ahsante kwa elimu nzuri. nmeeelewa huyu katumwa na nani kujib la mkubwa wake
HUYU NDIYE RAIS WA NCHI 2020
Na, Thadei Ole Mushi
Kuna watu bado wanaamini kuwa propaganda inafanya kazi kwenye siasa zetu za Tanzania. Propaganda zilikiwa zinafanya kazi kuanzia Kipindi cha Mkapa Kurudi Nyuma ila kwa sasa propaganda hazifanyi kazi sana.
Ni maeneo machache sana na kwa aina fulani ya watu ambao bado aina hii ya siasa inafanya kazi.
Hata vyama vyetu vya siasa vingi vimefuta vitengo vyao vya propaganda na kuanzisha kitengo cha uenezi ambavyo kwa baadhi ya vyama wameweka idara za utafiti. Kwa maana hiyo tumeingia kwenye siasa za utafiti maana yake tumeingia kwenye siasa Za Kusema ukweli.
Sio kwamba wanasiasa wanapenda kufanya siasa za aina hii hapana bali wapiga kura ndio waliowalazimisha kuingia kwenye siasa za aina hii. Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wasomi Tanzania na kukua kwa Technolojia ya habari na mawasiliano moja kwa moja imebadili aina ya wapiga kura huwezi kuwadanganya tena kwa Propaganda.
USHINDI WA RAIS 2020 HUU HAPA
Sensa ya mwaka 2012 inatuambia kwa statistics kwamba idadi kubwa ya watu waliopo Tanzania ni watoto na vijana. Watoto ni asilimia 44 huku vijana wakiliwa asilimia 35. Ikumbukwe kuwa watoto ni vijana wa kesho.
Hadi kufikia mwaka 2012 takwimu za sensa zilikuwa zinaeleza kuwa kwa kila watu 10 wa Tanzania, wanne ni vijana ambao umri wao ni kati ya miaka 15 na 35. Hao sita wengine waliobakia ni watoto na watu wazima.
Takwimu hizi zinaoana na wale waliojitokeza kujiandikisha kupiga kura mwaka 2015 ambapo vijana kati miaka 18-35 waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 12,894,576 sawa na asilimia 57 ya wapiga kura wote. Japokuwa kwa takwimu hizi zinatuonyesha kuwa kuna vijana wengi sana ambao hawakujiandikisha kupiga kura kutokana na sababu mbalimbali.
Kama vijana wote watajiandikisha kupiga Kura 2020 basi idadi ya wapigakura inaweza kuwa asilimia 70 na zaidi ni vijana huku asilimia hizi zikionekana kuongezeka kutokana na kundi kubwa la watoto wanaoingia kundi la vijana.
TAFSIRI YAKE NI NINI?
Tafsiri yake ni moja tu kuwa atakayefanya siasa na kundi hili ndiye atakaye kuwa na wapiga kura wengi 2020.
Utafiti wa juzi wa Twaweza umeonyesha mwelekeo mzuri wa kukubalika kwa vyama vya upinzani kutoka kwenye kundi hili. Hivyo hili ndio kundi linalopaswa kupiganiwa na kila chama ili Kujihakikishia ushindi wa 2020.
Kundi hili Kubwa ni wamachinga, vijana waliomaliza vyuo na waliopo vyuoni huku wengine wakiwa madarasa ya juu ya shule za sekondari. Kwa CCM wajiangalie wamewagusa kundi hili kiasi gani na ni kwa nini hawaongei lugha moja na wao ili watatue changamoto zao ili wanufaike na kura hizi.
Hata kwa wenzetu Kenya angalieni kwenye Kampeni ndio kundi linaloonekana sana kwenye kampeni tofauti na wazee. Kwa maana hiyo ni kundi lililoamua kufanya siasa na hata ukiangalia matokeo ya Uraisi wa Kenya na Tanzania kura za wagombea Urais hazitofautiani sana. Lolote kwenye Siasa linawezekana.
Hitaji la kundi hili ni moja tu, nalo ni Ajira.
2. BUNGE.
Wabunge wengi wanapigania maisha yao kwa sasa kuliko wanavyopigania maisha ya wananchi wao. Yaani wabunge wengi akili zao hazijatulia kuwasaidia wananchi wao bali wanawaza kesho yao. Kwa Tafsiri rahisi ni kwamba Wabunge pamoja na wananchi wao kila mtu "anapambana na hali yake"
Kuna viashiria vingi sana vya kwamba wabunge wetu mfukoni mwao hakuna fedha hivyo anawaza kwanza maslahi yake kabla ya maslahi ya Umma.
Wakati Lisu anasafirishwa kwenda Kenya yule Mbunge aliyewakopeshea ndege kwa mali Kauli aliwaambia waandishi wa habari kuwa wakati wanatafuta ndege ile hakuna Mbunge hata mmoja aliyekuwa na Dola elfu moja. Sio kwamba walikuwa hawana mfukoni la hasha hata ukienda kwenye account zao utakuta mambo ni yale yale.... ndio maana ndege ikakopwa kwa mali Kauli.
Wabunge kushindwa kutoa sitting allowance yao ya Siku moja yote na kuishia kutoa nusu ni kiashiria Kingine cha hali ya mifuko yao.
Jana Spika kaomba Bunge liongezewe budget kwa manaana hiyo Mhimili huu una njaa kali kuliko huku mtaani. Kuna wanaohoji siku za vikao vya bunge na siku za utendaji wa kamati kupunguzwa, nafikiri hii ni Prediction tosha ya mawazo yao.
NINI KITATOKEA?
Wabunge wengi watashindwa kukamilisha ahadi zao. Wakishindwa maana yake wagombea wapya watakao jitokeza 2020 wana nafasi kubwa sana ya kushinda uchaguzi kutokana na ambao walikuwepo kushindwa kukamilisha ahadi zao.
Kila chama kinatakiwa kifanye tathmini ya wabunge wao wameshafanya nini mpaka sasa na kama hakuna kitu waanze kuandaa watu wapya.
Eneo hili litawaathiri zaidi CCM kwa kuwa wabunge wa CCM hawanaga utamaduni wa kukubali kushindwa kwenye kura za Maoni ni mpaka wapigwe mieleka kama Stephen M. Wasira hifadhini maneno haya.
3. CCM
CCM itoke sasa ndani iingie kwenye Uwanja wa Siasa. Swala la kutegemea tena wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kufanya siasa badala yao ni kuhatarisha uhai wa chama.
Jukumu la kwanza la wakuu wetu wa wilaya na mikoa ni ulinzi na Usalama wa maeneo yao jukumu la kupambana na vyama vya siasa linatakiwa liachiwe vyama vya siasa wenyewe.
Kitendo cha kuuachia mhimili huu wa dola kufanya siasa ni kuviingiza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwenye siasa.
Mkuu wa Mkoa au Wilaya akishindwa kwa hoja na vyama vya siasa unafikiri akili yake itamsukuma kufanya nini zaidi ya kuagiza flan akamatwe na flan akamatwe?
CCM wanapaswa kuwa mstari wa mbele kukabiliana na upinzani na kama kutaonekana kuna viashiria vya uvunjifu wa amani ndio hawa wakuu wa mikoa na wilaya wajitokeze kuweka mambo sawa.
Hili litasaidia kuviondoa vyombo vyetu kwenye siasa. Kama ni mfuatiliaji wa habari za Tanzania hawa Ma-RPC wetu hawakauki kwenye vyombo vya habari na wote wanatoa matamko ya kuwadhibiti wanasiasa utafikiri nchi ipo kwenye vita
Thadei Ole Mushi,
Kada wa CCM damu,
19/09/2017.
Kwa mujibu wa taratibu za kanisa katoliki,askofu pengo sio msemaji wa kanisa,Msemaji ni Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania,
Rais wa Baraza la Maaskofu ndio Bosi wa Maaskofu wote nchini na hata askofu pengo anakuwa yuko chini yake, pia kama askofu pengo hakiutumwa na Rais wa Baraza la Maaskofu,na yeye pia hana mamlaka ya kulisemea kanisa katoliki na alichosema ni maoni yake
Ukadinali wake ni kwa ajili ya kupiga kura kumchagua Papa tu,ila yeye akiwa Tanzania kicheo ni Askofu wa Jimbo la Dar es Salaam,anataka watu waone kwamba Ukadinali ndio Ukubwa wa kanisa,Mkubwa wa kanisa ni Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania,na ni askofu wa Iringa Askofu Ngalalekumtwa na anayefatia kwa Cheo ni huyo Niwemugizi, Pengo yuko chini yake Rais wa Baraza
"first among equals" Pengo hamzidi Askofu yeyote kwa cheo,ni sawa na rafiki yangu sheikh mkuu wa mkoa wa Dar ajione mkubwa kuliko mashehe wa mikoa mingine