Peniela (Story ya kijasusi)

LEGE kindly njoo utupe cha usiku kuelekea wk end
 
SEASON 2
SEHEMU YA 36
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ hallow mheshimiwa “ akasema mzee Augustine baada ya waziri mkuu kupokea simu
“ samahani kwa kukusumbua mheshimiwa waziri mkuu mkuu”
“ Bila samahani Augustine”
“ Mheshimiwa waziri mkuu unakumbuka mchana nilikupigia simu na kukwambia kwamba pengine ningeweza kuja kukuona jioni ya leo?
“ Ndiyo nakumbuka Augustine”
“ Ok mheshimiwa basi nahitaji kuja kukuona usiku huu.Nina jambo kubwa sana ambalo haliwezi kusubiri hadi kesho.” Akasema mzee Augustine
‘ Ok Mr Augustine.Kama unaweza kuja hapa katika makazi yangu nitakusubiri”
“ Ahsante sana mheshimiwa .Ninakuja hapo muda si mrefu.Naomba nikufahamishe vile vile kwamba nitaongozana na vijana watatu.” Akasema mzee Augustine na kukata simu
“Waziri mkuu amekubali kuonana nasi kwa hiyo hatuna muda wa kupoteza hapa.Twendeni nyumbani kwake tukaonane naye.” Akasema mzee Augustine na kuyabeba mafaili yale na kwa haraka wakaingia garini na safari ya kuelekea kwa waziri mkuu ikaanza.

ENDELEA………………..
Saa tatu na nusu za asubuhi Peniela akawasili katika makazi ya John Mwaulaya akapokelewa na Josh.
“ Karbu sana peniela” akasema Josh na kumuongoza Peniela hadi sebuleni ambako kulikuwa na vijana wengine wawili waliovalia nadhifu.
“ Peniela kutana na Jacob na Francis ,hawa wako ofisi kuu na wamekuja kwa ajili ya lile suala nililokueleza.” Akasema Josh.Peniela akasalimiana na wale vijana na kuketi
“ Haya niambieni mlichokuwa mnataka kuniambia”akasema Peniela ambaye alionekana kuwa na haraka “
“ Peniela ni kama vile nilivyokueleza simuni.kwanza ni kuhusiana na mtu wa kutuongoza japo kwa muda mfupi.Alipoanza kuumwa John mwaulaya alimteua Osmund awe kiongozi wetu hadi alipofariki.Kwa sasa hatuna tena mtu wa kutuongoza hasa katika kipindi hiki ambacho John mwaulaya anaumwa na tukjokatika operesheni kubwa .Sisi watatu tumekaa na kuona kwamba tukuchague wewe utuongoze kwa wakati huu ambao hatuna mtu wa kutuongoza.Jambo la pili ni kuhusiana na ugeni unaokuja leo hii.Kuna wageni sita wanakuja leo wakitokea makao makuu nchini marekani.Bado hatufahmu nini kinawaleta watu hawa kwa hiyo tunahitaji mtu wa kuwapokea wageni hawa na kufahamu kilichowaleta.Tunaaminikwambawewe unaweza ukalibeba jukumu hilo Peniela” Akasema Josh.Peniela akafikiri kwa sekunde kadhaa na kusema
“Kwa nini ninyi peke yenu mfanye maamuzi kama haya ya kunitaka mimi niwaongoze? Mna hakika wenzenu watakubaliana nanyi? Akauliza Peniela
“ Watu wote wamekuwa wakijiuliza kuhusiana na nani ambaye atatuongoza .Kila mmoja wetu anafahamu majukumu yake lakini kuna mambo ambayo hatuwezi kuyafanya bila ya kupewa ruhusa na maelekezo toka kwa kiongozi kwa hiyo sisi kwa niaba ya wenzetu tunakupendekeza wewe ili uwe kiongozi wetu japo kwa muda na nina imani kwamba hata wenzetu wote watakubaliana na mapendekezo yetu.Wewe ni mtu unayeifahamu vyema team Sc41 na unaweza ukatuogoza vizuri.Tunaomba utukubalie ombi letu la kutaka utuongoze” akasema Jacob.
“ kwa kuongezea hapo alipoisha Jacob,hata mzee John mwenyewe ameonyesha kukukubali sana na anakuamini .Nina hakika hata akisikia kwamba tumefanya maaamuzi ya kukuomba utuongoze atakubaliana nasi” akasema Josh.Peniela kama kawaida yake akanyamaza kidogo akawaangalia wale vijana na kisha akasema
“ Ok nitafanya mnavyotaka lakini ni kwa wakati huu tuu wanaokuja hawa wageni.Baada ya wageni kuondoka basi John au makao makuu watawachagulia mtu mwingine wa kuwaongoza.Ok tuachane na hayo ,wageni hao wanaokuja tayari wametafutiwa mahala watakapofikia? Akauliza Peniela
“ Masuala yote alikuwa akiyashughulikia Osmund na hatufahamu kama tayari walikuwa wametafutiwa sehemu ya kufikia au bado”
“ Ok isiwe taabu,kuna hoteli nyingi nzuri hapa jijini. Nadhani Maryrose 72 hotel itawafaa sana. Josh shughulikia suala hilo ili wageni hawa watakapowasili tuwe tayari tumewatafutia sehemu nzuri ya kufikia.Jacob na Francis tunakwenda uwanja wa ndege kuwapokea wageni.” Akasema Peniela na kabla hawajaondoka akaomba Josh ampeleke chumbani kwa John Mwaulaya akamuangalie.
John mwaulaya alipomuona Peniela ameingia mle chumbani kwake alifurahi na kujitahidi kutabasamu.
“ P..Pe.Peniela..” akasema John kwa sauti dhaifu.Peniela akamtazama mzee yule pale kitandani ambaye alikuwa amelala hajiwezi akamuonea huruma sana.Akamsogelea karibu.
“ Pole sana John.” Akasema Peniela
“ Ahsante Penny…Ahsante kwa kuja kuniona” akasema John mwaulaya na kumfanyia ishara peniela asogee karibu zaidi.
“ Peniela najua sina muda mwingi wa kuendelea kuishi.I’m going to die soon.Kama nikifariki kabla operesheni 26B haijakamilika ,tafadhali hakikisha kwamba unafanikiwa kuikamilisha kwani ni operesheni muhimu sana.Ikisha kamilika nenda kaendelee na maisha yako.Kuna mambo mengi ambayo nilitaka nikufanyie kablaya kufa ili niweze kuyatengeneza upya maisha yako niliyoyaharibu lakini kutokana na afya yangu kuzorota sina hakika kama nitaweza tena kuyanfanya kwa hiyo nakusihi hakikisha ukikamilisha operesheni hii unaachana kabisa na team SC41.Go far away from here and live your life.Find yourself a man and start a family” akasema John.Peiela akalengwa na machozi
“ John you are not going to die.Iwill do anything in my power to make sure that you get well” akasema Peniela
“ usisumbuke Peniela.Sina maisha marefu .Tafadhali shughulikia kwanza suala la operesheni 26B na baada ya hapo shughulikia kuyajenga upya maisha yako.Nilikukabidhi kasha moja na kukupa maelekezo nini cha kufanya pindi ukiikamilisha operesheni 26B .Fuata maelekezo yangu niliyokupa’ akasema john mwaulaya.
“ Usiseme hivyo John.Nitafanya kila linalowezekana mpaka nihakikishe umekuwa salama.Utapona John.Nakuhakikishia utapona.Doctors are on the way coming.You’ll be ok John” akasema peniela
“ Peniela najua unanipenda na unaumia kuniona hivi lakini nakuhakikishia kwamba hata ufanye nini sintaweza kupona.Tafadhali usipoteze muda na mimi tena.Nimekwisha ishi vya kutosha hapa duniani na sehemu kubwa ya maisha yangu nimeishi nikiwa ndani ya team SC41 .Nimefanya mambo mengi makubwa,nimetoa uhai wa watu wengi na sasa na mimi ni wakati wangu umefika.I have to face death” akasema John.Peniela akashindwa kujizuia kutoa machozi
“ John..! akasema peniela lakini John akamfanyia ishara asiseme chochote.
“ Peniela ninakiona kifo changu.Sina ujanja wa kuweza kukikwepa.Ninakusi usiendelee tena kuwa ndani ya Team SC41.Mimi nimefanya mambo mengi mabaya ndaniya kikundi hiki.Nilikuwa nikitoa roho za watu bila huruma na sikujua kwamba sikumoja na mimi nitachungulia kifo.Sitaki uishi maisha kama niliyoishi mimi ndani ya Team SC41 na ndiyo maana nakuomba ukiikamilisha operesheni 26B achana kabisa na team SC41 na uende ukaishi mbali uendeshe maisha yako.”akasema John.Peniela akashindwa kuendelea kumuona John katika hali ile akatoka huku akilia.Josh akamfuata.
“ Its ok peniela.Tafadhali usilie.John will be fine” akasema Josh.
“ jana nilikuwa na hasira na John na sikutaka hata kumuona lakini baada ya kumuoa akiwa pale kitandani hajiwezi nimejikuta nikiumia tena” akasema Peniela.halafu akafuta machozi na kuufungua mkoba wake akatoa mkebe wa poda akajipaka usoni .
“ Josh muda unakwenda sana ,shughulikia suala lile la hoteli ya kufikia wale wageni.Suala hili la ugonjwa wa John niachie mimi nitalishughulikia” akasema peniela na kisha akaongozana na akina Jacob wakaingia katika magari yao na kuondoka kuelekea uwanja wa ndege
“ Nilimchukia sana John kwa kitendo chake cha kumteka Jason na kumtesa lakini baada ya kumuona tena leo hasira zangu zote zimepotea na nimejikuta nikumuhurumia tena.Pamoja na yote mabaya aliyoyafanyia lakini kuna mengimazuri ameyafanya katiamaisha yangu kwa hiyo natakiwa na mimi nionyeshe japo msaada wangu mdogo kwake kama shukurani zangu.Ni kweli ni yeye aliyeyaharibu masha yangu lakini ni yeye ambaye alihakikisha ninalelewa na kukua bila tatizo lolote licha ya kutokuwa na wazazi.Nadhani sintafanya jambo jema kama nikiweka hasira mbele na kumuacha mzee yule ateseke kitandani bila ya msaada.Team SC41 ni kama wamemtelekeza.Nitawasiliana na yule daktari rafiki yake afanye haraka kuja ili aweze kumfanyia upasuaji “ akawaza peniela akiwa garini kuelekea uwanja wa ndege

******

Saa nne za asubuhi,Mathew kwa kufuata maelekezo aliyopewa na peniela,aliwasili katika kituo cha kulelea watoto ambako ndiko Peniela alikolelewa toka akiwa mdogo..
“ Kituo kizuri sana.” Akawaza Mathew na kushuka garini akaeleka getini kulikokuwa na mlinzi aliyemuuliza shida yake.Mathew akaeleza shida yake kwamba ni kuonana na Bi Bernadetha mkuu wa kile kituo.Mlinzi yule akamfahamisha kwamba kwa wakati huo Bernadetha alikuwa mgonjwa na alikuwa amelala ndani na hatakiwi kusumbuliwa.Mathew akasisitiza kwamba ana jambo la muhimu sana lililompeleka pale.Mlinzi yule bado aligoma kabisa kumruhusu Mathew kuingia hadi alipokabidhiwa noyto mbili za elfu kumi kumi .Huku akitabasamu akamuomba Mathew amsubiri pele pale getini akaingia ndani na baada ya kama dakika tano akatoka na kumruhusu Mathew aingie ndani.
Nyumba ya bi Bernadetha ilikuwa pembeni ya bweni la ghorofa la watoto yatima anaowatunza.Alikaribishwa sebuleni na msichana mmoja , akapatiwa kinywaji na baada ya kama dakika kumi hivi Bi Bernadetha akatokea.kwa kumuangalia tu ungetambua kwamba alikuwa anaumwa kwa namna alivyokuwa amedhoofika.likuwa akitembea taratibu na kwa msaada wa fimbo
“ karibu sana kijana “ akasema Bi bernadetha kwa sauti ya chini
“ Ahsante sana bibi.Shikamoo” akasema Mathew
“ marahaba mwanangu”akajibu yule bibi
“ Pole sana bibi unaendeleaje? Akauliza Mathew
“ Hivyo hivyo mwanangu,Mungu ananisaidia.Magonjwa yananiandama.Ninasumbuliwa na kisukari,shinikizo la damu, mara miguu inavimba yaani ni mateso kila kukicha.Huu uzee nao unachangia sana kuumwa umwa.” Akasema bibi Bernadetha.
“ Pole sana bibi Mungu atakusaidia na utapona tu”
“ nashukuru kijana wangu.Nimeambiwa una shida na unahitaji kuniona”
“ ndiyo bibi nimekuja kwako nina shida kidogo na samahani sana kwa kukusumbua.Mimi ninaitwa Mathew na jambo kubwa lililonileta hapa ni kutaka kupata taarifa kuhusu msichana mmoja aliyewahi kulelewa hapa anaitwa Peniela.” Akasema Mathew na mara tu bi Bernadetha alipolisikia jina Peniela akastuka kidogo
“Peniela!..”
“Ndiyo bibi”
“ Ni mwanangu huyu na muda mrefu sijamuona wala hajafika kunijulia hali yule mtoto.Yuko wapi ? Yuko salama? Anaendeleaje na maisha yake? Akauliza bi Bernadetha
“ Peniela ni mzima ila sina hakika kama anafahamu kuhusiana na ugonjwa wako.Nina imani angekwishakuja kukutazama.Mara ya wisho umeonana naye lini? Akaliza Mathew.Bi Bernadetha akakaa kimya kidogo akazama katika kumbu kumu zake na kusema
“ Ni zaidi ya mwaka mmoja uliopita.” Akasema
“ Kuna tatizo lilimpata Peniela na ndiyo maana alishindwa hata kuja kukutazama.” Akasema Mathew
“ Alipatwa na tatizo gani? Akauliza Bi Bernadetha kwa wasi wasi
“ Kuna matatizo yalimpata akawekwa kizuizini lakini kwa sasa matatizo hayo yamekwisha na yuko huru.” Akasema Mathew
“ masikini Peniela ndiyo maana sijamuona akija kunisalimu.Nilishangaa sana kwani haikuwa kawaida yake kupitisha mwezi mmoja bila kuja kunitembelea.Wewe ni nani wake? mume wake? Akauliza Bi Bernadetha na Mathew akacheka kidogo
“Hapana bibi.Mimi si mume wake.Peniela bado hajaolewa”
“ anasubiri nini huyu binti? Nimekuwa nikimsisitiza kwamba aolewe bado mapema ili niweze kuwaona wajukuu zangu lakini sijui kwa nini mpaka leo hii hataki kabisa kuolewa”akasema Bi Bernadetha na kimya kifupi kikapita Mathew akasema
“ Bibi nimekuja hapa kutaka kufahamu kuhusiana na historia ya Peniela.Alifikaje hapa? Ana ndugu zake ? Wewe ni mtu pekee ambaye anamfahamu vizur Peniela na historia yake na ndiyo maana nimekuja kwako kutafuta taarifa hizo.” akasema Mathew.Bi Bernadetha akaonyesha wasi wasi kidogo na kuuliza
“ Kwa niniunataka kufahamu kuhusu historia ya peniela? Kuna tatizo gani limetokea?
Mathew akamtazama yule bibi kwa makini na kuamua kumdanganya
“ Bibi nadhani itakuwa vizuri kama niikuwekawazi ili uweze kunielewa .Mimi ni mchumba wa Peniela na kama ikimpendeza Mungu tunaweza tukafunga ndoa.Kabla hatujafunga ndoa nahitaji kumfahamu mwenzangu vizuri,asili yake ametoka wapi,ndugu zake ni nani n.k.Alinieleza kwamba yeye ni yatima na amekulia hapa na ndiyo maana nimekuja hapa bila ya yeye kufahamu ili noweze kulithibitisha hilo na kumfahamu vizuri mwenzangu ikiwemo na tabia zake kwani wewe ndiye uliyemkuza.” akadanganya Mathew.Bi bernadetha akatabasamu kidogo baada ya kusikia uongo ule wa Mathew
“ Ouh kumbe wewe ndiye mchumba wa Peniela.Ungejitambulisha toka mwanzo baba.Nimefurahi sana kukujua mwanangu.Karibu sana.Mimi ndiye niliyemlea peniela toka akiwa mdogo kabisa.Ninampenda sana peniela kama mtoto wangu wa kumzaa mwenyewe.” Akasema bi bernadetha na kukaa kimya kidogo.Mathew alikuwa makini akimsikiliza bibi yule aliyekuwa akiongea kwa sauti ndogo.Bi Bernadetha akaendelea
“ Peniela aliletwa hapa akiwa mdogo sana na mtu mmoja aitwaye John Mwaulaya.Huu ndiye baba yake mzazi Peniela” akasema Bi Bernadetha na kumstua sana Mathew ingawa hakutaka kuonyesha mstuko ule mbele ya yule bibi
“ John alisema kwamba alimchukua Peniela kutoka kwa mama yake ambaye alikuwa na tabia za kukesha baa na kufanya ukahaba huku akimuacha mtoto nyumbani akiteseka nahivyo alimua kumchukua na kumleta hapa ili nimlee.Alinitaka nimlee kwa siri bila ya mtu kufahamu.John aliniambia kwamba hataki peniela afahamu kama yeye ni baba yake.Ninamsifu John kwani alijitahidi sana kutoa ushirikiano na misaada mingi katika kumlea peniela.Misaada toka kwa John mwaulaya ilikuwa ikimiminika kila leo na ndiye aliyejenga hilo bweni la ghorofa unaloliona hapo nje.Nilimfahamisha Peniela kwamba vile vitu vyote alivyokuwa akivipata vilitoka kwa mfadhili aliyejitolea kumsaidia .Alitamani sana kumfahamu mfadhili huyo ni nani lakini hadi anamaliza darasa la saba hakuwa ameonana na mfadhili wake ambaye ni baba yake mzazi.” Bernadetha akanyamaza kidogo na baada ya muda akaendelea
“Peniela alipomaliza darasa la saba John alimzawadia jumba kubwa la kifahari na hapo ndipo peniela akahama nyumbani kwangu na kuanza rasmi maisha yake.Pamoja na kuwa na maisha yake lakini bado tuliendela kuwa karibu.Nilikuwa namtembela mara kwa mara kuhakikisha anaendelea vizuri.Alifanikiwa kumaliza kidato cha sita na akafaulu vizuri sana na baadae akanitaarifu kwamba anaelekea marekani kwa masomo ya chuo kikuu.Alipomaliza masomo yake alirejea nchini na tuliendelea kuwasiliana na kutembeleana kama kawaida lakini ghafla akapotea na sikumuona tena na nikadhani labda amekwenda kuendelea na masomo zaidi.Sikupata nafasi ya kutafuta taarifa zake kwani na mimi nilianza kusumbuliwa na magonjwa .Nimestuka sana uliponiambia kwamba alikuwa amefungwa gerezani” akasema Bi Bernadetha
“ Bibi,Peniela sasa yuko huru na mambo yake yamekwisha malizika.”
“ Ouh ahsante sana Mungu kwa kumjalia mtoto Yule amekuwa huru tena.Alifanya kosa gani hadi akawekwa kizuizini? Akauliza Bi Bernadetha
“ Alisingiziwa kesi “ akajibu Mathew kwa ufupi halafu kukawa kimya tena
“ Bibi huyo John aliwahi kukueleza aliko mama yake Peniela ?
“ John hHajawahi kunieleza mahala aliko mama yake Peniela.Alichowahi kunieleza ni kwamba mama yake Peniela alikuwa na tabia mbaya na alikuwa akifanya biashara ya ukahaba na ndiyo maana aliamua kumchukua mtoto na kumleta hapa na hakutaka kabisa Peniela amfahamu mama yake “
“ Kwa nini John alikataa usimweleze Peniela kama yeye ni baba yake?
“ Sifahamu ni kwa nini alifanya vile.Kila nilipomuuliza hakutaka kunipa jibu na alisisitiza nimwele peniela kwamba yeye ni mfadhili wake.Sina hakika kama mpaka sasa Peniela amefaikiwa kuonana na John kwani alikuwa akikwepa mno kuonana naye.” akasema Bi Bernadetha.Mathew akainama akafikiri halafu akasema
“ Bibi nakushukuru sana kwa kunikaribisha na kunipa maelezo mazuri.Nimefurahi sana kwa maelezo uliyonieleza.Nakuahidi nitarejea tena hapa kwako siku si nyingi kujua maendeleo yako na nitamfahamisha peniela kuhusu ugonjwa wako ” Akasema Mathew
“ Ahnte sana kijana wangu lakini kuna jambonataka nikuweke wazi.Nimekueleza jambo hili lakini tafadhali sana naomba usimweleze Peniela kwani ndiyo yalikuwa makubaliano yangu na John na sikuwahi hata mara moja kuyavunja kwa kumueleza Peniela kwa hiyo naomba na wewe usithubutu kumweleza chochote.Iko siku John mwenyewe atamueleza “ akasema Bi Bernadetha
“ Nimekuelewa bibi na sintafanya hivyo.Nitakachofanya nitamueleza tu kwamba nimekuja kukutembelea na kukuta unaumwa na nitamsisitiza kwamba aje akutembelee.” akasema Mathew kisha akamuaga Bi Bernadetha na kuondoka
“ John Mwaulaya ni baba yake Peniela??..akajiuliza Mathew akiwa garini
“ Hapana hainiingii kabisa akilini eti John Mwaulaya awe ni baba yake Peniela halafuakatae mwanae kumfahamu.Hili ni jambolisilowezekana.Kama kweli ni baba yakena hakutaka peniela afhamu na badala yake akatambulishwa kwake kama mfadhili basi kuna kitu alikuwa anakificha na ambacho lazima nikifahamu.Amakweli dunia imekuwa ndogo sana.Hatimaye mimi na John mwaulaya tunakwenda kukutana tena uso kwa uso.This time I’ll be the one making him talk.” Akawaza Mathew

TUKUTANE SEHEMU IJAYO
 
SEASON 2

SEHEMU YA 37

“ Ahsante sana kijana wangu lakini kuna jambonataka nikuweke wazi.Nimekueleza jambo hili lakini tafadhali sana naomba usimweleze Peniela kwani ndiyo yalikuwa makubaliano yangu na John na sikuwahi hata mara moja kuyavunja kwa kumueleza Peniela kwa hiyo naomba na wewe usithubutu kumweleza chochote.Iko siku John mwenyewe atamueleza “ akasema Bi Bernadetha

“ Nimekuelewa bibi na sintafanya hivyo.Nitakachofanya nitamueleza tu kwamba nimekuja kukutembelea na kukuta unaumwa na nitamsisitiza kwamba aje akutembelee.” akasema Mathew kisha akamuaga Bi Bernadetha na kuondoka

“ John Mwaulaya ni baba yake Peniela??..akajiuliza Mathew akiwa garini
“ Hapana hainiingii kabisa akilini eti John Mwaulaya awe ni baba yake Peniela halafuakatae mwanae kumfahamu.Hili ni jambolisilowezekana.Kama kweli ni baba yakena hakutaka peniela afhamu na badala yake akatambulishwa kwake kama mfadhili basi kuna kitu alikuwa anakificha na ambacho lazima nikifahamu.Amakweli dunia imekuwa ndogo sana.Hatimaye mimi na John mwaulaya tunakwenda kukutana tena uso kwa uso.This time I’ll be the one making him talk.” Akawaza Mathew



ENDELEA…………………

Abiria waliokuja na ndege ya shirika la ndege la Emirates walianza kutoka nje ya uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere.Peniela akiwa ameongozana na Jacob na Francis tayari walikuwapo hapo uwanjani wakiwasubiri wageni wao waliofika na ndege hii.Mikononi mwao kila mmoja alikuwa na picha mbili za wageni wanaowasubiri kwani hawakuwahi kukutana nao hata mara moja.Ni Peniela aliyekuwa wa kwanza kumtambua mmoja wa wageni wale waliokuwa wakiwasubiri.Nickson Strawberry alitambulika kwa urahisi kutokana na mtindo wake wa nywele .Alikuwa na nywele ndefu alizozikusanya kwa nyuma na kuzifunga.

“ That’s Nickson “ akasema Peniela na kumuita Nickson akasimama akageuka na kutmazama Peniela, akamfuata.

“ hallow Nickson.karibu sana Tanzania” akasema Peniela

“ Ahsante sana.” Akajibu Nickson

“ Naitwa Peniela na hawa ni wenzagu Jacob na Francis” Peniela akafanya utambulisho mfupi
“ Peniela !.akashangaa Nickson
“ wewe ndiye Peniela?! Akasema Nickson na kumkumbatia Peniela kwa furaha
“ Nimefurahi sana kuonana nawe Peniela” akasema Nickson kisha akawaita wenzake akawatambulisha.Alikuwepo Joe Levernsky mmarekani mweusi ,alikuwepo pia Bill beherds,Stanley Phoenix,Alexander Piscat na Edwin Washington.Kisha salimiana wakaelekea katika maegesho wakaingia katika magari mawili waliyokuja nayo akina Peniela na kuondoka
“ Nilitegemea kumuona Osmund hapa uwanjani.Yuko wapi?akauliza Nickson aliyekuwa amekaa kiti cha mbele pembeni ya Peniela

“ Osmund? Peniela akashangaa

“ Ndiyo” akajibu Nickson

“ Ina manaa hamna taarifa? Peniela naye akashangaa

“ taarifa gani penela?

“ Kuhusiana na Osmund”
“ Hatuna taarifa zozote kuhusiana na osmund.Tulipopanga safari hii yeye ndiye tuliyekuwa tukiwasiliana naye kwani ndiye aliyekuwa akiongoza team SC41 badala ya John lakini kwa siku kama tatu hivi hapatikani simuni hivyo ikatulazimu kwenda nje ya taratibu za team Sc41 na kuwataarifu vijana ofisi kuu dare s salaam kuhusu ujio wetu.Mara nyingi safari kama hizi hufanyika kwa siri.Yuko wapi Osmund? akauliza Nickson

“ Nini kinaendelea katika Team SC41? Kama tukio linaweza likatokea huku Tanzania na ninyi makao makuu msilifahamu basi ni hatari sana.Inaonekana wazi kwamba hakuna mawasiliano kati ya ofisi ya Dar es salaam na ofisi kuu Marekani.Ninaamini Team SC41 Tanzania ina watu wengi ambao wangeweza kuwapa taarifa.Kwa nini washindwe kutuma taarifa za matukio yanayotokea huku ? akauliza Peniela
“ Unayosema Penielani ya kweli kabisa.Toka John mwaulaya alipoanza kuumwa kumekuwa na tatizo katika ofisi ya Dar es salaam.Alimteua Osmund lakini bado hali ilikuwa ile ile.lakini usijali tumekuja kuweka mambo sawa na kila kitu kitakwenda vizuri sana.Kuna taarifa gani ya kuhusiana naOsmund? Akauliza Nckson.Peniela aliyekuwa akiendesha akapunguza mwendo na kusimama katika foleni kisha akasema
“ Osmund amefariki dunia”

“ Osmund amefariki dunia? Lini ?Akashangaa Nickson

“ Ndiyo tena si Osmund pekee bali na Dr Burke ambaye alitumwa kuja kufuatilia hali ya ugonjwa wa John .” akawema Peniela na kumstua sana Nickson ,aliyebaki anamtazama Peniela hadi pale gari zilipoanza kusogea

“ Peniela taarifa hizi ni ngeni kabisa kwetu.Hatukuwa tukifahamu chochote kilichotokea.Hapa ndipo unapokuja ukweli kwamba John mwaulaya alikuwa na nafasi kubwa sana katika team SC41.Kabla hajaumwa mambo kama haya hayakuwepo kabisa.Hakuna mtu yeyote aliyekamatwa hadi hivi sasa kuhusiana na mauaji hayo? Akauliza Nickson

“ Hapana.hakuna aliyekamtwa hadi hivi sasa “ akajibu Peniela.Nickson akainama akafikiri halafu akainua kichwa na kusema

“ Peniela kuna tatizo kubwa Team Sc41 Tanzania.Kuna kitu kinachoendelea hapa kwa sababu haiwezekani watu wawili wote team SC41 wauawe kwa wakati mmoja.Lazima tulifanyie uchunguzi suala hili ili tufahamu ukweli.Ninahisi kuna kitu hakiko sawa ndani ya team SC41 na hii ni hatari sana” akasema Nickson

“ Unahisi Dr Burke na Osmund waliuawa na mtu toka ndani ya team SC41? Akauliza Peniela

“ Sina hakika bado kama ni mtu toka ndani ya team SC41 lakini mazingira ya vifo hivyo yanatia shaka sana kwani inaonekana wazi waliuawa na mtu aliyekuwa na sababu Fulani.Lakini tutafahamu kila kitu baada ya kufanya uchunguzi wa kina.” Akasema Nickson
“ Ninajiuliza endapo tusingekuja,tusingetaarifiwa kuhusu kifo cha Osmund na Dr Burke? Huu ni udhaifu mkubwa sana umeonekana katika Team Sc41.Kuna kazi kubwa inatakiwa kufanyika kuisuka upya team SC41. Ahsante sana Peniela kwa taarifa hizi.kazi yetu itakuwa kubwa sana tofauti na nilivyokuwa nikitazamia.Team SC41 tanzania inatakiwa isukwe upya ili iwe imara kama ilivyokuwa mwanzo.Tukiachana na hayo vipi hali ya John mwaulaya? Akauliza Nickson

“ hali ya John si nzuri hata kidogo.kwa siku kadhaa hapo kati kati hali yake ilikuwa nzuri na wote tukawa na matumaini kwamba muda si mrefu atapona lakini ghafla hali yake ilibadilika na mpaka leo bado si nzuri.Anahitaji matibabu makubwa,kuna rafiki zake madaktari wanaweza wakaingia muda wowote kwa ajili ya kuja kumfanyia upasuaji” akasema Peniela
“ hakuna haja tena ya hao madaktari.Tumekuja na madaktari bingwa wawili kwa ajili tu ya kuja kuangalia ukubwa wa tatizo la John na kumpatia tiba.John anatakiwa kupatiwa tiba toka kwa madaktari wanaotambuliwa na Team SC41 .Usijali atapona tu” akasema Nickson na safari ikaendelea kimya kimya
“watuhawa wanataka kuisuka upya Team SC41 ili iwe na nguvu kama zamani Wakati nikiwa katika mikakati ya kuisambaratisha.Nimekwisha azimia kulifanya hilo na lazima nihakikishe linafanikiwa.Halafu kuna kitu nimekikumbuka kuhusiana na mauaji ya Dr Burke na Osmund.Nina hakika kabisa John alihusika katika vifo vya Dr Burke na osmund.Hawa jamaa wakifanya uchunguzi wao na kugundua kwamba John alishiriki sijui watafanya nini,nahisi wanaweza hata wakamuua.” Akawaza peniela huku safari ikiendelea.
Josh alimtaarifu kwamba kila kitu kuhusiana na mahala pakufikia wageni wale kilikuwa kimekamilika,Peniela akawapeleka kwanza hotelini kila mmoja akapata chumba chake halafu wakaondoka tena kuelekea nyumbani kwa John Mwaulaya ambako walipokelewa na Josh na moja kwa moja wakapelekwa chumbani kwa John mwaulaya ambaye alifurahi kuonana tena na watu wale baada ya muda mrefu.Kisha salimiana wote wakatoka na kuelekea katika sebule ya John Mwaulaya kwa ajili ya maongezi.Nickson ndiye aliyeongoza kikao kile kifupi

“ Peniela ,Josh,Jacob na Francis,kwa niaba ya wenzangu wote napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana kwa mapokezi yenu mazuri.Sina haja ya kurudia kujitambulisha tena kwani tayari sote mnatufahamu kwa hiyo basi nitakwenda moja kwa moja katika mambo makuu yaliyotuleta hapa.’ Akasema Nickson
“ jambo kubwa la kwanza lililotuleta hapa ni kuhusiana na operesheni 26B.Hii ni operesheni muhimu sana kwetu kwa hiyo tmelazimika kuja na kuifuatilia kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kwamba inakwenda kama inavyotakiwa na inakamilika.Tulimpa maelekezo Osmund kwamba ndani ya mwezi huu tunatakiwa tuwe tumeikamilisha operesheni hii na kuipata package hiyo muhimu sana kwa marekani na dunia kwa ujumla.Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari ni kwamba mawasiliano kati ya Dr joshua na wanunuzi wa package hiyo yamekwisha anza na muda wowote wanaweza wakafikia makubaliano.Tayari akaunti za benki zimekwisha funguliwa ambako wanunuzi hao wanatakiwa kuweka kiasi kikubwa sana cha fedha na kisha watakabidhiwa mzigo wao.Kwa gharama zozote zile hatutaki jambo hili litokee kwa hiyo lazima tuhakikishe tunaipata hiyo package.kwa hiyo nahitaji kusikia toka kwenu mmefikia wapi hadi hivi sasa? Akauliza Nickson

“ Nadhani peniela anaweza akajibu vizuri zaidi swali lako kwani yeye ndiye kiongozi mkuu katika operesheni 26B” akasema Josh
“ Ni kweli kama alivyosema Josh.Mimi ndiye niliyekabidhiwa jukumu la kuhakikisha kwamba tunaipata pachage hiy😵peresheni hii ilisimama kwa muda wa kama mwaka mmoja hivi baada ya mimi kuingia matatizoni lakini baada ya matatizo kumalizika operesheni imeendelea tena na ninapenda kukuthibitishia kwamba tumepiga hatua kubwa tayari.Ili kujiweka katika hatua nzuri ya kuipata package hiyo tayari nimejenga uhusiano wa kimapenzi na rais Dr Joshua pamoja na katibu wake .Vilevile tunaye captain Amos.Huyu ni mshirika mkubwa wa rais katika bashara hii na yeye ndiye ambaye ananipa taarifa za kila kinachoendelea kwa hiyo ushirikiano baina yetu ni mkubwa na tunachoshubiri kwa sasa ni siku ambayo package hiyo itatolewa ikulu kisha tuichukue.” Akasema peniela
“ Hongera sana peniela.Umefanya kazi kubwa na nzuri.Sisi tutakuwa nyuma yako kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda vizuri.Tutapata wasaa mzuri wa kujadili kwa upana kuhusiana na namna bora tunavyoweza kulikamilisha jambo hili hapo baadae.”akasema Nickson.

“ Nickson kuna jambo nataka kuuliza .Hiyo package ina nini ndani yake? Nimeyatoa mhanga maisha yangu kwa ajili ya kitu ambacho sikifahamu.Nadhani ni wakati mzuri sasa wa mimi kufahamu kitu ambacho nimekuwa nikihangaikia kwa muda huu mrefu ni kitu gani hasa.” Akauliza peniela
“ peniela wewe ni teamSC41 na ukiwa ndani ya kikundi hiki unakuwa ni kama askari mpambanaji,ukiambiwa fanya kitu Fulani basi unakifanya bila kuhoji.Sintaweza kukueleza kwa sasa kwani ni nje ya taratibu za team SC41.Una swali lingine?”akasema Nickson.Peniela akatingisha kichwa ishara kwamba hana tena swakli lingine lakini moyoni alikuwa amekasirika sana

“ Tuendelee.Jambo la pili lililotuleta hapa ni kuhusiana na afya ya John Mwaula.Kama mnavyofahamu ni kwamba John Mwaulaya hawezi kutibiwa katika hospitali za serikali wala haruhusiwi kuonekana nchini marekani kwa hiyo anatakiwa kutibiwa na madaktari walio ndani ya team SC41 pekee na ndiyo maana katika ujio huu tumeambatana na madaktari bingwa wawili wa mambo ya mishipa ya fahamu na kazi iliyowaleta hapa ni kumuhudumia John.”akasema Nickson

“ jambo la tatu ambalo tutalifanya tukiwa hapa ni kuhakikisha Team SC41 inasukwa upya na inarejea kuwa na nguvu kama zamani kabla John hajaanza kuumwa na jambo la mwisho kabisa tutahakikisha mwili wa Dr Burke unarejeshwa nyumbani kwa mazishi.Hayo ndiyo mambo ambayo tuyafanya katika kipindi ambacho tutakuwa hapa Dar es salaam.” Akasema Nickson.Sebule yote ilikuwa kimya.Nickson akaendelea

“ Nadhani mpaka hapo tumeelewana kwa hiyo kinachofuata sasa hivi sote tutaelekea kupata chakula cha mchana na baada ya hapo madaktari watarejea hapa kwa ajili ya kuanza kumfanyia John uchunguzi na wengine tutaelekea katika ofisi kuu ya team SC41 Tanzania tutasalimiana na watu wote pale na shughuli itaanzia hapo.Tukisha pata chakula cha mchana madaktari watarejea hapa ili waendelee kumfanyia uchunguzi John wakati sisi tukiendelea na kazi nyingine.Ninachoomba toka kwenu ni ushirikiano wenu mkubwa kwani bila ninyi hakuna tutakachoweza kukifanikisha.Kipindi hiki kifupi tutafanya kazi usiku na mchana hadi tuhakikishe kwamba tumefanikisha mambo yote.” Akasema Nickson

“ Nickson ninashukuru sana kwa ujio wenu huu ambao utakuwa na faida sana kwetu sote na team SC41.Ninashukuru sana kwa kuwaleta madaktari kwa ajili ya kuangalia afya ya John.Kwa kuwa jioni ya leo tutakuwa pia na kikao kikubwa kujadili kwa upana kuhusu mambo haya yote hususan operesheni 26B basi kwa mchana huu sintaweza kupambatana nanyi kuna jambo la muhimu na kwenda kulishughulikia ambalo linahusiana pia na operesheni yetu.Jacob na Francis watawapeleka katika ofisi kuu na mtakutana na watu wengine wote huko” akasema Peniela.
“ sawa peniela hakuna tatizo.Tutaonana jioni ya leo” akasema Nickson kisha wakaagana na kuondoka na kuwaacha Josh na peniela
“ Kazi imeanza.Wiki hii itakuwa ni wiki ngumu sana kwa Team SC41.Mambo mengi yatafanyika ndani ya wiki hii” akasema Josh,Peniela akamtazama kwa makini na kusema
“ Josh kuna kitu nataka kukuuliza na tafadhali naomba unipe jibu la kweli” akasema Peniela

“ Uliza chochote Peniela nakuahidi nitakueleza ukweli” akasema Josh.Peniela akamtazama na kuuliza
“ nani alimuua Dr Burke na Osmund?
Swali lile likamstua sana Josh.Alibabaika akasindwa ajibu nini

“ Naomba unijibu Josh.Nani alimuua Osmund na Dr Burke? Uko karibu sana na John muda wote na John hakuwa akimtaka kabisa Dr Burke aje na nina hakika ni yeye ndiye aliyetoa amri Dr Burke auawe .Kwa kuwa yeye hawezi kuifanya kazi hiyo lazima alimtuma mtu toka ndani ya team SC41.Niambie nani alifanya mauaji yale? Nina hakika unafahamu.” akasema Peniela.
“ Kwani kuna nini Peniela? Dr Burke na Osmund wamekwisha fariki na suala hili liko mikononi mwa polisi wakilifanyia uchunguzi”

“ Unawaona watu hawa waliokuja? Tayari wamehisi kwamba kuna mtu ndani ya Team SC41 ndiye aliyefanya mauaji yale na wanaanza uchunguzi wao mara moja na nina hakika lazima watampata na wakimjua nadhani unafahamu kitu watakachomfanyia.Josh kama unamfahamu mtu aliyefanya mauaji yale tafadhali nieleze” akasema Peniela.Sura ya Josh ilibadilika na alionekana kuogopa sana..
“ Peniela its me” akasema Josh.Peniela akamuangalia kwa mshangao mkubwa.

“ katika watu wote sikutegemea kama ni wewe ambaye unaweza ukafanya kitendo hiki” akasema peniela

“ Peniela nilifanya kwa kuwa John aliniomba nifanye.Siku zote nimekuwa mtiifu kwa John na hata aliponituma nikaifanye kazi hii sikusita kufanya hivyo.John alidai kwamba Dr Burke alikuwa na lengo la kumuua na tulitakiwa kumuwahi.Kama tusingemuwahi Burke basi angemuua John.Tafadhali Peniela kama kuna lolote unaloweza kunisaidia katika hili naomba unisaidie” akasema Josh.Peniela akainama akafikiri kidogo na kusema
“ Kwa kuwa ni John ndiye aliyekutuma nitakusaidia,tutatafuta namna ya kuweza kulitatua jambo hili.” Akasema Peniela.


*****


“Lazima leo nionane uso kwa uso na John mwaulaya.Lazima ukweli kuhusiana na Peniela ujulikane leo.Jason anapafahamu nyumbani kwa John kwani ndiko alipelekwa siku aliyotekwa”akawaza Mathew baaad ya kutoka katika kituo cha kulele watoto yatima alikolelewa Peniela.Akachukua simu akampigia Jason.
“ habari za asubuhi Jason” akasema Mathew baada ya Jason kupokea simu
“ habari nzuri sana Mathew.Habari za toka jana? Akauliza Jason

“ habari nzuri Jason.Uko wapi mida hii?
“ kwa sasa niko ofisini kwangu.”

“ Jason nahitaji kuonana nawe.Nielekeze mahala ofisi yako ilipo ili nikufuate hapo” akasema Mathew na Jason akamuelekeza mahala iliko ofisi yake .

“Kwa mara ya kwanza bada ya miaka mingi hatimaye nakwenda kukutana ana kwa ana na John Mwaulaya mtu ambaye aliiteketeza familia yangu.Kwa leo sintamfanya lolote kwani ninakwenda kwa ajili ya suala la Peniela lakini safari nyingine nitamfuata rasmi kwa ajili yangu na ninahisi huo utakuwa ndio mwisho wake.Kwa kumpa salamu tu,leo lazima aeleze ukweli wote kuhusiana na Peniela.Wakati ule John ndiye aliyekuwa na nguvu na kunifanya hadi nikaikimbia nchi yangu lakini safari hii mambo yamebadilika na mimi ndiye mwenye nguvu kuliko yeye.He will talk “ akawaza Mathew na mara simu yake ikaita.Alikuwa ni rafiki yake wa kutoka nchini Israel ambaye alimtumia zile karatasi zilizoibwa ikulu zilizokuwa zimeandikwa fomula za kisayansi
“ hallow Yash “ akasema Mathew

“ Mathew habari za Dar es salaam?
“ habari za huku nzuri sana .habari za huko?
“ Hata huku kwema tu” akajibu yash
“ Mathew tayari nimeikamilisha ile kazi uliyoniomba nikusaidie.Samahani imechukua muda kidogo lakini ilinilazimu kukutana na wanasayansi wakubwa ili kuweza kutambua kilichoandikwa katika zile karatasi.Nimekutumia kila kitu katika anuani yako ya barua pepe utasoma na kuelewa kila kitu”akasema Yash
“ Ahsante sana yash kwa msaada wako mkubwa.” Akajibu Mathew

“ Mathew karatasi zile umezitoa wapi? Akauliza Yash

“ Kuna jambo nalichunguza kwa sasa na ndani ya uchunguzi huo nikazipata karatasi hizo.Kwa nini umeuliza hivyo Yash?
“ nimeuliza hivyo kwa sababu ya ukubwa wa kitu kilichoandikwa ndani ya zile karatasi.Kama ni kitu hicho kipo kweli basi ni kitu cha hatari kubwa sana lakini kama hakipo basi karatasi hizo ni za kutunza sana kwani ni hatari mno na sijui zimefikaje huko.”
“ unaweza ukanipa japo kwa ufupi ni kitu gani hicho ? Akauliza Mathew

“ Nimekufafanulia kila kitu katika barua pepe niliyokutumia.” Akasema Yash
“ Ahsante sana Yash”

“ Mathew ,nitakupigia tena simu jioni ili tuongee vizuri zaidi” akasema Yash na kukata simu

“ Nini kimeandikwa katika zile karatasi kiasi hata cha kumstua Yash ? Lazima kitakuwa ni kitu kikubwa na kizito na ndiyo maana akina Edson walitaka kuziuza kwa mabilioni ya pesa” Akawaza Mathew akiwa njiani kuelekea ofisini kwa Jason
Aliwasili katika ofisi za Jason wakasalimiana na bila kupoteza wakati Mathew akauliza

“ Jason unaweza kupakumbuka nyumbani kwa John Mwaulaya ulikopelekwa siku ile”

“ Ndiyo ninapakumbuka.” Akajibu Jason

“ Ninaomba unipeleke” akasema Mathew
“unataka kwenda nyumbani kwa John mwaulaya? Jason akashangaa
“ Ndiyo nataka kwenda kuonana na John Mwaulaya.Kuna mambo ambayo anatakiwa kuyaweka wazi kuhusiana na Peniela”
“ mambo gani hayo Mathew? John ni mgonjwa unadhani anaweza akakueleza chochote kwa hali aliyonayo ? akauliza Jason
“ He will talk.Take me there” akasema Mathew.Jason huku akiwa na wasi wasi akavaa koti lake na kutoka wakaingia katika gari la Mathew na kuondoka kuelekea nyumbani kwa John Mwaulaya.Safari ilitawaliwa na maongezi machache sana hadi walipofika katika jumba la John mwaulaya.

“ Hapa ndipo nyumbani kwa John mwaulaya” akasema Jason
“ Wow ! jumba kubwa na la kifahari.Hawa watu ni kweli wanalipwa pesa nyingi sana kama alivyosema peniela.” Akasema Mathew na kisha akasimamisha gari katika geti .

“ Shuka kabonyeze kengele “ akasema Mathew.Jason akashuka na kwenda getini akabonyeza kengele mara tatu halafu akasuburi.Baada ya dakika tano mlango wa geti ukafunguliwa .Aliyeufungua alikuwa ni Josh ambaye alipatwa na mstuko mkubwa alipoonana uso kwa uso na Jason.Kwa sekunde kadhaa walibaki wanatazamana.
“ Jason !!..akasema Josh
“ What brings you here? Akauliza Josh.Jason akafumbua mdomo kutaka kusema kitu lakini akasita baada ya kusikia mlango wa gari unafunguliwa hakujibu kitu akageuka baada ya kusikia mlango wa gari ukifunguliwa,akashuka Mathew.Josh alimtazama vizuri sana na kuikumbuka ile sura.Ni yule mtu aliyeonekana katika kamera za nyumbani kwa Peniela.Akaingiwa na woga

“ hallow “ akasema Mathew
“ Josh .Naitwa Josh “ akasema Josh na kumpa mkono Mathew

“ Josh naitwa Mathew” akasema Mathew
“ Karibuni sana.Niwasidie nini? akauliza Josh
“ Nahitaji kuonana na John Mwaulaya.”
“ John Mwaulaya? Nani kawaambia John anaishi hapa? Akauliza Josh
“ Josh naomba usinipotezee muda wangu.Utatupeleka kwa John mwaulaya au nitumie nguvu? Akasema Mathew huku akipeleka mkono mahala iliko bastora yake.Josh akaogopa akafungua geti Mathew akamwambia Jason aingize gari ndani .Jason akalitambua gari la Peniela lililokuwamo mle ndani.
“ Peniela yuko hapa? Akauliza Jason
“ Ndiyo yupo”akajibu Josh

“ Ok vizuri sana.Tupeleke aliko John” akasema Mathew na Josh akaanza kuwapandisha ghorofani kilipo chumba cha John mwaulaya.Ndani ya chumba cha John alikuwemo Peniela na Dr martin ambaye amekuwa akimuhudumia John mwaulaya kwa muda mrefu.Mlango ukafunguliwa akaingia Josh akiwa amefuatana na Mathew na Jason.Wote mle chumbani wakastuka sana.

“ Mathew ! Jason !..akasema peniela kwa mshangao na kumfanya John Mwaulaya ageuze shingo yake na kutazama mlangoni.
“ mungu wangu ! akasema John mwaulaya kwa sauti ndogo .Naye pia alikuwa ameogopa sana.Mathew akasogea hadi karibu na kitanda cha John Mwaulaya akamtazama kwa macho makali sana.Peniela akaogopa
“ John mwaulaya,hatimaye tumeonana tena uso kwa uso .” akasema Mathew
“ Mathew what are you doing here? Akauliza Peniela

“ peniela nimekuja kuonana na John Mwaulaya.Nimefurahi sana kukukuta na wewe hapa ili usikie kile ambacho ninataka John akieleze mbele yako”

“ Mathew ,John is sick and he cant talk” akasema Peniela kwa wasi wasi.

“ he will talk” akasema Mathew.

“ Mathew !!..what are you doing? Akasema peniela huku akipiga hatua kumuendea Mathew.Jason akamzuia.
“ John mwaulaya,japokuwa imepita mika ming lakini nina hakika sura hii bado unaikumbuka vizuri sana.kama umeisahau nitakuja siku nyingine kukukumbusha lakini kwa leo nimekuja kwa ajili ya jambo moja tu, Peniela.” Akasema Mathew na kumstua kidogo Peniela.John mwaulaya alikuwa anatetemeka.
“ Ulimpeleka Peniela usiku katika kituo cha kulelea watoto yatima na ukadai kwamba umemchukua toka kwa mama yake na ukataka alelewe pale.Ulimwambia mama mwenye kile kituo kwamba peniela ni mwanao lakini hukutaka afahamu kama wewe ni baba yake na badala yake ukajiita mfadhili wake.Umemfanyia Peniela mambo mengi mabaya na kuyaharibu kabisa maisha yake,umemuingiza katika Team SC41 na umezifuta kabisa ndoto za maisha yake na mmekuwa mkimtumia kwa kazi zenu kwa manufaa ya serikali ya marekani.Ninataka mbele ya Peniela uungame ukweli wewe ni baba yake mzazi? Akauliza Mathew kwa ukali.Peniela alipigwa na butwaa asiamini kile alichokisikia .Akamkazia macho John mwaulaya kusikia atatoa jibu gani.

“ John answer me!!..akafoka Mathew

“ Sifahamu chochote juu ya hayo unayoyasema” akasema John kwa sauti ndogo.

“ John nitazame vizuri machoni.Nina uhakika na ninachokisema na sina utani hata kidogo.” Akasema Mathew na kumuinamia John
“ John nitazame vizuri machoni.I’m a monster kwa hiyo naomba usiniudhi.Nataka useme ukweli kwamba wewe ni baba yake mzazi Peniela? Akasema kwa ukali Mathew

“ I don’t know anything” akajibu John kwa sauti ndogo .

“ John this is the last chance ..are you Peniela’s father? Akauliza Mathew kwa ukali.John akajibu kwa kumfanyia ishara kwamba haelewi chochote.Mathew akakasirika na kuchomoa bastora yake.Peniela akaogopa sana
“ Mathew what are yo doing? Akauliza lakini Mathew hakumjali

“ Mathew unataka kufanya nini? Akauliza Peniela kwa wasi wasi
“ I’ll count to three and if you cant answer me I’m going to kill you John ! akasema kwa ukali Mathew

“ Mathew No ! Don’t do that !! akasema Peniela huku akilia
“ Jason hold her” Mathew akamuamuru Jason amshike Peniela ili asimsogelee.

“ Three…..!!!akaanza kuhesabu Mathew huku amemuelekezea John bastora
“ Two ….!!!!
“ Mathew noo!!!!..dont do that !!..akapiga kelele peniela.
“ On………..” Kabla Mathew hajamaliza kutamka John Mwaulaya akasema
“ Ok ok..I’ll tell you..put your gun down” akasema John mwaulaya aliyekuwa akitetemeka
“ ok tell her the truth! akasema kwa ukali Mathew huku akimtazma John kwa macho ya hasira
John akamfanyia ishara peniela asogee karibu na kuanza kumsimulia kilichotokea kuhusiana na wazazi wake.Alisimulia mkasa mzima uliotokea na kupelekea kuwaua wazazi wote wa peniela.Peniela alibubujkwa na machozi mengi.John akamgeukia Mathew
“ Hiyo ndiyo historia ya Peniela.Nilishindwa kabisa namna ya kumueleza nikiogopa kumuumiza na ndiyo maana nilitaka afahamu kuhusu yeye baada ya mimi kufariki dunia.Nilijua lazima atanichukia sana akifahamu kwamba mimi ndiye niliyewaua wazazi wake.Nilimuwekea kila kitu kuhusiana na historia yake katika makasha matatu ikiwamo na picha za wazazi wake.” Akasema John.Peniela alimuangalia kwa hasira huu machozi yakimtoka.

“Leo nilikuja kwa ajili ya Peniela.Safari ijayo nitakuja rasmi kwa ajili yangu.Jiandae “ akasema Mathew na kutoka Peniela akamfuata

“ Mathew thank you so much.Umenisaidia nimefahamu jambo kubwa sana.Sikuwa nikifahamu chochote kuhusiana na wazazi wangu.John amenificha siri hii kwa miaka mingi.I hate that bastard so much.”akasema Peniela

“ Elibariki aliniomba nikusaidie kuufahamu ukweli kuhusiana na asili yako na ninashukuru ukweli umedhihiri.Naomba ukweli huu usivuruge mipango yetu.”

“hakuna kitakachovurugika Mathew.I’m a very strong woman.Kila kitu kitakwenda kama tulivyokipanga.hata hivyo nina swali nataka kukuuliza.”

“ Uliza Peniela”

“ Ulipomuelekezea John bastora na kuanza kuhesabu,ulidhamiria kumpiga risasi kama asingesema chochote ?
Mathew akatabamu kidogo na kusema

“ No ! I just wanted him to talk”

“ ahsante Mathew.Ahsante sana.Tutaonana jioni .Mwambie Elibariki nashukuru sana kwa kunijali.Bila yeye kuwa na mawazo haya nisingeufahamu ukweli kuhusu wazazi wangu“ akasema peniela na kurejea tena ndani akakuta hali ya John mwaulaya imebadilika ghafla.Ikawalazimu wawaite haraka wale madaktari wawili waliokuja toka marekani kwa lengo la kuja kuangalia afya yake.


MCHAKATO WA KUIPATA PACKAGE MUHIMU UMESHIKA KASI NA KILA UPANDE UNAJIANDAA KUIPATA NINI KITATOKEA ? FLAVIANA MKE WA JAJI ELIBARIKI BADO YUKO MAHUTUTI HOSPITALI NINI HATIMA YAKE? NINI HATIMA YA JOHN MWAULAYA? KIKUNDI KIDOGO CHA WATU WENYE NGUVU NA USHAWISHI KIKIONGOZWA NA RAIS MSTAAFU KINAPANGA KUMUONDOA MADARAKANI DR JOSHUA NA WANAFIKIRIA KUMPENDEKEZA JAJI ELIBARIKI KUWANIA NAFASI HIYO JE WATAFANIKIWA LENGO LAO ? MWISHO WA SIMULIZI YA PENIELA SEASON 2..TUKUTANE TENA KATIA SEASON 3 HIVI KARIBUNI
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…