UTPC
Journalists' Union
- Apr 17, 2026
- 51
- 38
Katika shule za msingi na sekondari mkoani Mwanza, watoto wenye ulemavu bado wanakabiliwa na mazingira ya kujifunzia yasiyo rafiki, kutoka vyoo visivyofikika hadi madarasa yasiyo na njia salama za kupita. Hali hii imeendelea kujitokeza licha ya uwepo wa sera na sheria zinazotambua haki ya watoto wenye ulemavu kupata elimu katika mazingira jumuishi.
Sehemu hii ya pili ya makala inachunguza kwa sababu za kiuwajibikaji ambazo zimechangia kuendelea kuwepo kwa changamoto za miundombinu isiyo rafiki kwa watoto wenye ulemavu katika shule za msingi na sekondari katika wilaya ya Nyamagana, Ilemela na Misungwi mkoani Mwanza, ikichambua kwa nini wajibu wa kisheria umeendelea kubaki kwenye maandiko badala ya kuonekana ukitekelezwa.
Nchini Tanzania, viongozi wa umma wana wajibu wa moja kwa moja kulinda haki za msingi za raia. Kwa mujibu wa Ibara ya 11 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, serikali ina wajibu wa kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kijamii, ikiwemo elimu kwa wananchi wake.
“Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki ya kujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi au hali ya ulemavu, na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi,” imeeleza Katiba.
Wajibu huu umetiliwa mkazo zaidi na Sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010, hususan Kifungu cha 27 kinachotambua haki ya watu wenye ulemavu kupata elimu katika mazingira jumuishi.
“Watu wenye ulemavu wa rika zote na jinsia zote watakuwa na haki sawa ya kupata elimu, mafunzo katika mazingira jumuishi, pamoja na kunufaika na matokeo ya tafiti kama raia wengine,” imeeleza sheria.
Endapo viongozi wa kisiasa wanaposhindwa kuweka kipaumbele cha miundombinu rafiki kwenye mipango na bajeti za elimu, wanakiuka dhamana ya kikatiba na kisheria ya kulinda haki ya elimu kwa watoto wenye ulemavu.
Katika ngazi ya utekelezaji, sheria imeweka wajibu wa wazi kwa mamlaka za kiutawala. Kifungu cha 35 cha sheria hiyo ya watu wenye ulemavu, kimezitaka mamlaka husika kuhakikisha majengo ya umma yanayotoa huduma kwa wananchi yanakuwa yanayofikika kwa watu wenye ulemavu.
Licha ya takwa hilo la kisheria, bado wanafunzi wenye ulemavu katika shule za msingi na sekondari wilaya ya Nyamagana, Ilemela na Misungwi mkoani Mwanza, wanakumbana na kadhia ya miundombinu isiyo rafiki kwao.
Katika hotuba yake ya Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka 2025/26, Prof. Adolf Mkenda alisema kuwa katika jitihada za kuimarisha elimu jumuishi, serikali itaendelea kutoa ufadhili kwa walimu wanaofundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum.
“Serikali itaendelea kutoa ufadhili wa masomo kwa walimu 2,000 watakaosoma Stashahada ya Ualimu wa Elimu Maalum na kuendelea kuimarisha utoaji wa elimu jumuishi kwa wanafunzi na walimu wa elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu,” alisema Prof. Mkenda.
aziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka 2025/26, Mei 12, 2025 Bungeni Jijini Dodoma.Hata hivyo, jitihada hizi za serikali zinaonekana kutofua dafu, kwani katika mkoa wa Mwanza bado kuna kilio cha uchache wa walimu wa kufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule za msingi na sekondari.
Mmoja wa walimu wa Shule ya msingi Nyamagana (Jina limehifadhiwa) amesema bado kuna uhaba wa walimu wenye taaluma ya kufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule za msingi na sekondari mkoani Mwanza.
“Vifaa na mazingira ya kujifunzia ni mabovu, kwanza hata aina ya walimu ambao wanatakiwa wawepo,” amezungumza mwalimu.
Akizungumza Bungeni jijini Dodoma, aliyekuwa Waziri wa TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa alisema kuwa serikali imefanikiwa kuongeza idadi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum hadi kufikia asilimia 175, bila kutaja idadi ya wanafunzi hao.
“Mtoto wa Kitanzania, popote alipo hawezi tena kuzuiwa na umbali na hawezi tena kusahaulika kwa sababu ya ulemavu; elimu sasa ni haki ya kila mmoja na Tanzania mpya inaanzia darasani,” alisema Mchengerwa.
Kibonzo kuhusu wanafunzi wenye ulemavu wakiwa katika mazingira ya shule yenye miundombinu mibovu, wakilalamika juu ya kukosekana kwa uwajibikaji. Picha na ChatGPT.Wakati Mchengerwa akitoa kauli yenye matumaini kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, Joasen Julius, mkazi wa Bulale, kata ya Buhongwa jijini Mwanza, mwenye ulemavu wa miguu na kuzungumza, amesema serikali ina wajibu wa kufuatilia pesa inazotoa, na kuwafikilia wanafunzi wenye ulemavu pindi wanapoweka mipango yao.
“Serikali ikitoa pesa inabidi iangalie pande zote, watu wenye mahitaji maalum na wengine. Mfano, wakitoa pesa za madawati, inatakiwa waangalie je, lile dawati litamfaa mwenye ulemavu? Kuna wengine wana matatizo ya uti wa mgongo, hawawezi kukaa kwa muda mrefu,” amezungumza Julius.
Kauli ya Julius inaungwa mkono na Sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010, ambayo imeweka wajibu wa kisheria kwa serikali kuhakikisha miundombinu ya umma inakuwa rafiki kwa watu wenye ulemavu. Kwa mujibu wa Kifungu cha 35 (1) cha sheria hiyo, “Waziri, kwa kushauriana na Waziri mwenye dhamana ya majengo, na kwa kadri itakavyowezekana, atahakikisha kuwa kila jengo la umma pamoja na majengo mengine yanayotoa huduma kwa umma yanafikika kwa watu wote wenye ulemavu,” kwa kuwa shule za msingi na sekondari ni majengo ya umma yanayotoa huduma ya elimu, yanapaswa kutekeleza matakwa haya ya kisheria.
Zaidi ya hapo, sheria imeweka wajibu wa wazi kwa taasisi zote zinazotoa huduma kwa umma. Kupitia Kifungu cha 35 (2), inaelekezwa kuwa “Waziri, kwa kushauriana na Baraza, ataandaa kanuni zitakazobainisha upatikanaji wa majengo ya umma kwa madhumuni ya kutoa mwongozo kwa taasisi za umma na binafsi,” aidha, Kifungu cha 35 (3) kinasisitiza kuwa kila taasisi ya umma au binafsi inapaswa kuzingatia kanuni hizo, hususan “wakati wa ujenzi, ukarabati mkubwa au upanuzi wa jengo la umma,” au pale ambapo kufanya hivyo kutawezesha watu wengi zaidi wenye ulemavu kupata huduma kwa ufanisi zaidi. Hii inaonesha kuwa mipango ya ujenzi wa shule inapaswa kuzingatia mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu tangu katika hatua za awali.
Moja ya choo cha Shule ya Msingi St. Benjamin iliyopo Mwasonge wilayani Misungwi, katika mkoa wa Mwanza, kikiwa hakina ngazi maalum za kuingia kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu. Picha na Dominic AllenSheria hiyo pia inatambua changamoto zilizopo katika majengo ya umma yaliyokwisha kujengwa. Kupitia Kifungu cha 35 (4), inabainisha wazi kuwa “Kila jengo la umma litarekebishwa ili liweze kuzingatia matakwa ya upatikanaji kwa mujibu wa sehemu hii.”
Masharti haya yanaweka wajibu wa moja kwa moja kwa serikali na halmashauri kuhakikisha shule zilizopo zinaboreshwa ili ziwe rafiki kwa wanafunzi wenye ulemavu. Hivyo, hoja ya kufuatilia matumizi ya fedha za umma na kuhakikisha miundombinu inawafikia watoto wenye mahitaji maalum, ni wajibu unaotambuliwa kisheria.
Magege Hailala Magege, ambaye ni mkazi wa kata ya Nyamanoro, Ilemela kwa takriban miaka 40, pia ni Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani hapo amesema moja ya sababu zinazopelekea wanafunzi wenye ulemavu kukumbana na kadhia ya miundombinu isiyo rafiki, ni kutokuwajibika kwa viongozi wa serikali za mitaa, ambapo hawashirikiani na kamati za shule, akitolea mfano wa eneo analoishi.
“Uongozi wa serikali za mtaa haushirikiani na hizo kamati za shule, kwa sababu hizi kamati za shule ndiyo zinazopanga kila kitu kwenye shule, walimu kazi yao ni utekelezaji,” ameeleza Magege.
Magege amesema hata katika kamati za shule kuna changamoto, hasa kukiwa na hakuna wazazi ambao wana watoto wenye ulemavu, jambo linalosababisha watoto hawa kutopewa kipaumbele.
“Kwenye hizi kamati za shule wazazi wanaochaguliwa, wanachaguana wenyewe kwa wenyewe kupata ile kamati. Kwa hiyo usipompata mzazi mwenye mtoto mlemavu kuwepo kwenye hiyo kamati, basi kamati hiyo haitaendeshwa kwa kuwakumbuka wale watoto wenye ulemavu,” Magege akizungumzia changamoto za kamati za shule.
Hata hivyo, Magege ameona kuwa jamii pia ina jukumu katika kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata haki ya elimu. Lakini katika eneo analoishi jamii haijaweka kipaumbele kwenye suala hilo.
“Mwamko wa jamii, wanaotoa msaada au wanaojali ni wale ambao wana mtoto wa aina hiyo, siyo jamii ambayo inajali kuona mtoto wa mwenzio au mtoto mlemavu kama anavyoweza kumjali wa kwake,” amezungumza Magege.
Robert Kahema ambaye ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwasonge A wilaya ya Misungungwi, ameona halmashauri za maeneo husika ndiyo zinawajibika zaidi katika kuhakikisha miundombinu ya majengo na mingine inakuwa rafiki kwa watoto wenye ulemavu.
“Bila shaka halmashauri ndiyo inafahamu, kwamba wao ndiyo wanapaswa watekeleze miundombinu. Kwa hiyo, kama walijisahau au kama kuna utaratibu wa kufuatilia…halmashauri ina wajibu mkubwa kwa ajili ya kushughulikia suala hili la miundombinu,” ameleeza Kahema.
Abdulrahman Kange, akiwa ni Diwani wa kata ya Nyamanoro kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), anaona uwajibikaji ni suala la pamoja, yaani jamii, wadau na serikali kwa ujumla.
“Suala la elimu ni suala jumuishi…kwa hiyo ni jambo ambalo tunatakiwa kukaa kwa pamoja kuangalia ni namna ya kuweza kutatua changamoto hiyo ya watoto wetu wenye ulemavu,” amesema Diwani Kange.
Mbarala Maharagande, akiwa ni Katibu wa Idara ya Haki za Binadamu na Vyombo vya Uwakilishi wa Wananchi, ACT Wazalendo Taifa, ameinyooshea kidole Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisema kuwa ina wajibu wa moja kwa moja kuhakikisha suala la changamoto ya miundombinu isiyo rafiki kwa watoto wenye ulemavu litapatiwa dawa, na ndiyo imesababisha kuwepo kwa tatizo hili.
“Ni serikali tu, kwa sababu ndiyo inayokusanya kodi na ndiyo inayopanga matumizi ya kodi ambayo ni fedha za wananchi…kwa hiyo ndiyo yenye wajibu, na ndiyo imesababisha uwepo wa tatizo hili,” ameeleza Maharagande.
Kwa upande wake Abdulrahman Lugone, Mweka Hazina mstaafu wa Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA), amesema tatizo la kukosekana kwa miundombinu rafiki limeendelea kuwepo kutokana na uwajibikaji mdogo kuanzia kwenye utekelezaji wa sera na usimamizi wa sheria husika.
“Uwajibikaji mpaka sasa umekuwa mdogo, haujakuwa kamilifu kwa upande wa utekelezaji wa sera ya huduma kwa watu wenye ulemavu na sheria inayohusu matunzo kwa watu wenye ulemavu. Ustawi wa jamii wanapaswa wawajibike, wazazi wanapaswa wawajibike, serikali za vijiji na mitaa zinapaswa ziwajibike, halmashauri zinapaswa ziwajibike kwa mujibu wa sheria,” maoni ya Lugone kuhusu uwajibikaji.
Makumba Mwemezi, ambaye ni Mkuu wa idara ya utafiti, ubunifu na uchambuzi wa sera kutoka shirika la HakiElimu, amesema serikali ina wajibu wa moja kwa moja kuhakikisha kuwa watoto wenye ulemavu wanapata haki ya elimu bora.
“Ni serikali kwa ujumla, lakini vilevile sheria na miongozo inataka ushirikiano kati ya serikali na wadau. Na hatuitupii lawama serikali peke yake, na wadau vilevile,” ameeleza Mwemezi.
Mwemezi amesema kuwa miongoni mwa mambo ambayo yanachangia kuwepo kwa changamoto hii ya miundombinu mibovu isiyo rafiki kwa watoto wenye ulemavu shuleni, ni pamoja na suala la ufadhili wa fedha.
“Unapozungumza kuhusu miundombinu na mahitaji ya watoto wenye mahitaji maalum na wengine, unazungumzia fedha, na kimuundo zipo fedha ambazo zinatakiwa zitoke serikalini na zingine kutoka halmashauri kupitia mapato yao ya ndani. Kwa hiyo, changamoto kubwa ni kutofikiwa kwa kiwango cha fedha kulingana na mahitaji,” amesema Mwemezi.
Suala la kukosekana kwa uwajibikaji katika ngazi mbalimbali za uongozi linaonekana pia kuwa ni kiini cha tatizo la miundombinu mibovu katika shule za msingi na sekondari nchini Tanzania, linaloendelea kukatisha ndoto za wanafunzi wenye ulemavu.
“Eneo la pili ni suala la uwajibikaji, na uwajibikaji hapa kuna ngazi maalum. Kuna ngazi ambazo zinawahusu viongozi, kuna zile ngazi ya halmashauri, viongozi wa elimu, lakini vilevile ngazi za shule, kamati za shule, bodi za shule…na hili sasa tunawagusa watendaji moja kwa moja,” Mwemezi akizungumzia suala la uwajibikaji.
Tatizo la miundombinu isiyo rafiki kwa watoto wenye ulemavu katika shule za msingi na sekondari katika mkoa wa Mwanza sio la bahati mbaya, bali ni matokeo ya mifumo ya uwajibikaji isiyoridhisha. Wajibu wa kikatiba na kisheria umeendelea kubaki kwenye makaratasi, huku utekelezaji wake ukikosa nguvu katika ngazi zote. Matokeo yake, watoto wenye ulemavu wanaendelea kusukumwa pembezoni mwa mfumo wa elimu, licha ya sheria kutamka wazi kuwa wana haki sawa ya kujifunza katika mazingira jumuishi.
Kadri lawama zinavyosambaa kati ya viongozi wa kisiasa, watendaji wa serikali za mitaa, kamati za shule na jamii kwa ujumla, swali la msingi linaendelea kubaki, “Ni wapi hasa uwajibikaji unapaswa kuanzia, na kwa nini umeendelea kukwepwa?” Sehemu ya tatu ya makala hii itaangazia mwelekeo wa hatua zinazoweza kuchukuliwa, ili watoto wenye ulemavu wasiendelee kulipia gharama ya kutotekelezwa kwa sera na sheria zinazolenga kuwalinda.
ANDIKO LA: Dominic Allen
Makala imeandaliwa na Mwandishi anayeshiriki katika programu maalum ya kukuza uandishi wa maslahi kwa umma (Public Interest Journalism Fellowship) inayoratibiwa na UTPC kwa kushirikiana na IMS.
Pia soma ~ Miundombinu duni yakwaza elimu kwa Watoto wenye ulemavu Mkoani Mwanza
Sehemu hii ya pili ya makala inachunguza kwa sababu za kiuwajibikaji ambazo zimechangia kuendelea kuwepo kwa changamoto za miundombinu isiyo rafiki kwa watoto wenye ulemavu katika shule za msingi na sekondari katika wilaya ya Nyamagana, Ilemela na Misungwi mkoani Mwanza, ikichambua kwa nini wajibu wa kisheria umeendelea kubaki kwenye maandiko badala ya kuonekana ukitekelezwa.
Nchini Tanzania, viongozi wa umma wana wajibu wa moja kwa moja kulinda haki za msingi za raia. Kwa mujibu wa Ibara ya 11 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, serikali ina wajibu wa kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kijamii, ikiwemo elimu kwa wananchi wake.
“Mamlaka ya nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki ya kujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi au hali ya ulemavu, na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi,” imeeleza Katiba.
Wajibu huu umetiliwa mkazo zaidi na Sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010, hususan Kifungu cha 27 kinachotambua haki ya watu wenye ulemavu kupata elimu katika mazingira jumuishi.
“Watu wenye ulemavu wa rika zote na jinsia zote watakuwa na haki sawa ya kupata elimu, mafunzo katika mazingira jumuishi, pamoja na kunufaika na matokeo ya tafiti kama raia wengine,” imeeleza sheria.
Endapo viongozi wa kisiasa wanaposhindwa kuweka kipaumbele cha miundombinu rafiki kwenye mipango na bajeti za elimu, wanakiuka dhamana ya kikatiba na kisheria ya kulinda haki ya elimu kwa watoto wenye ulemavu.
Katika ngazi ya utekelezaji, sheria imeweka wajibu wa wazi kwa mamlaka za kiutawala. Kifungu cha 35 cha sheria hiyo ya watu wenye ulemavu, kimezitaka mamlaka husika kuhakikisha majengo ya umma yanayotoa huduma kwa wananchi yanakuwa yanayofikika kwa watu wenye ulemavu.
Licha ya takwa hilo la kisheria, bado wanafunzi wenye ulemavu katika shule za msingi na sekondari wilaya ya Nyamagana, Ilemela na Misungwi mkoani Mwanza, wanakumbana na kadhia ya miundombinu isiyo rafiki kwao.
Katika hotuba yake ya Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka 2025/26, Prof. Adolf Mkenda alisema kuwa katika jitihada za kuimarisha elimu jumuishi, serikali itaendelea kutoa ufadhili kwa walimu wanaofundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum.
“Serikali itaendelea kutoa ufadhili wa masomo kwa walimu 2,000 watakaosoma Stashahada ya Ualimu wa Elimu Maalum na kuendelea kuimarisha utoaji wa elimu jumuishi kwa wanafunzi na walimu wa elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu,” alisema Prof. Mkenda.
aziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka 2025/26, Mei 12, 2025 Bungeni Jijini Dodoma.
Mmoja wa walimu wa Shule ya msingi Nyamagana (Jina limehifadhiwa) amesema bado kuna uhaba wa walimu wenye taaluma ya kufundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule za msingi na sekondari mkoani Mwanza.
“Vifaa na mazingira ya kujifunzia ni mabovu, kwanza hata aina ya walimu ambao wanatakiwa wawepo,” amezungumza mwalimu.
Akizungumza Bungeni jijini Dodoma, aliyekuwa Waziri wa TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa alisema kuwa serikali imefanikiwa kuongeza idadi ya wanafunzi wenye mahitaji maalum hadi kufikia asilimia 175, bila kutaja idadi ya wanafunzi hao.
“Mtoto wa Kitanzania, popote alipo hawezi tena kuzuiwa na umbali na hawezi tena kusahaulika kwa sababu ya ulemavu; elimu sasa ni haki ya kila mmoja na Tanzania mpya inaanzia darasani,” alisema Mchengerwa.
Kibonzo kuhusu wanafunzi wenye ulemavu wakiwa katika mazingira ya shule yenye miundombinu mibovu, wakilalamika juu ya kukosekana kwa uwajibikaji. Picha na ChatGPT.
“Serikali ikitoa pesa inabidi iangalie pande zote, watu wenye mahitaji maalum na wengine. Mfano, wakitoa pesa za madawati, inatakiwa waangalie je, lile dawati litamfaa mwenye ulemavu? Kuna wengine wana matatizo ya uti wa mgongo, hawawezi kukaa kwa muda mrefu,” amezungumza Julius.
Kauli ya Julius inaungwa mkono na Sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010, ambayo imeweka wajibu wa kisheria kwa serikali kuhakikisha miundombinu ya umma inakuwa rafiki kwa watu wenye ulemavu. Kwa mujibu wa Kifungu cha 35 (1) cha sheria hiyo, “Waziri, kwa kushauriana na Waziri mwenye dhamana ya majengo, na kwa kadri itakavyowezekana, atahakikisha kuwa kila jengo la umma pamoja na majengo mengine yanayotoa huduma kwa umma yanafikika kwa watu wote wenye ulemavu,” kwa kuwa shule za msingi na sekondari ni majengo ya umma yanayotoa huduma ya elimu, yanapaswa kutekeleza matakwa haya ya kisheria.
Zaidi ya hapo, sheria imeweka wajibu wa wazi kwa taasisi zote zinazotoa huduma kwa umma. Kupitia Kifungu cha 35 (2), inaelekezwa kuwa “Waziri, kwa kushauriana na Baraza, ataandaa kanuni zitakazobainisha upatikanaji wa majengo ya umma kwa madhumuni ya kutoa mwongozo kwa taasisi za umma na binafsi,” aidha, Kifungu cha 35 (3) kinasisitiza kuwa kila taasisi ya umma au binafsi inapaswa kuzingatia kanuni hizo, hususan “wakati wa ujenzi, ukarabati mkubwa au upanuzi wa jengo la umma,” au pale ambapo kufanya hivyo kutawezesha watu wengi zaidi wenye ulemavu kupata huduma kwa ufanisi zaidi. Hii inaonesha kuwa mipango ya ujenzi wa shule inapaswa kuzingatia mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu tangu katika hatua za awali.
Moja ya choo cha Shule ya Msingi St. Benjamin iliyopo Mwasonge wilayani Misungwi, katika mkoa wa Mwanza, kikiwa hakina ngazi maalum za kuingia kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu. Picha na Dominic Allen