Pentagon kuja na Bomu la Nyukilia lenye nguvu mara 24 zaidi ya lile la Hiroshima, Japan

Idara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza kuja na bomu jipya la nyuklia, B61-13, ambalo litakuwa na nguvu mara 24 zaidi ya lile lililoangushwa huko Hiroshima wakati wa Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1945.

Bomu hilo jipya la nguvu ya nyuklia la B61-13 lililopendekezwa na Marekani litabebwa na kuangushwa kutoka kwenye ndege.

Bomu hilo litakuwa na mavuno ya juu ya kilotoni 360, yani mara 24 ya takriban kilotoni 15 ya mavuno ya bomu ambalo lilirushwa kwenye jiji la Japan la Hiroshima mnamo Agosti 6, 1945.

Bomu lililorushwa Nagasaki siku tatu baadaye lilikuwa na mavuno ya takriban kilotoni 25.

Mabomu ya nyuklia ya Nagasaki na Heroshima yaliangushwa bila kuongozwa (free fall due to gravity) lakini hili jipya litakuwa na vifaa maalumu vya kuliongoza na kusaidia kulenga shabaha kwa ufasaha na kulifanya kuwa sahihi zaidi.

Mpango huu unakuja siku chache baada ya China kupanga kuongeza ghala lake la silaha za nyuklia (Nuclear Warheads) hadi zaidi ya 1,000 kufikia 2030.

Kwa sasa Marekani ina vichwa 3,700 vya nyuklia (Nuclear Warheads), na kati ya hivyo 1,419 vimetumwa kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kukaa chonjo dhidi ya vita yoyote itakayojitokeza.

Hata hivyo Bomu la B61-13s litakuwa na chini ya theluthi moja (⅓) ya uwezo wa silaha kubwa zaidi ya nyuklia ya Marekani - Bomu la Nyukilia la B83 - ambalo lina mavuno ya megatoni 1.2, mara 80 ya bomu lililoangushwa Hiroshima, nchini Japan.

Vyanzo: Fox News, Daily Mail UK, Defense News
Wenzao walitemgeneza 1961 wakaona ni ujinga wakaachana nao. Wao ndiyo wanaanza sasa hivi?

Na watampiga nalo nani wakati na wenzao wanalo?
 
Idara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza kuja na bomu jipya la nyuklia, B61-13, ambalo litakuwa na nguvu mara 24 zaidi ya lile lililoangushwa huko Hiroshima wakati wa Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1945.

Bomu hilo jipya la nguvu ya nyuklia la B61-13 lililopendekezwa na Marekani litabebwa na kuangushwa kutoka kwenye ndege.

Bomu hilo litakuwa na mavuno ya juu ya kilotoni 360, yani mara 24 ya takriban kilotoni 15 ya mavuno ya bomu ambalo lilirushwa kwenye jiji la Japan la Hiroshima mnamo Agosti 6, 1945.

Bomu lililorushwa Nagasaki siku tatu baadaye lilikuwa na mavuno ya takriban kilotoni 25.

Mabomu ya nyuklia ya Nagasaki na Heroshima yaliangushwa bila kuongozwa (free fall due to gravity) lakini hili jipya litakuwa na vifaa maalumu vya kuliongoza na kusaidia kulenga shabaha kwa ufasaha na kulifanya kuwa sahihi zaidi.

Mpango huu unakuja siku chache baada ya China kupanga kuongeza ghala lake la silaha za nyuklia (Nuclear Warheads) hadi zaidi ya 1,000 kufikia 2030.
1
Kwa sasa Marekani ina vichwa 3,700 vya nyuklia (Nuclear Warheads), na kati ya hivyo 1,419 vimetumwa kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kukaa chonjo dhidi ya vita yoyote itakayojitokeza.

Hata hivyo Bomu la B61-13s litakuwa na chini ya theluthi moja (⅓) ya uwezo wa silaha kubwa zaidi ya nyuklia ya Marekani - Bomu la Nyukilia la B83 - ambalo lina mavuno ya megatoni 1.2, mara 80 ya bomu lililoangushwa Hiroshima, nchini Japan.

Vyanzo: Fox News, Daily Mail UK, Defense News
mwisho wa dunia hautaletwa na MUNGU,2namsingizia bure MUNGU wangu,,,,tutaleta wenyewe sisi binadam!!!!!
 
Mhhh mbona tayari madude yapo kitambo tu na yapo yenye vichwa mpaka 5 ambapo kila kichwa kina uwezi mara 60 ya lile la 1945??
 
Back
Top Bottom