SEHEMU YA KWANZA:
Tangu utotoni nilijuwa kuwa nimejaliwa uzuri wa maumbile na sura. Nikiwa mtoto wa kike wa pekee na wa mwisho wa Mzee Erasto Malyamkono (mtaani alijulikana kama Mzee Mswahili) nilikuwa nimedekezwa nikadekeka. Kaka zangu walikuwa wakinichunga utadhani mboni ya jicho vile, na hakuna kitu nilichotamani ambacho sikukipata. Nilijitahidi kuitunza heshima yangu na heshima ya familia hususan maswala ya wanaume. Nilimaliza kidato cha nne kule Bwiru Mwanza na baadaye kujiunga na shule ya Masista wa Damu Takatifu kule Kifungilo Lushoto. Hadi naanza kidato cha tano nilikuwa bado bikira.
Kabla ya hapo vijana wengi kule mtaani maeneo ya Isamilo walikuwa wakinitaka na kunifukuzia. Nawakumbuka kina Maiko, John, Almasi na Mugisha (alikuwa na umbo kubwa na kakichwa kidogo, utadhani hana shingo) wa pale magorofa ya Benki jinsi walivyokuwa wakinisarandia. Nilikuwa mcheshi na sikuwa na maringo yoyote. Yangu yalikuwa ni maneno na ahadi kem kem, lakini kuwavulia chupi la!! Nilikula vi pesa vyao vya sangara n(a kujinoma kwa tuzawadi twao.) Mademu wengi pale mtaani walinichukia sana, na hawakuficha wivu wao. Wengi waliokuwa wakinitaka walikuwa ni watoto wa wakubwa (miongoni mwao walikuwemo mtoto wa Jaji maarufu na mwingine alikuwa ni mtoto wa RPC). Namkumbuka mhindi mmoja ambaye naye alikuwa akinifukuzia ile mbaya. Nilijiona mimi ni malkia wa mbingu nikiitetemesha nchi kila nipitapo.
Ilikuwa ni huko Lushoto ndiko nilikopata kwa mara ya kwanza kuonja joto la mapenzi. Ilikuwa ni likizo ya pili ndipo nilipokutana na Petro J Shekitondo (Alipenda kuitwa PJ). Basi letu lilisimama pale Mombo kwa ajili ya kujipatia chakula kabla ya kuendelea na safari yetu hadi Moshi. Yeye alikuwa ni mfanyakazi katika Hoteli ya Usambara, mojawapo ya hoteli mashuhuri pale Mombo. Nilikuwa nimekaa kwenye meza moja na marafiki zangu wawili; Sakina Mwanakibili (mtoto wa Mbunge) na Grace Chambi (mtoto wa Katibu wa Wizara, ambaye boyfriend wake alikuwa Mbunge mmoja).
Tukiwa tunapeana gumzo, tulikatishwa mazungumzo yetu na kijana mrefu, aliyevalia suruali ya jeans na T-Shirt yenye maandishi ya Daytona Beach Kifuani. Alikuwa ni mtanashati na sote watatu tulijikuta tukipoteza mtiririko wa mawazo kwa sekunde.
Habari zenu Alitusalimia kwa sauti nzito yenye upole
Powa Tulimjibu kwa pamoja huku tukijifanya hatumjali Mko tayari kuagiza chochote Alituuliza tena akituangalia kwa kutupokeza.
Tupe dakika chache Nilisema kwa niaba ya wenzangu, ambao waliafiki kwani muda wote huo tulikuwa tukipiga gumzo wala hatukuaangalia ile menu ubaoni.
Clara Grace aliniita
Nini Nilimjibu
Mbona unamuangalia kaka wa watu utadhani unataka kummeza! Aliniambia
Hamna kitu, nilikuwa mbali tu Nilimjibu, laiti wangejua ni umbali gani nilikuwa!!
aha! Walihamaki wote wawili kana kwamba hawakuamini maneno yangu. Aliporudi tena alijitambulisha kwetu kwa jina na kuchukua oda zetu.
Tulikula kwa haraka haraka kwani tulianza kusikia honi ya basi letu ikianza kulia. Kama kawaida tuliangalia alipokaa dereva na demu mmoja wakila, hatukuwa na haraka. Tulipomaliza kula tulijiandaa kuondoka. Kabla hata hatujafika nje tukasikia mtu akituita.
Samahani kina dada Alikuwa ni PJ Shekitondo.
Nini tena Tulimuuliza tukishangaa labda tumesahau kitu.
Dada wewe akinionyesha mimi, naomba nikuulize kitu alisema. Tukasogea chemba. Akaja karibu yangu kiasi cha kusikia joto la mwili wake na akasogea kuninongoneza jambo.
Tangu uingie hapa hotelini macho yangu yalikuwa kwako, natamani tufahamiane Aliniambia na sauti kakamavu ilivunja vunja kila vizuio nilivyokuwa navyo. Sikuamini kuwa mwanamme anaweza kunigusa kihisia namna hiyo.
Mbona basi letu liko karibu kuondoka Nilimjibu kwa aibu na kudengua kidogo
Si unasoma Kifungilo Alinijibu kumbe alishajua mimi ni Mwanafunzi.
Umejuaje? Kwani tuna alama kwenye paji? Nilimjibu kwa aibu.
Nimeshawahi kukuona mlipokuja Mazinde Juu kwa debate Alinijibu. Dereva wa basi alitoka nje na kuelekea kwenye basi. Nikajua nilazime niamue haraka.
Sikiliza John Nilimwambia, Ninarudi tena shuleni mwezi ujao katikati, labda tuwasiliane wakati huo au vipi? Nilimwambia.
Poa tu Alinijibu.
Alichukua kipande cha karatasi na kuandika namba yake ya simu na kuniambia kuwa siku nikiwa njiani kurudi nimpigie ili tukutane. Nilimwahidi kuwa nitampigia simu wakati nikirudi toka likizo. Nilikimbilia kupanda basi. Rafiki zangu waliniangalia kwa mshangao jinsi uso wangu ulivyongara kwa aibu na soni. Wakataka niwasimulie yaliyotokea. Nilisubiri kwa hamu siku ya kurudi toka likizo.
Itaendelea.... (hakikisha unarudi kusoma posti hii ya kwanza kwa mwendelezo)...