PENIELA
SEASON 4
EPISODE 13
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Mathew maelezo uliyonipa yamenifumbua macho na sasa nimeelewa kilichotokea na kinachoendelea .Nashukuru kwa kunieleza ukweli halisi bila kujali kama ukweli huo utaniumiza ama vipi.Ni kweli nimeumia mno kwa mambo uliyonieleza na hasa kwamba baba yangu ndiye muhusika mkuu wa matukio ya vifo vya mama na Flaviana.Kwa namna moyo wangu unavyosononeka kwa vifo vya watu niliowapenda na kwa sababu hiyo nitaungana nanyi katika kuhakikisha wale wote waliosababisha vifo hivyo awe ni baba au nani lazima wanafikishwa mbele ya sheria.Tafadhali naomba nieleze Mathew unahitaji nini ili tuweze kuwafikisha hawa watu mahakamani? Unahitaji nikusaidie jambo gani? Niko tayari kufanya jambo lolote hata kama ni la hatari kiasi gani ili mradi nihakikishe watuhumiwa wote wanafikishwa mbele ya sheria tukianza na baba yangu.” Akasema Anna huku akifuta machozi.Mathew akamtazama kwa makini usoni
“ She’s deeply hurt and she’s ready to do anything.Huyu atakuwa msaada mkubwa kwetu” akawaza Mathew.
ENDELEA………………..
“ Anna kwanza nashukuru sana kwa kukubali kuniskiliza ,pili kwa kunielewa na tatu kwa kukubali kuungana nasi katika operesheni yetu.Umechagua jambo jema na ninakuahidi kwa niaba ya wenzangu kwamba hakuna yeyote ambaye amehusika katika mambo haya yote atakayesalimika.Lazima wote wafikishwe mbele ya sheria.Pamoja na hayo nataka nikuweke wazi kwamba jambo hili ni la hatari kubwa kwa hiyo utafakari kwa makini na uwe tayari kwa lolote ,muda wowote .Ukumbuke pia kwamba hapa tunazungumzia kumuangusha mtu mwenye mahusiano makubwa na wewe,Dr joshua ambaye ni baba yako mzazi kwa hiyo inahitaji moyo mgumu kuweza kukubali kumuona baba yako akienda mbele ya sheria”
“ Mathew najuta kuwa na baba mwenye roho ya kishetani kama huyu.I hate him so much.Ninakuhakikishia Mathew kwa namna nilivyotokea kumchukia baba yangu niko tayari hata sasa hivi kumuona akianguka katika mkono ya sheria.Sintaumia kabisa kumuona akisimama mahakamani kujibu kwa mambo maovu aliyoyafanya.Mtu kama yule na wenzake wanastahili kifungo kirefu gerezani.Theu are monsters.They don’t have souls! Akasema Anna kwa hasira
“ Ok good.Sasa ni hivi kuna mambo mawili ambayo nataka uyafanye ambayo yanaweza kuwa na msaada kwetu.Kwanza jenga ukaribu na Elibariki na uchunguze ni kitu gani kinachoendelea kati yake na Dr Joshua.Jaji Elibariki lazima atakuwa amemueleza Dr Joshua mipango yetu yote ili kumfanya amuamini na ninaamini kabisa kwamba taarifa iliyotolewa leo asubuhi kwamba Elibariki alikuwa ametekwa na majambazi ni mojawapo ya njia za kumsafisha Elibariki na hapo ndipo unapoweza kuona kuwa kwa sasa Elibariki ni mtu muhimu sana kwa Dr Joshua na ninahisi anaweza akamshirikisha hata katika baadhi ya mipango yake.” Akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“ Jambo la pili linaweza kuwa gumu kidogo kwako lakini hatutalifanya kwanza hadi hapo tutakapofanya maandalizi”
“ Ni jambo gani Mathew? Nimekwambia kwamba niko tayari kwa jambo lolote lile hata kama ni gumu na hatari kiasi gani mimi nitalifanya.Tell me what to do and I’m going to do it” akasema anna kwa kujiamini.Mathew akavuta pumzi ndefu akamtazama Anna kwa makini na kusema
“ We need someone who can have access to President office.Can you do that?
Bila kufikiri mara mbili Anna akasema
“ Ile ni ofisi ya baba yangu na ninaingia mara nyingi sana.Unahitaji nini katika ofis ya rais? Tell me Mathew and I’m going to do it!!
“ Dah ! Nimependa sana ujasiri wa Anna.Haogopi anafaa sana kufanya naye kazi” akawaza Mathew
“ Kwa kuwa nina uhakika kwamba mpaka mida hii tayari Dr Joshua na wenzake watakuwa na mipango mipya baada ya kuelezwa kila kitu kuhusu mipango yetu na jaji Elibarki,njia pekee ya haraka ya kukipata kirusi Aby kabla ya Dr Joshua hajakikabidhi kwa Hussein ni kwa kuingia wenyewe mahali kilipohifadhiwa na kukichukua.Mpaka kesho jioni nina uhakika tayari nitakuwa nimeonana na mtu huyo na nitakuwa na taarifa kamili kuhusu mahali kilipo kirusi Aby.Kwa hiyo basi naomba ujitahidi kupata taarifa zozote zinazoweza kutusaidia kutoka kwa Elibariki na wakati huo huo mimi nikifanya taratibu za kuonana na huyo mtu ambaye anafahamu mahala kilipo kirusi hicho.Tutakapokutana tena tutapanga vizuri mpango mzima”
“ Nimekuelewa vizuri Mathew and I’m ready to find justice for my mother and my sister.I’m not scared to take down my own father!! Akasema Anna
“ Usijali Anna.Haki itatendeka na wote waliohusika kwa namna yoyote na vifo vya Flaviana na Dr Flora hakuna atakayesalimika.Wote watakutana na mkono wa sheria
“ "Thank you Mathew.Lakini bado nina maswali kama mawili au matatu kama hutajali”
“ Uliza Anna”
“ Hicho kirusi Aby kilifikaje ikulu? Kilitokea wapi?
“ Hiyo ni habari ndefu kidogo nitakufahamisha siku nyingine endapo tutakuwa na muda wa kutosha”
“ Sawa Mathew swali la mwisho,Kareem anafahamu chochote kuhusu mambo haya uliyonieleza?
“ Hapana hafahamu chochote”
“ Good.Hatakiwi kufahamu chochote .Ni mtifi sana kwa baba na akifahamu chochote kinaendelea kuhusu baba lazima atamueleza.Mambo haya yanatakiwa yawe siri kubwa.Amekwenda wapi kwani?
“ Wapo chumba kingine wakiongea ili mimi na wewe tupate nafasi nzuri ya kuzungumza bila bugudha na bila ya Kareem kusikia chochote”
“ Unaweza kumuita ili tuondoke? Mda unazidi kwenda na ninadhani tayari tumeongea mengi ya kutosha lakini kabla hatujaondoka nitaomba unipatie namba yako ya simu ili tuweze kuwasiliana “ akasema Anna ,wakabadilishana namba za simu halafu Mathew akaenda moja kwa moja katika chumba cha ofisi alimokuwamo Anitha
“ Anna yuko tayari kuondoka,mstue Kareem” akasema Mathew
“ Mambo yamekwendaje lakini?
“ Kila kitu kimekwenda vizuri.Go get him .Anna is waiting” akasema Mathew na kutoka akarejea sebuleni.Baada ya dakika tatu Kareem akatokea na Mathew na Anitha wakawasindikiza hadi katika gari lao wakaondoka
“ Mambo yamekwendaje? Akauliza Anitha wakati wakirejea sebuleni baada ya akina Kareem kuondoka
“ Tutaongea .Nitawaelezeni kila kitu but I need to see Peniela first if she’s ok”
“ Peniela is ok” akasema Anitha,wakaingia ndani na kuelekea katika ofisi yao na muda huo huo Peniela akatokea
“ How did it go? Akauliza Peniela
“ Mambo yamekwenda vizuri .It wasn’t easy lakini nashukuru amenisikia na kunielewa”
“ Good” akasema Peniela
Mathew akawaeleza kila kitu walichokiongea na Anna
“ I was right then.Anna ni msaada mkubwa kwetu atatusaidia kufanikisha mipango yetu”
“ Ndiyo.Ulikuwa sahihi.Anna atakuw ana msaada mkubwa kwetu.Nimemsoma ,ana nia ya dhati ya kulipiza kisasi kwa vifo vya mama na dada yake.Kwa msaada wake tunakwenda kuchukua kirusi ikulu ,hatuna namna nyingine ya kufanya ili kumuwahi Dr Joshua kabla hajakikabidhi kirusi hicho kwa Hussein.Kwa kuwa nyote wawili hamkuwa tayari kwa mpango wangu wa kumuua Dr Joshua kwa hiyo basi hii ni nafasi nyingine imetokea na tunatakiwa kuwekeza nguvu zetu zote kufanikisha kukichukua kirusi Aby toka mahala kilipofichwa.Tunachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kuwasiliana na Deus Mkozumi yeye atatupa maelezo ya mahala kirusi hicho kilipo.Wakati wa uongozi wake Deus Mkozumi alihakikisha kwamba anakilinda kirusi Aby kwa nguvu zake zote kwa hiyo hayuko tayari kumuona Dr Joshua akikiuza kirusi hicho.Nina uhakika lazima ataungana nasi na atatusaidia katika mipango yetu.” Akasema Mathew
“ Mathew mpango huu ni mzuri sana kuliko ule wa kumuua Dr Joshua.Nina uhakika mkubwa tutafanikiwa .Kuhusu kuonana na Deus Mkozumi hilo halina shaka hata kidogo.Nitalifanikisha hilo.Kama mtakumbuka mara ya mwisho nilipoonana naye alionyesha wazi kuvutiwa sana nami.Huo ni mwanya ambao tunatakiwa kuutumia vyema”
“ No Peniela.You’ve done enough.This time mwili wako hauwezi kutumika kama chambo .We’re going to find another away”
“ Mathew najua unanijali sana na hupendi kuona nikiutumia mwili wangu kama chambo lakini kwa hatua tuliyofikia sasa sina budi kufanya hivyo.Bila kufanya hivyo katu hatutaweza kupata kile tunachokihitaji.Please let me do this”
“ Hapana Peniela imetosha.Safari hii tutakwenda sote kuonana na Deus Mkozumi ,tutamweleza ukweli and he will help us”
“ No Mathew.That wont work.Deus Mkozumi si mtu rahisi kama unavyodhani.Please let me do this my way.Nina hakika tutafanikiwa” akasema Peniela lakini Mathew akatikisa kichwa ishara ya kutokubaliana naye
“ Mathew trust me I’m good at this and I’ve never fail” akasema na kusisitiza Peniela
“ Mathew let Peniela do this” akasema Anitha.Mathew akafikiri kidogo na kusema
“ Sawa Peniela tufanye hivyo unavyotaka lakini moyoni I’m not happy .Tutafanya maandalizi baada ya kurejea kutoka kulichukua kasha alilokupa John lako.Nadhani muda huu ni muafaka kabisa wa kwenda huko mahala ulikolihifadhi
“ Kasha ?!! Anitha akashangaa
“ Ndiyo Anitha.sikukufahamisha kuhusu jambo hili lakini kuna kasha ambalo John Mwaulaya alimpatia Peniela na ambalo lina mambo muhimu sana yanayomuhusu Peniela .Kutokana na unyeti wake Peniela alilihifadhi kasha hilo katika nyumba aliyopewa na Dr Joshua na ambako ndiko tunakwenda kulichukua”
“ Mathew nitakwenda huko peke yangu ,ninyi mtabaki hapa,sintachukua muda mrefu” akasema Peniela
“ Hapana Peniela siwezi kuliruhusu hilo.Kokote utakakokwenda sisi tutakuwa nyuma yako.Tutakwenda sote huko na hakuna mjadala katika hilo.Jiandaeni tuondoke ili tuwahi kurudi” akasema Mathew na kuondoka akaelekea chumbani kwake.
*******
Mara tu baada ya shughuli za mazishi kumalizika,Rosemary Mkozumi alizungukwa na viongozi mbali mbali wakimpa pole kwa masahibu yaliyomkuta.Wengine walimpongeza kwa uamuzi wake wa kutaka kugombea urais na kumpa moyo asikate tamaa aendelee kupambana.Hiki ndicho alichokuwa anakitafuta Rosemary .Wakati akiendelea kusalimiana na watu mbali mbali ,alikuwa macho sana kuangaza huku na kule kumtafuta Dr Joshua.Alihitaji kupata wasaa wa kuongea naye mawili matatu lakini mara ghafla msaidizi wake akamfuata na kumnong’oneza kitu sikioni
“ Madam twende garini kuna jambo nataka nikueleze”
“ Not now !! Bado ninahitaji kuonana na rais..” akajibu Rosemary
“ Madam kuna dharura imetokea.”
“ Dharura gani? Nini kimetokea? Akauliza Rosemary
“ Twende garini” akasema Rita msaidizi wake.Rosemary akaagana na watu ambao bado walikuwa na hamu ya kuongea naye akaelekea garini
“ Rita nini kimetokea? Akauliza baada ya kuingia garini.
“ Kuna taarifa niliyoipokea muda si mrefu kidogo ambayo si nzuri lakini sikuweza kukufahamisha mapema kutokana na shughuli iliyokuwa inaendelea”
“ Niambie Rita nini kimetokea?
“ Ni Fernando”
“ Fernando? Kafanya nini?
“ Is dead”
“ Dead ??.Rosemary akapatwa na mstuko mkubwa
“ When? How?? Akauliza
“ Kwa mujibu wa taarifa niliyopewa ni kwamba Fernando aliondoka nyumbani akiwa na msichana mmoja ambaye alikuwa na hali mbaya na akadai kwamba anaelekea hospitali .Haijulikani nini kimetokea ila Fernando amejirusha toka ghorofa ya tano ya benki na akafariki dunia”
Dakika tatu zikapita Rosemary Mkuzumi akiwa kimya.
“ Please take me home..Hurry !! akamuamuru dereva wake naye akaliondoa gari kwa kazi
“ Ni msichana yupi ambaye Fernando ametoka naye akiwa hoi? Kuna wasichana wawili mle ndani,Anitha na Naomi,ni yupi kati yao ? Naomba isije kuwa ni Anitha kwani nitakuwa nimepoteza kila kitu.Halafu kwa nini ajirushe ghorofani? Hizi taarifa zimenistua mno. Fernando ni mtu ambaye nilikuwa namtegemea mno katika kazi zanu nyingi.Nini hasa kilichomsibu hadi akaamua kuchukua uamuzi wa kujirusha ghorofani?Hapana lazima kuna sababu kubwa,au kuna watu wamemuua?.Nitaufahamu ukweli” akawaza Rosemary Mkozumi.
Alifika nyumbani kwake na kabla hajapokea maelezo yoyote toka kwa walinzi wake akaelekea moja kwa moja katika chumba alimokuwa amefungwa Anitha,nguvu zikamuisha akataka kuanguka bahati nzuri mlinzi wake alikuwa karibu akamdaka na kumketisha kitini.Anitha hakuwemo mle chumbani
“ She’s gone.Msichana aliyeondoka na Fernando ni Anitha.Amempeleka wapi?Mambo haya mbona yanazidi kunichanganya kichwa change kila uchao?.Lazima kuna mahala alimpeleka Anitha .Nina wasiwasi kwamba yawezekana Anitha au wenzake ndio waliosababisha kifo cha Fernando.Nitamsaka kokote hadi apatikane,siwezi kumuacha akapotea hivi hivi.Kitu kingine kinachonisumbua akili kwa nini Fernando alitaka kumpeleka Anitha hospitali wakati anafahamu utaratibu kuwa kama kuna mtu anateswa hata awe katika hali mbaya vipi huwa hapelekwi hospitali na badala yake Dr Abdul huitwa hapa hapa nyumbani kuja kumuhudumia.Ilikuaje hadi Fernando akataka kumpeleka Anitha hospitali? NI kweli alitaka kumpeleka hospitali au kuna kitu kingine kilitokea? I’m confused “ akawaza Rosemary Mkozumi .Akawaomba walinzi wake wamsaidie awe kurejea chumbani kwake.
“ Sintokubali hata kidogo kumpoteza Anitha.Lazima apatikane haraka iwezekanavyo .She knows too much arleady. yeye na timu yake wanaweza kuharibu mipango yangu yote kwani tayari wananifahamu mimi ni nani” akawaza Rosemary akiwa amejilaza kitandani
“ I have to go back and talk to Dr Joshua about this.yeye anao mtandao mkubwa na itakuwa rahisi kwa kutumia vyombo vyake kumsaka Anitha kwani mwanamke Yule ni hatari kwetu sote” akawaza Rose na kuanza kujiandaa kurejea nyumbani kwa Dr Joshua.
********
Idadi kubwa ya wageni waliohudhura mazishi ya Flaviana tayari walikwisha ondoka na hivyo kumpa nafasi Dr Joshua kuendelea na ratiba zake nyingine .Kwa usiku huo alitakiwa kuonana na mjumbe maalum aliyetumwa kutoka Marekani.Kabla ya kwenda kuonana na mjumbe huyo ambaye hakujua ametumwa kitu gani,alihitaji kwanza kuonana na Abel Mkokasule ambaye tayari alikuwa katika chumba ha maongezi ya faragha akimsubiri.
“ Siku imekuwa ndefu mno.Karibu sana Abel” akasema Dr Joshua
“ Ahsante mzee.Pole sana kwa siku ngumu ya leo.Ninafahau ugumu uliopo katika kumzika mwanao kipenzi”
“ Ni kweli Abel ,kumzika mwanao ni jambo linaloumiza sana lakini kama ujuavyo sisi wanaume machozi yetu si machoni sisi tunalia moyoni.Tuachane na hayo naomba unipe ripoti kuna chochote umekipata kutwa nzima ya leo?
“ Tumeendelea kumfuatilia Kigomba kama ulivyoagiza lakini kutwa nzima ya leo ameshinda pale nyumbani kwako ufukweni .Bado vijana wangu wanaendelea kumfuatilia.” Akasema Abel
“ Good.Hajaonana tena na Jacob?
“ Hapana mzee,kwa mchana wa leo hakuonana naye “
“ Vizuri ,najua yeye na Jacob kuna mambo wanayapanga ,leave them to me I know what to do “
“ Sawa mzee ,halafu kuna wale vijana uliiambia kwamba niwaweke tayari kwa ajili ya kazi Fulani ya kuifanya usiku wa leo”
“ Kwa usiku wa leo endeleeni kumfuatilia Kigomba ,kazi niliyotaka muifanye usiku wa leo nimeahirisha hadi kesho.Mfuatilieni Kigomba kwa karibu sana endapo mkiwaona yeye na Jacob wakiwa pamoja unitaarifu mara moja.”
“ Sawa mzee tutafanya hivyo” akasema Abel na kuinuka tayari kwa kuondoka”
“ Abel nashukuru sana kwa kazi nzuri” akasema Dr Joshua na kuagana na Abel
“ I know Kigomba and Jacob are planning something.Kuna kitu wanataka kukifanya .I wont give them a chance to do what they want t do,Im going to surprise them.Hauna wa kushindana na mimi.Yeyote ambaye ataonekana kuwa kikwazo kwangu lazima nimuondoe.Kama niliweza kumkata pumzi mke wangu ,sembuse Kigomba na Jacob? Hawa kwangu ni kama udongo tu ambao muda wowote ninaweza kuufinyanga nitakavyo.Ngoja kwanza nikaonane na mgeni wangu nifahamu ametumwa nini kwangu” akawaza Dr Joshua na kumpigia simu Dr Kigomba akamuuliza endapo maandalizi yote yamekamilika kule nyumbani kwake.Kigomba alimtaarifu kwamba kila kitu kiko tayari na bila kupoteza muda Dr Joshua akaondoka kwenda kuonana na mgeni wake.
********
Hakukuwa na maongezi ndani ya gari wakati Kareem na Anna wakirejea nyumbani.Kila mmoja alikuwa anawaza lake.
“ Baba yangu ni rais wa nchii,we’re the first family,ninaishi maisha mazuri,ninapata kila ninachokihitaji lakini pamoja na hayo yote badala ya kufurahi ninajiona ni mtu mwenye mkosi mkubwa kuliko wote.Najuta kuwa na baba kama huyu asiye na hata chembe ya ubinadamu.Ana roho ya kishetani kabisa.Why could he be so cruel ?? He took away from me all the important people ,the people that I loved the most.Edson, mama na Flaviana walikuwa ni watu walioyafanya maisha yangu yawe ya furaha lakini kwa roho yake mbaya na kwa tamaa zake za utajiri amewaua kikatili bila hata huruma.Kwa hili katu sintomsamehe.Nitashirikiana na Mathew mpaka tuhakikishe baba na mtandao wake wote wanafikishwa mbele ya sheria na kujibu mashtaka ya mauaji.Mambo aliyonieleza Mathew yanaogopesha sana.Amenifumbua macho na nimefahamu kile kinachoendelea.Amenifanya nimfahamu baba vizuri ni mtu wa namna gani.Sikujua kuwa watu niliowaheshimu mno wana roho za kishetani namna hii.Mtu kama Amos sikutegemea kabisa kama anaweza kuwa anashirikiana na baba na akamuua mama yangu.Kitu kama Kigomba ni mtu ambaye ninamuheshimu mno lakini kumbe naye ni shetani tu kwa wenzake.I swear hawa wote lazima nihakikishe wanalipa uovu wao “ akawaza Anna
“ Inanibidi kuanzia sasa niwe makini mno katika kila jambo nitakalolifanya kwani endapo baba atagundua kwamba ninashirikiana na akina Mathew lazima atanifanyia kitu kibaya sana .Kama aliweza kumtoa mama uhai hatashindwa kwangu.” Akaendelea kuwaza Anna na kumkumbuka Mathew
“ Namsifu sana Mathew ni mtu jasiri mno.Amekumbana na misuko suko mingi ikiwamo kusalitiwa na Elibariki lakini bado hajakata tamaa ,amesimama imara kuhakikisha anaiokoa nchi dhidi ya janga baya kabisa linaloweza kutokea endapo baba atakitoa kirusi na kikasambaa hewani.Laiti kama ningemfahamu mapema ,yawezekana hata vifo vya mama na Flaviana vingeweza kuzuilika.Hata hivyo bado sijachelewa nitahakikisha ninampa Mathew kila aina ya msaada ili aweze kufanikisha mpango wake.Akipate kirusi hicho na vile vile kumkamata baba na mtandao wake wote.Nataka kabla baba hajamaliza kipindi chake cha uongozi basi awe mshtakiwa na mimi naapa nitasimama mahakamani kutoa ushahdi wangu dhidi ya baba yangu mzazi.Ninamchukia mno.Hii itakuwa ni funisho kwa marais wengine wajao kuwa ikulu si mali yao.wanapaswa kupaheshimu sana.” Akawaza Anna halafu kuna kitu akakikumbuka
“ Nakumbuka Mathew aliniambia kwamba anashirikiana na Peniela ambaye ni adui wangu mkubwa lakini kwa kuwa sote tuna azma moja sina namna ya kufanya zaidi ya kuweka pembeni tofauti zetu na kufanya kazi pamoja.Itanilazimu niwe mvumilivu japokuwa nitaumia sana kila nikikumbuka kwamba yeye ndiye aliyevunja uhusiano wangu na Edson.”
“ Anna !! Kareem akaita na kumstua Anna toka mawazoni,akainua kichwa na kumtazama
“ Unasemaje Kareem? Akauliza
“ Naomba unisamehe sana kwa jambo nililolifanya la kukudanganya.Sikukueleza ukweli kwa kuwa nilijua hutaweza kukubali kuja .Ukweli ni kwamba sikutumwa na rais nikulete huku bali…”
“ Its ok Kareem,usijali” Anna akakatisha Kareem
“ Anna tafadhali naomba jambo hili lisimfikie rais kwani akijua nimefanya hivi nitakuwa katika wakati mgumu sana” akaomba Kareem
“ Usijali kareem hatajua chochote ila siku nyingine usinidanganye tena,unieleze ukweli”
“ Ahsante sana Anna” akajibu Kareem na safari ikaendelea.Baada ya muda mfupi Kareem akauliza
“ Anna Yule jamaa ni nani? Kwa nini alihitaji kukuona? Anna akamtazama kwa makini na kuuuliza
“ You don’t know him?
“ Sina mahusiano naye ya karibu japokuwa tumewahi kuonana mara kadhaa ila ninayefahamiana naye ni Yule mpenzi wake Anitha Yule dada aliyetukaribisha ndani.Anitha ndiye aliyeniomba nikulete ili uonane na mpenzi wake kuna jambo la muhimu maana anataka kuzungumza nawe” Kareem akamdanganya Anna
“ Kwa hiyo ulinipeleka kwa mtu ambaye humfahamu? Vipi kama angekuwa na nia mbaya ya kunifanyia jambo baya kama ilivyomtokea Flaviana? Akauliza Anna kwa sauti ya juu.
“ Nafahamu nilifanya kosa Anna na ndiyo maana nilitanguliza samahani lakini hata hivyo ninamuamini Anitha na nilikubali kukupeleka kwa kuwa nilijua hakuna jambo lolote baya ambalo lingeweza kutokea .Akihitaji nini Yule jamaa” Kareem akazidi kudadisi
“ Yule ni rafiki wa Flaviana na kuna vitu vya Flavana viko sehemu Fulani na alitaka kunipa maelekezo ya namna ya kuvipata.” Akasema Anna kwa ufupi na kuinamisha kichwa ishara kwamba hakuhitaji tena maongezi.
“ Bado siamaini kama leo nimempata Peniela.Dah ! Yule mtoto anayafahamu mapenzi.Japo ni kwa muda mfupi lakini alinifanya nione kama nina fanya mapenzi na kiumbe mwingine asiye binadamu kutokana na raha niliyokuwa naisikia.Sasa nimegundua kwa nini Dr Joshua humuelezi kitu kuhusu Peniela.Ni kutokana na mambo makubwa aliyonayo .Wanasema bucha ni tofauti lakini nyama ni ile ile lakini kwa Peniela nyama ni tofauti.Ile ni habari nyingine kabisa.I swear I’ll come back.Kazima nimtafute tena Peniela.Amenionjesha asali lazima nirudi tena nionje tena na ikibidi nichonge mzinga kabisa” akawaza Kareem
TUKUTANE SEHEMU IJAYO