Pengo kwenye Muungano

Pengo kwenye Muungano

Na mie nichangie hapa,
haya majeshi ya kmkm,jeshi la mafunzo, valantia, jku zanzibar na kikosi cha zima moto yanaitwa vikosi vya smz au idara Maalum za smz na kamanda mkuu wa idara maalum au vikosi vya smz ni raisi wa zanzibar na kuna wizara ya vikosi vya smz (majeshi ya zanzibar) na waziri wake anateuliwa na raisi wa zanzibar, na wakuu wa majeshi haya wanateuliwa na raisi wa zanzibar,kwa maana hivyo serikali ya zanzibar ina mamlaka kamili juu ya majeshi haya,na serikali muungano haina mamlaka hata chembe kwenye majeshi haya wala haina uhusiano wowote na majeshi haya ya zanzibar.maelekezo na amri zote zinazoelekezwa kwa majeshi haya zinatolewa na raisi wa zanzibar moja kwa moja au kupitia waziri wake.

Hapo juu nlitaja jku(jeshi la kujenga uchumi) hii ifahamike kuwa jku zanzibar (JKUZ) na jku tanzania (JKUT)ni ni majeshi tafauti wala hayaingiliani popote,kila moja linajibu kwa waziri wake na serikali yake

Hii hapa nukuu ya katiba ya zanzibar kuhusu majeshi au vikosi vya serikali ya zanzibar,

1. Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM).

2. Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKUZ).

3. Idara ya Chuo cha Mafunzo (MF).

4. Idara ya Zimamoto na Uokozi (KZU).

5. Idara ya Valantia (KVZ).

Aidha kwa mujibu wa ibara ya 123(1) Kamanda Mkuu wa Idara Maalum za SMZ ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Ambapo Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ ndie msimamizi wa Afisi inayosimamia Idara Maalum za SMZ.

Muungano na serikali zake unahitaji matengenezo makubwa sana,kuna matatizo mengi ambayo yapo kwenye msingi wa muungano na hayaingii akilini na yanakiuka moja kwa moja muundo wa serikali za nchi
Excellent Mkuu! Safi sana, this is amazing! umetupa maarifa ya kufafanua na kuelimisha; na mapendekezo yako umetoa, very mature! Kama utakumbuka niliomba kwenye post yangu kuwa mtu mwenye maarifa na Katiba ya Znz atujuze na umefanya hivyo. Aidha, nimegundua pana tatizo la tafsiri ya baadhi ya maneno ambapo kwenye tasnia ya sheria tafsiri huwa ni jambo nyeti sana. Hii ni sababu iliyonifanya nipendekeze kuwa Rais wa Znz aongezewe kwenye titles zake "Amiri Jeshi" (siyo Amiri Jeshi Mkuu) kwasababu majeshi kote duniani yanaamuriwa na Amiri Jeshi/Mkuu. Katiba za pande zote mbili zidurusiwe kuakisi mabadiliko haya ya titles za Rais wa Znz ili kuvipa hadhi pia Vikosi vya SMZ. Na nikashauri kwamba bora Vikosi vya SMZ viwekwe kwenye Wizara ya Ulinzi ya JMT ili vipate hadhi ya kuamuriwa na Amiri Jeshi Mkuu kama yalivyo majeshi yote duniani na hii nikasema itaipunguzia SMZ zigo la bajeti ya kuviendesha ambapo sasa vitaendeshwa na serikali ya Muungano kupitia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambapo tayari tangu 1964 wizara hii ni ya Muungano.
 
Zanzibar ina Rais, ina wimbo wa taifa, ina bendera ya taifa na ya Rais, ina Baraza la Wawakilishi, ina Baraza la Mapinduzi, ina Valantia, Mafunzo na KMKM, ina Serikali Kamili ya Mapinduzi SMZ, ni taifa kamili lililoungana na Tanganyika kutengeneza Tanzania bila kupoteza utaifa wake.

Mojawapo ya sifa za Rais ni kuamuru majeshi yoooote ya Ulinzi na Usalama kwa cheo chake cha Amiri Jeshi Mkuu. Tanzania ina Amiri Jeshi Mkuu mmoja tu anayeamuru majeshi (JWTZ, JKT, Polisi, Magereza, Mgambo, Jeshi Usu la Uhifadhi; Katiba ya JMT Ibara ya147 (2) na (4) ingawa ibara ndogo ya 4 haijataja Jeshi la Mgambo, Jeshi Usu la Uhifadhi, Mafunzo Znz, Valantia na KMKM) ambaye ni Rais wa Muungano (isome Ibara ya 147 pamoja na Ibara ya 148 inayohusu madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu ili upate muktadha mzuri):-

1. Je, vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM vinaamuriwa na Amiri Jeshi Mkuu (Rais wa JMT)? Au vinaamuriwa na Rais wa SMZ (Zanzibar) ambaye siyo Amiri Jeshi Mkuu?

2. Na kama Rais wa JMT hana Mamlaka kuamuru vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM je, vinaamuriwa na nani?

3. Je, ni vibaya kama tukifanya marekebisho ya Katiba ili Rais wa Znz ambaye (naomba nitumie neno huenda) ndiye anayeamuru vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM aitwe Amiri Jeshi wa Vikosi vya SMZ (tumuongezee hiyo title) ili kuweka perspective vizuri kwa vikosi vya SMZ kuamuriwa na Amiri Jeshi pia kama ilivyo itifaki ya majeshi duniani kote? Kwahiyo Rais wa Znz atakuwa na titles za Rais wa SMZ, Mwenyekiti wa BMZ (Baraza la Mapinduzi Zanzibar), Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na AMIRI JESHI WA VIKOSI VYA SMZ (kwa minajili ya itifaki tusimuwekee neno #Mkuu kwenye maneno “Amiri Jeshi Mkuu”).

4. Katiba ya Muungano (ambayo inafanyakazi Znz pia) inazuia mtu, shirika, kikundi isipokuwa serikali kuanzisha majeshi soma Sehemu ya Nane, Sura ya Tisa (Majeshi ya Ulinzi), Ibara ya 147, Ibara ndogo ya (1), uk. 203. Sasa basi, Ibara hii imetaja serikali ndiyo inayoruhusiwa kuunda majeshi lakini haijabainisha ni serikali ipi, ya JMT, ya SMZ au zote?

5. Na kama ni hivyo je, vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM vimeanzishwa na nani? Vinaamuriwa na nani? Anayeviamuru ana wadhifa wa Amiri Jeshi au Amiri Jeshi Mkuu? Je, vikosi hivyo si vinafanyakazi ndani ya mipaka ya JMT? Nani anaamuru ulinzi wa mipaka ya nchi (JMT)?

6. Kama suala la Ulinzi na Usalama ni suala la Muungano je, ni Rais wa JMT ndiye anayeamuru vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM? Au vinaamuriwa na Rais wa SMZ ambaye siye Amiri Jeshi Mkuu na wala siye Rais wa Muungano?

7. Kama tukiruhusu Rais wa Zanzibar awe Amiri Jeshi kwa vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM je, Zanzibar itakuwa na Waziri wake wa Ulinzi (wa vikosi?)

Mwenye ufahamu na Katiba ya Zanzibar atujuze.

Tuko tayari kujifunza ambayo siyo dhambi hii.
Kabla hujaanzisha hizi mada uwe unasoma katiba kwanza na vyanzo vingine mbalimbali.

Unaanzisha mada za kikatiba wakati katiba na sheria hujui.

Na maandiko yako yanaonyesha una uelewa mdogo sana wa masuala ya kiutawala.
 
HUU SI MUUNGANO NI UVAMIZI ULIOPEWA JINA LA MUUNGANO
Mkuu,
Kinadharia hakuna Muungano mzuri ila Muungano mzuri ni ule unaoboreshwa mara kwa mara na huu wetu umeendelea kuboreshwa mara kadhaa na utaboreshwa hadi zaidi ya vitukuu. USSR iliboreshwa kupitia Perestroika iliyoanzishwa na Leonid Brezhnev 1979 na kukolezwa moto na Mikhail Gorbachev, EU imeboreshwa kupitia Brexit, OAU nayo imeboreshwa kuwa AU nk.
 
Mkuu, naleta mada ili wanaojuwa (siyo wewe usiyejuwa kitu kama ulivyonirejea na mimi) watuelimishe ukiwemo wewe. Usisubiri mtu mwingine aingie maktaba, adadavue, alete hapa, ndipo wewe uhujumu intellectual copyright (u-plagiarise) ya uelewa wa wenzio waliovuja jasho library. Aidha, nimegundua una uwezo sana na mada kama za TIKTOK kuliko za JF ndiyo maana mada zinapokuja huwa unakaa kimya kuvizia nani aanze kwanza kudadavua ili ndipo wewe ujichomeke humo katikati (rejea posts nyingi sijakuona ukiwa front-liner wa kujibu bali zaidi backbencher anayesubiri nani atasema nini/atachangia kwanza), hii syndrome kwenye academia inaaminika ni complete intellectual suicide. Nakushauri ukubali huu udhaifu wako ili usaidike, mimi kama ulivyonidescribe kwamba nina uelewa mdogo #ninakubali na ninafanya bidii kupost ili wenye ufahamu wanifinyange kupitia majibu yao kuwa mmoja wao, hivyo basi na wewe kubali dose hii ninayokupa ili upone usiendelee na syndrome hiyo inayokufanya intellectual suicide victim, usipokubali dose hii na kuchagua kupona basi tuna kila sababu kuwa macho na posts zako maana zitasababisha intellectual genocide kwenye JF. Extremism and Fundamentalism are twins b/o idea dropout.
 
Kabla hujaanzisha hizi mada uwe unasoma katiba kwanza na vyanzo vingine mbalimbali.

Unaanzisha mada za kikatiba wakati katiba na sheria hujui.

Na maandiko yako yanaonyesha una uelewa mdogo sana wa masuala ya kiutawala.
Katiba siyo Msahafu kwamba imetimia. Hata nadharia ya Isaac Newton ilikuwa na makosa na imefundisha (kwa makosa hayo hayo) Maprofesa wa heshima za juu sana ambao hawakubaini makosa hayo hadi mwanafunzi wa umri mdogo tu ndiye akaja kumkosoa Isaac Newton.

A 23-year-old physics student has discovered an error in Sir Isaac Newton's ''Principia'' that had gone undetected since the work laid out the laws of motion and gravity 300 years ago.
 
Ni wazo zuri. Kwenye 2. Nani anaamrisha jeshi usu la uhifadhi na mganbo wakati hayakutajwa kwenye katiba? Katiba yetu inaitambua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hivyo serikali kuunda vikosi maalum - siyo jeshi - inayo mamlaka. Rais kule Zanzibar ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekititi wa BLM na sio Rais wa serkali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mimi naunga mkono katiba kutazamwa upya na kufayiwa marekebisho kwa maslahi ya pande zote mbili na sio upande mmoja tu.
Safi sana mkuu mawazo yako, aidha, mchango wako umeendelea kutufikirisha zaidi hasa hapo uliposema nanukuu kipande "na sio Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar", sasa kwa JMT serikali ina Rais (ni mkuu wa mhimili wa serikali) kwa Znz siyo, hii nayo kama ulivyosema ina invite constitutional review (zote mbili).
 
HUU SI MUUNGANO NI UVAMIZI ULIOPEWA JINA LA MUUNGANO
JPM mwanzo wa utawala wake aliwahi kusema kwa habari ya Muungano kwamba haoni sababu ya kizazi hiki kuendelea kuishi kwa kulumbana kwenye historia, akachagiza kwamba tusiuishi Muungano kihistoria bali tuuishi kiuhalisia. Aligusa uelewa wa wengi kwa falsafa yake hii!
 
Mkuu, naleta mada ili wanaojuwa (siyo wewe usiyejuwa kitu kama ulivyonirejea na mimi) watuelimishe ukiwemo wewe. Usisubiri mtu mwingine aingie maktaba, adadavue, alete hapa, ndipo wewe uhujumu intellectual copyright (u-plagiarise) ya uelewa wa wenzio waliovuja jasho library. Aidha, nimegundua una uwezo sana na mada kama za TIKTOT kuliko za JF ndiyo maana mada zinapokuja huwa unakaa kimya kuvizia nani aanze kwanza kudadavua ili ndipo wewe ujichomeke humo katikati (rejea posts nyingi sijakuona ukiwa front-liner wa kujibu bali zaidi backbencher anayesubiri nani atasema nini/atachangia kwanza), hii syndrome kwenye academia inaaminika ni complete intellectual suicide. Nakushauri ukubali huu udhaifu wako ili usaidike, mimi kama ulivyonidescribe kwamba nina uelewa mdogo #ninakubali na ninafanya bidii kupost ili wenye ufahamu wanifinyange kupitia majibu yao kuwa mmoja wao, hivyo basi na wewe kubali dose hii ninayokupa ili upone usiendelee na syndrome hiyo inayokufanya intellectual suicide victim, usipokubali dose hii na kuchagua kupona basi tuna kila sababu kuwa macho na posts zako maana zitasababisha intellectual genocide kwenye JF. Extremism and Fundamentalism are twins b/o idea dropout.
Comment ya aya tatu tu umeijibu kwa Gazeti lote hilo nikiamua kutumia ujuzi wangu wa katiba si utarudi chuo wewe ?
 
Zanzibar ina Rais, ina wimbo wa taifa, ina bendera ya taifa na ya Rais, ina Baraza la Wawakilishi, ina Baraza la Mapinduzi, ina Valantia, Mafunzo na KMKM, ina Serikali Kamili ya Mapinduzi SMZ, ni taifa kamili lililoungana na Tanganyika kutengeneza Tanzania bila kupoteza utaifa wake.

Mojawapo ya sifa za Rais ni kuamuru majeshi yoooote ya Ulinzi na Usalama kwa cheo chake cha Amiri Jeshi Mkuu. Tanzania ina Amiri Jeshi Mkuu mmoja tu anayeamuru majeshi (JWTZ, JKT, Polisi, Magereza, Mgambo, Jeshi Usu la Uhifadhi; Katiba ya JMT Ibara ya147 (2) na (4) ingawa ibara ndogo ya 4 haijataja Jeshi la Mgambo, Jeshi Usu la Uhifadhi, Mafunzo Znz, Valantia na KMKM) ambaye ni Rais wa Muungano (isome Ibara ya 147 pamoja na Ibara ya 148 inayohusu madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu ili upate muktadha mzuri):-

1. Je, vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM vinaamuriwa na Amiri Jeshi Mkuu (Rais wa JMT)? Au vinaamuriwa na Rais wa SMZ (Zanzibar) ambaye siyo Amiri Jeshi Mkuu?

2. Na kama Rais wa JMT hana Mamlaka kuamuru vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM je, vinaamuriwa na nani?

3. Je, ni vibaya kama tukifanya marekebisho ya Katiba ili Rais wa Znz ambaye (naomba nitumie neno huenda) ndiye anayeamuru vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM aitwe Amiri Jeshi wa Vikosi vya SMZ (tumuongezee hiyo title) ili kuweka perspective vizuri kwa vikosi vya SMZ kuamuriwa na Amiri Jeshi pia kama ilivyo itifaki ya majeshi duniani kote? Kwahiyo Rais wa Znz atakuwa na titles za Rais wa SMZ, Mwenyekiti wa BMZ (Baraza la Mapinduzi Zanzibar), Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na AMIRI JESHI WA VIKOSI VYA SMZ (kwa minajili ya itifaki tusimuwekee neno #Mkuu kwenye maneno “Amiri Jeshi Mkuu”).

4. Katiba ya Muungano (ambayo inafanyakazi Znz pia) inazuia mtu, shirika, kikundi isipokuwa serikali kuanzisha majeshi soma Sehemu ya Nane, Sura ya Tisa (Majeshi ya Ulinzi), Ibara ya 147, Ibara ndogo ya (1), uk. 203. Sasa basi, Ibara hii imetaja serikali ndiyo inayoruhusiwa kuunda majeshi lakini haijabainisha ni serikali ipi, ya JMT, ya SMZ au zote?

5. Na kama ni hivyo je, vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM vimeanzishwa na nani? Vinaamuriwa na nani? Anayeviamuru ana wadhifa wa Amiri Jeshi au Amiri Jeshi Mkuu? Je, vikosi hivyo si vinafanyakazi ndani ya mipaka ya JMT? Nani anaamuru ulinzi wa mipaka ya nchi (JMT)?

6. Kama suala la Ulinzi na Usalama ni suala la Muungano je, ni Rais wa JMT ndiye anayeamuru vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM? Au vinaamuriwa na Rais wa SMZ ambaye siye Amiri Jeshi Mkuu na wala siye Rais wa Muungano?

7. Kama tukiruhusu Rais wa Zanzibar awe Amiri Jeshi kwa vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM je, Zanzibar itakuwa na Waziri wake wa Ulinzi (wa vikosi?)

Mwenye ufahamu na Katiba ya Zanzibar atujuze.

Tuko tayari kujifunza ambayo siyo dhambi hii.
Kimsingi katiba ya Zabzibar inasema wazi kuwa rais wa Zanzibar ndiye "Kamanda mkuu" wa vikosi vya SMZ na imempa madaraka ya kuviamrisha kufanya mission yoyote atakayoona inafaa kwa maslahi ya Zanzibar.

Kimsingi wazanzibar wana jeshi, na jeshi lao ni vikosi vya SMZ.

Amiri jeshi mkuu hawezi kuamuru vikosi vya SMZ mpaka apitie kwa rais wa Zanzibar amruhusu!
 
Mpaka sasa bara imebeba mzigo wote wa Zanzibar
Mzigo wa hiari huo, mkichoka utupeni chini tuu. Wenyewe tupo tutaokota na kuendelea na safari. Zanzibar ilikuwepo kabla ya Tanganyika na itakuwepo hata baadae vile vile inshallah.
 
Mkuu,
Kinadharia hakuna Muungano mzuri ila Muungano mzuri ni ule unaoboreshwa mara kwa mara na huu wetu umeendelea kuboreshwa mara kadhaa na utaboreshwa hadi zaidi ya vitukuu. USSR iliboreshwa kupitia Perestroika iliyoanzishwa na Leonid Brezhnev 1979 na kukolezwa moto na Mikhail Gorbachev, EU imeboreshwa kupitia Brexit, OAU nayo imeboreshwa kuwa AU nk.
Siongelei muungano mzuri naongelea uvamizi uliopewa Jina la muungano . Uvamizi ambao Tanganyika chini ya Laanatullahi Nyerere aliivamia Zanzibar Na kumkamata waziri mkuu wake aliyechaguliwa Na wananchi Shamte pamoja Na baraza lake la mawaziri Na kuwafunga katika jela Za Tanganyika kwa zaidi ya miaka 10.
Uvamizi ulipewa jina la muungano Mwezi wa April tarehe 26.
Shamte Na wenzake walikamatwa Januari Na kufungwa Tanganyika mwezi huohuo.

Kuna muungano hapo?

Zanzibar haihitaji Muungano inahitaji uhuru.
Chini ya huu uvamizi milele Itakuwa masikini.

Na hatukubali ni Bora tukose sote
 
Comment ya aya tatu tu umeijibu kwa Gazeti lote hilo nikiamua kutumia ujuzi wangu wa katiba si utarudi chuo wewe ?
I will write a book (not only gazeti) then as that has been my career for couple of decades now, I have never feared the fearful! When you share any lunacy you don't only address me personally, you address the JF audience, so if I don't answer, any JF Member will answer (will share his/her understanding). More so, allow me to repeat that, I derive and cherish comfort in learning, as the Author, I learn lifelong, so if you send me back to college to learn more that is equal to crowning me, not disapproving me, mkuu. I hope this settles the matter.
 
JPM mwanzo wa utawala wake aliwahi kusema kwa habari ya Muungano kwamba haoni sababu ya kizazi hiki kuendelea kuishi kwa kulumbana kwenye historia, akachagiza kwamba tusiuishi Muungano kihistoria bali tuuishi kiuhalisia. Aligusa uelewa wa wengi kwa falsafa yake hii!
Yeye Si mwathirika wa uvamizi , Na aliowaambia Pia Si waathirika wa uvamizi uliopewa Jina la muungano
Na ndiyo wakaguswa . Mzigo wa mwenzako kwako ni ganda la usufi
 
Siongelei muungano mzuri naongelea uvamizi uliopewa Jina la muungano . Uvamizi ambao Tanganyika chini ya Laanatullahi Nyerere aliivamia Zanzibar Na kumkamata waziri mkuu wake aliyechaguliwa Na wananchi Shamte pamoja Na baraza lake la mawaziri Na kuwafunga katika jela Za Tanganyika kwa zaidi ya miaka 10.
Uvamizi ulipewa jina la muungano Mwezi wa April tarehe 26.
Shamte Na wenzake walikamatwa Januari Na kufungwa Tanganyika mwezi huohuo.

Kuna muungano hapo?

Zanzibar haihitaji Muungano inahitaji uhuru.
Chini ya huu uvamizi milele Itakuwa masikini.

Na hatukubali ni Bora tukose sote
Ebu tupe maarifa, UN chini ya Katibu Mkuu wake U Thant ilimchukulia Mwl. Nyerere hatua gani kwa uvamizi huo? OAU chini ya M'kiti wake wa wakati huo Haile Selassie ilimchukulia Mwl. Nyerere hatua gani? Hata Mwenyekiti mpya wa OAU 1965 Kwame Nkrumah hasingemkalia Mwl kimya given kwamba Mwl alikuwa kinyume na wazo la Nkrumah la kuunganisha Afrika yote kwa wakati mmoja. Ni Mwl huyu huyu ndiye aliyelazimisha Wazungu waipe China uanachama wa kura ya turufu kati ya wajumbe wa 5. Ni Mwl huyu huyu ndiye aliyewaondoa Makaburu kwenye Commonwealth (wazungu walikuwa wakifaidika na utawala wa Makaburu kimyakimya), iweje aivamie Znz na dunia ikae kimya? Mwl alipotaka kuunga mkono kujitenga Biafra dunia ilipingana naye, iweje walikaa kimya kwa suala la Znz? Kwa taarifa tu, ijulikane leo kwamba Znz iliomba kujiunga na Kenya kabla ya Tanganyika lakini Jomo Kenyatta aliweka sharti gumu kwamba lazima yeye ndiye awe rais Karume awe RC kwasababu Muungano walioutaka ulikuwa ni wa nchi moja (kupoteza sovereignty zao) ilhali Muungano aliouasisi Mwl ulibakisha sovereignty ya Znz na ndiyo maana hata leo wameendelea kutambulika kupitia alama nyingi za kitaifa kama bendera, wimbo wa taifa, nk je, muungano wa Mwl siyo kwamba ulikuwa mzuri kuliko ule wa Jomo Kenyatta? Na je, msaliti wa Znz kupitia Muungano ni Mwl? Ni Jomo Kenyatta? Au ni Karume mwenyewe aliyeasisi wazo hilo na kuanza kulinadi kimataifa mara Kenya, mara Tanganyika? Je, mbona Mwl alikubali kupoteza Tanganyika na kubakisha Znz sasa je, nani anapaswa kulalamika ni Znz inayoendelea kushi au Tanganyika iliyopotelea mbali?
 
At least hujaniambia hayo niliyokuandikia kuwa Si kweli.

Huyo Laanatullahi Nyerere alipinduliwa Na wanajeshi Na waliomrudisha madarakani ni waingereza. Hivi lini Mkoloni alimweka kiongozi madarakani burebure Tu ,yaani apeleke Askari Wake wakauliwe ,wakuweke madarakani halafu iwe basi ?

Sasa ningalipenda usome kitabu

Kwaheri ukoloni kwaheri uhuru

Unaweza kukisoma online Andika kwenye Google Tu utakipata
 
Tanganyika ipo imelivaa koti la muungano Kwa kujiita Tanzania

At least hujaniambia hayo niliyokuandikia kuwa Si kweli.

Huyo Laanatullahi Nyerere alipinduliwa Na wanajeshi Na waliomrudisha madarakani ni waingereza. Hivi lini Mkoloni alimweka kiongozi madarakani burebure Tu ,yaani apeleke Askari Wake wakauliwe ,wakuweke madarakani halafu iwe basi ?

Sasa ningalipenda usome kitabu

Kwaheri ukoloni kwaheri uhuru

Unaweza kukisoma online Andina kwenye Google Tu utakipata
Uliyoyasema yanabaki kuwa propaganda za kiitikadi-shindanishi, siyo ukweli hadi hapo utakapothibitisha kwa ushahidi maana hata rekodi za Mahakama si zipo? Rekodi za Magereza si zipo? Thibitisha propaganda ili kuzifanya kuwa ukweli unaoweza kutumika hata kwenye rejea za kitaaluma. Mfano umesema Nyerere alipinduliwa, ebu thibitisha yafuatayo:-

1. Nani alikuwa Rais aliyechukuwa Tanganyika baada ya kumpindua Nyerere?

2. Nani alikuwa kiongozi wa mapinduzi kwa upande wa jeshi?

3. Nini ilikuwa hatima za waliompindua Nyerere?

4. Kama ushahidi wa Kimahakama na Kimagereza vimefichwa je, kuna ripoti zozote za Ki-media za nje zinazoweza kurejelewa kwamba Nyerere alipinduliwa?

5. Nani alimrudisha Nyerere kwenye Urais baada ya kupinduliwa?

6. Kuna rejea zozote kwenye Jumuiya za Kimataifa ambazo Tanganyika ni mwanachama kuthibitisha kwamba kiongozi wa nchi mwanachama wao amepinduliwa?

7. Je, kuna rekodi zozote za Jumuiya yoyote ya Kimataifa kulaani mapinduzi yaliyomng'oa Nyerere madarakani?

8. Je, kuna ushahidi wowote wa Katiba ya Tanganyika kuwa-suspended na jeshi lililompindua Nyerere?

9. Unaweza kutupatia majina ya viongozi wa mapinduzi waliounda serikali ya mpito baada ya kumpindua Nyerere?

10. Je, kuna ushahidi wowote duniani wa Tanganyika kuongozwa na serikali ya mpito baada ya mapinduzi yaliyomng'oa Nyerere?

11. Je, kama Nyerere alipinduliwa tena labda baada ya kifo cha Karume mwasisi mwenzake wa muungano kwanini Znz haikutumia mwanya huo wa Nyerere kupinduliwa kujiondoa kwenye muungano? Au ilinogewa na mahaba ya muungano huu?

NB.
Hili jambo liko kwenye mtaala wa masomo wa Znz labda?

Nijuavyo mimi ni kuwa kuliwa na jaribio la mapinduzi lakini siyo mapinduzi kamili. Matumizi ya lugha wakati fulani yanatusuta, tuwe makini.
 
Back
Top Bottom