Pendekezo: Tuunde umoja wa wakulima humu JamiiForums

Pendekezo: Tuunde umoja wa wakulima humu JamiiForums

Naunga mkono hoja na upande mwingine itasaidia cost sharing ya logistics mf munaweza kuweka mafuta.na kutumia gari moja au au kusafirisha mbolea au mbegu kwa cost sharing etc.
 
Binafsi nimelipenda hili wazo kwakuwa hamchangii gharama, kila mtu anakua na shamba lake cha msingi mnakubaliana tu mnalima nini. Hii pia itasaidia wakati wa kuuza mnaweza mkamtafuta hata mnunuzi mkubwa kwakuwa mtaweza kutosheleza uhitaji wake (mtakua na mzigo wa kutosha as a group). Ni wazo zuri tukilifanyia kazi. Natamani kuwa mmoja wao hasa kwenye mazao ya mboga mboga
 
Basi tulio tayari tutafute namna ya kukutana, tujadili. Binafsi naona Tanzania ni kubwa sana, nashauri tukutane kikanda au kimkoa, au vile itakavyoonekana inafaa ili kuleta hamasa na urahisi katika usimamizi na uendeshaji wa shamba
 
Natoa ushauri; wazo ni zuri, commitment ya wajumbe wote ni kitu kizuri haswaaa. Hili jambo siyo mara ya kwanza kulisikia, wengi wamefeli hapo kwenye commitment na uaminifu + uadilifu.

Yafaa kikundi kiwe na katiba ambamo mambo yote yataoneshwa, ili kila mtu afate hiyo, au kama ulivopendekeza kila mtu amiliki na kutekeleza mradi wake. Vinginevyo lawama haziishi.
 
Nilikuwa kwenye kundi la mtandao wasap! kilichotokea ni majonzi! hamasa ikawa juu, tukabun mradi wa mahindi, na pili pili. mahindi tukaweka mmoja wetu, akashindwa kufuatilia maji, mahind yakakauka karibu yatoe mbelewele. pia nilikuwa na mrad mwingine na yeye, mahind yakakomaa, na nikayaona. baadaye ananiambia yameibiwa shamba, akaokoteza kapata gunia 3, ilikuwa eka 2. nikamwambia uza unitumie gawio. gawio hakutuma, enz izo gunia n elfu 30. nikamfata, nikaambulia elfu 20. nyingine ikawa danadana, had nikakata tamaa. nilichangia lak 7 katika huo mradi, na ule mwingine lak na nusu. haya, kwenye pili pili, sikuchanga, ila watu 10 kila mmoja alitoa laki 2, then mhazin akatokomea. asee! kwa sasa mim ni manager wa shamba fulan kubwa tu, pia nina lakwangu! kulima na usiyemjua ni tabu, ni bora ukala hiyo hela unenepe
Pole sana, mungu akipenda ntakutafuta skumoja unifunze machache
 
Nimefikiri kitu kimoja baada ya kuona kuwepo watu wengi kutafuta partner/ mtu wa kushirikiana nae katika kilimo.

Kuna changamotoAdd hii no 0753962832ingi sana katika kushare biashara maana kila mtu anakuwa ana malengo yake wengi huwa wanaumia na kulia na wengine huwa washangilia kwa mafanikio.

Nimeona tufanye hivi; mnajiunga mnakuwa labda 5 mnaingia Morogoro kwenda kulima maharage mnakodi heka 10.

Zile heka kumi mtagawana kulingana na uhitaji wa mtu mwenyewe, kila mtu atagharamia kivyake. Hii ni kuchangia ujuzi na sio fedha kwa sababu mtakuwa mnalima karibu karibu.

Ukisema mmoja atoe pesa na mwingine atoe ujuzi mara nyingi mwisho wake sio mzuri. Lakini hii itakusaidia kukujengea kujiamini na uzoefu na ujuzi zaidi.

KWA MTAZAMO WANGU
tuunde kikundi ambacho tutakutana whatsapp ambapo tutajadili tulime nini na tukalime wapi na nikiasi gani cha heka kitahitajika, hii itamsaidia hata yule mwenye uwezo wachini kupata hata robo au nusu heka.

Endapo tutakuta na kufanikiwa kuunda hicho kikundi na kuingia shambani kuanzia kuandaa shamba, kupanda yaani hatua zote tufanye wenyewe ili kuongea ujuzi zaidi.

Pia itatuwezesha kupaza sauti kwa serikali kama kutakuwa tunahitaji msaada maana tutakua ni vijana wa mfano katika taifa. Naimani viongozi na mawaziri hasa wa kilimo watatupeleka mbali.
Lazima tujigawa katika kilimo kutakuwa na watu watakao lima maharage, mpunga, karanga, labda na ufuta hapo lazima taifa litutambue maana sisi ndio tutakua wakwanza na njia rahisi sana ya kupata mikopo ya kifedha na dhana za kilimo.
Add
 
Back
Top Bottom