PENIELA SEASON 3
SEHEMU YA 22
MTUNZI : PATRICK.CK
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Ninafahamu matatizo uliyoyapata ya kusingiziwa kesiya mauaji,ninafahamu kwa sasa uko katika mahusiano na jaji Elibariki,ninamfahamu Johnmwaulaya alikuwa ni rafiki yangu wa siri na wakati wa uongozi wangu alinisaidia mambo mengi niliyohitaji kuyafanya kwa siri.kwa ujumla ninafahamu mambo mengi kuhusu wewe” akanyamaza akanywa pombe yake katika glasi na kuendelea.
“ Amos amekuwa ni kijana wangu kwa muda mrefu na kifo chake kimeniumiza sana.Amekuwa akinipa kila taarifa za kinachoendelea ikulu na siku kadhaa zilizopita alinipa taarifa kwamba kuna watu ambao wanataka kumuua jaji Elibariki nikampa maelekezo kwamba afanye kila linalowezekana ili kumuokoa Elibariki kwani tuna mipango naye mikubwa.Amos alijitahidi kwa kila alivyoweza na kufanikiwa kumuokoa Elibariki akamkabidhi kwako” akasema Deus.
“ You knew about that? Akauliza Peniela kwa mshangao
“ Yes I knew na mimi ndiye niliyetoa amri Elibariki aokolewe.”
Peniela akabaki anashangaa.Mathew na Anitha ndani ya gari pia wakatazamana
ENDELEA………………………….
“ Elibariki was saved by a woman.Do you know her? Akauliza Peniela
“ Nilimpa maagizo Amos ya kuhakikisha kwamba Elibariki hadhuriki katika tukio hilo lililopangwa na watu wa Dr Joshua kwa hiyo sifahamu aliokolewa vipi na nani.Nilichohitaji mimi ni jaji awe mzima tu so to answer your question I don’t know her” akajibu Deus.Peniela akanywa mvinyo kidogo kisha akauliza
“ Why you saved him?
Deus Mkozumi akamtazama Peniela kisha akainuka akaeleka katika kabati la kioo lililokuwa na chupa kadhaa za pombe kali akalifungua na kuchukua chupa moja akaitazama na kutabasamu
“ This whisky is called Labellion.Its one among the expensive whisky on earth.,”akasema na kuitazama tena ile chupa.
“ Aliyeitengeneza whisky hii anaitwa David Labellin aliyekuwa mwanajeshi mstaafu wa jeshi la ufaransa na mpaka leo anaheshimika duniani kote kwa umahiri wake wa kutengeneza kinywaji kama hiki. Whisky hii hunywewa na watu maarufu duniani.Most of them are leaders of powerfull nations on earth .Would you like to try it? Akauliza Deus.Peniela akatabasamu na kutikisa kichwa.Amos akamimina katika glasi mbili na moja akampatia Peniela kisha akanywa pombe yote iliyokuwamo katika glasi kisha akafumba macho kwa sekunde kadhaa na kusema
“ Kama nilivyokwambia kwamba marais wenye nguvu kubwa duniani hupendelea sana kutumia kinywaji hiki and I’m happy that I’m one of them.Pamoja na kwamba nimemaliza uongozi wangu lakini bado ni mtu mwenye nguvu katika taifa hili..” akanyamza na kumtazama Peniela halafu akaendelea
“ Nilipokaribia kumaliza uongozi wangu nilimpendekeza Dr Joshua aweze kunirithi nikiamini kwamba ni mtu sahihi na ambaye anaweza akafuata misingi ile mizuri ya uongozi niliyoiweka.Kwa bahati mbaya alipoingia madarakani Dr Joshua alibadilika na hakufuata kabisa kile ambacho sote tuliomuweka pale tulitarajia.Uongozi wake umekuwa na kasoro nyingi sana kiasi kwamba lawama zote zinakuja kwangu kwa sababu ni mimi niliyempendekeza ndani ya chama na nikawahakikishia watu kwamba anafaa kupewa dhamana hii kubwa ya kuwatumikia watu.He failed me.” Deus akanyamaza kidogo akamimina tena mvinyo kidogo akanywa na kuendelea
“ Dr Joshua anakaribia kumaliza muda wake wa uongozi na ni nafasi yangu tena kutafuta mtu ambaye nina hakika kabisa kwamba anaweza akaiongoza nchi hii vizuri kwa namna ninavyotaka mimi.Nimejaribu kuangalia sana watu mbali mbali nani ambaye anaweza akafaa kuongoza nchi nikampata jaji Elibariki.Ni mtu ambaye binafsi nina uhakika naye mkubwa sana kwamba anaweza akafaa kupewa nafasi kama hii baada ya Dr Joshua.Hiyo ni sababu sikutaka jaji Elibariki auawe.”akasema Deus.
“ peniela muulize nini sababu ya Elibariki kutaka kuuawa? Mathew akamwambia Peniela
“ Deus unafahamu ni kwa nini jaji Elibariki alitakiwa auawe? Akauliza Peniela.
“ Ni kwa sababu aliufahamu ukweli ambao hakutakiwa kuufahamu na ndiyo maana ikatolewa amri auawe ili siri aliyoigundua isivuje” akasema Deus
“ aligundua kitu gani? Akauliza Peniela
“ Ouh peniela mbona una maswali mengi ? Elibariki aligundua siri ya kuhusu kifo cha Dr Flora mke wa Dr Joshua.”
“ Unataka kuniambia kwamba Dr Flora aliuawa? Akauliza Peniel
“ yes Dr Flora aliuawa .”
“ who killed him?
“ Amos did.Captain Amos ndiye aliyemuua Dr Flora kwa amri iliyotoka kwa rais mwenyewe.”
“ Ouh my gosh ! so he killed his own wife? But why would he do that? Akauliza Peniela
“ Dr Flora aligundua kuhusu jambo fulani kubwa analotaka kulifanya mumewake na hakukubaliana naye hata kidogo na ndiyo maana suluhisho peke likawa ni kumuua” Deus akanyamaza halafu kikapita kimya kifupi akasema
“ Kuna uovu mwingi ambao umefanyika wakati wa kipindi cha Dr Joshua na ndiyo maana safari hii ninataka mtu ambaye ni msafi na hawezi kufanya mambo kama aliyoyafanya Dr Joshua.Ninamtaka jaji Elibariki.I want to make him very powerfull president na wewe ukiwa kama mwandani wake you’ll be the next first lady.Hiyo ndiyo mipango tuliyonayo juu yako wewe na jaji Elibariki ambao Amos alitaka kukwambia. Both of you will be very powerfull..What do you think about that? Picture yourself being a first lady ,what do you see? Akauliza Deus
Peniela akatoa tabasamu pana sana halafu akapeleka glasi ya mvinyo mdomoni akanywa kidogo
“ What a beautifull lady..akitabasamu anafanana na wale viumbe wazuri wanaotajwa katika simulizi za kale.I’ve never met with such a beautifull queen like this one.She deserve to be the next first lady””akawaza Deus kisha akasema
“ Natumai tayari umekwisha pata picha ni namna gani utakavyokuwa ukiwa mke wa rais.Do you like to be in that position? Akauliza dues
“ Kila mtu anapenda kuwa katika madaraka na nafasi fulani lakini katika hili ulilolisema ninaomba muda wa kulifikiria.”
“ Good. You have all the time in the world to think about it..what do you say about elibariki.Do you think he can agree to be the next president? Akauliza Deus
“ I don’t know..” akajibu Peniela
“ Anyway where is he now? Can you tell me? Akauliza Deus
“ Siwezi kukwambia kwa sasa yuko wapi kwa sababu anatafutwa kila kona akihusishwa na shambulio lililosababisha kifo cha mke wake”akasema Peniela
“ Ouh I heard about that and I’m so sorry for his loss lakini hizi zote ni njama za Dr Joshua na genge lake.Wanamtafuta Elibariki kwa udi na uvumba kwani wanafahamu yeye ni kikwazo kikubwa katika kufanikiwa mambo yao. Anyway tell me ,huko aliko Elibariki is he well protected? Akauliza Deus
“ yes he’s safe and well protected”akajibu Peniela
Deus akachukua tena ile chupa ya Labellion na kumimina katika glasi yake kisha akamtazama Peniela
“ More whisky?akauliza
“ Yes ofcourse”akajibu Peniela na Deus akamimina tena whisky kidogo katika glasi yake.
“ Deus kuna kitu ninataka kukifahamu kutoka kwako.”
“ Ouh Peniela una maswali mengi sana le😵k ninakupa nafasi ya maswali matatu tu ya mwisho “akasema Deus
“ Ok thank you Deus”akajibu Peniela na kunywa whisky kidogo kisha akauliza
“ Amos alikuwa mtu wako ndani ya ikulu na alikuwa akikupa taarifa za kila kinachoendelea kule.Hivi sasa,Dr Joshua anataka kuiuza package ambayo imehifadhiwa ikulu .Wewe umekuwa mstari wa mbele sana katika kuzuia jambo hili lisifanyike.Nataka kufahamu nini kilichomo ndani ya package hiyo?
Deus akamimina tena whisky katika glasi akanywa na kusema
“ Nilipokabidhiwa ofisi na rais aliyenitangulialia mojawapo ya vitu ambavyo nilikabidhiwa ni hicho kitu anachotaka kukiuza Dr Joshua.Japokuwa hakuna kiapo rasmi lakini niliapa kwamba nitailinda package ile kwa nguvu zangu zote na wala sintathubutu kwa namna yoyote ile kuruhusu iguswe na mtu mwingine yeyote na wala kufahamika mahala ilipo .Nilitimiza kiapo change kwani hadi ninamaliza uongozi wangu package ile haikuwa imeguswa na mtu yeyote..Nilipomkabidhi Dr Joshua ofisi nilimkabidhi pia na package ile ailinde kama mboni ya jicho lake .Aliapa kufanya hivyo lakini aliingiwa na shetani wa tamaa na sasa anataka kuiuza .Nimekuwa mstari wa mbele sana kuzuia jambo hili lisifanyike na si mara moja nimewahi kumpigia simu na kumfahamisha kwamba ninafahamu mambo anayoyafanya na kumtaka aache kabisa mipango yake hiyo ya kutaka kuiuza package ile. Badala yake ameniweka katika kundi la maadui zake na tayari alianza kusuka mipango ya kuniua kwa bahati nzuri mtu ambaye alitaka kumtumia katika mpango huo ni kijana mtiifu kwangu . Kuhusu nini kilichomo ndani ya hiyo package sintaweza kukwambia kwani ni siri niliyoapata kuilinda hadi ninaingia kaburini.”akasema Deus akanyamaza kidogo na kusema
“ second question “
“ Kuna nyaraka za siri ziliibwa ikulu na aliyeziiba ni Amos akishirikiana na kijana mmoja anaitwa Edson na aliyekuwa nyuma ya mpango huu wote ni Rosemary Mkozumi mke wako wa zamani.Nyaraka hizo zina kanuni ambazo zinaelekeza namna ya kutengeneza kirusi hatari na kinachoweza kusababisha maangamizi makubwa sana.Unafahamu chochote kuhusu jambo hili? Swali lile likamstua sana Deus
“ What ?! I didnt know anything about that.Nyaraka zile zimeibiwa? Deus akashangaa sana
“ Ndiyo Deus na kinara wa mpango huo ni mkeo “ akasema Peniela na Deus akasimama.
“ Amos was a devil.Sikutakiwa kumuamini kiasi kile !! akasema Deus
“ Amos was working with your wife “ akasema peniela
“ peniela naomba niweke rekodi sawa.Yule si mke wangu.Mimi na yeye tumekwisha tengana kitambo kwa hiyo haipendezi kumtaja kama mke wangu.Nilimuamini sana Amos na sikutegemea kama angeweza kunigeuka na kushirikiana na mke wangu.Nyaraka hizo unazozisema ni moja wapo ya vitu ambavyo niliapa kuvilinda kwa nguvu zangu zote kwani ni mojawapo ya nyaraka hatari sana na ndiyo maana zikafichwa ikulu sehemu ya siri kabisa .Amos hakuwahi kuniambia kama nyaraka zile zimeibwa na wala sikujua kama anashirikiana na Rosemary.Laiti ningelifahamu jambo hili toka mapema basi ningemuondoa mapema sana.Rosemary ni mtu hatari sana na ndiyo maana mimi na yeye kwa hivi sasa ni chui na paka.Niliishi naye ikulu na anayafahamu mambo mengi ya ikulu kwa sababu nilimshirikisha kwa kuwa nilimuamini kama mke wangu lakini baadae niligundua kwamba nilikuwa ninaishi na nyoka na si binadamu na ndiyo maana nikatengana naye.”akasema Deus kwa hasira kali kisha akamimina tena mvinyo katika glasi akanywa kwa fujo
“ Peniela muulize kuhusu Hasheem Abdullah” Mathew akamwambia Peniela
“ Do you know someone called Hasheem Abdullah ? akauliza Peniela na kumstua sana Deus
“ Hasheem Abdullah ?!! Do you know him? Akauliza Deus.
“ Hasheem is working with Rosemary Mkozumi” akasema Peniela.Deus akamtazama kwa makini sana na kusema
“ Peniela who are you working with?
“ kwa nini unauliza Deus?
“Ninahitaji kufahamu.Ninajua unafanya kazi na Team SC41 lakini na hakika kanisa kwamba mambo haya unayonielea hayajatoka katika Team SC41.” Akasema na kumtazama Peniela
“ Whoever you are working with ,they must be a very professional people..”akasema Deus.
“ This guy Hasheem do you kow him? Akauliza peniela.Deus akanyamaza kidogo akafikiri kisha akasema
“ Hasheem Abdullah ndiye aliyetufanya mimi na Rose tukatengana.Niligundua kwamba Rose alikuwa na mahusiano na mtu huyu hatari ambaye anayetajwa kufadhili vikundi vya kigaidi.” akasema Deus
“ Do you know that your wife is working with terrorists? Akauliza Peniela
“ I’ve answered your three questions now its my turn to ask” akasema Deus
“ Kitu cha kwanza ninachotaka kufahamu ni kuhusu zile nyaraka ,mmefahamu mahala zilipo? Akauliza Deus
“ usihofu Deus nyaraka zile tayari tunazo mikononi mwetu na tuliziwahi kabla hazijauzwa kwa mtu mmoja anaitwa Habib soud raia wa Saudiarabia ambaye anatajwa kufadhili vikundi vya kigaidi.Ziko salama ” akajibu Peniela
“ Thank you Lord ” akasema Deus
“ Second question.Uliniambia kwamba unamfahamu aliyemuua Amos?
“ yes I know her.Ni yule mwanamke aliyemuokoa Elibariki ” akasema Peniela
“ The same woman? Are you sure Peniela ? akauliza Deus
“ yes I’m sure.I saw her face that night and I saw her face today, its her”
“ Ouh my God .kwa nini alimuua?
“ Sifahamu kwa nini alimuua lakini inaonekana wazi kwamba hakutaka Amos anieleze kuhusiana na mipango mliyonayo juu yangu na Elibariki.”
“ Ninashindwa kupata jibu kwa nini hakutaka kufahamu kuhusiana na mpango huu? What’s going on? Akauliza Deus.
“ Anyway nitafanya uchunguzi wangu na kufahamu undani wa jambo hili.Naomba unieleze ni wapi alipo Rosemary? Nani anayemshikilia na kwa nini? Akauliza Deus
“ Sintaweza kukueleza ni akina nani ambao wanamshikilia Rosemary lakini yuko sehemu ambako si rahisi kufikiwa na watu anaoshirikiana nao .Anahojiwa kuhusiana na kushirikiana na magaidi.I’m sorry Deus but your wife is very dangerous.“ akasema Peniela
“ Ninalifahamu hilo na ni mojawapo ya sababu iliyonifanya nikaachana naye na hasa nilipogundua kuhusu mahusiano yake na Hasheem ,lakini sikutegemea kama itafikia hatua hii aliyofika.Amefikia hatua mbaya sana.Naomba sana Peniela kama unafahamiana na watu ambao wanamshikilia Rosemary waambie tafadhali wasimuachie kabisa Yule ni mtu hatari sana.In anyway Rosemary hatakiwi kabisa kuachiwa.Ninawapongeza sana waliomkata kwani ana mtandao mkubwa na amekwisha jihakikishia kwamba hawezi kukamatwa. Mtandao wake wote unatakiwa ufahamike na watiwe nguvuni.Rosemary ni mtu muhimu sana ambaye anaweza akawaongoza na kufanikisha kuufumua kabisa mtandao wa kigaidi hapa nchini .” akasema Deus akamtazama Peniela kwa makini na kusema
“ Jambo lingine.Nilimtegemea sana Amos katika kupata taarifa kuhusiana na package anayotaka kuiuza Dr Joshua lakini kwa sasa baada ya Amos kuuawa I don’t have any connection with the president kwa hiyo sintajua kinachoendelea.Package ile haitakiwi kutua mikononi mwa mtu yeyote Yule.Inatakiwa ihifadhiwe sehemu salama sana .Ninafahamu wewe na team Sc41 mko pia katika harakati za kuipata package hiyo lakini ninakusihi Peniela usiache package ile ikatua mikononi mwa team SC41.fanya kila uwezavyo kuweza kuipata wewe mwenyewe na kisha unikabidhi mimi niihifadhi sehemu salama ambako nina uhakika kwambaitakuwa salama.Endapo utahitaji msaada wowote ule mimi niko tayari kukusaidia ili package hiyo isipotee .We’re doing this for our country,our children’s children and for the whole world..Can I trust you on this?
“ Yes you can.I’ll try to do that “ akajibu Peniela
“ Good.sasa tuachane na hayo tuzungumzie masuala yetu ya msingi.”
“ masuala gani hayo Deus? Akauliza Peniela.
Deus akamsogelea Peniela pale sofani.
“ about me and you” akasema Deus na Peniela akatabasamu
“ Peniela I want to make you the most powerfull woman in this country.I want to make you the first lady.Every woman wants to be the first lady so I want to make your dream come true.Utatembea na msafara ,utakuwa na walinzi na utapata kila unachokitaka.Hii ni fursa ya kipekee kabisa unaipata.tafadhali usiiache na ninajua kabisa kwamba huwezi kuikataa.. “
“ Peniela mkubalie anachokitaka.mwambie uko tayari” Mathew akampa peniela maelekezo
“ Ok Deus siwezi kuikataa nafasi kama hii adimu kabisa kupatikana.”
“ Good.I’ll make you the first lady.But I need something in return” akasema Deus
“ What do you need in return Deus? Akauliza Peniela
“ I need you.!akasema Deus
“ Me?! Peniela akashangaa
“ yes I need you.I want to spend time with you especially tonight.I need ypu so badly..”akasema Deus
“ peniela mkubalie lakini mwambie na wewe kuna kitu unataka kutoka kwake” amathew akamwambai peniela
“ Ouh Deus ,utaniweza mtu kama mimi..?akaulzia Peniela
“ kwa nininisikuweze peniela?
“ Ok tutaona lakini mimi niko tayari kukuachia mwili wangu but I also need onething in return”akasema peniela
“ What do you need beautiful angel?
“ mwambie akwambie nini kilichomondani ya package” akasema Mathew
“ I want you to tell me whats in the package”
“ peniela ! peniela..nimekwisha kwambia kwamba hii ni siri yangu hadi siku ninaingia kaburini.tafadhaliombakitu kingine chochote na si hicho.Katu sintaweza kukuambia” akasema dues
“ peniela wakati wa kuondoka sasa.”Mathew akamwambia peniela
“ Deus ninashukur sana kwa kuipata nafasi hii ya kukaa nawe japo wa dakika chache.Ninashukuru kwa ushirikiano wako na kama Mungu akipenda tutaonana tena.Niko tayari kukaa nawe hata kwa usiku mzima lakini hadi pale tu utakaponieleza kuhusu kilichomo ndaniya package.” Akasema peniela huku akiinukana kuuchukua mkobawake tayari kwa kuondoka.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………..