Pendekezo: Tuunde umoja wa wakulima humu JamiiForums

Naunga mkono hoja na upande mwingine itasaidia cost sharing ya logistics mf munaweza kuweka mafuta.na kutumia gari moja au au kusafirisha mbolea au mbegu kwa cost sharing etc.
 
Binafsi nimelipenda hili wazo kwakuwa hamchangii gharama, kila mtu anakua na shamba lake cha msingi mnakubaliana tu mnalima nini. Hii pia itasaidia wakati wa kuuza mnaweza mkamtafuta hata mnunuzi mkubwa kwakuwa mtaweza kutosheleza uhitaji wake (mtakua na mzigo wa kutosha as a group). Ni wazo zuri tukilifanyia kazi. Natamani kuwa mmoja wao hasa kwenye mazao ya mboga mboga
 
Basi tulio tayari tutafute namna ya kukutana, tujadili. Binafsi naona Tanzania ni kubwa sana, nashauri tukutane kikanda au kimkoa, au vile itakavyoonekana inafaa ili kuleta hamasa na urahisi katika usimamizi na uendeshaji wa shamba
 
Natoa ushauri; wazo ni zuri, commitment ya wajumbe wote ni kitu kizuri haswaaa. Hili jambo siyo mara ya kwanza kulisikia, wengi wamefeli hapo kwenye commitment na uaminifu + uadilifu.

Yafaa kikundi kiwe na katiba ambamo mambo yote yataoneshwa, ili kila mtu afate hiyo, au kama ulivopendekeza kila mtu amiliki na kutekeleza mradi wake. Vinginevyo lawama haziishi.
 
Pole sana, mungu akipenda ntakutafuta skumoja unifunze machache
 
Add
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…