SAUTI YAKO
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 2,953
- 2,044
Hongereni moja ya taasisi iliyo transform positively ni nyie.Habari, Ndugu Wateja Wetu.
Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kujibu ujumbe wenu kupitia Jamii Forums. Tulipata changamoto ya muda kwenye akaunti yetu, lakini kwa sasa huduma imerejea katika hali ya kawaida.
Tunawashukuru kwa maoni, ushauri na mrejesho wenu kuhusu huduma zetu. Kwa wateja wote waliopata changamoto, tunawapa pole na kuwahakikishia kuwa tupo tayari kuwasaidia. Tafadhali msisite kuendelea kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu kuhusu changamoto, maswali au maoni yenu, nasi tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha mnapata msaada stahiki.
Aidha, TANESCO hutoa taarifa mbalimbali kuhusu huduma zake kupitia njia rasmi za mawasiliano, ikiwemo ujumbe mfupi wa simu (SMS) na makundi yetu rasmi ya WhatsApp yaliyopangwa kulingana na mikoa, wilaya na maeneo mbalimbali.
Iwapo kwa sasa hupokei taarifa hizi na ungependa kuzipata kwa wakati, tafadhali tutumie namba yako ya WhatsApp kupitia inbox pamoja na jina la wilaya na mkoa unaoishi. Tutakusaidia kukuunganisha kwenye kundi husika la WhatsApp na pia kuhakikisha namba yako inaingizwa kwenye mfumo wetu wa kupokea taarifa kupitia ujumbe mfupi wa simu (Bulk SMS).
Asante kwa kuendelea kutuamini na kutumia huduma zetu. Tunathamini ushirikiano wenu na tutaendelea kujitahidi kuboresha huduma zetu ili kukidhi matarajio yenu. ^GK
Habari, Ndugu Mteja.Hongereni moja ya taasisi iliyo transform positively ni nyie.
Tulipotoka hadi sasa na mnapoelekea mnaenda kuweka standard za juu kabisa za viwango vya huduma.
Najua bado mnachangamoto lakni ni zile zinazovumilika na kueleweka.
Endeleeni kufanya mapinduzi.
Piganieni kushusha gharama za nishati, maana ni kilio kikubwa sana kwa wananchi.
Habari, johnmashilatu, na asante sana kwa kuwasiliana nasi.Ni lini mtaanza utaratibu wa token kuingia moja kwa moja kwenyemita, tofauti na ilivyo sasa?
Habari, johnmashilatu, na asante sana kwa kuwasiliana nasi.
Ndiyo, hilo linawezekana. Zoezi linaloendelea nchini kupitia kampeni ya "Mita Janja" linalenga kuwafungia wateja wetu mita janja zinazokuwezesha kununua umeme, ambapo taarifa za ununuzi huingia moja kwa moja kwenye mita bila kuhitaji kuingiza token.
Kwa sasa, huduma ya kufungiwa mita janja ni bure, inafanyika kwa hiari na kwa awamu. Hivyo, zoezi litakapofika katika eneo lako, nawe utafungiwa mita bila gharama yoyote.
Tunakuomba uwe na uvumilivu wakati zoezi hili linaendelea. Litakapokufikia katika eneo lako, usikose fursa ya kupata huduma hii.
Asante na karibu sana. ^FL
Mimi swali nje ya mada:Habari, ndugu mteja.
Asante sana kwa wazo lako na kwa kuonesha nia ya kushirikiana nasi.
Tafadhali fahamu kuwa masuala ya aina hii yanahusisha taratibu za kiutawala na kibiashara, hivyo yanahitaji kufanyiwa majadiliano rasmi na viongozi husika.
Kwa hiyo, kama mwenzetu alivyoshauri, ni vyema kuanza kwa kuwasilisha barua kwa Mkurugenzi Mkuu, au kutembelee ofisi zetu zilizo karibu nawe na uonane na Kiongozi wa Kituo kwa maelezo na mwongozo zaidi kuhusu utaratibu unaopaswa kufuatwa.
Asante sana na Karibu.
Habari, Ndugu Mteja.Mimi swali nje ya mada:
Je utaratibu upoje kuweka meter ya ziada kwenye nyumba ambayo tayari ina meter.
Mfano nina oven, deep freezer, induction na majagi sasa nahitaji mita binafsi kuepusha kelele za wapangaji wengine na kuzimiana umeme
Gharama ipoje?Habari, Ndugu Mteja.
Asante kwa kuwasiliana na TANESCO Huduma kwa Wateja.
Ndiyo, unaweza kuomba kuwekewa mita ya ziada kwa matumizi yako binafsi. Ili kuanza mchakato huo, tafadhali wasilisha ombi kupitia mfumo wetu wa NIKONEKT. Baada ya ombi kupokelewa, afisa wetu wa tathmini (Surveyor) atafika eneo husika kufanya tathmini, kisha hatua zinazofuata zitakuelekezwa, ikiwemo kutengewa Control Number kwa ajili ya malipo.
Unaweza kuwasilisha ombi kupitia tovuti ifuatayo: nikonekt.tanesco.co.tz/application
Wakati wa kujaza fomu:
1. Purpose, chagua "Residential"
2. Application Category, chagua "Separating Supply"
Endelea kujaza taarifa nyingine zinazohitajika, na sehemu ya mita namba weka namba ya mita iliyopo kwa sasa.
Iwapo utahitaji msaada wowote wakati wa kujaza ombi, tafadhali usisite kuwasiliana nasi.
Asante na karibu sana. ^GK.
Baada ya surveyor au fundi kuja kufanya thamnini ndo utajua bei ambayo utailipa kwa namba ya malipo. Ila kwa utaratibu za awali kama kutuma maombi katika mfumo ni bure.Gharama ipoje?
Hapa unaongelea mita mpya na sio kile kifaa cha kutenga matumizi ya umeme katika mita moja ambacho hufungwa zaidi katika nyumba zenye mpangaji zaidi ya mmoja?Baada ya surveyor au fundi kuja kufanya thamnini ndo utajua bei ambayo utailipa kwa namba ya malipo. Ila kwa utaratibu za awali kama kutuma maombi katika mfumo ni bure.