiambia kafungue buti la ile gari pale uweke, nilivyoenda nikakuta ndoo ndogo ya maji imejaa elfu 5 na elfu 10, nikabaki nashangaa, alivyoona nachelewa kuondoka akanikoromea "wewe hapo unasubiri nini nimekwambia weka uondoke"

Kama wapo watatu mwisho wa siku wanagawana, na wakishaona njia hiyo "wameshayapiga mkono" magari ya kutosha wanahamia njia nyingine, tembeeni muone.

mkuu kumbe wameshindikana, kwa ubunifu huu hakuna namna sijui watabanwaje.
 
Back
Top Bottom