Pengo la mtu kama Balozi Sefue linaonekana Serikali hii

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Pamoja na kwamba hakuwa mwanasiasa Sefue alikuwa mtu kama vile Consultant kwenye serikali ya Kikwete. Kwanza hakuwa mbunge, hakuwa waziri lakini aliziba pengo kwenye sehemu muhimu za kitaifa. Kwanza alikuwa ni mtu ambaye anajua biashara za kimataifa, alikuwa balozi aliyebobea, alijua miradi mingi na kuona mbali.

Lakini kikubwa Sefue alikuwa ni mtu ambaye Kikwete alimwamini na kumuuliza wakati akiwa na ulakini kama ushauri wa kukutana na upinzani au uhusiano wa nchi nyingine. Wakati wa Sefue Kikwete alifanikiwa kumleta Presdident Bush na Tanzania ikawa nchi chache sana zilizopewa pesa za millennium fund na kuweka umeme na kujenga barabara nyingi.

Lakini vilevile sera ya kilimo kwanza Sefue alisimamia. Vilevile Sefue alikuwa mtu ambaye anaweza kumwambia kila kitu wazi Kikwete bila woga kwa manufaa ya nchi. Sitaki tuanze kumfananisha na katibu mkuu wa sasa maana sio lazima kazi hii ifanyike na katibu mkuu.

Cha kujiuliza Je ni nani ambaye anaweza kumwambia Magufuli ukweli wakati mambo yanaenda kombo bila kuogopa? Tungesema Prof wetu wa mambo ya nje na EA lakini tatizo hana uzoefu wa kitaifa na ndiyo maana tunaona hata hizi barua za kuzuiwa na US nachukuwa muda kwasababu hana uzoefu au inabidi afanye kwa kumfurahisha Magufuli na sio kila wakati ni jasiri wa kusema ukweli.

Je, ni nani anaweza kumwambia na kuaminiwa na Magufuli kiasi kwamba akamwambia ukweli kwamba bila chaguzi huru tutaweza kabisa kuingizwa kwenye vikwazo vya kitaifa. Nani anaweza kumwambia ukweli kwamba tume huru ni muhimu na kama nchi tumetegwa.

Nani Tanzania anaweza kuwa rafiki wa kweli na kumwambia Magufuli bila kupindapinda kwa manufaa ya nchi yetu. Kwa mawazo yangu tungefaidika kama nchi kuwa na mtu mmoja wa hivi na sio lazima awe mwanasiasa lakini inabidi awe na uzoefu sehemu nyingi hata kama ni kutoka kwenye sera binafsi. Hii sio topic ya siasa ni ya kitaifa na wote hawa nawaongelea hapa ni chama hichohicho
Pascal Mayalla
 
Kamundu, Lile genge ndo lilimharibu akawa anatoa siri za ikulu siri mojawapo ile ya mita za mafuta kuwashtua wazifugue.

Kwa maana hiyo genge fisadi liliharabu sana viongozi wetu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je ni nani anaweza kumwambia na kuaminiwa na Magu kiasi kwamba akamwambia ukweli kwamba bila chaguzi huru tutaweza kabisa kuingizwa kwenye vikwazo vya kitaifa. Nani anaweza kumwambia ukweli kwamba tume huru ni muhimu na kama nchi tumetegwa.
Mkuu Kamundu, naunga mkono hoja, Yahana na Yohani ni ma skulmetes, hivyo ni kweli Yohani hawezi kuweleza kitu Yohana!.

Ila uchaguzi wetu ni uchaguzi huru na wa haki, na tume yetu ni tume huru, kilichofanyika serikali za mitaa ndio kinakwenda kufanyika October, 2020, kama Watanzania sisi wenyewe tumekubali, kwanini beberu aje kutuingilia na haya ni mambo yetu ya ndani?.
P
 
Kuandika kinyume nyume kumesababishwa uchukiwe sana humu.
Najua unang'ata na kupuliza
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Pascal, kumbuka uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji haukuwa na waangalizi wa kimataifa. Endapo uchaguzi huu utagubikwa na kasoro nyingi basi tutegemee kama taifa na vikwazo vingi sana vya kiuchumi tuelekeapo 2025. Usifikiri mabalozi wa nchi za nje hawakuyaona hayo wala kutoyatolea taarifa zake za kidiplomasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…