PENIELA SEASON 3
EPISODE 3
MTUNZI : PATRICK .CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Hallow Mathew ,uko wapi? Akauliza Anitha baada ya kupokea simu
“ Tayari nimerejea nyumbani.Wewe uko wapi? Akauliza Mathew
“ Niko njiani ninarejea nyumbani.Nimetoka kuonana na Peniela na tayari nimemkabidhi vile vifaa na jioni ya leo atakapokutana na Dr Kigomba tutaanza kupata kila taarifa toka kwa Dr Kigomba.” Akasema Anitha
“ Good job Anitha.Ninakusubiri hapa nyumbani.Kuna suala zito linalotukabili”
“ Kuna jambo jipya ? akauliza Anitha kwa wasi wasi kidogo
“ Si jipya sana lakini ni mwendelezo wa kile ambacho tumekuwa tunaendelea nacho” akasema Mathew
“ Sawa Mathew .Niko njiani ninakuja sasa hivi” akajibu Anitha na kukata simu
ENDELEA…………………
Baada ya kuachana na Anitha ,Peniela hakutaka tena kwenda sehemu yoyote ile zaidi ya nyumbani kwake.Alihisi kichwa chake kizito sana hivyo alihitaji mapumziko.Mambo mengi yalikuwa yametokea ndani ya muda mfupi.
Alifika nyumbani kwake na moja kwa moja akaelekea chumbani ,akajitupa kitandani.Kichwa kilijaa mawazo mengi sana.Picha ya kile kilichotokea chumbani kwa John bado iliendelea kuzunguka kichwani kwake na kumjaza mawazo .Sauti ya John Mwaulaya akitamka namna alivyowatoa uhai wazazi wake bado iliendelea kupenya na kusikika masikioni mwake.Machozi yakamtoka
“ Nilijitahidi nisiseme chochote kwa wakati ule kwani sikutaka watu wagundue kwamba nimeumizwa na taarifa ile lakini ukweli katika maisha yangu sijawahi kuumizwa kama nilivyoumizwa leo na taarifa ile kuhusiana na wazazi wangu.John ni binadamu mwenye roho ya kishetani kabisa.Hana hata chembe ya utu ndani yake.He killed my parents !!..Sikupata hata nafasi ya kuonja upendo wa mama yangu kipenzi.!!..akawaza Peniela na kuangua kilio .Aliumizwa mno kwa kuufahamu ukweli kuhusiana na wazazi wake.
“ Kwa mujibu wa maelezo ya John ,baba yangu alikuwa ni mtu mwenye wadhifa mkubwa serikalini na kutokana na nafasi yake kubwa aliyokuwa nayo hakutaka kuwa na kashfa yoyote ya kumpa mimba mama yangu ambaye alidhamiria kwenda kumshtaki mahakamani kwa kitendo cha kumtelekeza yeye na mtoto yaani mimi.Kwa kuogopa kashfa hiyo ,baba akaamuru John akamuue mama pamoja na mimi.The first monster was my own father.He ordered me killed.Hakuwa na huruma hata kidogo na damu yake kupotea.Natamani niione sura ya binadamu huyu ambaye hakuwa na hata chembe ya huruma kwa mtoto wake mwenyewe ambaye yeye kwake wadhifa ni muhimu zaidi kuliko hata damu yake.” Akawaza Peniela na kuendelea kulia kwa uchungu mkubwa.
“ Kwa maelekezo ya baba,John alimuua mama yangu lakini kwa mara ya kwanza katika historia ya maisha yake,John akaingiwa na moyo wa huruma na akaenda kinyume na amri aliyopewa akaamua kuniacha hai,akanichukua na kunihudumia akahakikisha ninapata huduma zote na ninaishi maisha mazuri.Kwa hili ninamshukuru sana kwani bila yeye nisingeweza kufika umri huu. Kwa upande Fulani sipaswi kumchukia au kumlaumu sana John kwani alikuwa anatekeleza amri aliyopewa na baba yangu.Mtu pekee ambaye ninapaswa kumchukia hapa ni baba.How could he be so cruel?? Akajiuliza Peniela na kuendelea kulia .Alihisi mwili wote kumuisha nguvu.
“ Tayari nimekwisha fahamu historia yangu na nimelia vya kutosha.Nimemwaga machozi mengi kumlilia mama yangu ambaye aliuawa kwa sababu yangu.Aliuawa akiwa katika harakati za kunitetea mimi.Ninachotakiwa kukifanya kwa sasa baada ya kuufahamu ukweli ni kumfahamu vyema mama yangu.Kuifahamu familia yake,kuwafahamu ndugu zake na kujua kama alikuwa na mtoto au watoto wengine.Pamoja na unyama na ukatili wake lakini nitahitaji pia kumfahamu baba yangu pia ili nijue alikuwa ni mtu wa namna gani,vile vile nifahamu kama nina ndugu zangu wengine.” Akawaza Peniela na kuchukua kitambaa akajifuta machozi
“Siku ile nilipoonana na John kwa mara ya kwanza alinikabidhi kasha na akaniambai kwamba kama akifariki nihakikishe ninayakamilisha makasha matatu na baada ya kukamilika yote ndipo nitakapoweza kufahamu mimi ni nani.Ninahisi historia yangu yote iko ndani ya makasha hayo.Inavyoelekea katika makasha hayo kuna mambo makubwa na ya msingi sana.Nitahakikisha ninayapata yote.” Peniela akastuliwa toka mawazoni na mlio wa simu .Ilikuwa ni simu ile ambayo huitumia kuwasiliana na Dr Joshua.Akainuka na kwenda kuichukua akabonyeza kitufe cha kupokelea.
“ Hallow” akasema Peniela.Zikapita sekunde kadhaa bila kujibiwa,Peniela akapatwa na wasi wasi
“ Hallow Dr Joshua” akasema tena .Safari hii akasikia mtu akivuta pumzi ndefu na kusema
“ Hallow Peniela ,unaendeleaje malaika wangu? Sauti ile ya Dr Joshua ikamshangaza kidogo Peniela kwani haikuwa ile ambayo amezoea kuisikia.
“ Dr Joshua are you ok? Akauliza Peniela
“ I’m ok Peniela.Hofu yangu ni kwako tu.You sound so strange today na ndiyo maana ulipopokea simu nilisita kidogo kuongea.Have you been crying? Akauliza Dr Josha
“ No Dr Joshua.Nimerudi sasa hivi nyumbani and I’m very tired.Vipi maendeleo ya Flaviana?
“ Pole sana kwa uchovu lakini sauti yako inaonyesha wazi kwamba ulikuwa unalia.Any way kuhusu Flaviana tayari amesafirishwa leo kwenda afrika ya kusini kwa matibabu zaidi na kwa taarifa nilizozipata muda si mrefu tayari wamefika salama na tayari ameanza kushughulikiwa japo bado hali yake si nzuri.Tuzidi kumuombea” akasema Dr Joshua
“ Pole sana Dr Joshua.Tuzidi kumuombea na Mungu atamponya.By the way aren’t you suppose to be there with your family right now? Akauliza Peniela
“ Ni kweli Peniela,natakiwa nikaungane na familia yangu sasa hivi lakini kilichonifanya nisiambatane nao ni kikao kikubwa cha wakuu wa nchi za afrika mashariki. Lakini usiku wa leo nitaondoka kwenda kuungana na familia yangu afrika ya kusini.Natamani sana kama ningeonana nawe kabla sijaondoka.Hiki ni kipindi kigumu sana kwangu and I think I need some comfort and the only person who can comfort me is you Peniela.” Akasema dr Joshua
“ Dr Joshua pole sana .Nafahamu ni wakati gani ulio nao sasa hivi lakini nasikitika kwamba sintaweza kuonana nawe kwa leo kabla hujaondoka.Nitaonana nawe utakaporejea toka afrika ya kusini ila naomba ufahamu kwamba niko pamoja nawe katika kipndi hiki kigunmu sana kwa familia yako” akasema Peniela
“ Sawa nimekuelewa Peniela.Nitaonana nawe baada ya kurejea .Tuzidi kumuombea Flaviana ili Mungu amjaklia nafuu ya haraka.Kabla hatujaagana una tatizo lolote? Kama kuna chochote kinachokusumbua na kukuumiza kichwa tafadhali naomba usisite kunieleza.” Akasema Dr Joshua
“ Ahsante sana kwa kunijali Dr Joshua ila kwa sasa sina tatizo lolote isipokuwa ni Yule mjomba wangu niliyekueleza hali yake imezidi kuwa mbaya na tayari nimempeleka katika ile hospitali na wamekwisha anza kumshughulikia”
“ Pole sana Peniela.Pole sana malaika wangu.Ulipaswa kunitaarifu mapema walau na mimi nifike nimjulie hali. “Akasema Dr Joshua
“ Usijali Dr Joshua,huna haja ya kupoteza muda wako kwa kwenda hospitali.Una mambo mengi yanayokukabili kama mkuu wa nchi .Msaada mkubwa ulionipatia wa hospitali unatosha sana.”
“ Ouh Peniela my queen usiseme hivyo.Kukusaidia wewe ni jukumu langu.Thamani yangu kwako hailinganishwi na chochote kile kwa hiyo ninajiona ni mwenye bahati sana kuwa ni sehemu ya msaada kwako.Hata hivyo nitawasiliana na daktari mkuu wa hospitali ile ili walipe uzito unaostahili suala la ugonjwa wa mjomba wako” akasema Dr Joshua
“ Nashukuru sana kwa kunijali Dr Joshua.Nakutakia safari njema na tafadhali unijulishe maendeleo ya Flaviana mara utakapowasili afrika ya kusini.”
“ Nitakutaarifu Flaviana .Ubaki salama na ninaomba nikukumbushe kwamba ninakupenda kuliko kitu chochote” akasema Dr Joshua na kumalizia kwa busu kisha akakata simu.Peniela akaitupa simu kitandani
‘ Hili zee halina akili nzuri hata kidogo.Laiti lingenifahamu mimi ni nani lisingethubutu kuniita mimi malaika wake.Siku inakuja na atanitambua mimi ni nani” akawaza Peniela halafu akainuka na kuelekea bafuni.
“ Imekuwa ni siku mbaya na ngumu sana kwangu.Hata hivyo namshukuru sana Mathew kwa kunisaidia kuufahamu ukweli.Bila yeye katu nisingefahamu chochote kuhusiana na wazazi twangu.Natamani hali ya John ingekuwa nzuri ili anieleze kwa kina kuhusiana na wazazi wangu.Kuna mambo mengi ambayo nahitaji kuyafahamu kutoka kwake namuomba Mungu asimchukue mapema kwani yawezekana kuna mambo mengine mengi nisiyoyafahamu kuhusu mimi” akawaza Peniela na picha ya John ikamjia
“ Pamoja na yote aliyonifanyia lakini najikuta bado nikimuonea huruma sana Yule mzee.Nadhani ni kwa sababu ya wema wake mkubwa kwangu.Toka nikiwa mdogo alihakikisha ninapata matunzo na malezi mazuri .Hakuna kitu ambacho nimewahi kupungukiwa.Ni kwa sababu yake nimesoma vizuri,nimeishi maisha mazuri.Kuwa na hasira naye kwa sasa haitanisaidia chochote.John ni mtu ambaye nimekuwa nikitamani sana kumuona toka nikiwa mdogo lakini nimepata bahati ya kukutana naye katika kipindi kama hiki akiwa mgonjwa na hajiwezi,anahitaji msaada wangu.Anyway ngoja niyaweke pembeni mambo ya John na nielekeze akili yangu katika suala kubwa lililoko mbele yangu.Jioni ya leo nina miadi na Dr Kigomba.Huyu ni mtu muhimu sana ambaye atatusaidia katika kufanikisha operesheni yetu .Ninashukuru kwa sababu tayari naye amekwisha nasa katika himaya yangu na kwa sasa nina uhakika mkubwa kwamba operesheni yetu itakwenda vizuri.Nataka tulimalize suala hili na niachane kabisa na aina hii ya maisha .Nimekuwa nikitumika kwa muda mrefu na Team SC41 kama chombo chao cha kuwatafutia taarifa na katika hilo mwili wangu umekuwa ni kama bidhaa kwa kutumiwa na wanaume ili nipate taarifa muhimu.Sitaki kuendelea na aina hii ya maisha na kitu pekee kitakachonifanya nisiendelee kuishi maisha ya namna hii ni kujiondoa kutoka team Sc41 na kuimaliza kabisa.Najua ni kazi ngumu lakini lazima nipambane hadi nihakikishe nimefanikiwa kuimaliza team Sc41.” Akawaza Peniela halafu akatoka bafuni na kupanda kitandani kujipumzisha kabla ya kuonana na Dr Kigomba jioni ya siku hiyo
********
Bado zoezi la uchunguzi wa ugonjwa unaomsumbua John Mwaulaya liliendelea.Dr Edwin na Dr Alex waliendesha uchunguzi ule wakishirikiana na madaktari bingwa wengine watatu toka katika ile hospitali.Josh na Dr Martin Desmond walikaa katika sehemu ya kupumzikia wakisubiri kupewa taarifa ya matokeo ya uchunguzi pindi utakapokamilika.
Wakiendelea na maongezi ya kawaida,mara akatokea Dr Edwin na kumuita Josh wakaenda kusimama mahala kusikokuwa na watu
“ Dr Edwin nini kinaendelea? Uchunguzi umekamilika? Akauliza Josh kwa wasi wasi.
“ Josh ni mapema mno kusema chochote kwa sasa kwani uchunguzi bado haujakamilika.Tutakapokuwa tayari tutakutaarifuni.Kwa sasa nimekuita kwa jambo moja la muhimu” akasema Edwin na kunyamaza ,akatazama huku na huko na kuhakikisha hakuna anayesikia kile wanachokiongea kisha akasema
“ Hali ya John Mwaulaya ilibadilika ghafla baada ya sisi kuondoka pale nyumbani kwake na kwa mujibu wa Martin ni kwamba kuna watu wawili walifika chumbani kwa John na kuanza kumuhoji na kumsababishia mstuko mkubwa.Je ni kweli? Akauliza Dr Edwin.Josh akainama
“ Niambie ukweli Josh kwani tayari tunafahamu kila kitu.Nataka tu unithibitishie kwamba suala hili ni la kweli.” Akasema Dr Edwin
“ Ni kweli.Kuna watu wawili walikuja kuonana naye baada ya nyie kuondoka na hapo ndipo hali ya John ilipobadilika” akajibu Josh
“ Vizuri .Unawafahamu watu hao ni akina nani? Nimeambiwa wewe ndiye uliyekuwa mlinzi wa John kwa kipindi kirefu je uliwahi kuwaona watu hawa nyumbani kwa john hata mara moja? Ni watu ambao wamekuwa wakishirikiana na John? Akauliza Dr Edwin
“ Watu wale siwafahamu vizuri ila ninamfahamu mmoja wao anaitwa Jason.Huyu niliwahi kupewa maelekezo na John ya kumfanyia mahojiano ili kufahamu mambo kadhaa kutoka kwake .Huyu mwingine aitwaye Mathew leo ndiyo nimemuona lakini wote hawa ni marafiki wa Peniela.Nadhani endapo utamuuliza Peniela anaweza akakueleza vizuri zaidi kuhusiana na huyu Mathew”
“ Ahsante Josh.Ila kwa mujibu wa Martin ni kwamba huyu Mathew aliahidi kurejea tena kwa John.Inaonekana yeye na John ni watu wanaofahamiana na nina wasi wasi lazima kuna jambo ambalo sisi hatulifahamu kuhusiana na John na Mathew.Nina wasi wasi kwamba kama mtu huyu anamfahamu sana John basi anaweza akawa anaifahamu team Sc41.Nina hitaji kumfahamu mtu huyu.Pale nyumbani kwa John kuna kamera za ulinzi naomba unipatie picha zote zilizopigwa na kamera wakati wale jamaa wakiingia.Nahitaji sana kumfahamu huyu Mathew” akasema Dr Edwin
“ Usijali Dr Edwin.Ninakwenda kushughulikia suala hilo” akajibu Josh
“ Nashukuru sana Josh” akajibu Dr Edwin na kurejea ndani.
********
Anitha alirejea nyumbani na kusalimiana na jaji Elibariki aliyekuwa amekaa sebuleni akitazama filamu.Anitha alionekana kuchoka sana.
“ Pole sana Anitha.Unaonekana umechoka sana leo” akasema jaji Elibariki
“ Ni kweli ninahisi uchovu mwingi.Nahisi nahitaji mapumziko.Mathew yuko wapi?
“ Mathew naye amejipumzisha chumbani kwake.Vipi huko utokako mambo yanakwendaje?
“ Mambo yote yamekwenda vizuri kama tulivyopanga na tayari nimempatia Peniela vile vifaa kwa hiyo tutaanza kupokea taarifa jioni ya leo pindi atakapoonana na Dr KIgomba.Kila kit………” Anitha akakatisha maongezi baada ya kusikia sauti ya Mathew
“ Hallow Anitha” akasema Mathew aliyetoka chumbani kwake alikokuwa amejipumzisha
“ Ouh Mathew .Jaji kaniambia ulikuwa umejipumsisha”
“ Ndiyo .Nilikuwa nimejipumzisha kidogo.Kichwa changu kilikuwa kizito sana.Vipi huko utokako kila kitu kimekwenda vizuri?
“ Huko kila kitu kimekwenda vizuri.Tayari nimempatia Peniela vile vifaa na jioni ya leo tutaanza kupokea taarifa toka kwa Dr Kigomba.Vipi huko ulikokwenda ulifanikiwa? Uliniogopesha kidogo uliposema kuna jambo zito” akasema Anitha
“ Nilikokwenda kuna mafanikio.Elibariki alikuwa sahihi kuhusiana na asili ya Peniela.Tumefahamu kila kitu kuhusiana na Peniela.” Akasema Mathew kisha akamsimulia Anitha kila kitu kilichotokea na alichokigundua
“ Ouh Mungu wangu.Nimestushwa sana na taarifa hiyo.Huyu John mwaulaya ni shetani kabisa.Nimesikia taarifa zake za kikatili lakini sikuwahi kuhisi kama anaweza akawa mkatili kiasi hiki.Lakini mbona nilipoonana na Peniela hakuonyesha dalili zozote za kama kuna jambo zito lilimtokea.Alikuwa katika hali ya kawaida kabisa” akasema Anitha
“ Peniela is a strong woman.Hata kama kuna jambo linamsumbua huwa si rahisi kuonyesha kwa nje but I know she’s deeply hurt” akasema jaji Elibariki
“ Namuonea huruma sana Peniela” akasema Anitha
“ Anyway tuachane na masuala hayo ya peniela,kwa sasa kuna suala lingine kubwa limejitokeza.Yash amerejesha majibu ya zile karatasi “
“ Real ?!!...Amegundua nini? Akauliza Anitha
“ Anitha its something very serious” akasema Mathew na kuwafanyia ishara Elibariki na Anitha wamfuate ofisini.
“ Yash kwa kushirikiana na jopo la wanasayansi wamegundua kwamba kilichoandikwa katika karatasi zile ni kanuni za kutengeneza kirusi ambacho kinatajwa kuwa hatari sana na ambacho kinaweza kutumika kufanya maangamizi makubwa .” Akasema Mathew
“ Ouh my God !..Anitha akastuka sana.
Mathew akaendelea kumueleza kwa undani kuhusiana na kile alichokiandika Yash.
“ Sasa picha imeanza kuja” akasema Anitha baada ya Mathew kumaliza kumpa maelezo
“ Ni kweli ,lakini kuna maswali ambayo lazima tujiulize na tuyatafutie majibu.Kwanza tunatakiwa kumfahamu aliyeandika kanuni zile ni nani? Yuko wapi ? Karatasi zile zimefikaje katika ikulu yetu? Kitu kingine ambacho tunatakiwa tukitafutie majibu ni kwamba kama karatasi zile zilikuwa ikulu basi kutokana na unyeti wake ni lazima zilikuwa zimehifadhiwa mahala pa siri kubwa na ambapo si rahisi kwa mtu kama Edson kuweza kuzifikia na kuziiba.Edson alikuwa ni mfanyakazi wa kawaida katika idara ya habari ikulu na asingeweza kabisa kujua mahala nyaraka nyeti kama hizi zilikohifadhiwa kwa hiyo basi nashawishika kuamini kwamba lazima kuna watu au mtu ambaye alifanikisha kwa Edson kuweza kuzipata kirahisi.Nahisi Edson alitumiwa tu ili kuweza kuzipata kirahisi nyaraka zile.Na kama hisia zangu ni kweli basi lazima mtu huyo ndiye atakayekuwa kinara wa mpango huu wote.Kingine kikubwa ambacho tunatakiwa tukifahamu ni kama kirusi hicho kimekwisha tengenezwa ama bado na kama tayari kiko wapi? Kama bado hakijatengenezwa ni kufuta kabisa mpango wowote wa kukitengeneza kwa kuhakikisha tunalichimba jambo hili hadi mzizi wake na kuwapata wahusika.Guys we’re going into something very dangerous so we need to get prepared for this.This is a victory or death.Siwaogopeshi lakini hiyo ndiyo hali halisi na ninapenda niwe muwazi kwenu.” Akasema Mathew
“ Binafsi hufurahi sana ninapofanya kazi pamoja nawe Mathew.Una akili kubwa ya kuchambua mambo.Ni kweli tunalazimika kutafuta majibu ya maswali hayo uliyoyaorodhesha.Katika jambo ulilolisema mwishoni kuhusiana na mtu ambaye anaweza akawa nyuma ya mpango huu nakubaliana nawe kabisa.Si rahisi kwa akina Edson peke yao kulifanikisha jambo kubwa kama hili.Kufanikiwa kuiba nyaraka ikulu si jambo dogo lazima ni mpango mkubwa uliobuniwa na watu makini na ambao walifahamu mahala nyaraka hizo zilipo.”akasema Anitha
“ We need to find out who is behind this.Tukimpata huyo anaweza akatusaidia sana katika kupata majibu ya baadhi ya maswali yetu” akasema Mathew
“ Jamani kwa mtazamo wangu mimi nadhani mtu ambaye yuko nyuma ya jambo hili lazima atakuwa ndani ya ikulu.Si rahisi kwa mtu wa nje akafahamu kuhusu uwepo wa karatasi muhimu kama hizi na mahala ziliko.Nina wasi wasi sana na Dr Joshua mwenyewe au wasaidizi wake.” Akasema jaji Elibariki
“ Hapana .Sina hakika kama Dr Joshua anaweza akahusika katika jambo hili.Yule ni mtu mkubwa na hawezi kufanya jambo kubwa na la hatari na watu wadogo kama akina Edson.Nina wasi wasi na wasaidizi wake.Lakini tusiseme chochote kwa sasa hadi hapo tutakapofanya uchunguzi wa kina wa jambo hili.Nadhani sehemu nzuri ya kuanzia uchunguzi wetu ni kwa wale wazee wawili waliokuwa katika mtandao mmoja na Edson.Mzee Kitwana na mzee Matiku” Akasema Mathew
“ Lakini Mathew wazee hawa,Kitwana na Matiku wamekwisha fariki kitambo,unadhani tutafanikiwa kupata taarifa zozote za kuweza kutusaidia kupata ufumbuzi wa jambo hili kutoka kwao? Wazo langu mimi ni kwamba ,kwa kuwa tayari tunamfahamu mtu ambaye alikuwa akihitaji kuzinunua karatasi hizo ni kwa nini basi tusimfanyie uchunguzi yeye na kufahamu kwanza alikuwa akiwasiliana na akina nani hapa nchini na pia tunaweza kujua alikuwa na lengo gani na zile karatasi? Akasema Anitha
“ Anitha wazo lako ni zuri sana na hapo kabla nilijadiliana na Elibariki kuhusiana na kumfanyia uchunguzi wa kina huyu mtu anayetajwa kuzitaka karatasi hizo.Tutalifanya hilo lakini kabla ya kulifanya hilo nadhani ingekuwa vizuri kama tungewafanyia uchunguzi hawa wazee wawili tukizipitia taarifa zao za mawasiliano ya mwisho ili tuweze kuwafahamu watu ambao walikuwa wakiwasiliana nao mara kwa mara na katika hao tunaweza tukampata kinara wao.Katika hili Eva atatusaidia sana.Kama nilivyowahi kuwaambia kwamba Eva anafanya kazi katika idara ya usalama wa taifa kwa hiyo ana taarifa nyingi sana na katika hili hatashindwa kutusaidia.” Akasema Mathew
“ Are you sure she will help us? Nakumbuka mara ya mwisho alipoondoka hapa alikuwa na hasira mno na baada ya Yule msichana Sabina kufariki sina hakika kama bado atakuwa tayari kutusaidia” akasema Anitha
“ Believe me Anitha,she will help us” akasema Mathew
“ Nitakwenda kuonana naye sasa hivi.Wewe utabaki hapa ukisubiri taarifa toka kwa Peniela.Sintakawia sana.Endapo kuna jambo lolote kubwa litajitokeza utanitaarifu” akasema Mathew na kuingia chumbani kwake akajiandaa na kuondoka kuelekea kwa Eva.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO…