Peniela (Story ya kijasusi)

Peniela (Story ya kijasusi)

SEASON 2

SEHEMU YA 16

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPA

“ Huyu mzee anaonekana kifo cha mkewehakijamgusa kabisa.Hainiingii akilini eti hata mkewe hajamaliza siku moja kaburini tayari ameanza kufikiria masuala ya kuioa.laiti angenijua wala asingeongea upuuzi ule .Lakini mbona ninaanza kuingiwa na shaka sana kuhusiana na kauli hizi za Dr Joshua? Toka kipindi kile hata mkewe bado hajafariki alikuwa akinitamkia kwamba mke wake atakufa hivi karibuni na mimi nitakuwa first lady.Ninapatwa na wasiwasi kwamba ya wezekana kifo cha dr Flora kikawa ni cha kupangwa ili mambo anayoyataka Dr Joshua yaweze kutimia” akawaza peniela wakati aiingia chumbani.Akaiweka simu mezani na kupanda kitandani akajilaza pembeni ya jaji Elibariki

“ Elibariki kuna kitu nataka kukuuliza” akasema Peniela
“Uliza Penny”akasema Elibariki

“ Nini kilimuua Dr Flora? Akauliza Peniela na kumstua sana Elibariki

” kwa nini unauliza hivyo Penny?

“ Ninahitaji tu kufahamu” akasema Penny

“ Dr Flora alikufa kwa shinikizo la damu”

“ Are you sure? Akauliza penny

‘ yes I’m sure” akajibu jaji Elibariki na kuendelea kushangaa kwa nini Peniela alimuuliza maswali kama yale.



ENDELEA……………..



Peniela aliendelea kumtazama jaji Elibariki kwa macho malegevu huku akimsugua sugua kifuani.Alijisikia furaha sana moyoni
“ Haya ni maisha ambayo nimekuwa nikiyaota kila siku kuishi yaani kuwa na mtu wangu ambaye ninaamini ni wangu peke yangu ambaye nitakuwa nikilala naye na kuamka naye.Elibariki ameifufua ndoto yangu ya miaka mingi ambayo nimekuwa nikiota kumpata mwanaume wangu lakini kwa sababu ya Team SC41 imeshindwa kutimia.Safari hii lazima ndoto yangu iwe kweli lazima nimpate mwanaume ambaye moyo wangu utafunguka kwake.Nadhani Elibariki ni mtu anayenifaa sana japokuwa ni mume wa mtu lakini silijali hilo kwani yeye mwenyewe amekwisha onyesha kila dalili kwamba ananipenda na ndiyo maana pamoja na kilichotokea siku ile lakini bado amechagua tena kuja kukaa hapa kwangu.Amekwisha nitamkia kwamba ananipenda sana na hata mimi ninahisi kumpenda.Ni mwanaume mwenye vigezo vyote vya kuwa mume.Amenitamkia yeye mwenyewe kwamba kwa sasa yeye na mke wake wana mikwaruzano nadhani hii ni fursa pekee ya kuanza kuandaa mazingira ya kumuweka katika himaya yangu ili nitakapokamilisha tu opreseheni 26 B basi tayari kuwe na mzizi imara na nianze maisha mapya na Elibariki kwani sitaki tena kufanya kazi yoyote na Team SC41 na hata John amenihakikishia kama hataki tena mimi kuwa sehemu ya Team SC41 na baada ua kukamilisha opereshen 26B basi nitaanza maisha mapya.” Akawaza Peniela.

“ kwa mara ya kwanza leo hii umenifanya nibadili msimamo wangu.Ninataka kuendelea kuishi tena kwa sababu yako.Nataka niyatengeneze maisha yako upya kwani ni mimi niliyeyaharibu kwa kukuingiza huku Team SC41.”

Kauli hii ya John Mwaulaya ikamjia kichwani.Akafumba macho na kwambali akahisi macho yake yakiloa machozi

“ Kwa nini John aliamua kuningiiza katika Team SC41? Kwa nini hakuniacha nikaishi maisha yangu ya kawaida niliyokuwa nikitaji kuishi ? Ndoto yangu kubwa ilikuwa ni kuwa mtaalamu wa wanyama lakini badala yake nimeangukia katika mikono ya Team SC 41 na kufanya kazi ambazo sikuwahi kuota kuzifanya.” Peniela akageukia upande wa pili ili Elibariki asigundue kama analia .

“ Siwezi kuisahahu siku ile ,siku ambayo maisha yangu yaliharibika” akawaza Peniela na kumbu kumbu zikamrudisha mbali sana baada ya kumaliza kidato cha sita
Ni siku ya jumanne Peniela akiwa ametulia sebuleni katika jumba lake kubwa mara akapigiwa simu ya mmoja wa rafiki zake akimtaarifu kwamba matokea ya kidato cha sita yametoka.Haraka haraka Peniela akachukua kompyuta yake akafungua tovuti ya baraza la mithani la taifa na kutazama matokeo.Ilikuwa amefaulu vizuri sana kwa daraja la kwanza.Aliruka kwa furaha sana .
‘ Thank you Lord.Nilijua tu lazima nitafanya vizuri.Sasa ndoto zangu zinakwenda kutimia” akasema Peniela kwa furaha kubwa.
Jioni ya siku ile akapigiwa simu na kupewa pongezi na mfadhili wake John Mwaulaya .

“ Peniela pamoja na pongezi zote nilizokupa nina zawadi nyingine kwako.”

“ Zawadi gani baba? Akauliza Peniela ambaye alizoea kumuita John baba
“ Unakwenda kusoma nje ya nchi.Na tayari nimekwisha kutafutia chuo kizuri sana kinachotoa elimu bora.” Akasema John.Peniela akashindwa kuizuia furaha yake machozi yakamtoka
“ Ninashukuru sana baba kwa zawadi hii.Ni ndoto yangu kubwa sana kwenda kusoma nje ya nchi .Ninaamini zile ndoto zangu zote zinakwenda kutimia.” Akasema Peniela

“ Usijali Peniela kila kitu kitatimia.Kila kitu tayari kimekwisha andaliwa na safari ni jumatatu ijayo kwa hiyo anza kufanya maandalizi madogo madogo “ akasema John
Siku zilienda kwa kasi na hatimaye siku ya Peniela kuondoka nchini ikawadia.Ilikuwa ni siku yake yenye furaha sana na iliyojaa matumaini.Dege alilopanda lilipaa na kuiacha ardhi ya Tanzania .
“ Ningejua siku ile kama maisha yangu yatakwenda kubadilika kule Marekani nisingeingia katika ile ndege.” Akawaza Peniela na machozi yakamtoka na kumbu kumbu zimkamrejesha tena alipofika jijini New York Marekani
Donald Stevens alimpokea Peniela katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jf kennedy .
“ Karibu sana New York” akasema Donald na kumuongoza Peniela hadi katika gari moja la kifahari akafunguliwa mlango akaingia na moja kwa moja akapelekwa katika hoteli kubwa ijulikanayo kama The Plaza.Peniela hakukaukiwa na tabasamu kwa kila alichofanyiwa.Hakuwa ametegemea mapokezi yale makubwa aliyofanyiwa na kumfanya azidi kujiuliza huyu mfadhili wake John mwaulaya ni mtu wa namna gani hadi akamfanyia yale yote? Alikaa katika hoteli ile ya kifahari kwa siku saba akimsubiri mwenyeji wake Donald ili ampeleke katika chuo alichokuwa ameandaliwa.Wakati wote aliokuwa pale hotelini alikuwa akiwasiliana na John na kumfahamisha namna alivyopokelewa na namna anavyohudumiwa.
Ilikuwa ni siku ya jumatatu Donald alipomfuata Peniela pale hotelini na kumtaka achukue mizigo yake kwani anampeleka katika chupa alichokuwa ameandaliwa.Peniela alifurahi sana na kuchukua mizigo yake wakaelekea uwanja mdogo wa ndege wakapanda ndege ndogo ambayo ukiacha na rubani abiria walikuwa ni wawili tu peniela na Donald.
Ndege le ilitua katika uwanja mmoja mdogo wa ndege wakashuka.Kulikuwa na majengo kadhaa mahala pale na palionekana kama chuo Fulani.Vijana wawili waliovalia nadhifu wakampokea Peniela mizigo yake na kuondoka nayo halafu yeye na Donald wakaelekea katika jengo moja la ghorofa tatu.ndani ya jengo lile wakaingia katika ofisi moja kubwa iliyokuwa kama chumba cha mikutano na kuwakuta watu zaidi ya saba wakiwa wameizunguka meza na ilionekana wazi kwamba walikuwa wakimsubiri Peniela awasili.Mara tu Peniela alipoingia ndani ya kile chumba wakasimama na kusalimiana naye kwa heshima na kisha akakaribishwa kiti pale mezani.Bado Peniela alikuwa akishangaa sana kwa namna watu walivyokuwa wakimnyenyekea na mwanzoni alidhani labda watu wale walikuwa ni wakuu wa chuo alichokwenda kukisoma.

“ Peniela karibu sana ,hapa ni chuo cha mafunzo cha Team SC41 “akasema mzee yule aliyefahamika kama Michael macksons .

“ team SC41 ? Peniela akashangaa.
“Ndiyo hapa uko katika chuo cha Team SC41” akajibu Michael

“ Sikuambiwa kama ninakuja kusoma katika chuo hiki.Hapa mnatoa kozi gani? Akauliza Peniela kwa mshangao
“ Kuna kozi nyingi zinazotolewa hapa lakini nakuomba usiwe na haraka sana na utafahamishwa kila kitu”
Peniela alianza kueleweshwa kuhusu team SC41 ilivyo ,nia na madhumuni yake vilevile na faida yake kwa Marekani na kwa nchi ambazo zina vikosi vya team SC41.Pamoja na maelezo mengi aliyopewa lakini Peniela alishindwa kukubaliana nao na hakutaka kuendelea kukaa pale akaomba wamruhusu aondoke kwani kilichompeleka marekani ni kusomea masuala ya wanyama na si kusomea mambo ya Team SC41.

“ Juhudi za kumashawishi Peniela akubali kujifunza masuala ya Team SC41 zilishindikana ikawalazimu kutumia nguvu.Waliitwa watu wawili wakamchukua Peniela na kwenda kumfungia katika kiti Fulani katika chumba kilichokuwa na mitambo mingi.Kilichofuata hapo taa zikazimwa na chumba chote kikawa giza.Peniela hakujua chochote kilichoendelea baada ya hapo kwani alifumbua macho na kujikuta akiwa amelala katika chumba kimoja na wasichana wawili mmoja wa kijapani na mwingine mzungu.Hawa walikuwa rafiki zake na kwa pamoja wote walikuwa wakijifunza kuhusiana na Team SC41.

“ Sielewi watu wale walinifanya nini kwani nilipofumbua tu macho sikuwa tena na ule upinzani wangu niliokuwa nao kabla ya kuingizwa katika chumba kile.Nilijikuta nikitamani sana kuifahamu Team SC41.Lakini ninaamini kuna kitu wale jamaa walinifanyia ndani ya kile chumba .Walicheza na akili yangu .Pale ndipo waliponiharibia maisha yangu kwani baada ya kutoka ndani ya kile chumba sikuwa ni mimi Peniela wa zamani.Nilijiona kama mtu mpya kabisa mwenye mawazo mapya.Nilijisikia fahari kuwa mmarekani na sikutaka kabisa kuitwa Mtanzania.They destroyed me” akawaza Peniela na kushindwa kujizuia kulia kwa kwikwi na kumstua jaji Elibariki aliyekuwa pembeni yake

“ Peniela kuna nini? unalia nini ? Akamuuliza jaji Elibariki na kumeuza Peniela akamtazama usoni.Macho yake yalikuwa yameloa machozi

“ Unalia nini Peniela? Una tatizo lolote Penny? Tafadhali nieleze nini kinakuliza? Akasema jaji Elibariki.Peniela akafuta machozi na kusema
“ Elibariki nimekuwa nikiwaza sana kuhusiana na maisha yangu na namna ulivyonitendea nikajikuta nikishindwa kujizuia kuangusha machozi.Ninawaza nini nitakuiipa kwa wema wako ule ninashindwa kupata jibu” akadanganya Peniela

“ Ouh Peniela come here” akasema jaji Elibariki na kumkumbatia Peniela.

“ Hutakiwi kudondosha machozi Peniela.Uso huu wa kimalaika unatakiwa kuwa na furaha wakati wote.Niliweza kukuachia huru wakati ule kwa sababu niliamini kwamba hukutenda lile kosa.Wengine walikuwa wakikutazama kwa macho ya kawaida lakini mimi nilikuwa nikikutazama kwa macho ya moyoni na ndiyo maana pamoja na ushahidi wote uliotolewa mahakamani ambao ungeweza kukutia hatiani lakini bado niliweza kufanya maamuzi yale niliyoyafanya na nilifanya vile kwa sababu mbili .Moja ni kwa sababu hukutenda kosa na pili ni kwa sababu moyo wangu tayari ulikwisha kupenda.Peniela niamini kwamba nilikupenda sana toka siku ya kwanza nilipokabidhiwa kesi yako.Nilipokuona tu mahakamani moyo wangu ulistuka sana na nikajua kwamba wewe ndiye yule ambaye uliumbwa kwa ajili yangu.Niliumia sana kwa wewe kuendelea kukaa mahakamani na ndiyo maana kesi yako haikuchukua muda mrefu kama kesi nyingine.Sikutaka uendelee kuteseka mahakamani”akasema jaji Elibariki
“ Elibariki nashukuru sana na sina neno zuri la kuweza kusema ahsante lakini ni Mungu pekee anayeweza kujua namna moyo wangu unavyokushukuru.Lakini naomba nikuulize swali moja dogo sana”

“ Uliza Penny”
“ Endapo ungeridhika kwamba nina hatia na kweli nimeua ungenifunga gerezani?
Swali lile likambabaisha kidogo jaji Elibariki akatabasamu na kusema

“ Peniela swali lako gumu lakini zito sana.Walisema kwamba mapenzi ni upofu na katika penzi kila kitu kinawezekana.kwa kuwa tayari moyo wangu ulikwisha niambia kwamba wewe ndiye yule ambaye ninaaminini mtu sahihi kwangu basi nisingekupa adhabu yoyote.Ningekuachia huru hata kama ungekuwa na hatia.Ningepindisha sheria ili kuhakikisha kwamba unakuwa huru.”

“ real ?! akauliza Peniela kwa mshangao

“ Ndiyo nigefanya hivyo.Siwezi kumuacha mwanamke ninayempenda afungwe gerezani .Niko tayari kwa lolote lile kwa sababu ya mtu ninayempenda”akasema jaji Elibariki na kuufanya mwili wa Peniela usisimke sana.Peniela akamkumbatia kwa nguvu na kumpa busu zito

“ Ahsante Mungu.Huyu ndiye mwanaume niliyekuwa nikimuota.Mwanaume ambaye yuko tayari kufanya lolote kwa ajili yangu.mwanaume ambaye yuko tayari kuipoteza furaha yake kwa sababu yangu.Elibariki ndiye mtu sahihi kwangu na ambaye ninataka kuanza maisha mapya nikiwa naye.”akawaza Peniela.
“ Elibariki bado kuna swali naomba nikuulize” akasema Peniela

“ Uliza kitu chochote Peniela usihofu”

“ Do you love your wife?
Ilimchukua zaidi ya dakika moja jaji Elibariki kulijibu swali lile

“ Peniela nilikwambia kwamba maswali yako madogo lakini mazito sana.Kwa ufupi ni kwamba nilikutana na Flaviana wakati tukiwa chuoni.Mimi nilikuwa nasomea shahada ya pili ya sheria na yeye alikuwa shahada ya kwanza.Mazingira ya kukutana kwetu yalikuwa ya kiajabu sana kwani nilikutana na Flaviana katika sherehe ya kuwakaribisha wanachuo wapya.Siku hiyo Flaviana alilewa sana pombe na rafiki zake wakaniomba nimsadie kumbeba na kumpeleka chumbani kwake.Nilifanya hivyo na kesho yake akanitafuta kunishukuru kwa msaada wangu ule.Huo ukawa ni mwanzo a kujuana kwetu na hadi tukafikia hatua ya kufunga ndoa.Kukujibu swali lako ni kwamba ninaishi katika kiapo cha ndoa lakini si kila anayeapa kanisani ana mapenzi ya kweli na mwenzake.Hata mimi sina hakika kama kilichokuwepo wakati ule tunaapa kanisani kipo hadi leo hii.Sina hakika kama tunapendana kweli” akasema Jaji Elibarii

“ Elibariki nimekuuliza swali ambalo jibu lake ni fupi tu .Ulipaswa kunjibu ndiyo au hapana na si kutoa historia.Nataka kusikia kwa ulimi wako je unampenda mkeo? Akauliza Peniela

“ I’m not sure if I still love her” akajibu jaji Elibariki

“ Ahsante sna ,hilo ndilo jibu nillokuwa nataka kulisikia toka kwako.Naomba sasa ulale upumzike Elibariki.Ninakupenda sana
“ akasema Peniela na kumbusu .Halafu akachukua zile namba za simu za daktari alizopewa na John akaziandika katika simu yake akatoka mle chumbani na kupiga.Simu ikaita na baada ya muda ikapokelewa

“ hallow” ikasema sauti ya mwanamke upande wa pili

“ hallow.Naongea na nani” akasema Peniela
“ Unaongea na Dr Christine .Wewe ni nani mwenzangu? Akauliza Dr Christne

“ Ninaitwa Peniela ninapiga simu toka Tanzania.Dr Christine uko wapi?
“ Niko nchini Israel .Nikusaidie nini Peniela? Akauliza Dr Christne
“Nimepewa namba zako na John Mwaulaya”
“ John Mwaulaya? Akauliza Christine

“ Unamfahamu John?

“ Ndiyo ninamfahamu sana John japokuwa ni muda mrefu hatujawasiliana.Anasemaje John ?

“ John anaumwa sana kwa sasa.Ana tatizo katika mishipa ya fahamu na anahitaji msaada wa matibabu na amenitaka niwasiliane nawe nikueleze hivyo”

“ Ouh masikini John.Ninalifahamu tatizo lake kwa muda mrefu na anahitaji kufanyiwa upasuaji na nililimshauri kwa muda mrefu lakini hakuwa tayari kuusikia ushauri wangu.”

“ Dr Christine naomba umsaidie John.Kwa sasa yuko tayari kufanyiwa upasuaji.Tafadhali sana naomba umsaidie .Hali yake si nzuri hata kidogo”

“ Wewe ni nani wake?

“ Mimi ni mtoto wake.Ninaitwa Peniela”

“ Mtoto wake? John Mwaulaya hakuwahi kunitamkia kama ana mtoto “

“ Mimi ni yatima na amekuwa akinilea toka nikiwa mtoto mdogo kwa hiyo nimamuheshimu kama baba yangu.”
“ Ok vizuri kwa kuwa sasa hivi niko likizo basi nitakuwa na nafasi nzuri ya kuja kumuangalia ,nitawaomba wataalamu wengine wawili waongozane nami kuja kumshughulikia John.Lakini kuna kitu ambacho nitakihitaji ili kuweza kufanya upasuaji huo”
“ sema chochote Dr Christine” akasema Peniela

“ Ntahitaji kufanya upasuahi huo katika hospitali kubwa yenye vifaa vya kufankisha upasuaji huo kwa hiyo mwambie John kwamba aanze kufanya mipango kutafuta hospitali ambayo tutaitumia kwa upasuaji huo” akasema Dr Christine na kuagana na Peniela akamuahidi kumpigia simu mara tu atakapokamilisha taratibu za safari ya kuja Tanzania

“ Ahsante sana Mungu .Leo imekuwa ni siku nzuri sana na kila kitu kinakwenda vizuri.Kuhusu suala la hospitali hakuna shida nitaongea na Dr Joshua.Kwangu hana kauli na anawea kufanya kila jambo kwa ajili yangu.Kwa sasa nina hakika John atakuwa mzima.Bado nina mambo mengi sana ambayo ninahitaji kuyafahamu toka kwake. “ akawaza Peniela


******



Ni saa tano na nusu za usiku,Gari moja aina ya BMW lenye rangi nyeusi linawasili katika makazi ya John Mwaulaya na kufunguliwa geti.Toka ndani ya gari lile wakashuka watu wawili mwanamke na mwanaume na kisha wakaongozwa na Josh hadi katika chumba cha John mwaulaya.John mwaulaya aliyekuwa amekaa kitandani akijisomea kitabu chake uso wake ukachanua kwa tabasamu baada ya kuwaona watu wale wawili
“ hallow John” akasalimu yule mwanaume

“ Captain Amos hujambo kijana wangu?

“ Sijambo mzee vipi maendeleo yako ?
“ninamshukuru Mungu ninaendelea vizuri sana kwa sasa .” akasema John na kumtupia macho yule mwanamke alyekuwa ameambatana na Captain Amos
“ Jesica hujambo mama ? Akasema John

“ Sijambo mzee shikamoo”

“ Marahaba .karibuni sana vijana wangu.Nimefurahi sana kuwaona.Natumai mmekuja na habari nzuri zenye matumaini” akasema John mwaulaya.Captain Amos na Jesica wakavuta viti na kuketi kandoni mwa kitanda cha john
“ Mzee ni muda kidogo umepita hatujaleta ripoti yoyote lakini leo hii tumekuja na ripoti nzuri yenye kutia matumaini” akasema captain Amos

“ Operesheni inakwenda vizuri sana japokuwa kumekuwa na vizingiti vya hapa na pale.Kuna watu ambao walilifahamu jambo hili na kutaka kulivuruga.Wa kwanza alikuwa ni Dr Flora mke wa Dr Joshua .Huyu aliambiwa kinachoendelea na mume wake na akataka kuwaeleza mabinti zake lakini rais alilifahamu hilo na akaamuru tumuwahi kabla hajawaeleze wanae kitu kinachoendelea.Dr Flora tulimuondoa lakini kikaibuka tena kikwazo kingine,kuna mtu alifanya uchunguzi wa nini kilichomuaa Dr Flora na kugundua kwamba alichomwa sindano ya sumu.Huyu ni jaji wa mahakama kuu na amemuoa mtoto mkubwa wa rais.Rais aliogopa kwamba jaji Elibariki anaweza kuwa hatari na akaamuru tumuue lakini nilimpa maelekezo Jessica ahakikishe kwa namna yoyote ile jaji Elibariki hauawi kwani ni mtu muhimu sana kwetu na tunaweza tukamtumia.Jesica alilifanikisha hilo na kufanikiwa kumuokoa Elibariki.Labda kwa kukufahamisha tu ni kwamba huyu ndiye jaji ambaye alimuachia huru Peniela”

“ Good Job Jessica.Ulifanya vizuri sana kutomuua.Huyu jaji anaweza akawa ni msaada mkubwa sana kwetu.Yukowapi sasa hivi?
“ Nilipomuokoa nilimtaka anieleze sehemu ipi anadhani inaweza kuwa salama sana kwake kujificha na moja kwa moja akachagua kwa Peniela.Kwa hivi sasa yuko kwa Peniela”

“ Peniela?! John mwaulaya akastuka
“ Ndiyo yuko kwa peniela.Inavyoonekana kuna kitu kinaendelea kati yao na ndiyo maana Elibariki akachagua kwenda kujificha pale”

“ Mna hakika kwa Peniela ni sehemu salama ambayo Elibariki hatagundulika? Kwa sasa vyombo vya usalama vitakuwa vikimtafuta katika kila kona je itakuwaje iwapo atagundulika yuko pale? Sitaki Peniela apatwe na tatizo lolote”

“ Usiogope mzee suala hili liko ndani ya uwezo wetu na endapo kutatokea jambo lolote lile la kuhatarisha usalam a Peniela basi tutalishughulikia” akasema Captain Amos

“ Ok good,operesheni 26B inakwendaje?

“ Operesheni inakwenda vizuri.Jioni ya leo rais ametuita mimi na Dr Kigomba na kutueleza kwamba kwa kuwa kumeanza kujitokeza vikwazo kadhaa katika biashara ile kwa hiyo ameamua kwamba biashara ifanyike haraka sana .Amesema ataongea na wale wanunuzi ili wajiandae na baada ya wiki mbili wawe tayari mchakato wa mauziano uanze.Hii ni fursa yetu ya kuikamilisha operesheni yetu.”

“ Good Job Amos.Mmefanya kazi nzuri sana.Mpaka sasa hvi hakuna wasiwasi wowote kwamba wewe na Jessica ni sehemu ya team SC41? Hawajawatilia shaka yoyote? Akauliza John
“Dr Joshua tayari ameanza kuwa na hisia kwamba kuna mtu anayetoa habari.Tukio la kunusurika kwa jaji Elibariki limempa wasiwasi sana na anahisi kwamba huenda vijana tunaowapa kazi kuna mmoja wao atakuwa amevujisha siri kwa Elibariki na kumfanya atoroke.Ameamuru uchunguzi ufanyike lakini hakuna watakachoweza kukifahamu kwa hiyo usitie shaka kuhusu jambo hilo.Hawataweza kamwe kugundua chochote kuhusu sisi “

“ Ok vizuri sana Cap[tai Amos kwa hiyo nini kinafuata i?
“ Kuna kitu ambacho tunatakiwa tukifanye” akasema Captain Amos.Akamtazama John kisha akaendelea

“ Ni Dr Joshua pekee ambaye anafahamu mahala mzigo ule ulipo . Atauchukua mzigo ule halafu atamkabidhi Dr Kigomba ambaye atauficha na yeye ndiye atakayefanya makabidhiano yote na wanunuzi.Kitu ambachotunatakiw a kukifanya kwa sasa Peniala anatakiwa aanzishe mahusiano ya haraka sana na Dr Kigomba”
“ Again?! Mahusiano mengine tena? Akauliza John
“ John ili tuweze kufanikisha operesheni hii tunamuhitaji sana Peniela.Bila yeye hatuwezi kuimaliza operesheni hii.Please I beg you John.Najua unampeda sana Peniela lakini katika hili hakuna namna tunavyoweza kufanikiwa bila ya Peniela.” Akasema Captain Amos.John akafumba macho akawaza na kusema

“ ok hatuna namna nyingine ya kufanya .Itabidi afanye hivyo” akasema John


TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
 
EASON 2


SEHEMU YA 17


ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Ok vizuri sana Captain Amos kwa hiyo nini kinafuata i?

“ Kuna kitu ambacho tunatakiwa tukifanye” akasema Captain Amos.Akamtazama John kisha akaendelea
“ Ni Dr Joshua pekee ambaye anafahamu mahala mzigo ule ulipo . Atauchukua mzigo ule halafu atamkabidhi Dr Kigomba ambaye atauficha na yeye ndiye atakayefanya makabidhiano yote na wanunuzi.Kitu ambachotunatakiw a kukifanya kwa sasa Peniala anatakiwa aanzishe mahusiano ya haraka sana na Dr Kigomba”

“ Again?! Mahusiano mengine tena? Akauliza John

“ John ili tuweze kufanikisha operesheni hii tunamuhitaji sana Peniela.Bila yeye hatuwezi kuimaliza operesheni hii.Please I beg you John.Najua unampeda sana Peniela lakini katika hili hakuna namna tunavyoweza kufanikiwa bila ya Peniela.” Akasema Captain Amos.John akafumba macho akawaza na kusema
“ ok hatuna namna nyingine ya kufanya .Itabidi afanye hivyo” akasema John


ENDELEA…………………


Baada ya Captain Amos na Jessica kuondoka John Mwaulaya alibaki katika mawazo mengi sana.Suala la kutakiwa kumruhusu Peniela aingie katika mahusiano mengine na katibu wa rais Dr Kigomba lilimchanganya sana akili yake.

“ Amos amenichanganya sana kwa kutaka Peniela aingie katika mahusiano mengine tena na Dr Kigomba .Kwa sasa Peniela amekuwa ni kama chombo cha starehe ,mwiliwake umekuwa ukitumika kama silaha ya kufanikisha mipango ya Team SC41.Ninaumia sana kwa kumfanya Peniela namna hii.” Akawaza John
“ Lakini kwa hapa tulipofikia tuko mwishoni mwa operesheni yetu na hakuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kukubali Peniela aingie katika mahusiano mengine na Dr Kigomba.Ninaumia sana lakini sina namna nyingine.Nitahakikisha baada ya operesheni hii kumalizika ninamfanyia Peniela mambo makubwa kulipia yale mambo ambayo nimemfanyia.Nitayatengeneza upya maisha yake.Nitamfanya awe ni mwenye furaha na hata kama nikifa basi niwe nimuacha Peniela ni mwenye amani na anayafurahia maisha yake tofauti na sasa ambapo amekuwa ni kama chombo kinachotumika ili kuwastarehesha watu na kufanikisha mipango ya Team SC41.Lazima nimuondoe katika kundi hili pindi tu operesheni hii itakapokamilika.” Akawaza John halafu akabonyeza kitufe cheusi kilichokuwa chini ya kitanda chake na Josh mlinzi wake akaingia.

“ Josh naomba uwasiliane na Peniela na mwambie kwamba ninahitaji kumuona kesho saa tatu za subuhi “ akasema John na kumpatia Josh namba za simu za Peniela na bila kupoteza wakati Josh akampigia simu .
Peniela akiwa kitandani na jaji Elibariki mara simu yake ikaita akainuka na kwenda kuipokea.Namba zlizoonekana katika kioo cha simu zilikuwa ngeni kabisa katika simu yake

“ hallow” akasema penny

“ hallow peniela,ni Josh hapa ninaongea kutoka kwa John Mwaulaya”

“ Ouh Josh,habari yako? Kuna nini hadi ukanipigia usiku huu?

“ Nimeelekezwa na John nikwambie kwamba anahitaj kukuona kesho saa tatu asubuhi hapa nyumbani kwake”
“ Ok ahsante sana kwa taarifa nitafika muda huo.Hali yake inaendeleaje?
“ Hali yake inaendelea vizuri “ akajibu Josh na kukata simu .



*******


Kumekucha tena Tanzania na habari kubwa magazetin i bado ilikuwa ni ya kupotea kwa jaji Elibariki .Peniela kama kawaida yake aliamka asubuhi na mapema akafanya mazoezi halafu akafanya usafi wa nyumba na kumuandalia jaji Elibariki kifungua kinywa.

“ Najisikia furaha sana kuamka asubuhi na kumuandalia Elibariki kifungua kinywa.Natamani kama maisha yangu yangekuwa namna hii ningefurahi sana.Hata hivyo nina tumaini siku moja na mimi nitaishi maisha ya kawaida kama wenzangu.Nitaamka asubuhi na kumuandalia kifungua kinywa mume wangu na kama Mungu akinijalia nitakuwa na watoto wawili .Hayo ndiyo maisha ambayo nimekuwa nikiota kuyaishi kwa miaka mingi kabla ya kuingia katika kundi hili la Team SC41.” Akawaza Peniela wakati akiendelea na kuandaa mlo wa asubuhi. Alipomaliza akamfuata jaji Elibariki chumbani akiwa amebeba sinia llilosheheni mlo wa asubuhi.

“ Wake up Elibariki.Its a new day “ akasema Peniela akiwa na uso uliopambwa na tabasamu zito.jaji Elibariki akatabasamu
“Ahsante sana Peniela kwa kunijali.Sijawahi kujaliwa kama unavyonijali.”
“ Usijali Elibariki.Unastahili kupewa kila aina ya huduma.Amka upate kifungua kinywa” akasema peniela .

“ Nashukuru sana Peniela” akasema jaji Elibariki na Peniela akamuandalia kifungua kinywa pale pale kitandani.
Kisha pata kifungua kinywa jaji Elibariki akaingia bafuni kwa ajili ya kujimwagia maji,alihisi joto.Wakati akiendelea kuoga Peniela akaingia na wakaoga pamoja .Kisha oga Peniela akajindaa kwa ajili ya kuelekea kwa John Mwaulaya.
“ Elibariki nitakuacha tena kwa siku ya leo kwa masaa machache kuna mahala nitaelekea lakini sintakawia sana.Kuna mtu ambaye ninahitaji kumuona “ akasema Peniela

“ usihofu Peniela.Unaweza ukaendelea na shughuli zako wala usiwe na wasi wasiwowote na mimi.”

“ Nashukuru sana Elibariki kwa kunielewa .Nitakapotoka huko nitapita kununua mahitaji kwa ajili yetu.” Akasema Peniela na simuyake ikaita akataarifiwa kwamba dereva atakayemchukua kumpeleka kwa John Mwaulaya tayari amekwisha wasili.Peniela akamsogelea Elibariki akambusu na kutoka mle chumbani
“ Dah ! Peniela ameniteka akili yangu yote.Ni mwanamke mrembo sijapata kuona na mambo anayonifanyia yanazidi kunipagawisha na kunifanya nisitake hata kuondoka hapa kwake.Nitafanya nini ili niweze kuwa na huyu msichana? Nina hakika huyu ndiye mwanamke ambaye ninatakiwa kuwa naye maishani.Ana kila kitu ninachokihitajikwa mwanamke ninayemuhitaji katika maisha yangu.Peniela yuko tofauti sana na Flaviana na wanawake wengine.Pamoja na uzuri wake lakini hana dharau,ana adabu na anajali kupita kiasi,anajua kuliwaza na hata mapenzi mamboyale ya kitandani amebobea vilivyo..Flaviana hajawahi kunifanya mambo kama haya anayonifanyia Peniela .” akawaza jaji Elibariki akiwa dirishani akichungulia nje kulikokuwa na bustani nzuri .

“ laiti kama ningeweza kuitengua ndoa yangu ili niweze kuishi na peniela ningefurah I sana.lazima nikubaliane na ukweli kwamba ndoa yangu kwa sasa inapumulia mashine.Ndoa yangu haina uhai mrefu.Hilo ni jambo ambalo siwezi kupingana nalo.Ni wakati sasa wa kuchukua maamuzi magumu kwa ajiliya kuitafuta furaha ya maisha yangu.Lazima nifanye kila linalowekana ili niweze kuwa na Peniela.Najua ni suala lenye changamoto nyingi lakini nitakabiliana nazo tu.Siwezi kuendelea kuishi maisha ya maigizo ,tukiigza kwamba tunapendana na ndoa yetu ina fuaha na amani wakati ukweli ni kwamba mapenzi hakuna katika ndoa yetu tofautina watu wanavyofikiri.Lazima nifanye maamuzi.Lazima nifanye kila linalowezekana niachane na Flaviana.Ninahitaji mwanamke ambaye atanipenda na kunijali kama anavyonijali peniela.Nahitaji mwanamke ambaye atakuwa tayari kunizalia mtoto.Umri unazidi kwenda na Flaviana mpaka leo haonyeshi dalili zozote za kutaka kunizalia mtoto.Nimechoshwa na maisha haya.” Akawaza jaji Elibariki.

“ japokuwa ninampenda Peniela na nina hakika moyovvvh wangu umemkubali lakini bado ninahitaji sana kumfahamu vizuri.Nahitaji kujua anakwendaga wapi kila siku? Anakwenda kuonana na nani? Halafu mbona kuna baadhi ya simu akipigiwa huwa hataki kuongelea mbele yangu? Kuna kitu gani anakificha? Jioniya leo lazima nitamuuliza kuhusiana na mambo haya.Mimi nimekuwa huru kumueleza kila kilichomo moyoni mwangu lakini kuna vitu ambavyo amekuwa akinificha ficha.Lazima nimuulize jioni ya leo ili nimfahamu kwa sababu muda si mrefu nitafanya maamuzi magumu kwa sababu yake.” akawaza jaji Elibariki na picha za shambulio lile ikamjia kichwani

“ Natamani sana kufahamu kinachoendelea huko nje.Natamani sana kufahamu kama watu waliofanya shambulio lile wamekamatwa au bado.Natamani kuwasiliana na watu wangu wa karibu lakini siwezi kufanya hivyo.Yule mwanamke aliyeniokoa alinikataza kuwasha simu yangu kwa sababu za kiusalama.Lakini nitaishi hivi hadi lini? Nitaendelea kukaa humu ndani hadi lini? Lazima juhudi zifanyike ili kulimaliza suala hili na mimi niweze kuwa huru.Suala hili litamalizwa kwa kuwapata watu waliofanya jambo hili na mtu pekee anayeweza kufanya kazi hii ni Mathew.Nitawasiliana naye jioni ya leo ili niweze kufahamu maendelo yake na kama Noah amekwisha zikwa ama bado.” Akawaza jaji Elibariki


*******


Peniela aliwasili katik a makazi ya John Mwaulaya na kupokelewa na Josh na kisha akamuongoza hadi ghorofani chumbani kwa John .

“ karibu tena Peniela.Nimefurahi sana kukuona tena” akasema John
“ Ninashukuru john ,hata mimi nimefurahi kupata nafasi ya kukuona tena baba yangu.Mungu ni mkubwa kwa sababu kila siku afya yako inazidi kuboreka na uso wako unaonyesha nuru “ akasema Peniela na kukaa katika kitanda cha John

“ unajisikiaje leo? Akauliza Peniela
“Ninajisikia vizuri sanaPeniela.maendeleo yangu si mabaya.Ninaanza kupata nguvu kidogo kidogo. Kwa leo ninaweza hata kunyanyua mguu “ akasema John Mwaulaya

“ Nafurahi sana kusikia hivyo .Hizo ni habari nzuri za kutia matumaini,halafu baba sijamuona Osmund kuanzia jana na nikashangaa nilipopigiwa simu na Josh jana usiku badala ya Osmund.Ossy Amesafiri? akauliza Peniela.John akamtazama Peniela kwa makini usoni na kumwambia

“ Osmund hayuko tena na sisi.He’s dead”
“ Ouh jamani.Nini kimemuua?! Peniela akastuka sana
“ Osmund alifanya makosa makubwa sana ambayo yameigharimu Team SC41 kwa hiyo ilimlazimu kuondolewa kwani hakufaa katika uongozi.”

“ This is weird John.Is this how team SC41 works? Mtu akikosea anauliwa? Akauliza Peniela

“ Hapana si hivyo Peniela lakini kuna sababu nyingine ambayo ilipelekea pia auawe”

“Ni sababu gani hiyo? Na yule daktari aliyesema anakuja kukuangalia Dr Burke yuko wapi? Haji tena? Akauliza Peniela

“ Dr Burke naye hatuko naye.Naye amefariki pia”

“ John whats going on? Kwa nini watu wawili wote wamekufa kwa wakati mmoja? Kuna kitu gani hapa?

“ Peniela siwezi kukuficha kitu ukweli ni kwamba Dr Burke alikuwa anakuja kwa lengo la kunai kuniua na si kuja kuchunguza afya yangu.?

“ kukuua? Peniela akashangaa

“ Kukuua kwa kosa lipi ?

“ Peniela naomba tuachane na mambo hayo yana historia ndefu.Vipi wewe maendeleo yako? Unaendeleaje? Maisha yako yanaendeleaje?
“ Mimi ninaendelea vizuri sana na maisha yangu pia yanaendelea vizuri.Hofu kubwa iko kwako.Lakini hata hivyo nimekuja na habari njema .Jana nimeongea na Dr Christine kumbe anakufahamu sana na tatizo lako analifahamu pia.Anasema kwamba siku nyingi amekuwa tayari kukufanyia upasuaji lakini wewe hukuwa tayari hata hivyo baada ya kumueleza hali yake amesema kwamba anajiandaa kwa safariya kuja Tanzania yeye na wataalamu wenzake watatu kwa ajili ya kuja kukufanyia upasuaji.Hata hivyo kitu ameombakifanyike kabla hajafika”
“Nashukuru sana Peniela.Ni kweli mmi na Dr Christine tunafahamiana kwa miaka mingi na ni kweli alikuwa tayari kunifanyia upasuaji lakini mimi sikuwa tayari kwa sababu sikuwa na tumaini la kupona.Kwa sasa ninataka niendelee kuishi kwa sababu yako.Ameomba kitu gani kifanyike?
“ Anataka tutafute hospitali ambako uasuaji huo utafanyika.Anasema kwamba anahitaji hospitali kubwa ambayo itakuwa na vifaa vya kumuwezesha kuufanya upasuaji huo.”
“ Mhh ! kitu anachokiomba ni kigumu sana na hakiwezekani. Wewe ulimjibu nini? Akauliza John

“ Relax father.Jambo hili liko ndani ya uwezo wangu na nitalishughulikia.Tutapata hospitali nzuri na yenye vifa anavyovihitaji Dr Christine.Nitafanya kila niwezalo hadi nihakikishe kwamba umekuwa mzima tena”akasema Peniela na kuufanya uso wa John ujenge tabasamu.
“ Ninashukuru sana Peniela.Bado naendelea kusisitiza kwamba nina deni kubwa kwako.Nina kazi kubwa ya kufanya kuyajenga upya maisha yako.Sitaki uendelee kuishi maisha ya namna hii.Nitayafanya maisha yako yawe mazuri sana yenye furaha na amani tofauti na maisha unayoishi sasa hivi” akasema John.
“ Ahsante sana John” akasema Peniela na baada ya muda John akasema

“ Peniela nimekuita kuna jambo ambalo nataka nikufahamishe.Ni kuhusu operesheni 26 B” akasema John akatulia na kumtazama Peniela kwa muda halafu akasema
“ Mambo yamebadilika kidogo katika operesheni ile na inaweza ikawa na urahisi kwetu tofauti na tulivyokuwa tumetegemea.Jana Captain Amos na Jessica wamekuja kuniona na kunipa taarifa nzuri za maendeleo ya operesheni yetu.Ni kwamba rais Dr Joshua tayari ameamua kufanya kuuza ule mzigo kwa kwa haraka zaidi baada ya kuingiwa na wasi wais kutokana na vikwazo ambavyo vimeanza kujitokeza.Usiku wa jana alikuwa na kikao na Captain Amos pamoja na katibu wake Dr Kigomba na kukubaliana kwamba ndani ya mwezi huu biashara ifanyike.Ana wasi wasi kuna watu tayari wamekwsha fahamu kinachoendelea.Ni Dr Joshua pekee anayefahamu mahala mzigo ulikofichwa ndani ya ikulu kwa maana hiyo basi atauchukua mzigo ule na kumkabidhi Dr Kigomba ambaye ndiye atakayefanya makabidhiano yote na wanunuzi kwa niabaya rais.Kwa hiyo basi kuna jambo ambalo lazima tulifanye japokuwa ni gumu na japokuwa siafikiani nalo lakini lazima lifanyike ili tuweze kuikamilisha operesheni hii.” Akasema John na kumtazama Peniela
“Hizo ni habari njema sana.Ni afadhali operesheni hii ikafikia ukingoni.Nina hamu sana ya kutaka kuishi maisa mapya.Ni jambo gani hilo ambalo ni lazima tulifanye ambalo huafikiani nalo?

“Peniela ,unatakiwa uinge katika mahusiano na Dr Kigomba “ akasema John na kimya kikatanda mle chumbani wakabaki wakitazamana.Baada ya muda John akasema
“ Peniela sikuwa tayari kwa wewe uingie tena katika mahusiano mengine lakini hatuna namna nyingine ya kufanya ili tuweze kuupata mzigoni zaidi ya kuingia katika mshusiano na Dr Kigomba. Inaniuma sana Peniela.Ninaumia sana kuyafanya maisha yako yawe namna hii na ndiyo maana nikasema kwamba nina deni kubwa kwako la kuhakikisha kwamba ninayatengeneza upya maisha yako ambayo ni mimi ndiye niliyaharibu.Ni mimi ndiye niliyepoteza ndoto zako zote za maisha kwa kukuingiza katika Team SC41.” Akasema John kwa uchungu.Peniela akamtazama halafu akasema

“ Usisikitike sana nitafanya hivyo.Ninatamani sana hata jambo hili limalizike leo ili na mimi nianze maisha yangu mengine kama ulivyoniahidi.Nitaingia katika mahusiano na Dr Kigomba kwa kusudi moja tu la kukamilisha operesheni hii.Nitaomba kabla ya kukutana naye nipatiwe taarifa zake na kisha a Amos atengeneze tukio ambalo ,litanikutanisha na Dr Kigomba.”

“ Peniela ahsante sana kwa kulikubali hilo.Narudia tena kukuahidi kwamba baada ya kumalizika kwa operesheni hii basi utakuwa ni mwisho wako ndani ya Team SC41.Naomba uniamini “
“ Ninakuamini John.Ninakuamini baba yangu lakini naomba iwe kama hivyo unavyoniahidi”

“ Usijali Peniela.Kila kitu kitakwenda kama nilivyokuahida.Ila unatakiwa uwe makini sana .Simfahamu Kigomba lakini nasikia ni mtu hatari ,unatakwa uwe naye makini.Kwake kutoa roho ya mtu ni kitu cha sekunde moja tu” akasema John
“ Usijali mzee,kama niliweza kumuingia rais ,siwezi kushindwa kwa Kigomba.Nitafanya kazi nzuri na tutaimaliza operesheni hii .”
“ Nashukru sana Peniela.”
“ Usijali baba.Wasiliana na Amos na umtaarifu kwamba nimekubali na nitaingia katika mahusiano na Kigomba na aanze kufanya mipango ya kunikutanisha naye tu na mimi nitamaliza kila kitu.Kwa sasa naomba niondoke ninakwenda kuanza kushughulikia suala la kupata ile hospitali kwa ajili ya operesheni yako” akasema Peniela huku akichukua mkoba wake

“ Peniela kabla hujandoka kuna jambo nataka kukuuliza”
“ Ni jambo gani?Uliza usiogope”
“ Ni kuhusu jaji Elibariki.Nimeambiwa kwamba yuko kwako”
Peniela akastushwa sana na taarifa zile na kushindwa ajibu nini

“ Usiogope Peniela sijakuuliza kwa ubaya.Kuna kitu ambacho nataka ukifahamu ni kwa nini Elibariki alitaka kuuawa na nani aliyetaka kumuua.” Akasema John
“ Unawafahamu waliotaka kumuua? Akauliza Peniela

“ Ndiyo ni Dr Joshua .”

“Dr Joshua? ! Peniela akashangaa.

“ Dr Joshua alimuua mke wake baada ya kutaka kuvujisha siri za kuhusiana na biashara anayotaka kuifanya.Jaji Elibariki akishirikiana na wenzake walifanya uchunguzi na kugundua kwamba Dr Flora alichomwa sindano yenye sumu.Baada ya kugundua kwamba siri ya kilichomuua m,ke wa rais imevuja, Dr Joshua akaamuru Elibariki auawe haraka na ndiyo maana shambulio lile likapangwa.Kwa msaada wa captain Amos Elibariki akaokolewa na Jessica ambaye naye yupo katika mtandao wetu na ndipo alipoamua kuja kujificha kwako.” Akasema John .Peniela bado aliendelea kumtumbulia macho hakuwa na cha kuongea

“ Kwa sasa kuna juhudi kubwa za kumtafuta Elibariki yuko wapi na ndiyo maana nikawa na wasi wasi kidogo endapo itagundulika kwamba yuko kwako inaweza ikakuletea matatizo na kuharibu mipango yetu” akasema John na Peniela akajibu

“ Ni kweli niko na Elibariki na sikuwa nimekueleza kuhusiana na jambo hili kwa sababu sikutaka mtu yeyete afahamu na nimestuka sana baada ya kusikia kwamba tayari unafahamu jambo hili.Ukweli ni kwamba nilipigiwa simu na msichana mmoja nadhani ndiyo huyo Jesica akanitaka nikamchukue Elibariki sehemu fulani alikonielekza.Nilimkuta akiwa amejeruhiwa na alinieleza mkasa mzima namna tukio zima lilivyotokea nikamuonea huruma sana.Alihitaji sehemu ya kwenda kujificha hivyo na aliamini kwangu atakuwa salama hivyo nikaondoka naye na kwenda kumhifadhi nyumbani kwangu na mpaka sasa ninaishi naye pale kwangu.Usihofu chochote hakuna anayeweza kufahamu kama Elibariki yuko pale kwangu.Ni sehemu salama sana kwake kwa sasa.Alinisaidia sana katika kesi yangu na mimi lazima nimsaidie.”akasema Peniela

“ Peniela umefanya jambo zuri kukubali kumsaidia jaji Elibariki Lakini kuna jambo moja ambalo nahitaji kulisikia toka kwako.Do you love him? Akauliza John na Peniela akabiki anamuangalia.Alistukizwa swali ambalo lilimpa ugumu kidogo kujibu
“ usiogope kunijbu Peniela.Mimi ni mtu ambaye hutakiwi kunificha jambo na zaidi ya yote nina maana yangu kukuuliza hivyo” akasema John.Peniela akatafakari na kusema

“ yes I do love him.Lakini tayari ana mke wake”
“ How do you feel around him? Are you happy? Akaulzia John

“ I feel more than happy around him.”
“ Kama angekuwa hana mke unadhani anasifa za mwanaume ambaye umekuwa ukimuota awe mume wako? Akaulzia John.Peniela akatabasamu na kusema

“ Endapo angekuwa hana mke basi Elibariki ni mtu ambaye ana kila sifa ya mwanaume ninayemuhitaji katika maisha yangu.Ana vigezo vyote vya kuwa mume mzuri”
“ Ahsante nashukuru sana kwa kuwa muwazi kwangu..”
“kwa nini umeniuliza hivyo? Akauliza Peniela

“ Nilihitaji tu kuufahamu ukweli wako.Na kwa kuwa hujanificha kitu sasa unaweza kwenda kuendelea na shughuli zako nitawasiliana nawe baada ya kuongea na captain Amos” akasema John na kisha Peniela akatoka mle ndani akaingia garini na kuondoka

“ Sasa nimepata jibu nililokuwa nalitafuta .Kumbe ni Dr Joshua ndiye aliyemuua mke wake na ndiye aliyetoa amri ya kuuawa kwa Elibariki.Namshukuru sana Captain Amos kwa kumuokoa Elibariki.Sasa nimeamini Team SC41 ni mtandao uliokita mizizi yake hadi ikulu.Sikuwa nikimfahamu yule mwanamke Jessica kama naye ni mmojawapo wa Team SC41..” Akawaza Peniela wakati akitoka chumbani kwa John na kuingia garini akamuamuru yule dereva ampeleke mjini kwa ajili ya kufanya manunuzi aliyoyahitaji.Akiwa ndani ya gari akachukua simu ambayo huitumia kuwasiliana na Dr Joshua na kumpigia
“ Hallow Peniela.Habari yako malaika wangu” akasema Dr Joshua
“ Habari nzuri Dr Joshua.Unaendeleaje?”

“ Ninaendelea vizuri sana.Usiku mzima wa jana nilikuwa nakuota wewe tu.Unasemaje malkia wangu ? si kawaida yako kunipigia muda kama huu” akasema Dr Joshua na kumfanya Peniela atabasamu

“ Dr Joshua nimekupigia ili kukuomba kama utapata nafasi nionane nawe leo jioni katika ile nyumba mpya.Nina hamu sana ya kukuona.Nimekukumbuka sana .Unaweza kupata nafasi ? akauliza peniela

“ Kwa leo nina kazi nyingi muhimu lakini kwa ajili yako nitafanya kila niwezalo kupata muda ili nije nionane nawe.Hata mimi ninakuwaza sana Peniela.”
“ Nashukuru sana Dr Joshua.Nitakuwepo pale nyumbani kuanzia saa mbili za usiku wa leo.” Akasema Peniela na kukata simu.

“ Nina imani atakuja tu.Hana kauli juu yangu .Nimemteka akili yake yote haambiwi lolote ju yangu .Angejua ninavyomchukia yule mzee..Siku nikiachana naye sijui nitaoga na sabuni gani ili kuondoa shombo yake.Simpendi sana” akawaza Peniela akiwa garini kuelekea supermarket kufanya manunuzi ya vitu mbali mbali vya ndani


********


Saa sita za mchana gari nne nyeusi ziliwasili katika makaburi ya mkwajuni. Mojawapo ya gari hizo lilikuwa limebeba jeneza lenye rangi nyeupe.Magari yalisimama na watu wakashuka.Wanaume sita wakalitoa jeneza lile ndani ya gari na kulibeba hadi katika kaburi liilokwisha andaliwa. Wakaliweka pembeni katika meza na watu wale wasiozidi ishirini wakalizunguka kaburi lile.Wote walikuwa wamevaa mavazi meusi .Mchungaji aliyekuwa ameongozana na watu wale akaanzisha ibada fupi kabla ya mazishi.Haya yalikuwa ni mazishi ya Noah .Familia yake ilisafiri kutoka jijini Harare na kuja kumzika jijini dare s salaam .
Mchungaji aliongoza ibada fupi na kutoa maneno machache ya kuwakumbusha waombolezaji kuhusiana na kujiweka tayari saa yoyote kwani kifo hakina hodi.Baada ya ibada ile fupi kilifuata kipindi cha kila mmoja aliyekuwapo pale makaburini kutoa maneno machache ya namna alivyomfahamu Noah.Alianza baba yake ,halafu kaka yake.Mama yake alishindwa kabisa kuongea chochote kutokana na huzuni kubwa aliyokuwa nayo.Zamu ya dada yake naye alishindwa kuongea chochote.Mathew aliongea kwa niaba ya marafiki wa Noah.Alikuwa amesimama akimtegemeza Anitha ambaye hakuwa na nguvu Baada ya hapo jeneza likashuswa kaburini na mafundi wakaanza mara moja kazi ya kulifunika.Kaburli lilipofunikwa watu wakaingia katika magari yao na kuondoka.Safari ya maisha ya Noah ikaishia hapo.Ilikuwa ni siku ngumu sana kwa Mathew na Anitha ambao walikuwa ni watu wa karibu sana wa Noah.
Toka makaburini wakaelekea moja kwa moja katika hoteli walikofikia familia ya Noah kulikokuwa kumeandaliwa chakula na baada ya kula wakaendelea kukaa na wafiwa wakiwafariji .Saa kumi na mbili za jioni Mathew ,Anitha na Jason ambayealikuwa nao katika kipindi chote cha msiba wa Noah wakawaaga wafiwa wakaondoka na kurejea nyumbani.

“ Ni vigumu sana kuamini kama sintamuona tena Noah maishani.Inauma sana” akasema Anitha akiwa amekaa sofani baada ya kufika nyumbani kwa Mathew

“ Anitha kifo tumeumbiwa sisi wanadamu na hakizoeleki.Ni vigumu kuelezea uchungu nilionao kwa kifo cha Noah lakini pamoja na hayo lazima tukubaliane kwamba Noah is gone and we’ll never see him again.Life goes on and we have to move on too.Kwa sasa nguvu yetu kubwa tunatakiwa tuielekeze kwa Elibariki ili kuhakikisha usalama wake” akasema Mathew
“ Elibariki sijui yuko wapi .Mpaka sasa juhudi za kumtafuta zinaendelea lakini hajapatikana.Nina wasi wasi atakuwa alitekwa nyara na watu waliofanya shambulizi lile” akasema Jason amabey naye alikuwapo pale sebuleni
“ Elibariki yupo hai na yuko salama’ akasema Mathew
“Yuko salama? Mnafahamu mahala aliko? akaulzia Jason

“ ndiyo yuko sehemu salama .Baada ya kuokoka katika shambulio lile amekwenda kujificha kwa peniela”akasema Mathew akiamini Jason na Elibariki ni marafiki wakubwa.Hakuwa na taarifa za kilichotokea kati yao.
“ Peniela?! Jason akastuka sana.
“ Elibariki yuko kwa Peniela? akauliza
“ Ndiyo .Amekwenda kujificha kwa Penela. Kuna tatizo lolote? Akauliza Mathew baada ya kugundua Jason alistuka sana baada ya kusikia Elibariki yuko kwa Peniela.
“ Hakuna tatizo lolote Mathew .” akasema Jason na kuomba kuondoka .
“ Elibariki yuko kwa Peniela ! akawaza Jason akiwa garini.
“ Nilitegemea baada ya kipigo cha siku ile basi asingerejea tena kwa Peniela lakini bado hajakoma na amerejea tena.Huyu jamaa ana mke wake kwa nini anaingilia mali za watu? Peniela ni mpenzi wangu mimi na sintokubali Elibariki anipindue na siwezi kukubali aendelee kukaa pale kwa Penny.Siwezi kukubali aendelee kukaa na mwanamke ambaye nimemuhangaikia mpaka nikamuweka huru.Ninampenda Peniela na kwa ajili yake niko tayari kwa lolote.Nikizubaa ninaweza kunyang’anywa mtu wangu hivi hivi nikiona.Lazima nipambane na Elibariki.lazima nimtoe kwa Peniela na asikanyage tena pale.Najua atakuwa amemdanganya Peniela kwamba yeye ndiye aliyemuachia huru.Mimi ndiye niliyefanikisha hadi peniela akaachiwa huru.Bila mimi kusimama imara na kutoa ushahidi wenye nguvu asingepata nguvu ya kumuachia huru peniela.Nilipambana kufa na kupona kwa sababu ninampenda Peniela.Vita hii na Elibariki haitakwisha na lazima nimuonyeshe kwamba sisi ndio watoto wa mji huu” Akawaza Jason


JASON ANATAKA KUFANYA NINI ? TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………..
 
SEASON 2


SEHEMU YA 18

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Nilitegemea baada ya kipigo cha siku ile basi asingerejea tena kwa Peniela lakini bado hajakoma na amerejea tena.Huyu jamaa ana mke wake kwa nini anaingilia mali za watu? Peniela ni mpenzi wangu mimi na sintokubali Elibariki anipindue na siwezi kukubali aendelee kukaa pale kwa Penny.Siwezi kukubali aendelee kukaa na mwanamke ambaye nimemuhangaikia mpaka nikamuweka huru.Ninampenda Peniela na kwa ajili yake niko tayari kwa lolote.Nikizubaa ninaweza kunyang’anywa mtu wangu hivi hivi nikiona.Lazima nipambane na Elibariki.lazima nimtoe kwa Peniela na asikanyage tena pale.Najua atakuwa amemdanganya Peniela kwamba yeye ndiye aliyemuachia huru.Mimi ndiye niliyefanikisha hadi peniela akaachiwa huru.Bila mimi kusimama imara na kutoa ushahidi wenye nguvu asingepata nguvu ya kumuachia huru peniela.Nilipambana kufa na kupona kwa sababu ninampenda Peniela.Vita hii na Elibariki haitakwisha na lazima nimuonyeshe kwamba sisi ndio watoto wa mji huu” Akawaza Jason



ENDELEA……………..


“ Sikuwahi kuota kama Peniela anaweza akawa ni msichana mrembo namna hii.Dah ! ni kama ninamuona malaika” akawaza jaji Elbariki akiwa kitandani akimshuhudia Peniela akijiandaa kwa ajili ya kutoka.
“ Moyo unaniuma sana kutokujua mahala anakokwenda Peniela. Anakwenda kuonana na nani? Ninasikia wivu mkubwa labda kuna mwanaume anakwenda kuonana naye.Siwezi kuvumilia atakaporudi leo lazima nimuulize ili nifahamu mahala anakokwenda” akawaza jaji Elibariki akimuangalia Peniela akimalizia kujipodoa.Alikuwa amevaa gauni refu jekundu lililompendeza sana.

“ Elibariki I have to go now.Nitarejea baadae kidogo kuna mtu nahitaji kuonana naye usiku huu” akasema Peniela huku akitabasamu

“ Ni mchumba wako? Akauliza jaji Elibariki

“ Hapana si mchumba wangu.Nilikwambia kwamba sina mchumba.Ni mtu ambaye nina maongezi naye ya kibiashara” akasema Peniela na kumsogelea jaji Elibarki akambusu
“ Don’t open the door to anybody” akasema Peniela
“ Usijali Peniela sintafanya hivyo na hakuna yeyote anayeweza kujua kama niko hapa” akasema Elbariki na Peniela akachukua funguo za gari lake akatoka na kulitoa gari lake gereji akafungua geti na kutoa gari nje kisha akafunga geti kwa kufuli kubwa ili yeyote atakayekuja ajue kwamba hakuna mtu mle ndani.

“ Kuna kitu nimekigundua kwa Elibariki.Hakufurahishwa na mimi kuondoka usiku huu.Macho yake yanaonyesha alikuwa anaona wivu mkubwa.He loves me.Kwa hilo sina shaka nalo hata kidogo.Lakini sitaki afahamu kwamba nina mahusiano na baba mkwe wake.Akigundua jambo hili nitampoteza .Sitaki hilo litokee na nitafanya kila linalowezekana ili Elibariki asiweze kugundua chochote kuhusiana na mahusiano yangu na rais.Ninamuhitaji sana na hatabanduka katika mikono yangu” akawaza Peniela akiwa katika mwendo mkali kuelekea katika nyumba aliyopewa na Dr Joshua
Aliwasili katika jumba lile lililokuwa kandoni mwa bahari.Katika geti la kuingilia kulikuwa na vijana wawili waliokuwa wamevalia suti nzuri nyeusi,Penny akawatambua vijana wale ni walinzi wa rais akasalimiana nao wakamfungulia geti akaingia ndani.Akaegesha gari na kufungua mlango akawasha taa

“ The house is too quiety and big for me” akawaza Peniela na kuelekea moja kwa moja katika chumba cha kulala na kukaa kitandani akachukua simu yake na kumpigia Dr Joshua ili kumtaarifu kwamba tayari amekwisha fika lakini simu ya Dr Joshua ikaita bila kupokelewa.
“ Mbona hapokei simu? Labda atakuwa kwenye kikao.” Akawaza penny na kisha akampigia simu Kareem mlinzi wa Dr Joshua na kumuomba amtaarifu Dr Joshua kwamba tayari amekwisha wasili pale nyumbani.
Saa tatu kasoro dakika kumi mlango mkubwa wa sebuleni ukafunguliwa wakaingia walinzi wanne wa Dr Joshua halafu baada ya muda akaingia Dr Joshua mwenyewe

“ thank you guys” Dr Joshua akawaambia wale walinzi wake halafu wawili wakatoka na kusimama nje ya mlango , wengine wawili wakaongozana naye hadi katika chumba cha kulala alimo Peniela.Akagonga mlango na ukafunguliwa na Peniela.Dr Joshua akaingia ndani wale walinzi wake wakasogea mbali kidogo na pale chumbani
Peniela akamrukia Dr Joshua na kumkumbatia kwa furaha kubwa na kuanza kumporomoshea mabusu mazito.Dr Joshua akapagawa.
“ Dr Joshua I missed you so much my love” akasema Peniela
“ I missed you too peniela.I missd you so badly” akasema Dr Joshua huku akihema mfululizo .Peniela akamvua koti halafu akamfugua tai na kumvuta kitandani

“ Dr Joshua nimekuita hapa kwa kazi moja tu.To make me happy” akasema Peniela na kulivua gauni lake akabaki mtupu.Dr Joshau akazidi kupagawa .Damu ilimchemka.Peniela alisisimua kumuona akiwa mtupu
Dr Joshua alishindwa kuendelea kusubiri zaidi kwani hata yeye alikuwa na hamu sana na Peniela,akamvuta na shughuli ikaanza.Baada ya dakika kumi mzunguko wa kwanza ukamalizika.Dr Joshua alikuwa akihema kwa kasi.Mwendo aliopelekwa na Penny haukuwa mdogo

“ Nina bahati sana ya kukupata Peniela.Unajua kunifurahisha.Unajua kunipa raha.Kwa ajili yako niko tayari kukupa kitu chochote kile.Umeifanya akili yangu ikuwaze kila sekunde.”akasema Dr Joshua kijasho kikimtiririka.Peniela aliyekuwa pembeni yake akatabasamu na kumbusu kisha akasema
“ Dr Joshua kuna jambo nataka nikuombe”
“ Omba chochote peniela.Kitu chochote ukitakacho nitakupatia”

“ Ahsante sana Dr Joshua na ndiyo maana nakupenda,unajua kujali.laiti kama wanaume wote wangekuwa kama wewe wanawake tungesikia fahari kubwa sana.” akasema Peniela na uso wa Dr Joshua ukajenga tabasamu.
“ Mimi ni namba moja hapa nchini na kila kitu kiko chini yangu.Unataka nikupatie kitu gani? Chochote ukitakacho nitakupatia” akajigamba Dr Joshua

“ Dr Joshua,nina mjomba wangu ambaye ni mgonjwa sana na anahitaji kufanyiwa upasuaji wa kichwa.” Akasema Peniela na kumstua Dr Joshua
“ kwa nini siku zote hizi hujaniambia kama una mjomba wako anaumwa? Ningekwishamsafirisha kwenda nje ya nchi kwa matibabu.”

“ Ahsante sana Dr Joshua lakini hakuna haja ya kumpeleka nje ya nchi.Yeye ana marafiki zake ambao ni madaktari wanatoka je ya nchi watakuja kumfanyia upasuaji huo kwa hiyo wanachohitaji wao ni kupata hospotali yenye vifaa vya kuwawezesha kumfanyia upasuaji huo.Kwa kuwa wewe una nguvu na sauti ninaomba unisaidie kuweza kupata hospitali hiyo ili mjomba wangu aweze kufanyiwa upasuaji huo.” Akasema Peniela.Dr Joshau akamsogeza kwake akambusu na kusema

“ Siku nyingine kama una tatizo lolote hata liwe kubwa kiasi gani usisite kuniambia.Mimi niko kwa ajili yako na nitakufanyia chochote kile unachokitaka.Usijali kuhusu ombi lako.Kuna hospitali moja nzuri sana imefunguliwa hivi majuzi hospitali hii ndiyo hutumika kututibu sisi viongozi wa serikali.Ni hospitali yenye kila kifaa na wataalamu.Huna sababu ya kuwa na wasi wasi.Mjomba wako atatibiwa pale na atapona tu”
“ Nashukuru sana Dr Joshua lakini kuna jambo moja nataka nikuombe kuhusiana na suala hili” akasema peniela
“ peniela wewe ni first lady omba chochote kile.Nchi hii ni ya kwetu” akasema Dr Joshua.Peniela akatasamu na kusema
“ Ninaomba jambo hili liwe la siri kubwa na hata upasuaji huo ufanyike kwa siri na muda wote ambao mjomba wangu atakuwa akitibiwa pale hospitali basi kuwe na usiri mkubwa.Unaweza ukanisaidia na hili pia? Akauliza Peniela.Dr Joshua akafikiri kidogo na kusema
“ Huyo mjomba wako ni nani? Kwa nini atibiwe kwa siri? Akauliza .
“ Ni mtu ambaye hapendi famiilia yake ifahamu kuhusiana na upasuaji huo kwa hiyo anataka aufanye kwa siri bila ya mtu yeyote kufahamu.”

“ usijali Peniela.Kwa ajili yako kila kitu kinawezekana.Nitawasiliana na daktari mkuu wa pale na nitakuunganisha naye ili maandalizi yaweze kufanyika.Utapata kila unachokihitaji”
“ Asante sana Joshua” akasema Peniela na kuanza kuzichezea nyeti za Dr Joshua kwa ufundi mkubwa hukuDr Joshua akitoa migumo kwa raha aliyokuwa akiipata.Alishindwa kuvumilia wakaingia tena katika mzunguko mwingine


*******


Anitha hakuwa akijisikia kuinuka pale sofani alipokaa.Alihisi mwli wake wote hauna nguvu hata kidogo.Bado alikuwa na mawazo mengi sana kuhusiana na kifo cha Noah.Macho yake bado yaliendelea kutoa machozi kila alipomkumbuka Noah.Taratibu akainuka na kuelekea chumbani kwa Noah ambako Mathew alikuwa akipakia vitu vya Noah katika sanduku kwa ajili ya kuwakabidhi ndugu zake hapo kesho.

“ N vigumu kuamini kama kweli Noah hatuko naye tena”akasema Mathew
“ Inauma sana Mathew.Inaniuma sana” akasema Anitha.Mathew akaacha ile kazi aliyokuwa akifanya akamshika Anitha mkono na kumketisha kitandani.
“ Anitha kama nilivyokwambia awali kwamba lazima tukubaliane na ukweli kwamba Noah amekwenda na hatutamuona tena hadi siku hiyo ya mwisho.Kitu kikubwa ambacho tunaweza kukifanya kwa sasa katika kumuenzi ni kuwatafuta wale wote waliomuua.lazima tuendeleze mapambano na tusimame imara kuhakikisha kwamba kazi tuliyoianza tunaimaliza .Pamoja na maumivu tuliyonayo lakini lazima tuendelee na kazi yetu na kazi kubwa kwa sasa ni kuwabaini wale wote waliofanya kitendo hiki na tunaweza tu kuwapata kwa kuhakikisha kwamba Elibariki anaendelea kuwa salama.Ni yeye ndiye anayeweza kutupa picha kamili nini hasa kilitokea siku ile na nina hakika anaweza kuwa anawafahamu wauaji.”akasema Mathew.Anitha akafuta machozi na kumtazama Mathew

“ Kwa hiyo tutafanya nini Mathew kumlinda Elibariki?Nina wasi wasi sana na maisha yake.”Akasema Anitha

“ Kuna kitu ninakifikiria.Tunahitaji kuonana na Elibariki na kumshawishi awe kuja hapa kwetu ambako ni salama zaidi kuliko kule kwa Peniela.Kwa kuwa wewe hujisikii vizuri na umechoka mimi ngoja nikaonane naye usiku huu halafu nitakwambia ni kitu gani tumeongea.Nitakaporudi nitakuwa na jibu la nini kinaendelea “ akasemaMathew

“ Hapana Mathew siwezi kubaki hapa peke yangu.Ninaogopa sana.Hata kama sina nguvu lakini nitaongozana nawe.” Akasema Anitha

“ Are you sure? Akauliza Mathew

“ yes I’m sure” akajibu Anitha.
Dakika kumi baadae wakaingia garini na kuondoka kuelekea nyumbani kwa Peniela

“ Mke wa Elibariki anafahamu kama mume wake yuko kwa Peniela? Akauliza Anitha wakiwa garini

“ Sina hakika kama anafahamu .Elibariki hawezi kuwa mjinga na kumueleza mke wake kwamba amejificha kwa mwanamke mwingine.” Akajibu Mathew

“ lakini wanaume ! kwa nini anamfanyia hivi mke wake?
“ Anitha wewe hauko katika ndoa na huyafahamu mambo yaliyomo ndani ya ndoa.Nina hakika siku na wewe ukiingia katika ndoa yanaweza yakakukuta kama yanayomkuta mke wa Elibariki” akasema Mathew na kumfanya Anitha acheke.Ilikuwa ni mara ya kwanza Anitha anacheke toka ulipotokea msiba wa Noah.

“ Hii ndiyo sabau ambayo inanifanya nisitake kabisa kuolewa.Sitaki matatizo kama hayo.Napenda niishi mwenyewe .Nahisi amani na furaha .Wanaume siku hizi wamekuwa wadanganyifu sana”

“ Si wanaume tu hata wanawake nanyi siku hizi mmekuwa na udanganyifu mkubwa.Hakuna mkweli zama hizi.Wote tundanganyana tu” akasema Mathew

“ Lakini usikate tamaa Mathew siku moja unaweza ukapata mwanamke ambaye atakufaa.Wanawake wazuri bado wapo”
“ Jambo hilo nimekwisha litoa kabisa katika akili yangu.Nilimpenda mwanamke mmoja tu na alipouawa aliondoka na mapenzi yote na sina tena mapenzi kwa mwanamke mwingine yeyote” akasema Mathew

“ Hata mimi hunipendi? Akauliza Anitha na kumfanya Mathew acheke kicheko kikubwa

“ Usinichekesha Anitha.Niache kukupenda wewe? Wewe ni kila kitu kwangu kwa sasa.Kupenda nilikokuwa nakuongelea ni kutafuta mwanamke wa kuishi naye.”

“ Ikitokea ukanipenda ninafaa kuwa mke? Akauliza Anitha na kumfanya Mathew azidi kucheka.
“ Anitha leo umenifurahisha sana.Mimi na wewe katu hatuwezi kufika huko. “

“ kwa nini hatuwezi kufika huko? Kwani sisi tumekosa nini? Akauliza Anitha

“ Sisi tuko tofauti sana.” Akasema Mathew

“ Unajua mathew kuna kitu nimejifunza kutokana kifo cha Noah.”

“ Kitu gani? akauliza Mathew
“ Noah amekufa bado kijana mdogo sana na hakuweza kutimiza malengo yake mengi.Maisha haya ni mafupi na hakuna anayefahamu nini kitatokea kesho.Noah amekufa hana mke wala mtoto.Hana kumbu kumbu yoyote aliyoiacha hapa duniani.Kazi hizi zinatufanya tunajisahau kabisa kwamba tunahitaji na sisi furaha maishani.We need to be happy.Tusijisahau kabisa na tukafa kifo kama cha Noah.Nimetafakari sana kuhusu jambo hili na kuna jambo nimelifikiria ”akasema Anitha
“ Jambo gani Anitha ? akauliza Mathew wakati akikata kona kuingia katika mtaa anaoishi peniela na mara ghafla akafunga breki ..
“ Kuna nini? Akaulizia Anitha
“ Ouh my God !..akasema Mathew .Anitha naye akaelekeza macho yake mbele.Katika geti la nyumba ya Peniela kulikuwa na kundi la askari polisi waliojihami kwa silaha.

“ Pale ni nyumbani kwa Peniela “ akasema Mathew
“ Askari wale wanatafuta nini pale kwa peniela? Akauliza Anitha

“ Ninahisi kuna jambo limetokea au tayari wamekwisha fahamu kwamba Elibariki yuko mle ndani kwa Peniela” akasema Mathew

“ What are we going to do Mathew.Are you sure Elibariki is ok?Nina wasi wasi sana na maisha yake” Akasema Anitha ambye alikuwa na wasi wasi mwingi.
“ Ngoja nijaribu kuwasiliana na Peniela anifahamishe kuna kitu gani kinaendelea” akasema Mathew na kuchukua simu yake akazitafuta namba za simu za peniela akapiga.Simu ikaita bila kupokelewa.

“ Mbona hapokei simu? Akauliza Mathew.
“ jaribu kupiga tena” akasema anitha.mathew akapiga tena na simu ikaendelea kuita.
Peniela akiwa katikati ya mzunguko akimpagawisha Dr Joshua simu yake ikaita lakini akaipuuzia.Ilipoita mara ya pili ikamlazimu kuakatisha mzunguko na kwenda kuipokea.Hakuzifahamu namba zile zilizompigia ni za nani akabonyeza kitufe cha kupokelea simu
“ hallow ‘ akasema
“ hallow Peniela? Akauliza Mathew
‘ Ndiyo,naongea na nani? Akauliza Peniela

“ unaongea na Mathew,rafiki wa jaji Elibariki”

“ Unasemaje? Akauliza Peniela

“ Hapa nyumbani kwako kuna askari wako getini na inaonekama wanajadiliana namna ya kuweza kuingia ndani.Kuna kitu gani kinachoendelea hapa kwako? Elibariki ni mzima?
“ Nyumbani kwangu? !!..peniela akashangaa

“ Ndiyo .” akajibu mathew na kumchanganya peniela.

“ pemiela wewe uko wapi? Uko ndani? Akauliza Mathew

“ hapana nimetoka sipo nyumbani”

“ Elibariki yuko wapi? Yuko ndani?

“ Ndiyo .Mathew naomba unisubiri kidogo niangalie namna ya kufanya” akasema Peniela halafu akamfuata Dr Jshua

“ peniela kuna nini? Mbona umebadilika ghafla? Akauliza Dr Joshua ambaye jasho liliendelea kumtiririka
‘ Dr Joshua nina tatizo limetokea na ninanahitaji msaada wako wa haraka”

“ Una tatizo gani peniela? Hebu naomba utulie na unieleze vizuri nini kimetokea? Akasema Dr Joshua.Peniela akamtazama kwa makini na kusema
“ Dr Joshua hivi tunavyoongea nyumba yangu imezingirwa a askari na wanataka kuingia nyumbani kwangu.Sielewi wanachokitafuta nini .Tafadhali Dr Joshua naomba unisaidie.Wewe una amri juu ya majeshi yote naomba uwaamuru waondoke pale nyumbani kwangu mara moja” akasema Peniela.DrJoshau akainama akafikiri kwa muda halafu akasema

“ Kuna kitu gani wanakitafuta pale kwako? Kuna kitu chochote ambacho kinaweza kusababisha wakafika pale kwako usiku huu?
“ Sina kitu chochote cha kuwafanya wafike pale kwangu usiku huu.Maisha yangu unayafahamu sina tatizo na mtu yeyote sasa kwa nini wakaizingira nyumba yangu kana kwamba ninauza dawa za kulevya? Tafadhali naomba uwaondoe pale kwangu mara moja” akasema Peniela.
“ Ok penny consider it done “ akajibu Dr Joshua na kuinuka akajifunga taulo na kuvaa fulana halafu akaufungua mlango .Walinzi wawili walikuwa wamesimama hatua chache toka chumba kile akawaita na kuongea na mmoja wao halafu akarejea tena chumbani.Baada ya sekunde kadhaa mlango ukagongwa akenda kuufungua
“ Mzee tayari kamanda wa kanda maalum yuko hewani.” Akasema yule mlinzi na kumpatia simu Dr Joshua
“ hallow Kamishna habari za usiku huu.samahani kwa kukusumbua” akasema Dr Joshua
“ Bila samahani mzee.” Akajibu Mkuu wa polisi kanda maalum ya dare s salaam

“ Nimekupigia kuomba msaada wako.” Akasema Dr Joshua

“ Ndiyo mzee nakusikiliza”
“ Kuna vijana wako muda huu wameizingira nyumba ya binti mmoja anaitwa Peniela una taarifa hizo?
“ Ndiyo mzee ninazo taarifa hizo”
“ Kuna nini hapo katika hiyo nyumba hadi izingirwe?

“ Mzee ,tumepokea taarifa kwamba Jaji Elibariki ambaye tumekuwa tukimtafuta ili kufahamu yuko wapi,amenonekana ndani ya ile nyumba na ndiyo maana vijana wangu wamekwenda pale ili kumkomboa kwani tuna hisi lazima atakuwa ametekwa nyara.”

“ Mna hakika na taarifa hizo za kuonekana kwa jaji Elibariki mahala pale?
“ Chanzo kilichotoa taarifa hizo ni chanzo cha ukakika ,ni mtu wa karibu wa peniela ambaye ni wakili aliyemsimamia kesi yake na akashinda.Mtu kama yule hawezi kutoa taarifa za uongo”

“Ok kamishna nimekuelewa lakini kuna jambo ninaliomba,naomba uwaondoe vijana wako kwa usiku huu na kesho zifanyike taratibu za kawaida za kufanya upekuzi katika nyumba ileili kubaini kam Elibariki yumo humo ndani au hayumo.Naomba unisaidie sana kwa hilo “
“sawa mkuu nitafanya hivyo.Nitawaondoa vijana wangu toka pale sasa hivi”
“Ahsante sana kamishna” akasema Dr Joshua na kukata simu

“ tayari .Kila kitu kimemalizika lakini naomba uniweke wazi Peniela ,kamishna wa kana maalum ya Dar es salaam anadai kwamba jaji Elibariki ameonekana nyumbani kwako.Hizi ni taarifa za kweli?
“ Elibariki ?! Peniela akashangaa

“ Ndiyo.Niliyekuwa nikongea naye ni kamanda wa kanda maalum ya kipolisi dare s salaam anasema kwamba askari wameizingira nyumba yako baada ya kupata taarifa za kuonekana jaji Elibariki nyumbani kwako.Taarifa hizi ni za kweli? Akauliza Dr Joshua.Peniela akamtazama na kusema

“ Do you trust them? Do you trust what they say?
“ Peniela niambie si kweli na nitakuamini”
“ Ahsante sana kwa kuniami Dr Joshua.Mimi sina mahusiano yoyote na Elibariki na wala hawezi kuja kujificha kwangu.Aliyewapa taarifa hizi atakuwa amewadanganya”
“Lakini inasemekana taarifa hizi zimetoka kwa mtu wako wa karibu sana.wakili wako aliyekuwa akikutetea katika kesi yako”

“ Jason? ! peniela akashangaa
“ Sifahamu kama ni huyo ama vipi lakini ndiye aliyetoa taarifa hizo polisi kwamba Elibariki yuko pale kwako.”
Peniela alipatwa na mshangao mkubwa sana kwa kusikia kwamba ni Jason ndiye aliyetoa taarifa zile kwa polisi.Haraka haraka akaanza kuvaa nguo zake
“ Kuna nini Peneila? Mbona unavaa nguo?
“ nataka nikaonane na Jason.kwa nini anifanyie hivi? Kwa nini anisingizie jambo zito kama hili?
“ Hakuna haja peniela jambo hili limekwisha malizika.Hakuna mtu atakaye ingia pale kwako.Mimi ndiye mkuu wa majeshi yote na kauli yangu ni ya mwisho kwa hiyo naomba utulize hasira tuendelee na mambo yetu” akasema Dr Joshua
“ hapana Dr Joshua .Siwezi kuendelea tena.Akili yangu imekwisha tibuka.usijali tutaonana tena siku yoyote ukiwa na nafasi.” Akasema na kumbusu Dr Joshua halafu akatoka kwa kasi akamuacha Dr Joshua akishangaa.
Peniela akaingia garini na kuondoka kwa kasi.Akiwa barabarani akapunguza mwendo wa gari na kuegesha pembeni akachukua simu yake na kumpigia Mathew

“ Mathew bado uko karibu na nyumbani kwangu?

“ Ndiyo niko hapa karibu na kwako”

“ Nini knaendelea hapo? Askari wamekwisha ingia ndani?
“ Hapana nimeshangaa wameingia katika magari yao na kuondoka”
Peniela kashusha pumzi
“ Ahsante Mungu.Dah ! hakuna siku niliyowahi kuogopa kama leo” akawaza Peniela na kuwasha gari lake akaendelea na safari
“ Mathew ninakuja niko njiani.tafadhali naomba usiondoke” akasema Peniela
“ Jason amefahamuje kama Elibariki yuko pale kwangu? Kwa nini akaenda kutoa taarifa polisi? Nadhani lengo lake ni kunikomoa mimi na Elibariki.Alijidanganya sana.Hakujua kama nina uwezo mkubwa zaidi yake.Nilikuwa na muheshimu sana na ,kumuona kama rafiki wa kweli lakini kumbe ni kijana ambaye hana akili hata moja.Nimemdharau sana na sitaki tena mahusiano naye na akiendelea kunifuatilia atakuwa ametangaza vita na mimi na nitamfunza adabu.” Akawaza Peniela

“ kwa sasa baada ya Elibariki kugundulika yuko pale kwangu lazima nimuhamishe.lazima nitafute mahala ambako nitakaa naye kwa raha mustarehe.sitaki nikae naye mbali .Tayari amekwiha niingia katika kila mshipa wa mwili wangu” akawaza Peniela


TUKUTANE SEHEMUJAYO…
 
SEASON 2


SEHEMU YA 19


ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“ Mathew bado uko karibu na nyumbani kwangu?

“ Ndiyo niko hapa karibu na kwako”
“ Nini knaendelea hapo? Askari wamekwisha ingia ndani?

“ Hapana nimeshangaa wameingia katika magari yao na kuondoka”
Peniela kashusha pumzi

“ Ahsante Mungu.Dah ! hakuna siku niliyowahi kuogopa kama leo” akawaza Peniela na kuwasha gari lake akaendelea na safari
“ Mathew ninakuja niko njiani.tafadhali naomba usiondoke” akasema Peniela

“ Jason amefahamuje kama Elibariki yuko pale kwangu? Kwa nini akaenda kutoa taarifa polisi? Nadhani lengo lake ni kunikomoa mimi na Elibariki.Alijidanganya sana.Hakujua kama nina uwezo mkubwa zaidi yake.Nilikuwa na muheshimu sana na ,kumuona kama rafiki wa kweli lakini kumbe ni kijana ambaye hana akili hata moja.Nimemdharau sana na sitaki tena mahusiano naye na akiendelea kunifuatilia atakuwa ametangaza vita na mimi na nitamfunza adabu.” Akawaza Peniela

“ kwa sasa baada ya Elibariki kugundulika yuko pale kwangu lazima nimuhamishe.lazima nitafute mahala ambako nitakaa naye kwa raha mustarehe.sitaki nikae naye mbali .Tayari amekwiha niingia katika kila mshipa wa mwili wangu” akawaza Peniela



ENDELEA……………………


Peniela aliwasili nyumbani kwake,akasimamisha gari nje ya geti na kwa sekunde kadha akaangaza angaza pande zote kama kulikuwa na mtu maeneo yale.Alikuwa nawasiwasi mwingi sana .Hakukuwa na mtu yeyote maeneo yake ya karibunanyumba yake.Mtaa ule anaoishi ni moja kati ya mitaa yenye utulivu mkubwa sana.Alipohakikisha hakuna mtu yeyote pale karibu akashuka na kuelekea getini.Akalifungua kufuli kubwa alilokuwa amefungia geti akaliingiza gari ndani halafu akampigia simu Mathew na kumuomba asogee pale nyumbani kwake.Mathew akawasha gari wakasogea hadi nyumbani kwa peniela akawafungulia geti wakaingia ndani.Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Mathew na Anitha kukutana na peniela ana kwa ana
“Hallow Peniela” akasema Mathew kwani alikwishawahi kuonyeshwa picha ya Peniela na Jason
“ Hallow Mathew”akajibu Peniela huku akionyesha uoga Fulani.

“halow Penny.Naitwa Anitha.” Anitha naye akajitambulisha wakasalimiana .

“ Ahsanteni sana.Karibuni ndani ”
Peniela akawakaribisha ndani na kuwakirimu
“Mathew nashukuruni sana kwa taarifa ile.Bila ninyi Elibariki alikuwa katika hatari kubwa.”
“ usijali Peniela .Tulikuja kwa lengo la kuonana na Elibariki lakini ghafla tukakuta kuna vikosi vya askari ndiyo maana nikaamua kukupigia na muda mfupi tu baada ya kuongea nawe simuni askari wale wakapanda magari yao wakaondoka.Kuna kitu ulikifanya kuwaondoa askari wale? Akauliza Mathew

“ Sifahamu kwa nini waliondoka ghafla.Mna hakika hakuna askari aliyebaki hapa karibu kufanya uchunguzi ? Akauliza Peniela
“ Hakuna askari aliyebaki.Wote wameondoka ” akajibu Mathew.

“ Elibariki anaendeleaje?
“ Anaendelea vizuri .Alipatwa na majeraha madogo madogo ya michubuko ya risasi lakini anaendelea vizuri.Ngoja nikamuite yuko chumbani”
Peniela akawaacha akina Mathew akaelekea katika chumba cha kulala aliko jaji Elibariki.Tayari alikwishapitiwa na usingizi na alistuka baada ya kusikia mlango ukifunguliwa.
“ Ouh Peniela.Umenistua sana” akasema jaji Elibariki.Peniela hakusema kitu akamfuata pale kitandani na kumkumbatia kwa nguvu akambusu.
“ I missed you Elibariki.I missed you so much.”
“I missed you too Peniela.Nashukuru umerejea salama”
“ Mimi ndiye ninayepaswa kushukuru kwa kukukuta salama”
“ Usihofu kuhusu mimi.Niko salama na siku zote nitaendelea kuwa salama.Hapa kwako ni sehemu salama sana na hakuna yeyote atakayejua kama niko hapa.habari ya huko utokako?” akasema jaji Elibariki.Peniela akamtazama usoni na kusema.

“ Elibariki this place is not safe anymore” akasema Peniela
“Not safe, Why? Kwa nini unasema hivyo?

“ Please hold me tight Elibariki because I don’t want to loose you” akasema Peniela na Elibariki akamkumbatia kwa nguvu zaidi.

“ Niambie Peniela kuna tatizo?
Peniela akavuta pumzi ndefu na kusema
“ tayari wanafahamu uko hapa kwangu”
Elibariki akastuka na kumuachia Peniela akamtazama kwa mshangao
“ Wanajua kama niko hapa? Nani wamejua niko hapa? Akauliza Elibariki

“ Relax Elibariki usiwe na shaka ,tayari suala hilo limekwisha shughulikiwa”
“ Peniela naomba unieleze ni akina nani waliofahamu kama niko hapa kwako? Nini kimetokea? Akauliza jaji Elibariki kwa wasi wasi
“ Wakati nikiwa katika maongezi yangu ya kibiashara na yule mtu niliyekwamba ninakwenda kuonana naye usiku huu,rafiki yako yule uliyempigia simu siku ile usiku anaitwa Mathew alinipigia simu na kunitaarifu kwamba nyumba yangu imezingirwa na askari waliokuwa wakitafuta namna ya kuingia ndani.Nilistuka sana na kukatisha shughuli zangu na kuanza kurudi.Nikiwa njani Mathew akanifahamisha kwamba askari wale wameingia katika magari yao na wameondoka.Sifahamu walikuwa wakitafuta nini hapa kwangu.Nina wasiwasi kwamba yawezekana watakuwa wamekwisha pata fununu kwamba uko hapa na walipokuta kufuli getini wakashindwa kungia na kuondoka” akasema Pseniela

“ Mathew alipokupigia simu na kukupa taarifa za nyumba yako kuzingirwa na askari alikuwa wapi? Akauliza jaji Elibariki

“ Mathew na Anitha walikuwa wakija kuonana nawe hapakwangu kwani tayari walifahamu kwamba uko hapa na ndipo walipokuta tukio lile la nyumba yangu kuzingirwa na askari.Mathew na Anitha wako sebuleni na wanahitaji kukuona.Do you trust them?

“ yes I do trust them.Hawa ni rafiki zangu wakubwa. Noah yule jamaa aliyeuawa katika lile tukio ni mwenzao ” akasema Elibariki na kuinama akajawa na mawazo
“Mathew amefahamuje kwamba niko hapa kwa Peniela? akajiuliza
“Nakumbuka siku ile usiku nilipokuja kwa Peniela nilimpigia simu na kumfahamisha kwamba niko sehemu salama lakini sikumwambia niko wapi sasa amefahamuje kama niko hapa? Au yawezekana labda walifuatilia ile namba niliyoitumia kumpigia na wakagundua kwamba ni ya Peniela na ndiyo maana wakaja moja kwa moja hapa.? Askari waliokuja hapa usiku huu walinifuata mimi au kuna kitu kinginewalikifuata hapa nyumbani kwa Peniela? Lakini nina wasi wasi lazima watakuwa walipata taarifa kwamba hiko hapa na wakaamua kuja kunichukua kwani nina hakika jeshi la polisi hawalali wakitaka kufahamu mahala nilipo.Nani aliwapa taarifa hizo?” Akaendelea kuwaza Elibariki na kustuliwa na Peniela

“ Elibariki usiwaze sana mpenzi wangu.askari wale wameondoka na uko salama lakini nakuahidi nitafanya kila linalowezekana kukulinda na kuhakikisha unakuwa salama.yeyote yule mwenye nia ovu nawe hatafanikiwa.” akasema Peniela
“Ahsante sana Peniela lakini ninajiuliza Kama ni kweli polisi wamepata taarifa kwamba niko hapa nani kawapa taarifa hizo? kwa sababau hakuna yeyote anayefahamu kwamba niko hapa zaidiya Mathew na yule msichana uliyenikuta naye siku ile garini na toka nimefika hapa sijawasha simu yangu na zaidi ya Mathew,sikuwahi kumtarifu mtu mwingine yeyote mahala niliko ,sasa wamefahamuje kwamba niko hapa kwako? Akauliza Elibariki.Anitha akamtazama na kusema

“ Hawa marafiki zako Mathew na Anitha unawaamini? Una hakika si wao waliopeleka taarifa hizi polisi? Akauliza Peniela

“ Ninawaamini sana na katu hawawezi kufanya kitu kama hicho..” akajibu Elibariki

“ natamani nimweleze Elibariki ukweli kwamba ni jason ndiye aliyetoa taarifa zile polisi lakini sitaki afahamu chochote kuhusu jambo hili”
“ Elibariki usiwaze sana kuhusu jambo hili .Mathew na Anitha wanakusubiri sebuleni twende ukaonane nao.” Akasema Peniela.Elibariki akainuka wakaongozana kuelekea sebuleni..
“ Elibariki ! akasema Anitha kwa furaha baada ya Elibariki kutokea pale sebuleni.Akainuka na kumkumbatia.

“ Pole sana Elibariki.Mungu ni mkubwa” akasema Anitha

“ Nashukuru sana Anitha niko salama .Hata mimi siamini kama nilipona katika shambulo lile.Ni Mungu tu aliyeniwezesha kuwa hai hadi leo ”akasema jaji Elibariki na halafu akasalimiana na Mathew

“ Nashukuruni sana ndugu zangu kwa kuja kuniona.”akasema Elibariki
“ Vipi maendelo yako sasa hivi? Akauliza Mathew

“ kwa sasa ninaendelea vizuri sana.Sikupatwa na majeraha makubwa sana .Nilikuwa na michubuko ya risasi.Risasi zote ambazo zilipaswa kuingia mwilini mwangu alizibeba Noah na kuniokoa.” akasema jaji Elibariki na kushindwa kujizuia kutoa chozi

“ Its ok Elibariki.Huu si wakati wa kulia tena.Ni wakati wa kumshukuru Mungu uko salama.” akasema Mathew na kimya kikapita halafu Mathew akasema
“ Noah tumemzika leo katika makaburi ya mkwajuni.Familia yake iliamua azikwe Dar e s salaam.Mimi na Anitah tulikuwepo na tulikuwakilisha” akasema Mathew
“ Ahsanteni sana .Nilitamani kushiriki mazishi yake ili nitoe shukrani zangu lakini nashukuru kwa kuniwakilisha” akasema Elibariki halafu kikapita kimya kifupi

“ Mmejuaje niko hapa?Mmepafahamu vipi hapa kwa Peniela? Akauliza jaji Elibariki
“ Tulifuatilia namba ile ya simu uliyotumia kunipigia siku ile na tukagundua ni ya Peniela tukafahamu unaweza kuwa hapa na ndiyo maana tukaja kubahatisha kama tunaweza kukupata.Niliwahi kuja hapa siku moja na Jason kwa hiyo ninapafahamu.”
Peniela aliposikia jina la Jason likitajwa mwili ukasisimka.Mathew akaendelea
“Tulipofika hapa tukakuta kuna askari wameizingira nyumba .Niliogopa ikanibidi nimpigie simu Peniela kumuuliza kama kuna tatizo lolote na akaniambia kwamba hakuwepo ndani kwa wakati ule.Baada ya muda mfupi tukaona askari wale wakiingia katika magari yao na kuondoka zao.Elibariki nina wasi wasi sana yawezekana tayari umekwisha fahamika kwamba uko hapa na watu waliofanya shambulio lile hawalali wanakesha macho wakitaka kufahamu mahala ulipo na wanaweza hata kutumia vyombo vya dola kukutafuta ili lengo lao la kukuua litimie..” Akasema Mathew
“ hata mimi nina wasi wasi kwamba yawezekana wakawa wamefahamu kwamba niko hapa .Ninachojiuliza wamepataje taarifa za mimi kuwepo hapa? Akauliza Elibariki
“ Elibariki kwa sasa ni vigumu kupata majibu ya swali hilo.Kitu cha muhimu kwa sasa ni usalama wako.Hapa ulipo si sehemu salama kwa wewe kuendelea kukaa ” Akasema Mathew

“ Hata mimi nimekwisha liona hilo na nimeazimia kwamba kesho nitatafuta nyumba nyingine yenye usalama zaidi kwa Elibariki kuishi..” akasema Peniela

“ Peniela hatuwezi kusubiri hadi kesho.Elibariki anatafutwa na hatuwezi kutoa hata dakika moja kwa watu wanaotaka kumdhuru kutekeleza lengo lao.Elibariki tunaondoka wote usiku huu na kuelekea sehemu salama” akasema Mathew

“ No ! hamuwezi mkamchukua Elibariki namna hiyo Mathew.usalama wa maisha yake uko mikononi mwangu na hivyo nitafanya kila niwezalo kuhakiksha anakuwa salama.kesho nitamuhamishia katika nyumba nyingine yenye usalama zaidi.Msiwe na wasi wasi rafiki yenu atakuwa salama” akasema Peniela

“ Peniela ninachokisema hapa si ombi bali ni amri.Elibariki tutaondoka naye sisi na kwenda kumuhifadhi sehemu salama.Naomba tusiendelee kubishana katika hilo.Elibariki naomba ukajiandae tuondoke.Huu ni mwanya tumepata na tunatakiwa tuutumie vizuri.Muda wowote askari wale wanaweza wakarudi” akasema Mathew kwa sauti yenye amri ndani yake.Peniela alionyesha wazi kwamba hakuwa tayari kwa Elibariki kuondoka pale kwake

“Peniela naomba tukaongee chumbani.Mathew naomba mnisubirikwa muda nitarejea.”akasema Elibariki akaondoka na Peniela wakaelekea chumbani
“ Mathew kuna jambo ambalo nimekuwa nikjiuliza na sijapata jibu.Kwa nini wale askari waliondoka ghafla muda mfupi baada ya kumtaarifu Peniela ? Akauliza Anitha
“ hata mimi nilijiuliza sana swali lile bila majibu lakini kitu kikubwa na cha muhimu kwa sasa ni kumuondoa kwanza Elibariki hapa kwa Peniela halafu tutafute majibu ya maswali hayo.” akasema Mathew
“Peniela ameonyesha wazi hayuko tayari Elibariki andoke hapa kwake” akasema Anitha

“ Hili si ombi na hana namna ya kukataa.Lazima Elibariki aondoke hapa” akasema Mathew huku akichungulia nje.
Jaji Elibariki na Peniela wakaingia chumbani kwa ajli ya maongezi mafupi
“ Elibariki sintakubali katu uondoke na wale marafiki zako.I don’t trust them at all.Mimi ndiye niliyechukua dhamana ya kuhakikisha kwamba unakuwa salama na nitafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu kuhakikisha unakuwa salama” akasema Peniela
“ Peniela naomba unisikilize.Nilichagua kuja hapa kwako nikiamini ni sehemu salama na kwamba hakuna yeyote anayeweza akahisi niko hapa.Kitendo cha askari kuonekana hapa kwako usiku huu kimeniwashia taa nyekundu na kunipa tahadhari kwamba siko sehemu salama tena.Peniela roho yangu inatafutwa kwa gharama zozote zile.Niruhusu niondoke na hawa marafiki zangu.Ninawaamini sana kama ninavyokuamini wewe na usiwe na wasi wasi hata kidogo.” Akasema Jaji Elibariki naPeniela akazidi kumkumbatia
“ Elibariki nakupenda sana na sitaki uondoke katika maisha yangu.Kukuacha uondoke ni sawa na kukuacha upotee katika maisha yangu.Nina wasiwasi pengine nisipate tena nafasi ya kuonana nawe.Katika siku hizi chache nilizokaa na wewe nimegundua kwamba una sehemu kubwa sana katika maisha yangu.Nimegundua kwamba furaha ya moyo wangu iko kwako.Tafadhali Elbariki naomba usiende .Niamini nitakutafutia sehemu salama na tutaishi kwa amani bila matatizo .maisha yangu hayawezi kwenda bila yaw ewe” akasema Peniela

“ Peniela nafahamu kwamba unanipenda sana na kwa hilo sina shaka hata kidogo.katika kipindi hiki kifupi nilichokaa kwako nimefarijika sana na nimeiona fahari ya kupendwa.Narudia tena kukuhakikishia kwamba nilitua sehemu sahihi kabisa ninakotakiwa kuwepo.Ninakupenda Peniela lakini o ili tuweze kuyafurahia mapenzi yetu ni lazima tuwe salama.Kwa maana hiyo basi naomba uniache niende sehemu salama zaidi na mambo haya yakimalizika basi tutapata wasaa mzuri wa kuyafurahia mapenzi yetu.Hata mimi natamani kama ningeendelea kukaa hapa kwa miaka yote lakini hali ilivyo hivi sasa inanilazimu niondoke..Tafadhali usisikitike sana Peniela.” Akasema jaji Elibariki.Peniela akamkumbatia na machoziyakamtoka
“ kama una uhakika kwamba utakuwa salama huko unakoenda ninakuruhusu uende lakini uniahidi kwamba utakuwa ukiwasiliana nami kila siku na kunijulisha kuhusiana na maendeleo yako”

“ usijalikuhusu hilo Peniela nitakuwa nikiwasiliana nawe mara kwa mara na kukufahamisha kila kinachoendelea.Nashukuru sana kwa kila kitu,kwa huduma nzuri na kwa kunijali.Sikuzote utaendelea kupata nafasi ya juu zaidi katika moyo wangu.Natumai tutakapoonana tena mimi na wewe hatutakuwa na kizuizi chochote tena cha kutufanya tushindwe kuyafurahia mapenzi yetu.”akasema jaji Elibariki kisha akavaa nguo zake na kujiweka tayari kuondoka
“ Peniela this is it.I have to go now.They are waiting for me” akasema jaji Elibariki lakini Peniela hakuweza kujibu chochote alikuwa ameinama akilia.Jaji Elibariki akamsogelea akambusu
“ usilie Peniela,tutaonana muda si mrefu sana naomba uniamini”
“ Elibariki please take care “ akasema Peniela kisha akainuka wakaongozana na Elibariki hadi sebuleni

“ We can go now” akasema jaji Elibariki.Wakatoka pale sebuleni na kuiingia katika gari la Mathew wakaondoka.Peniela akarejea chumbani kwake na kujtupa kitandani alikuwa analia

“ I’ve lost him.Nimempoteza na Elibariki.Sikujua kama siku moja ninaweza kumpenda mwanaume kiasi hiki kama nilivyotokea kumpenda Elibariki lakini kwa nini kila pale ninapoanza kuipata furaha hutokea kizingizi na kuikata ghafla.Siku hizi mbili nilizoishi na Elibariki nimejiona kama mtu mpya.Elibariki ni mtu sahihi kwangu na nitafanya kila niwezalo hadi niwe naye katika maisha yangu yaliyobakia.” Akawaza Peniela


******


Ni katika chumba kidogo cha maongezi ya faragha katika makazi ya rais ikulu Dr Joshua alikuwa amekutana na washirika wake wa karibu ,katibu wake Dr Kigomba na daktari wa familia ya rais Captain Amos.Hii ilikuwa ni baada ya kutoka kuonana na Peniela. “ Jamani nimeona niwaiteni kwa dharura kuna jambo nimelipata usiku huu na ambalo hatuwezi kulala bila kulijadili na kulitafutia ufumbuzi.” Akasema Dr Joshua
“Nimepata taarifa usiku huu kwamba jaji Elibariki ameonekana nyumbani kwa Peniela”

“ Peniela?! Akashangaa Dr Kigomba.

“ Peniela yupi? Yule wa kesi ya Edson?
“ Ndiye huyo” akajibu Dr Joshua

“ Peniela ana mahusiano yoyote na jaji Elibariki ? Akauliza Dr Kigomba

“ Sifahamu kuhusu hilo na ndiyo manaa nimewaiteni ili niwaeleze kwamba tunatakiwa tuchunguze kama jambo hili ni la kweli ama si la kweli.”

“ Waliokupatia taarifa hizo wana hakika kwamba Elibariki yuko kwa Peniela? Akauliza Captan Amos
“kwa mujibu wa taarifa niliyoipata toka kwa jeshi la polisi ni kwamba taarifa za Elibariki kuwapo nyumbani kwa Peniela zimetoka kwa mtu wake wa karibu ambaye ni wakili aliyemsimamia kesi yake anaitwa Jason “ akasema Dr Joshua

“ Kama taarifa hizo zimetoka kwa mtu wa karibu namna hiyo basi zinaweza kuwa na ukweli ndani yake lakini lazima tuzifanyie uchunguzi na tuone kama zina ukweli wowote kwa sababu mtu anaweza akatoa taarifa tu za uongo kwa ajili ya kumkomoa mtu fulani “ akasema Captain Amos.

“ Kigomba nakukabidhi jambo hili ulishughulikie haraka na tuujue ukweli.Hili si jambo la kupuuza hata kidogo.Elibariki bado ni mtu hatari sana kwetu na tunatakiwa tumtafute kwa gharama zozote zile ” Akasema DrJoshua na kwa kuwa alikuw amechoka sana kwa gwaride la nguvu alilochezeshwa na Peniela akaagana na wenzake akaenda kupumzika
“ Jambo hili linashangaza sana.Elibariki kwenda kujificha kwa Peniela!!.. Akashangaa Dr Kigomba

“ Kigomba nataka nikushauri kitu chamuhimu.Ukitaka kuupata ukweli wa jambo hili usiutafute kwa mtu mwingine yeyote bali utafute kwa Peniela mwenyewe.jenga urafiki na Peniela.” Akasema Captain Amos

“ urafiki na Peniela? Dr Kigomba akashangaa.
“ Ndiyo,unatakiwa ujenge urafiki na Peniela na hapo utaweza kumchunguza vizuri kama kweli ana\mahusiano na Elibariki .”
Dr Kigomba akafikiri kwa muda kisha akasema
“ wazolako zuri lakini nitampata wapi huyo Peniela? Sijawahi hata kumtia machoni.”
“Hujawahi kuonana na Peniela? Akauliza Captain Amos
“ Hapana sijawahi kuonana naye hata mara moja.Ninachokifahamu kuhusu yeye ni kwamba tulimbebesha mzigo wa mauajiya Edson lakinisijawahi kumtia machoni.”
“ She’s Pretty.She’s an angel.Ni msichana mzuri ajabu.Wewe mwenyewe ukimuona utakubaliana nami.Unawea kuua ndege wawili kwa jiwe moja ” akasema Captain Amos
“ kwa kuwa nimepewa jukumu la kumchunguza basi fanya mpango nionane naye.Mabinti wazuri kama hao ndio ugonjwa wangu.”

“ Nitakufanyia mpango.Kuna watu ninawafahamu wanaweza wakanipatia mawasiliano yake na nikakukutanisha naye.Lakini angalia usije ukajisahau kabisa kwake . “ akasema Captain Amos

“ Hapan Amos siwezikufanyahivyo.Ninafahamu majukumu yangu na kamwe siwezi kutoka nje ya mstari.Fanya mpango nimpate huyo Peniela” akasema Dr Kigomba wakaagana na kila mmoja akaingia katika gari lake.

“ Elibariki anatakiwa aondolewe haraka sana pale kwa Peniela kwani tayari amekwisha gundulika na maisha yake yako hatarini.Huyu Jason ambaye ni mtu wa karibu kabisa Peniela kwa nini avujishe siri hii?? Akawaza Captain Amos.

“ Amesababisha Elibariki awe hatarini na hata Peniela pia.Dr Jason ameanza kuwa na wasiwas na endapo ikigundulika kwamba Peniela ana mahusiano na Elibariki basi mpango wetu mzima utaharibika .lazima Elibarii aondolewe haraka sana pale kwa Peniela” akawaza captain Amos na kufungua sehemu fulani katika gari lake ambako huhifadhi baadhi ya vitu vyake vya siri akachukua simu yake ambayo huitumia kwa mawasiliano ya siri akampigia Jessica na kumpa maelekezo fulani kisha akakanyaga mafuta hadi katika klabu moja ya usiku akaegesha gari akashuka na kuingia katika ukumbi ambao kulikuwa na muziki wa bendi.Watu walikuwa wengi katika ukumbi huo,akajichanganya kati kati ya watu halafu akapenya na kutokea upande wa nyuma ambako kulikuwa na maegesho nyingine ya magari aingia katika gari moja jeusi aina ya Rav 4 ambamo alikuwemo Jessica na kuliondoa gari kwa kasi.
“Una hakika hakuna aliyekuwa anakufuatilia? Akauliza Jessica

“ hakuna aliyekuwa ananifuatilia lakini lazima tuchukue tahadhari kubwa hivi sasa” akasema captain Amos
“ Wamegunduaje kwamba Elibariki yuko pale kwa peniela? Akauliza Jessica

“ Siri imevujishwa na Jason wakili wa Peniela .Sifahamu huyu jason amejua vipi kama Elibariki yuko pale kwa Peniela lakini jambo kubwa la kufanya kwa sasa ni kumuondoa Elibariki pale kwa Peniela ili mambo yetu yaweze kwenda vizuri.” Akasema captan Amos.
Jessica aliendesha gari kwa mwendo mkali wakafika kwa John Mwaulaya .Tayari Amos alikwisha wasiliana na Josh mlinzi wa John ambaye alikuwa akiwasibiri,akawaongoza hadi chumbani kwa John,
“ Amos karibuni sana.Nilikuwa nimelala Josh akaniamsha kwamba kuna jambo la dharura limetokea.Nini kimetokea? akasema John Mwaulaya baada ya akina Amos kuingia mle ndani
“ Tumetoka katika kikao cha dharura usiku huu na Dr Joshua na tayari wamefahamu kama Elibariki yukokwa Peniela”
“ tayari wamejua? Wamejuaje? Akauliza John kwa mshangao

“ Kwa mujibu wa Dr Joshua alyevujisha taarifa za Elibariki kuwepo nyumbani kwa Peniela ni Jason wakili wake.”
“ Huyu Jason amefahamu vipi kama Elibariki yuko pale kwa Peniela? Akaulzia John

“ Hilo ndilo swali ambalo tunatakiwa tulitafutie majibu. Laknikitu cha msingi ambacho tunatakiwa tukifanye kwa haraka n kumuondoa Elibariki pale kwa Peniela.Kuendelea kuwepo pale ni hatari kubwa sana kwetu .Dr Joshua amempaDR Kigomba jukumu la kufanya uchunguzi ili kubaini kama taarifa hizi ni za kweli .Nimeitumia fursa hiyo pia kumshawishi Dr Kigomba aajenge urafiki na Peniela .Hii ndiyo fursa tuliyokuwa tunaitafuta ya Peniela kuingia katika mahusiano na Dr Kigomba kwani rtayari amekwisha onyesha kila dalili za kuvutiwa na Peniela kwa hiyoPeniela anatakiwa aanze kujiandaa,kesho nitamkutanisha na Kigomba” akasema Amos
“Josh mpigie sismu Peniela niongee naye haraka” John akamwambia Josh na bila kupoteza muda akampigia

“ Hallow Peniela.Josh hapa ninaongea.”akasema Josh baada ya Penela kupokea simu
“ Unasemaje Josh?

“John anahitaji kuzungumza nawe’” akasema Josh na kumpatia simu John.

“ hallow Peniela” akasema John
“ hallow baba,unaendeleaje? ” akasema Peniela na kumstua kidogo John
“ Peniela unalia?

“ hapana ninasumbuliwa na mafua kidogo”

“ Pole sana Peniela.Ninajua unalia na ninafahamu kinachokuliza.Ni suala la Elibariki kujulikana yuko kwako”
“ Umekwishapata taarifa? Peniela akashangaa

“Mimi ni Team SC 41 na kila kinachoendelea serikalini ninakifahamu kwa hiyo tayari nina taarifa kwamba Elibariki amekwisha fahamika kwamba yuko kwako”
“ Ni kweli baba,jambo hilo limetokea lakini tayari nimekwisha limaliza.”
“ Umelimaliza? Akauliza John

“ Ndiyo nimekwisha limaliza hilo suala”

“ Umelimaliza vipi? Akahoji John.Peniela akamueleza kila kitu kilivyotokea.
“ Good.Umefanya vizuri sana Peniela .umenifurahisha kwanamna ulivyolishughulikia hili suala na kufanikiwa kumuondoa Elibariki hapo kwako.lakini kuna masuala mawili ambayo nahitaji kuyafahamu.Kwanza huyu wakili wako Jason amefahamu vipi kama Elibariki yuko hapo kwako? Pili nataka kufahamu huyu Mathew rafiki wa Elibariki ni nani? Ninaanza kuwa na wasi wasi yawezekana ukawa unazungukwa na watu wabaya “

“ Kwa kweli hata mimi mpaka hivi sasa sifahamu huyu Jason amefahamuje kama Elibariki yuko hapa kwangu kwa sababu mimi sijawahi kumweleza mtu yeyote kwamba Elibariki yuko pale kwangu na hata Elibariki mwenyewe hakuwahi kumpigia simu mtu mwingine yeyote na kumueleza kwamba yuko kwangu zaidi ya Mathew ambaye ni rafiki yake mkubwa .Kuna kitu kingine nimekigundua kuhusu huyu Mathew .Yeye na yule kijana aliyekufa katika gari la Elibariki walikuwa ni washirika wakubwa..” akasema Peniela

“ Ok niachie suala hii nitalishughulikia na tutaufahamu ukweli .Halafu kuna suala lingine nikwamba Dr Joshua amemuagiza Dr Kigomba kwamba akuchunguze kuhusiana na taarifa hizi za Elibariki kuonekana kwako.Kesho Amos atakuunganisha na Kigomba na tutaingia katika awamu ya mwisho ya operesheni 26B”
“ Sawa baba mwambei mimi niko tayarina awasiliane nami kwa maelekezo zaidi”akasema Peniela

“ahsante Peniela naomba tuoanane kesho asubuhi ilituongee zaidi
“ akasema John na kukata simu akamgeukia captain Amos.

“ Elibariki tayari ameondolewa pale nyumbani kwa Peniela na ameondoka na mtu mmoja anaitwa Mathew. Kuna watu wawili ambao lazima tuwafanyie uchunguzi wa haraka .Kuna huyu Jason wakili wa Peniela halafu kuna huyu Mathew ambaye ameondoka na Elibariki.Elibariki aliwahi kuwasiliana na Mathew akiwa pale kwa Peniela.Nataka kumfahamu ni nani huyu Mathew na ana mahusiano gani na Elibariki kwa sababu inasemekana kwamba yule mtu aliyefariki katika gari la Elibariki ni kundi moja na Mathew.Josh nataka mpaka kesho saa sita mchana Jason awe amepatikana na ahojiwe mpaka aeleze ni kwa nini alivujisha siri polisi.” akasema John
“ Josh unakumbuka kuna wakati niliwahi kutoa maelekezo ya kuweka kamera ya siri nyumbani kwa Peniela? Akauliza John Mwaulaya

“ Ninakumbuka mzee” akajibu Josh
“ Ok vizuri.Nahitaji kuona watu walioingia nyumbani kwa Peniela kuanzia saa moja za jioni.”

“ sawa mzee,ngoja niwasiliane na makao makuu kwani kamera zilizowekwa kwa Peniela zinapeleka picha katika kompyuta za kule makao makuu.”akasema Josh na kutoka na baada ya dakika kumi akarejea
Akiwa ameshika simu kubwa aina ya tablet mkononi
“ tayari nimetumiwa picha toka katika kamera iliyowekwa pale nyumbani kwa Peniela” akasema Josh na kumuonyesha John zile picha..

Sura ya John ikabadilika ghafla baada ya kuwaona watu wawili wakiwa wameongozana na Peniela wakiingia ndani

“ Hebu rudisha nyuma niwaone vzuri watu hao walioongozana na Peniela” akasema John.Josh akarudisha nyuma
“ Ok simamisha” akasema John na kuyaelekeza macho katika sura ya Mathew.

“ Sura hii ni kama ninaikumbuka.Hii si sura ngeni kwangu.Nimewahi kuiona wapi? Akawaza

“ Kumbu kumhu zangu ziko sawa kabisa sura hii nimewahi kuiona sehemu .Lazima nikumbuke nimewahi kuiona wapi? Akafumba macho na kujaribu kumbuka niwapi amewahi kuiona sura ile lakini kumbukumbu hazikuja

“ yawezelana nikawa nimeonana naye kwa miaka mingi iliyopita lakini sura hii ninaikumbuka kabisa na ninaifahamu.Nitarejesha kumbu kumbu hadi nimfahamu mtu huyu ni nani.” Akawaza John


JOHN MWAULAYA AMEIONA SURA YA MATHEW NA ANAHISI KUMFAHAMU.ATAFANIKIWA KUMKUMBUKA? ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII KATIKA SEHEMU IJAYO…………..
 
SEASON2
SEHEMU YA 20
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ tayari nimetumiwa picha toka katika kamera iliyowekwa pale nyumbani kwa Peniela” akasema Josh na kumuonyesha John zile picha..
“ Sura ya John ikabadilika ghafla baada ya kuwaona watu wawili wakiwa wameongozana na Peniela wakiingia ndani
“ Hebu rudisha nyuma niwaone vzuri watu hao walioongozana na Peniela” akasema John.Josh akarudisha nyuma
“ Ok simamisha” akasema John na kuyaelekeza macho katika sura ya Mathew.
“ Sura hii ni kama ninaikumbuka.Hii si sura ngeni kwangu.Nimewahi kuiona wapi? Akawaza
“ Kumbu kumhu zangu ziko sawa kabisa sura hii nimewahi kuiona sehemu .Lazima nikumbuke nimewahi kuiona wapi? Akafumba macho na kujaribu kumbuka niwapi amewahi kuiona sura ile lakini kumbukumbu hazikuja
“ yawezelana nikawa nimeonana naye kwa miaka mingi iliyopita lakini sura hii ninaikumbuka kabisa na ninaifahamu.Nitarejesha kumbu kumbu hadi nimfahamu mtu huyu ni nani.” Akawaza John


ENDELEA……………………….

“ Karibu tena nyumbani Eli.Hapa ni sehemu ambayo tunaweza kuamini ni salama zaidi kuliko kule ulikokuwa” Mathew akasema akimkaribisha nyumbani jaji Elibariki.
“ Ahsante sana Mathew.Niliamini kule ningekuwa salama na hakuna yeyote ambaye angeweza kuhisi kwamba niko kule lakini sifahamu nini kimetokea hadi nikafahamika.Hata hivyo nashukuru mmekuwa karibu name na mmenisaida kunitoa kule.” Akasema jaji Elibariki
“ Siku zote hapa ni nyumbani kwako na ni sehemu salama.Hapa tuna uhakika kwamba tutakulinda kwa gharama zozote zile hata kama ni kwa kuyatoa maisha yetu kama alivyofanya Noah.This is our job and that’s what we do” akasema Mathew.Kauli ile ikamkumbusha Elibariki kuhusu Noah,akaumia sana
“ Kila ninapomkumbuka Noah ninasikia uchungu mkubwa.Ninalikumbuka tukio lile Lilikuwa ni tukio la kutisha sana.Risasi zilivuma kama vile tuonavyo katika flamu lakini hii haikuwa filamu bali ni tukio halisi.” akasema jaji Elibariki.Kimya kikatawala mle sebuleni halafuMathew akasema
“Pole sana Elibariki.Tunashukuru umetoka salama katika ajali ile.Ninaamini huu ni mpango wa Mungu kukuacha hai.Kwa hiyo basi kwa vile wamekukosa sasa kinachofuata ni zamu yao.Tutawatafuta wale wote waliofanya tukio hili na tutawapata.Mimi na Anitha hatutalala usingizi hadi tuhakikishe kwamba tumewapata wale wote waliofanya shambulio lile na kumuua Noah.Tumeumizwa sana kwa mauaji yale ya kikatili .Hatusemi kwamba tunakwenda kulipiza kisasi bali tunataka waovu wapatikane na walipie uovu wao.Lazima tuwajue ni akina nani na nini lilikuwa lengo lao la kutaka kukuua.Ili kuwapata watu hawa tunahitaji sana msaada wako na ndiyo maana nikakuhakikishia kwamba tutakulinda kwa gharama zozote zile.Tutahakikisha unaendelea kuwa salama kwa hiyo basi kabla ya yote tungependa kusikia na kulifahamu kwa upana wake tukio lile lilivyotokea na kama kuna yeyote uliyemuona au unahisi anaweza akahusika na tukio lile.” Akasema Mathew.Jaji Elbariki akatazama juu kwa sekunde kadhaa halafu akasema
“ Kama utakumbuka nilikupigia simu na kukwambia kwamba kuna jambo ambalo ninahitaji kukueleza”
“ Ndiyo ninakumbuka Eli.” Akajibu Mathew
“ Jambo lenyewe lilianza katika ile taarifa ile ya kifo cha Dr Flora mke wa rais uliyonipatia” akasema jaji Elibariki akanyamaza kidogo halafu akaendelea tena
“ Niliiwasilisha taarifa ile kwa familia ya rais na tulimkabidhi rais mkononi na akaahidi kuifanyia kazi.Skuwa na wasiwasi hata kidogo na taarifa ile na niliamini itafanyiwa kazi.Jioni ya siku ile ambayo Dr Flora aliagwa katika viwanja vya ukombozi nilikuwa nimekaa na majaji wenzangu waliokuja kunipa pole kwa msiba wa mama mkwe,nikapigiwa simu na mke wangu na kunitaka nikaonane naye ndani.Nilikwenda kuonana naye na kumbe aliniita nikahudhurie kikao cha familia.Dr Joshua alifika katika kile chumba cha maongezi na ilionekana wazi hakufurahishwa na uwepo wangu pale lakini sikulijali hilo kwani nilikwisha zizoea dharau za familia ile.Kilichonistua ni baada ya kumsikia Dr Joshua akisema kwamba kikao kile ni kwa ajili ya kuisoma taarifa ya madaktari bingwa waliyoitoa baada ya kuufanyia uchunguzi mwili wa Dr Flora.Nilimuuliza Dr Joshua uchunguzi ule ni uchunguzi gani tena wakati nilikwisha leta taarifa za kilichomuua Dr Flora? Nilimchokoza nilipouliza vile na Dr Joshua akaanza kuniporomoshea maneno ya kashfa na dharau.Aliikosoa taarifa ile niliyompelekea na kuiita ni taarifa ya kihuni na ya kuungaunga.”
“ What ?!!..Aliikataaa taarifa ile tuliyoihangaikia usiku kucha? Akauliza Mathew
“ Ndiyo.Aliikataa kabisa na kusema kwamba ni ya kihuni na imejaa uongo mkubwa “
“taarifa iliyotoka kwa hao madaktari bingwa ilieleza nini? Akauliza Mathew
“ Taarifa hiyo ya madaktari bingwa ilisema kwamba Dr Flora alikufa kwa shinikizo la damu na hakukuonekana dalili zozote za sumu katika mwili wake.”
“ Unasema ?! Mathew akaendelea kushangaa
“ Taarifa ya madaktari bingwa ilionyesha kwamba Dr Flora alikufa kutokana na shinikizo la damu na hakukuonekana kuwapo kwa chembe chembe zozote za sumu katika mwili wake.”
“ This cant be..Taarifa hiyo si ya kweli.Ninawaamini madaktari wale waliofanya uchunguzi ule.Ni madaktari bingwa na walitumia muda mwingi kuutafuta ukweli.Kuna kitu kinafichwa kuhusiana na kifo hiki cha Dr Flora.Kuna kitu kinachoendelea ikulu” akasema Mathew na Dr Joshua akaendelea
“Familia ya rais wote walionekana kuikubali taarifa ile ya madaktari bingwa na hivyo taarifa ile ambayo tuliihangaikia ikatupwa kapuni.Nilikasirika sana na sikutaka tena kuendelea kukaa pale nikaondoka na kuja hapa nikakukosa .Nilipokuwa hapa mke wangu akanipigia simu na kunitaka nikaonane naye kuna masuala muhimu anataka kunieleza.Nilimuaga Noah lakini akaomba tuongozane kwa kuwa alikuwa amechoka kukaa nyumbani peke yake.Kwa kuwa nilikuwa nakwenda mara moja na kurudi nikakubali kuongozana na Noah bila ya kujua kwamba ile ilikuwa ni safari yake ya mwisho.Alisema kwamba alitaka kuufanyia mazoezi mguu wake uliopata jeraha wakati wa kumkomboa mke wa Dr Michael .Nilimuachia gari aendeshe na akaendesha vizuri sana tukafika katika makazi ya rais nikaonana na mke wangu lakini tukashindwa kuelewa.Nilimsisitiza kwamba taarifa ile inayodaiwa ni ya madaktari bingwa haikuwa na ukweli wowote ndani yake na kwamba kuna kitu kinajaribu kufichwa.Pamoja na kujitahidi sana kumuelewesha lakini hakuwa tayari kunielewa nikaachana naye na kuondoka.Nilipokishika tu kitasa cha mlango wa gari langu nikapigiwa simu na mwanamke ambaye sikumfahamu ni nani na akanieleza kwamba nisiingie katika gari langu kuna mpango wa kuniua.Hakunitajia jina lake na wala ni akina nani wanaotaka kuniua na kwa kuwa nilikuwa na hasira nilimpuuza na kuingia garini tukaondoka.Sikuwa na wasiwasi wowote kwamba tunaweza kutokewa na tukio lile.Tulipofika katika taa za kuongozea magari za makutano ya barabara ya Mkwavinyika na Kilimanjaro tulisimama katika foleni tukisubiri kuruhusiwa na ndipo lilipotokea shambulio lile. Ninachokumbuka ni kwamba zilitokea piki piki mbili na ghafla Noah akanirukia na kunigandamiza katika kiti na kilichofuata ni milio ya risasi.Nilimsikia Noah akigugumia kwa maumivu kadiri risasi zilivyokuwa zinaingia katika mwili wake.” Jaji Elibariki akashindwa kuendelea kusimulia akanyamaza .Anitha akashindwa kuendelea kukaa pale sebuleni akainuka na kuelekea chumbani kwake akilia.
“ Tuendelee” akasema Noah.
“Baada ya muda mlango wa gari ukafunguliwa na mwanamke mmoja aliyekuwa ameifunika sura yake akanitoa katika lile gari lililoharibiwa vibaya kwa risasi na kuniingiza katika gari lake tukaondoka kwa kasi eneo lile.Nilikuwa nimechanganyikiwa na sikuelewa alikuwa ananipeleka wapi.Mpaka leo hii simfahamu mwanamke yule ni nani na kwa nini aliniokoa.Tukiwa garini akaniuliza kama kuna sehemu ambayo ninaamini ni salama kwa mimi kwenda kujificha kwa muda na sehemu ya kwanza iliyonijia akilini ni kwa Peniela. Kwa bahati nzuri nimekuwa mwepesi sana wa kuzikariri namba mbali mbali za simu na hivyo nikazikumbuka namba za Peniela na Yule mwanamke akampigia na kumuelekeza sehemu atakayotukuta.Peniela akaja akanichukua na kunipeleka kwake.Nikiwa kule kwa Peniela niliwasiliana na wewe na kukufahamisha kwamba niko salama.Hivyo ndivyo namna tukio zima lilivyotokea “ akasema jaji Elibariki.Kimya kikatawala pale sebuleni .Anitha akarejea
“ samahani jamani nilishindwa kujizuia kulia kwa maelezo yale ya Elibariki” akasema Anitha
“ Its ok Anitha usijali” akasema Mathew na kumgeukia Elibariki
“ Elibariki pole sana .Kama nilivyosema awali uko hai sasa kwa uwezo wa Mungu tu na ana sababu zake za kwanini uko hai mpaka leo hii ” akasema Mathew
“ Kuna vitu ambavyo vimejitokeza katika maelezo yako ambavyo vimetuwashia mwangaza na kutuelekeza njia ya kupita ili kuwabaini waliofanya tukio hili.” Akasema Mathew
“kwanza ni hiyo ripoti inayodaiwa ni kutoka kwa madaktari bingwa,pili ni simu uliyopigiwa na mwanamke usiyemfahamu akikuonya kuhusiana na mpango wa kukuua na tatu ni mwanamke aliyekuokoa.Hivi ni vitu vitatu ambavyo vinaweza vikatufikisha mahala tunakopataka yaani kuwapata waliofanya shambulio lile .Sina shaka yoyote na ukweli wa taarifa ile niliyokupatia ambayo ninaamini ndiyo ya kweli kuhusiana na kilichomuua Dr Flora. Watu waliomuua Dr Flora toka mwanzo walifahamu kwamba kuna uwezekano wa kilichosababisha kifo cha Dr Flora kufahamika kwa hiyo wakajiandaa mapema.Kitu cha kwanza walidhibiti uchunguzi usifanyike kwani endapo uchunguzi wowote ule ungefanyika basi ingebainika sababu ya kifo chake na ndiyo maana taarifa za sisi kufanya uchunguzi zilipowafikia ziliwastua sana na kutuma kikosi cha wanajeshi waje watukamate.Hii inaonyesha wazi kwamba kwa gharama zozote zile kilichomuua Dr Flora kitaendelea kuwa siri.Tulipofanikiwa kuipata taarifa ilena ukaifikisha mikononi mwa rais ninaamini walistuka na wakaja na taarifa mpya wanayodai imetolewa na madaktari bingwa.Unaona mahalali walipojikoroga ? Mwanzo hawakutaka uchunguzi ufanyike lakini baadae wanakuja na taarifa ya uchunguzi wa madaktari bingwa.Hii inaonyesha wazi namna walivyochanganywa na taarifa ile ya kwetu.Ili tuwe na uhakika mkubwa na ushahidi mzito i tunatakiwa tuipate hiyo ripoti na tuifanyie uchunguzi ili kubaini ukweli wake.Nguvu kubwa inatumika kuuficha ukweli wa kifo cha Dr Flora ninaamini lazima kuna sababu kubwa nyuma yake ambayo tunatakiwa kuifahamu. Pili tunatakiwa tumfahamu mwanamke aliyekupigia simu ni nani.Huyu ni muhimu sana kwetu kwani ndiye anayewafahamu watu waliotaka kukuua.Huyu ni muhimu mno kumjua.Tatu ni mwanamkealiyekutoa eneo la tukio na kukukabidhi kwa Peniela.Tunataka kumfahamu ni Nani na kwa nini alikutoa pale katika eneo la tukio? Akasema Mathew
“ Mathew uko sahihi kabisa ingawa kuna jambo ambalo umelisema ambalo linaweza likawa na ugumu kidogo kutekelezeka . Ni kuhusu kuipata ripoti hiyo ya madaktari bingwa .Taarifa hiyo anayo rais na sina hakika kama anaweza akitoa kwa mtu mwingine yeyote.” Akasema Mathew
“ Mke wako ni mtoto wa rais kwa hiyo tutamtumia katika kuipata taarifa hiyo.Ninaamini hawezi kukataa kukusaidia ” Akasema Mathew
“ Sina hakika kama mke wangu anaweza akakubaliana nami kwani nimekwisha kwaruzana naye kuhusiana na jambo hili la kuhusiana na ripoti hizi ” akasema Elibariki
“ She’s your wife and you know how to make her understand you.Tumia kila ainaya ushawishi hadi akuelewe.Ni muhimu sana tukaipata ripoti hiyo .Anitha atakupatia simu ambayo utaitumia kuwasiliana na mkeo.Kitu cha pili tunatakiwa tuifanyie uchunguzi namba ile aliyoitumia yule mwanamke kukupigia na kukutaarifu kuhusiana na mpango ule wa kukuua.Anitha ni mtaalamu sana katika sehemu hiyo na atafanikiwa kumfahamu huyo mtu ni nani kisha tutamfuatilia.Tukisha mpata tutafahamu kama ndiye yule ambaye alikutoa eneo la tuko au ni watu wawili tofauti.” Akasema Mathew
“ Tukiachana na hayo” akaendelea Mathew
“ Kuna mambo kadhaa ambao tumeyagundua kuhusiana na kazi ile uliyotupatia ya kuchunguza kuhusu kifo cha Edson na nani alimuua.”
“Mmempata muuajiwa Edson tayari ? Akauliza Elibariki kwa mshangao
“Ndiyo tayari tunafahamu Edson aliuawa na nani ” akasema
“ Ulikuwa sahihi kumuachia huru Peniela kwani si yeye aliyemuua Edson.”
“ Ouh Ahsante Mungu.” Jaji Elibariki akainua mikono juu na kumshukuru Mungu
“ Kumbe nilikuwa sahihi kumuachia Peniela.Kulikuwa na kila ushahidi uliotosha kabisa kumtia hatiani lakini nafsi yangu ilikataa kabisa kwamba Peniela hakufanya kitendo kile .” akasema Jaji Elibariki
“ Nyie majaji ni watu ambao Mungu anawaongoza ili mtoe hukumu ya haki na ndiyo maana ukagundua kwamba Peniela hakuwa na kosa.” Akasema Mathew
“Uko sahihi kabisa Mathew.Kesi ile ni moja kati ya kesi ngumu kuwahi kuitolewa maamuzi.Nilimuomba sana Mungu anisaidie niweze kutenda haki.Ni nani waliomuua Edson? Akauliza jaji Elibariki
“ Kabla ya kifo chake Edson alikuwa amejiunga na matandao wa watu watatu,yaani yeye ,mzee Matiku na na mzee Mustapha.Kwa pamoja walikuwa na biashara ambayo endapo ingefanikiwa ingewaingizia mabilioni ya fedha.Kuna nyaraka zilizokuwa zinatakiwa kuibwa Ikulu na ili kuzipata nyaraka hizo iliwalazimu Mustapha na Matiku kumshirikisha Edson ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ikulu.Edson alifanikiwa kuziiba nyaraka hizo ikulu na kumpatia mzee Matiku.Kabla hawajaziuza ,kwa tamaa ya kupata fedha nyingi,Mzee Mustapha na Edson wakamzunguka mzee matiku na kuziiba zile nyaraka kwa kumtumia msichana aliyekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mzee matiku na nyaraka hizo akakabidhiwa mzee Mustapha.Matiku alipogundua kwamba ni Edson na Mustapha ndio waliofanya wizi ule wa nyaraka kwa lengo la kugawana pesa nyingi wenyewe, alikasirika sana na kuamua kuvujisha siri ile kwa viongozi wa Edson na baada ya wiki moja toka igundulike kwamba ni Edson ndiye aliyeziiba nyaraka zile ikulu akauawa na kesi ya mauaji hayo ikamuangukia Peniela.”
“ Oh my God ! akasema Elibariki.Alistushwa sana na taarifsa zile
“ Kwa hiyo Edson aliuawa na ikulu kutokana na wizi wa hizo nyaraka ambazo tunazo hapa nitakuonyesha.”akainuka Mathew na kuelekea chumbani kwake akafungua kabati analohifadhia nyaraka za siri akatoa ile bahasha iliyokuwa na zile karatasi zilizoibwa ikulu.
“ karatasi zenyewe ni hizi hapa”akasema Mathew na kumkabidhi Elibariki zile karatasi akazitazama akashindwa kuzielewa.
“ Hiki ni kitu gani ? Karatasi hizi ni za nini? Akauliza Elibariki akiendelea kuziangalia karatasi zile bila kuzielewa
“ Hizi ni fomula za kisayansi na sisi sote hapa hatuelewi nini kilichoandikwa humu.” akasema Mathew
“ Hizi ndizo karatasi alizoziiba Edson na ndizo zilizotoa uhai wake ? Akauliza jaji Elibariki
“ Ndiyo.Ni hizi karatasi,hata sisi tulishangaa sana tulipozipata .Hatua ya kwanza tumeimaliza na tayari tunafahamu ni kwa nini Edson aliuawa na sasa tunaingia katika hatua ya pili.Tunataka kulichimba suala hili kwa undani zaidi.Tunataka kulichimba suala hili hadi mzizi wake.Tunataka kufahamu karatasi hizi zina umuhimu gani na kwa nini walitaka kuziuza kwa mabilioni ya fedha.Mtu aliyekuwa akitaka kuzinunua karatasi hizi tumemfahamu , ni mtu tajiri sana anaitwa Habib soud anatokea nchi za kiarabu.” Mara Mathew akastuliwa na simu yake iliyoitwa.Alikuwa ni Eva.
“ hallow Eva” akasema Mathew
“ Mathew..!! akasema Eva huku akilia
“ Eva kuna nini ? Akauliza Mathew
“ Sabina ..Am…amefariki dunia”
Mathew akabaki kimya kwa dakika nzima ,halafu akasema
“ Pole sana Eva.Pole sana.” Akasema Mathew
“ Damu ya Sabina iko mikononi mwako.Wewe ndiye uliyemuua .I hate you Mathew !..akasema Eva na kukata simu.Mathew akasikitika sana na kumgeukia Anitha
“ Sabina is gone “ akasema Mathew.Anitha akastuka na kushika kichwa.
“ Sabina ni nani? Akauliza jaji Elibariki
“ Ni msichana ambaye alikuwa na hizi karatasi” akasema Mathew.
“ Mungu atampokea ameteseka sana.” Akasema Anitha kwa uchungu
“ yah.” Akajibu Mathew na kimya kikapita Anitha akasema
“ Yule jamaa tuliyemuweka mle chumbani una mpango naye gani?
“ hatuna kazi naye tena.”
“ Are we going to free him? Akauliza Anitha
“ Hapana hatuwezi kumuachia.Huyu ni jambazi sugu na yeye na wenzake wamekwisha fanya makosa mengi kwa hiyo tutamuweka humu ndani na baada ya kumaliza kazi zetu tutamkabidhi kwa vyombo vya usalama” akasema Mathew.
“ Ok tuendelee “
“ Kitu cha kwanza ambacho tunatakiwa kukifahamu kwa haraKa ni kwamba karatasi hizi ni za nini na kwa nini zina thamani kubwa namna hii ya mabilioni ya shilingi? Tunatakiwa tumpate mtu wa kutoka ndani ya ikulu ambaye anaweza akatufafanulia kuhusiana na umuhimu wa karatasi hizi na kwa kuzifanya ziwe na thamani ya mabilioni ya shilingi.Hapa ninamaanisha kwamba tukifanikiwa kumpata mheshimiwa rais inaweza ikawa ni vizuri zaidi kwani yeye anaweza akawa na ufahamu mkubwa zaidi wa kuhusiana na karatasi hizi.Kwa kuwa unaukaribu na rais inaweza ikawa ni rahisi kutuunganisha naye lakini kwa namna ulivyoniambia rais alivyolichukulia suala la ile taarifa uliyompelekea ya kifo cha dr Flora nimeanza kuingiwa na shaka kama anaweza akatusikiliza.Hata hivyo tutatafuta njia mbadala ya kufahamu karatasi hizi ni za nini.” Akasema Mathew. Elibariki alihisi kuchanganyikiwa hakujua aseme nini.
“ Mathew kwa kweli nimekosa neno la kusema.Kwanza ninapaswa niwashukuru sana kwa namna mlivyopambana hadi mkafanikiwa kumpata muuaji wa Edson.Nimestushwa sana na taarifa uliyonipa.Sikuwahi kutegemea hata siku moja kama kifo cha Edson kinaweza kutokea katika mazingira haya.Ahsnateni kwa kuufahamu ukweli na msijali ndugu zangu malipo yenu yako pale pale.Kila kitu tulichosainiana kitakuwa vile vile.”Akasema Elibariki
“ Elibariki huu si wakati wa kuwaza kuhusu malipo.Suala hili ni la kwetu wote na tunalifanya kwa moyo mmoja bila kuhitaji malipo ya aina yoyote..”akasema Mathew
“ Ahsanteni sana.Mimi nawaahidi kila aina ya ushirikiano hadi tulifikishe suala hili mwisho wake.Mambo uliyonieleza yamenifumbua macho sana na kuna kitu nimekigundua kuhusiana na kifo hiki cha Edson.Sijawahi kumueleza mtu yeyote jambo hili ni kwamba kilichonisukuma ili nifanye uchunguzi wa kifo cha Edson ni kutokana na shinikizo nililokuwa nalipata toka kwa rais la kutaka nimfunge Peniela gerezani” akasema jaji Elibariki.Mathew na Anitha wakabaki wanatazamana.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………………….
 
Thank you sana LEGE, hope tutapata na asubuh,si unajua binadamu haturidhiki so tuvumilie tu
 
Asante lege .haichoshi kusoma inaonyesha bado ni ndefu mno ila ni nzuri kwa kweli
 
[emoji102] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] vipi nachungulia mzigo bado, aiseeh ikishushwa mnitag
 
pamoja mkuu umeufanya usiku wangu kuwa wa raha
 
Back
Top Bottom