Peniela (Story ya kijasusi)

Peniela (Story ya kijasusi)

Mkuu hata sa hivi nimechoropoka mchezoni nilikiwa nachaji simu home. Nikasema muda huu kutakuwa na episode kadhaa za kusoma huku nakabenbeleza kabebi kangu kalale lakini nimeambulia patupu. Lege siamini kama umetuelibariki hivi!
Baby yupi mtto au mkubwa [emoji30][emoji30]
 
SEASON 1
SEHEMU YA 10
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Hallo Mathew” akasema Jaji Elibariki
“ hallo jaji.habari za siku? Leo umenikumbuka ndugu yangu lazima utakuwa na tatizo.”
“ Ni kweli nina shida ndugu yangu nahitaji kukuona” akasema Elibariki
“ Unataka tuonane saa ngapi?
“ sasa hivi.Uko wapi?
“ Niko nyumbani kwangu”
“ Ok njoo utanikuta lakini tafadhali naomba uje peke yako.Sitaki uwe umeambatana na mlinzi yeyote”

‘ Nitakuja mimi mwenyewe.dereva wangu ana matatizo ya kifamilia na nimempa likizo ya muda” akasema Elibariki
“ Good” akajibu Mathew na kukata simu.jaji Elibariki akainuka akavaa koti lake na kutoka
“ It’s time for action now” akasema jaji Elibariki huku akiingia garini.
“Mbivu na mbichi lazimazijulikane katika kipindi kifupi” akasema kwa sauti ndogo

ENDELEA…………………………………..

Jaji Elibariki waliwasili katika jumba moja kubwa lililozungushiwa ukuta mkubwa.Alipiga honi mara tatu na toka katika mlango mdogo wa geti akatokeza mlinzi akiwa na mbwa mkubwa akamfuata Elibariki katika gari
“ habari yako mkuu” Akasema Yule mlinzi aliyevalia sare za ulinzi za kampuni binafsi ya ulinzi
“ Habari nzuri.Nina miadi na ndugu Mathew” akasema jaji Elibariki
“ Wewe ndiye Elibariki? Akauliza Mlinzi
“Ndiye mimi”
“ Ok.taarifa zako ninazo” akasema Yule mlinzi huku akiingia ndani na kufungua geti.Jaji elibariki akaingia .

Mbwa watatu wakubwa wakalizingira gari lile na kuanza kubweka kwa nguvu.jaji Elibariki akaogopa kushuka ndani ya gari kwa namna mbwa wale walivyokuwa wakubwa.Mlinzi akafika mara moja na kuwatuliza akawapeleka katika nyumba yao.Elibariki akashuka na kuongozwa na mlinzi hadi ndani.Akakaribishwa sebuleni.Ilikuwa ni sebule kubwa yenye vitu vingi vya thamani.Baada ya dakika kama nne hivi Mathew akatokea.Ni mtu mmoja mfupi mwenye mwiliwa wastani.

“ Mheshimiwa jaji.habari za siku ndugu yangu?
“ habari nzuri Mathew.Maisha yanakwendaje?
“ maisha yanakwenda vizuri.Mungu ananiwezesha.Vipi wewe mambo yako yanakwendaje?
“ Mambo yangu yanakwenda vizuri lakinisi vizuri sana.”
‘Nini tatizo Elibariki? Mpaka uje kwangu lazima ni tatizo kubwa.Niambie nini tatizo? Niko tayari kukusaidia.Wewe ni rafiki yangu mkubwa.Hukuniacha wakati nina matatizo .” akasema Mathew huku akiwasha sigara yake na kuvuta
“ Mathew,kuna kijana mmoja anaitwa Edson alikuwa akifanya kazi katika idara ya mawasiliano ikulu,aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake.Baada ya mauaji hayo mpenzi wake alituhumiwa kwamba ndiye muuaji na kufunguliwa mashtaka.

Kesi imeendeshwa kwa muda wa mwaka mzima na wiki hii nimetoa hukumu na kumuachia huru Yule msichana.Hakuwa na kosa lolote.Hakumuua Edson lakini nguvu kubwa ilitumika kushinikiza mahakama imkute na hatia na hatimaye afungwe maisha gerezani.Shinikizo kubwa lilitoka ndani ya familia ya rais kwani kijana huyo Edson aliwahi kuwa na mahusiano na binti wa rais kabla ya kuachana naye na kuingia katika mahusiano na Penny. Kwa hivi sasa hali si shwari ndani ya ndoa yangu.Mke wangu na ndugu zake wananichukia sana kwa maamuzi niliyoyafanya ya kumuachia huru Penny .Wao wanaamini kwamba penny ndiye aliyemuua Edson.Nimekuwa nikidharauliwa mno na watu hawa kutokana tu na kutenda haki. Baada y kutafakari sana nimeamua kufanya jambo moja la muhimu.

Kumtafuta mtu aliyemuua Edson ili kwanza kuudhihirishia umma wa watanzania kwamba sikukurupuka katika kufanya maamuzi yale na pili kumlinda Penny.Watu ambao walitaka akutwe na hatia na hatimaye apewe adhabu hawatamuacha hivi hivi.Lazima watamuandama na kuhakikisha wanamuondoa kwa namna nyingine.Mathew nimekuja kwako sina msaada mwingine,sina mtu mwingine ambaye anaweza akanisaidia katika jambo hili “ akasema jaji Elibariki.Mathew akainuka na kuelekea katika kabati kubwa akalifungua na kuchukua chupa kubwa ya mvinyo akamimina katika glasi mbili na moja akampatia Elibariki.Akagugumia pombe yote iliyoko katika glasi halafu akavuta mikupuo miwii ya sigara na kupuliza moshi mwingi hewani kisha akasema

“ This is a serious issue than I thought” akasema Mathew kwa sauti ndogo.
“ Si suala dogo hili Mathew na ndiyo maana nimekuja kwako ili unisaidia.Wewe umebobea katika masuala haya ya uchunguzi,umekwisha fanaya kazi katikaidara ya ujasusi ya taifa na una uzoefu mkubwa wa masuala kama haya.Naomba unisaidie kumbaini nani muuaji wa Edson na kwa nini alimuua.Tukifanikiwa katika hilo kila kitu kitakuwa shwari kabisa” akasema Elibariki.Mathew akainama akafikiri tena na kusema
“This girl ..Pe.. Jina lake nani ? Limenitoka kidogo” akasema Mathew
“ Anaitwa penny”
“ Good.This girl Penny who is she to you? Swali lile likamchanganya kidogo jaji Elibariki akafikiri na kusema
“ She’s just an Innocent girl.

Ni mtuhumiwa ambaye hakuwa na kosa na ndiyo maana nikamuachia huru”
“ Eli haujajibu swali langu.Ninafahamu alikuwa mtuhumiwa na hakuwa na kosa .Ninachotaka kufahamu ni mahusiano yako na msichana huyu.Ni ndugu yako,rafiki yako au mpenziwako.Usiogope kuwa muwazi kwangu.” Akasema Mathew
“ Hatukuwahi kufahamiana hapo kabla hadi nilipoanza kuisikiliza kesi yake.Hatukuwahi kuwa na urafiki lakini kwa sasa naweza kusema kwamba tumekuwa marafiki.”
“ Urafiki wa namna gani? Wa mtu na mpenzi wake au urafiki wa kawaida? Akauliza Mathew
“ Ni urafikiwa kawaida tu .” Mathew akavuta sigara na kupuliza moshi halafu akasema
“ Eli nakufahamu vyema,usingeweza kupoteza wakati wako kulishughulikia suala hili kama msichana huyu hana maana yoyote kwako.Please be honnest with me.

I want to help you” “ Ok Mathew,umetaka niwe muwazi na ninakuwa muwazi.Ni kweli msichana huyu ametokea kunivutia sana na tayari nimeanza kuwa na hisia za kimapenzi kwake na ndiyo maana ninajitahidi kufanya kila linalowezekana ili kumlinda”
“ Sawa Eli,ahsante kwa kuwa muwazi.Nitakusaidia.” akasema Mathew halafu akavuta mikupuo miwili ya sigara na kuizima akatoa nyingine katika pakiti akaiwasha.

“ Kwanza naomba ufahamu kwamba hili si suala rahisi kama unavyolichukulia. Ni suala zito na la hatari kubwa.Lakini nakuhakikishia kwamba tutamtafuta muuaji wa huyo kijana kokote alipo na nitahakikisha ninampata.Sikuwa nikitaka kufanya kazi yoyote ya hapa nchini lakini nitaifanya kazi hii kwa sababu yako” akasema Mathew huku akivuta sigara na kupuliza moshi mwingi hewani
“Mathew ninashukuru sana kukubali kunisaidia katika suala hili.Hata hivyo siko peke yangu katika suala hili.Nina mwenzangu aitwaye Jason ambaye ni wakili wa Penny.Ndiye aliyemsimamia Penny katika kesi hii.”
“ Sawa nimekuelewa Elibariki.Mimi niko tayari kufanya kazi hiyo kwa kutumia uwezo wangu wote.

Naomba unipe muda kidogo wa kutafakari namna nitakavyoweza kuifanya kazi hii.Naomba nionane nanyi kesho asubuhi ili niwape mchakato mzima namna nitakavyoifanya hii kazi. Akasema Mathew halafu wakaendelea na maongezi mawili matatu Jaji Elibariki akaondoka

*********

Saa moja na nusu za jioni,jiji ni Arusha bado mvua za manyunyu zinaendelea.Katika hoteli ya kifahari ya Kobe Village Peniela yuko chumban kwake amejilaza..Pembeni ya kitanda chake kulikuwa na meza ndogo iliyokuwa na chupa kubwa ya mvinyo akiendelea kunywa tarataibu huku akifurahia muziki katika runinga.Kengele ya mlangoni ikalia kuashiria kwamba kulikuwa na mtu.Akainuka na kwenda kufungua mlango akakutana na muhudumu aliyevaa suti nzuri nyeusi akiwa na kifurushi mkononi
“ madam kuna mzigo wako umeletwa”akasema Yule muhudumu huku akimpa Penny karatasi ya kusaini kwamba amepokea mzigo.Akasaini karatasi ile na kujifungia chumbani akakifungua kile kifurushi kilichofungwa vizuri.
“ Lazima mzigo huu utakuwa umetoka kwa Kareem” akawaza Penny wakati akikifungua.Ndani ya boksi lile kulikuwa na simu nzuri sana ya gharama kubwa

“ Wow ! what a nice phone” akasema Penny huku akitabasamu.Toka ndani ya lile boksi kulikuwa na kikaratasi kidogo kilichomuelekeza penny aiwashe simu ile.Akaiwasha na kuichunguza ndani,hakukuwa na namba yoyote ya simu iliyoandikwamo.Wakati akitafakari ikapigwa simu akaipokea.Aliitambua sauti ya mpigaji,alikuwa ni Kareem.
“ Hallo Penny” akasema kareem
“ Hi Kareem.”

“ Habari za Arusha?akauliza kareem
“ habari nzuri ila kuna baridi sana huku.?
“ Ok.Usizime hii simu.Mzee atazungumza nawe baada ya dakika chache.” Akasema Kareem na kukata simu.Baada ya dakika kama nne hivi simu ikaita tena kwa namba nyingine tofauti na zile za mwanzo,akabonyeza kitufe cha kupokelea

“ Hallo Penny” ikasema sauti ya upande wa pili ambayo Penny aliitambua ilikuwa ni ya mheshimiwa rais Dr Joshua.
“ Hallo Dr Joshua. Habari yako ? akasema Penny kwa sauti laini “ Habari yangu nzuri.habari za Arusha?
“ huku Arusha kwema kabisa .Habari za Dare s salaam?
“ Huku ni kawaida tu” akasema Dr Joshua
“ Penny mimi ninakuja huo kesho kutwa jioni kwa ajili ya mkutano wa marais wa afrika mashariki utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia jumatatu ijayo.Katika siku hizo zote tatu nitakuwa nikionana nawe baada ya kumaliza shughuli zangu.

Nina mambo mengi sana ambayo nataka kuzungumza nawe na zadi ya yote ukumbuke ni mwaka mzima umepita sasa na sitapata ile raha ya aina yake toka kwako.Nataka unipe raha ,nifurahi “
“ Usijali Dr Joshua.Utapata kila unachokihitaji.Nimefurahishwa sana na namna unavyonijali na kunitunza.Nimeamini kwamba ni kweli umedhamiria kuufungua ukurasa mpya kati yetu.” Akasema Penny na kumfanya Dr Joshua acheke kidogo.

“ Ni furaha yangu kama umeridhika na huduma unayoipata Penny.Wewe ni malaika wangu tumia kitu chochote ukitakacho bila kujali gharama.Omba chochote ukitakacho nitakutimizia’ akasema Dr Joshua
“ Ahsante Dr Joshua.Mambo mengi tutaongea ukishakuja huku”
“ Ok Penny .Endelea kupumzika ,tutakuwa wote kesho kutwa.Nimefurahi kuongea na wewe” akasema Dr Joshua na kukata simu. Baada ya Dr Joshua kukata simu ikaingia tena simu nyingine toka kwa kareem
“ Halloo kareem” akasema Penny
“ Penny kuna jambo nimeona nikukumbushe.Simu hiyo ni maalum tu kwa ajili ya kuwasiliana na rais na mimi pekee.Usije ukathubutu kumpigia mtu mwingine yeyote.Isitoshe ukumbuke tulivyokubaliana hakuna kumpigia simu mtu yeyote Yule na kumweleza kwamba uko Arusha.Umenielewa penny?
“ Ndiyo kareem nimekuelewa” akasema Penny na kareem akakata simu
“ mambo yangu yote yanakwenda vizuri sana.Kila kitu kimekaa katika mstari na kinachofuatia sasa ni kuicheza karata yangu ya mwisho.Sitaki kufanya makosa safari hii.Hiki ndicho kipindi cha lala salama” akawaza Penny.

**********

Jaji Elibariki alirejea nyumbani kwake saa tatu za usiku na kumkuta mke wake Flaviana amekaa sebuleni akitazama filamu.Hakumsalimu akapita moja kwa moja hadi chumbani kwake akabadili nguo na kuingia bafuni akaoga halafu akajitupa kitandanina kuanza kusoma kitabu cha hadithi .Baada ya dakika kama ishirini hivi mke wake akaingia mle chumbani na kusimama pembeni ya kitanda.Alionekana wazi alikuwa na hasira
“ Eli ni tabia gani hiyo umeianza ya kuingia ndani bila hata salamu? Akauliza Flaviana.Jaji Elibariki akajifanya kama vile hajasikia akaendelea kujisomea kitabu chake cha hadithi

“Nakuuliza Eli ni tabia gani hiyo ya kuingia ndani bila hata ya kutoa salamu? Nini kinakupa kiburi siku hizi? Au ni hao wanawake unaowakingia kifua ndio wanaokupa kiburi siku hizi? akauliza kwa dharau Flaviana.Taratibu bila kuongea chochote Jaji Elibariki akainuka na kumfuata mkewe na kumzaba kibao kikali kinachomfanya apepesuke na kuangukia kitandani
“ Na iwe ni mwisho kunidharau nakunitolea maneno ya kashfa.Nimechoshoshwa na dharau zako .Nilikwisha kuonya kuhusiana na tabia hii ya dharau hukutaka kunisikia.”akasema kwa hasira Elibariki huku penny akiendelea kulia kwa nguvu.Ni mara ya kwanza toka wameoana Jaji Elibariki kumpiga kofi mke wake.

“ Ahsante Elibariki..ahsante sana..Wewe si mtu wa kunipiga mimi !...” akalia kwa uchungu Flaviana.
“ Toka nimezaliwa hata baba yangu hajawahi kunipiga kofi sembuse wewe ng’ombe ! ..Kauli ile ikampandisha hasira Elibariki na kuanza kumshushia mke wake kipigo kikali kilichomfanya apige ukelele mkubwa .Jaji Elibariki hakujali kelele zile akaendelea kumpa kipigo mkewe.Hadi anamuachia Flaviana alikuwa anavuja damu.

“ Siku nyingine usithubutu kabisa kunidharau paka wewe ..! akasema jaji Elibariki huku akitweta kwa hasira Huku akilia,Flaviana akaingia bafuni na kujifuta damu zilizotoka katika majeraha yaliyotokana na kipigo kikali
“ Eli umenipiga hadi kunitoa damu.Sasa nitakuonyesha mimi na wewe nani mwenye nguvu.I swear in heaven and earth lazima nikuonyeshe kazi na hautanisahau mpaka unaingia kaburini”akasema kwa hasira flaviana na kutoka kwa kasi akaingia katika gari lake na kuondoka kwa kasi
“ Nimechoshwa na dharau za familia hii.Yote hii ni kwa sababu baba yao ni rais .Hapana hawawezi kunitisha hata kidogo,hakuna aliye juu ya sheria.” Akasema jaji Elibariki kwa hasira.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…
Ok
SEASON 1
SEHEMU YA 9
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Baada ya kuachana na Jaji Elibariki,Jason aliamua kuelekea nyumbani kwa Peniela.Hakuwa ameongea naye toka asubuhi hivyo akaamua kwenda kuonana naye .

“ Ninakubaliana na Jaji Elibariki kwamba Penny ni mwanamke msiri sana.Ninaamini hakumuua Edson lakini nina imani kuna mambo ambayo anayafahamu kuhusiana na kifo cha Edson lakini hatyuko tayatri kuyaweka wazi.Anyway tutachunguza na tutapata jibu” akawaza Jason akiwa njiani kueleka kwa Penny Ilimchukua dakika thelathini kuwasili katika makazi ya Penny.Katika geti la kuingilia ndani kulikuwa na makufuli makubwa manne kuashiria kwamba hakukuwa na mtu ndani.Jason akatoa simu yake na kumpigia lakini hata simu yake haikuwa ikipatikana.Jason akaingiwa na wasi wasi mkubwa

ENDELEA………………………………

Dakika zilizidi kuyoyoma na Jason bado aliendelea kusimama nje ya nyumba ya Penny ,asijue la kufanya.Alikuwa na wasi wasi mwingi pengine Penny amepatwa na matatizo lakini kilichompa moyo ni yale makufuli yaliyokuwa getini ambayo yaliashiria kwamba hakukuwa na mtu yeyote ndani
“ Penny kaenda wapi? Na kwa nini amezima simu yake? Akajiuliza
“ Nina wasi wasi asijekuwa amepatwa na matatizo kwani hali ya usalama wake bado si nzuri hata kidogo.Kuna haja ya kuimarisha ulinzi hapa nyumbani kwake hadi hapo hali ya usalama itakapokuwa shwari.Nitaongea naye na kama atakuwa tayari nitamkodishia walinzi toka katika kampuni binafsi ya ulinzi ili wailinde nyumba yake na kila sshemu aendako.” Akawaza Jason akiwa nje ya gari lake

“ Lakini kwa nini niwe na wasi wasi kuhusu maisha ya Penny kiasi hiki? Na kwa nini niko hapa mida hii? Sikuwa na ratiba ya kufika hapa siku ya leo lakini tazama mahala nilipo sasa hivi,nipo nje ya geti la Penny.What am I doing here? Akajiuliza Jason
“Kuna kitu kimoja tu kilichonileta hapa.Kumuona Penny.Lakini kumuona Penny kwa makusudi yapi? Hapo ndipo ninapokosa jibu.Sina sababu yoyote ya msingi iliyonileta hapa.Mahusiano yangu na Penny ni katika masuala ya kisheria tu nasi vinginevyo kwa hiyo sipaswi kuwa na hofu yoyote kuhusu yeye wala kuyafuatilia maisha yake wala kuja hapa kwake mara kwa mara na kwa muda ninaotaka.Kazi yangu ilikuwa kumsimamia kesi na baada ya kesi kuisha natakiwa nimuache aendelee na maisha yake kama kawaida.Siku akiwa na tatizo atanitafuta” akawaza Jason halafu akaingia garini na kuondoka

“ Lakini moyo wangu unakataa kabisa kukaa mbali na Penny.Nimekuwa naye katika kipindi chote alichopata matatizo makubwa na tayari tumejenga ukaribu mkubwa kati yetu kwa hiyo si rahisi kuachana naye” akawaza Jason huku akiongeza mwendo wa gari na kulipita gari la mbele yake
“ Kuna kitu kimoja ambacho nimekuwa nakihisi kwa muda mrefu sasa lakini nimekuwa nikikwepa kuwa wazi.I’m falling in love with Penny.Kwa muda wmrefu nimekuwa na hisia hizi lakini nimekuwa nikijizuia ili kumaliza kwanza masuala ya kesi iliyokuwa ikimkabili.Kwa sasa baada ya kesi kumalizka na Penny yuko huru,sina sababu ya kuendelea kuzificha hisia zangu kwake.Siwezi tena kuendelea kujizuia.” Akawaza Jason na mara sura ya penny ikamjia kichwani akatabasamu

“ Penny ni msichanamwenye uzuri wa kipekee kabisa ambaye sioni wa kumfananisha naye.Mimi na yeye tunaendana karibu katika kila kitu na ana kila sifa ninayoihitaji kwa mwanamke wa maisha yangu.Lakini kuna kitu kimoja ambacho kimekuwa kinanila akili yangu toka jana.Nikiwa pale kwake jana alikuja Yule kijana nadhifu kuja kumchukua ili kumpeleka mahala. Ni wazi alikuwa na miadi na mtu Fulani tena inaonekana ni mtu mwenye uwezo mkubwa kifedha.Je mtu huyo ni nani na wana mahusiano gani? Akajiuliza Jason na kuvuta pumzi ndefu

“ Nitamfuatilia mtu huyo hadi nimfahamu ni nani na ana mahusiano gani na penny.Nasikia wivu mkubwa kila nikiwaza kwamba yawezekana pengine mtu huyo na penny wakawa na mahusiano ya kimapenzi.Natak
a penny nimmiliki mimi peke yangu” akawaza Jason.Moja kwa moja alielekea ofisini kwake na kitu cha kwanza baada ya kuingia ofisini alitoa simu yake na kujaribu kupiga namba za simu ya Penny lakini hazikuwa zikipatikana “ Penny yulo wapi leo?Amepatwa na nini?Nitaendelea kumtafuta hadi nimpate.Sintolala usingizi leo hadi nitakapoongea naye simuni na kujua kama yuko salama.” Akawaza Jason na kuendelea na kazi zake.

**********

Ni saa tano za asubuhi,jiji la Arusha likiwa na ubaridi uliotokana na mvua za manyunyu zilizoendelea kunyesha,lakini sughuli za kujitafutia kipato ziliendelea kama kawaida.Katika hoteli ya kifahari ya Kobe Village ,Peniela msichana mwenye uzuri wa kipekee alikuwa ghorofani akilitazama jiji hili lililobarikiwa uzuri wa kipekee kabisa,likionekana kwa uzuri kutokea hotelini pale
“ geneva of Africa” akawaza Penny huku akitabasamu.
“ Nimerejea tena katika maisha yangu niliyoyazoea.Haya ndiyo maisha niliyokuwa nikiishi na ninayotaka kuendelea kuishi.To live like a queen.Nina hakika baada ya kumaliza shughuli yangu nitaishi maisha kama haya au hata zaidi ya haya.” Akawaza na mara dada mmoja mwenye kuvalia nadhifu kabisa akamfuata na kumsalimia
“ Madam,wewe ndiye Penny?

Akauliza Yule dada mwenye sauti ya upole baada ya kusalimiana
“ Ndiye mimi” akajibu penny
“ Ok.Naitwa Zulfa,ninafanya kazi katika dula la mavazi na urembo hapa jijini Arusha liitwalo Samia Fashion.”
“ Ouh Samia Fashion,ninawafahamu sana hawa.Wana maduka yao makubwa hata jijini Dare s salaama na Nairobi.Ulikuwa unasemaje Zulfa?”
“Nimeelekezwa na bosi wangu nije nikuchukue nikupeleke dukani kwetu kwa ajili ya kufanya manunuzi ya nguo na vitu vingine.Amesema uchukue chochote kile unachohitaji” akasema Zulfa.

Huku akitabasamu Penny akaingia chumbani kwake akajiweka tayari halafu wakaondoka
“ Hii ni kazi ya kareem kwani alinikataza kubeba mzigo wowote na kuniahidi kwamba nitanunua kila kitu huku Arusha” akawaza Penny akiwa garini kuelekea Samia fashion Hakuna aliyekuwa akifahamu kwamba penny yuko jijini Arusha.Kareem mlinzi wa rais ambaye anamuamini mno na ambaye huwa anamtuma katika mambo yake mengi ya siri,ndiye aliyemsafirisha Penny toka Dar hadi Arusha baada ya kupewa maelekezo na rais. Saa tisa za usiku alimpigia simu penny na kumtaka ajiandae kwa safari ya kuelekea Arusha.Hakuwa na kipingamizi kwani alikwishapewa maelekezo ya kukubali chochote atakachoambiwa na rais.

Saa kumi na moja juu ya alama lilifika gari na kumchukua kumpeleka uwanja wa ndege akapanda ndege maalum ya kukodi kuelekea Arusha ambako alikwisha andaliwa chumba katika hoteli ya kifahari ya Kobe village. Katika duka la Samia FashionPenny alifanya manunuzi makubwa na kurejea hotelini kwake

“ Dr Joshua safari hii amepania hasa kuusuuza moyo wangu na ndiyo maana ananifanyia mambo haya makubwa kiasi najihisi kama malkia.Atapata anachokitaka lakini na mimi nitakipata ninachokitaka na baada ya hapo mimi na yeye mkataba utavunjwa na nitaishi maisha ya hali ya juu kuzidi haya.” Akawaza Peny akiendelea kujaribisha mavazi aliyonunua.
“ safari hi sintofanya tena kosa nikipata tu nafasi namaliza kila kitu.Ninachotakiwa kufanya kwa sasa ni kumpa Dr Joshua penzi la kiwango cha juu ambalo hajawahoi kupewa na mwanamke yeyote chini ya jua .Ninafahamu udhaifu wake ulipo na hapo ndipo nitatumia kumshikia na kumfanya asifurukute na baadaya hapo yeye mwenyewe ataniachia njia na nitafanya ninachokitaka” akawaza.

***********

Jaji Elibariki akiwa ofisini kwake akapigiwa simu na katibu muhtasi wake na kumfahamisha kwamba kuna mgeni wake ambaye ni Anna mtoto wa rais.jaji Elibariki akatoa ruhusa aruhusiwe kuingia ofisini i.
“Shikamoo shemeji” akasema Anna ambaye uso wake ulionyesha dhahiri kwamba alikuwa na hasira
“ marahaba Anna.Hujambo? “ Sijambo “ akajibu kwa ufupi na kuvuta kiti akaketi “ Nimekuja kusikiliza ulichoniitia” akasema Anna kwa sauti ya juu kidogo
“ Anna nashukuru kwa kufika kwako.Nilikuwa na hofu pengine hutafika” akasema Jaji Elibariki “ Go straight to the point ,sina muda mwingi wa kukaa hapa” akasema anna kwa sauti iliyoonyesha dharau kidogo
“ Anna nimekuita hapa ili tuongelee kuhusiana na jambo liilotokea siku mbili zilizopita kuhusiana na kesi iliyomalizika iliyomuhusisha Penny.” Mara tu alipotamka jina la Penny ,Anna akabadilika usoni
“ Please !..

I don’t want to hear anything about penny” akasema anna kwa ukali.
“ Tafadhali naomba tuliza jazba Anna ili tuongee kwa undani kuhusu suala hili”
“Tuongee kuhusu nini tena ?Tayari umekwisha toa hukumu na muuaji umemuachia huru sasa unataka tuongee nini zaidi?
“ tafadhali naomba unisikilize Anna kile nilichokita hapa ” akasema Jaji Elibariki

“ Nitakusikiliza kama una lingine la kuniambia lakini si suala la hukumu uliyotoa ukamuachia muuaji.Hujui ni namna gani nilivyompenda Edson.Kitendo cha kumuachia huru muuaji aliyemuua mtu niliyempenda wakati kuna kila aina ya ushahidi kuthibitisha kwamba penny alimuua Edson kimenifanya nikutoe thamani kabisa na sina hakika kama unafaa kuwa mmoja wa wanafamilia yetu.Tulikutegemea utende haki lakini umepindisha haki ukampendelea Yule kahaba…..”

Akasema Anna na kumpandisha hasira Jaji Elibariki ambaye alisimama na kumnyooshea Anna kidole kwa hasira
“ Anna naomba iwe ni mara yako ya kwanza na ya mwisho kunionyeshea dharau namna hii.Nimekuita hapa kwa lengo zuri tu ili tuongee na tusaidiane kumpata muuaji wa Edson lakini wewe hutaki kunisikiliza na badala yake unanifanyia dharau.Nimechoka kuwavumilia wewe na familia yenu yote kwa dharau mnazonifanyia.Mimi ni jaji wa mahakama kuu na sifanyi maamuzi kwa shinikizo la mtu yeyote awe ni rais au nani.Ninatenda haki kwa kila mtu.Naomba vile vile iwe ni mwanzo na mwisho kumuita Penny kahaba.Mara nyingine ukithubutu kuja na kutoa matusi katika ofisi hii nitasahau kama baba yako ni rais wa nchi na nitakuharibu sura yako.Toka haraka ofisini kwangu !! ” akasema kwa hasira jaji Elibariki.

Aliku wa amekasirishwa mno na maneno aliyoyatamka Anna
“ Sawa ninaondoka lakini ukae ukijua kwamba huna muda mrefu katika kiti hicho ambacho umepewa tu kwa hisani ya baba yangu” akasema Anna huku akiondoka.Maneno yale yakazidi kumkasirisha sana jaji Elibariki.Alitamani amrukie na kumuadhibu vikali lakini akajitahdii kujizuia na kumuacha aondoke.

“ Dah ! Sijawahi kukutana nafamilia yenye dharau kama hii.Nilimuita kwa nia njema tu ya kuja kuongea masuala ya msingi ili tushirikiane kumbaini muuaji wa Robin lakini nimeambulia matusi na dharau.Sijawahi kudharauliwa kiasi hiki katika kazi yangu na sintokubali kamwe kuendelea kudharauliwa hasa na familia hii.” Akawaza jaji Elibariki huku amefura kwa hasira.Akachukua simu yake na kuzitafuta namba fulani akapiga “ Hallo Mathew” akasema Jaji Elibariki

“ hallo jaji.habari za siku? Leo umenikumbuka ndugu yangu lazima utakuwa na tatizo.”
“ Ni kweli nina shida ndugu yangu nahitaji kukuona” akasema Elibariki
“ Unataka tuonane saa ngapi?
“ sasa hivi.Uko wapi?
“ Niko nyumbani kwangu”
“ Ok njoo utanikuta lakini tafadhali naomba uje peke yako.Sitaki uwe umeambatana na mlinzi yeyote”
‘ Nitakuja mimi mwenyewe.dereva wangu ana matatizo ya kifamilia na nimempa likizo ya muda” akasema Elibariki
“ Good” akajibu Mathew na kukata simu.jaji Elibariki akainuka akavaa koti lake na kutoka “ It’s time for action now” akasema jaji Elibariki huku akiingia garini.
“Mbivu na mbichi lazimazijulikane katika kipindi kifupi” akasema kwa sauti ndogo

TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………
 
Back
Top Bottom