Pendekezo: Tanzania tuwe na miji mikuu miwili ya nchi, Dodoma na Dar es Salaam

Unawezaje kuyarudisha kinyume nyume maamuzi yaliyokwisha kutekelezwa?

Makao yalikuwa Dar vizuri tu, kikaenda kikarudi yakahamishiwa Ddm kwa harambee ya mkono wa chuma kwa kupewa masaa watake wasitake, mwishowe utekelezaji kwa 100% ukakamilika.

Ddm pameshaanza kunawiri na Serikali imetulizana pale, zimeanza misafara ya weshimiwa kila siku kiguru na njia kwenda kufanyia kazi kwenye Ikulu kongwe ya Magogoni!

Wanaotenda hayo, walikuwepo kwenye maamuzi ya kupitisha kuhamia Ddm.

Nanyi wadau badala ya kulaani, mmeanza ngebe za kusapoti kinachofanywa na viongozi wabadhirifu wa fedha za umma kwa kufanya misafara isiyokoma ya nenda rudi Dar-Ddm!

Miji mikuu miwili for what!

Kunakuwa na mantiki gani kusapoti mambo ya kipumbaf yasiyo na tija kwa Taifa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…