Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Unawezaje kuyarudisha kinyume nyume maamuzi yaliyokwisha kutekelezwa?Kwa sababu Dar es Salaam bado ni mji muhimu sana katika utawala wa nchi kutokana na uwepo wa miondombinu ya kutosha na kuwa mji mkubwa wa kibiashara na pia kwa sababu kwa upande mwingine Dodoma ni mji muhimu sana kwa sababu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere alishaamua na kuelekeza uwe ndio mji mkuu wa nchi ni bora sasa tukafanye miji yote miwili ya Dar es Salaam na Dodoma kuwa miji mikuu ya nchi, baadhi ya taasisi ziwe Dodoma na baadhi ziwe Dar es Salaam.
Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza kuwa ni miji mikuu miwili, kuna nchi nyingine pia kama Malaysia, Sri-Lanka na Eswatini zenye miji mikuu miwili. South Africa yenyewe ina miji mikuu mitatu.
Makao yalikuwa Dar vizuri tu, kikaenda kikarudi yakahamishiwa Ddm kwa harambee ya mkono wa chuma kwa kupewa masaa watake wasitake, mwishowe utekelezaji kwa 100% ukakamilika.
Ddm pameshaanza kunawiri na Serikali imetulizana pale, zimeanza misafara ya weshimiwa kila siku kiguru na njia kwenda kufanyia kazi kwenye Ikulu kongwe ya Magogoni!
Wanaotenda hayo, walikuwepo kwenye maamuzi ya kupitisha kuhamia Ddm.
Nanyi wadau badala ya kulaani, mmeanza ngebe za kusapoti kinachofanywa na viongozi wabadhirifu wa fedha za umma kwa kufanya misafara isiyokoma ya nenda rudi Dar-Ddm!
Miji mikuu miwili for what!
Kunakuwa na mantiki gani kusapoti mambo ya kipumbaf yasiyo na tija kwa Taifa?