PENZI LILILOTAZWA.. (Based on A True Story)

PENZI LILILOTAZWA.. (Based on A True Story)

Na. M. M. Mwanakijiji


Moyo ulianza kunienda kwa kasi, viganja vilianza kulowa jasho, na koo lilinikauka nilipokuwa nikikata kona kuingia katika eneo la Hospitali ya Bombo, mjini Tanga. Moyo wangu ulikuwa umegubikwa na ubaridi utadhani alfajiri katika mji wa Makambako kule Iringa. Nilishikwa na huzuni, hofu, na nilihisi kuchanganyikiwa. Akili yangu ilikuwa ikinizunguka utadhani mkokoteni wa kisambaa. Nikifikiri mara milioni ni kitu gani ningekifanya tofauti kukwepa ukweli ambao ulikuwa unanikabili. Nilikuwa natembea kama akili zimeniruka nilipoingia katika geti za hospitali hiyo na hatimaye kwenye wodi ya kina mama. Nilikaribishwa hospitalini hapo na Nesi aliyevalia sare nyeupe na kikofia cheupe chenye mistari ya rangi ya hudhurungi.

"Tafadhali nifuate" Aliniambia Nesi Fatma Ally, ambaye alikuwa amevaa beji yenye jina lake. Walikuwa wananitarajia kwani Nesi Fatma aliniambia walikuta namba yangu ya simu na jina langu kwenye pochi ya mgonjwa.

Bila kufanya ajizi au kuuliza maswali nilimfuata kwa haraka huku miguu yangu nikiihisi kunitetema utadhani miti ya mianzi ipagwapo na upepo. Tuliingia katika Wodi namba tatu ambayo madirisha yake yaliangalia bahari ya ya Hindi. Vitanda vya wagonjwa vilipangwa kinadhifu na wodi nzima ilikuwa inang'ara kufuatia matengenezo ya hivi karibuni kutoka msaada wa serikali ya Ujerumani. Toka mbali niliweza kuona ngalawa na mitumbwi ikipita, wavuvi wakiendelea na uvuviw, na upeo wa mbali wa bahari hiyo niliweza kuona meli iliyotia nanga katika Gati ya Ras Kazone.

Sista Fatma (kama manesi wanavyoitwa) alinielekeza hadi kitanda namba 11 kilichokuwa kwenye kona. Nilisogea na moyo wangu nusura unitoke kwani mpenzi wangu wa moyoni, wa ubani wangu na aliyekuwa nuru ya maisha yangu alikuwa amelala chali akizungukwa na mipira na machine za kila aina zilizomsaidia kunusuru maisha yake.


SOMA ZAIDI HAPA (USIMWAMBIE MTU - NO UNDER 18)

Facebook phising teh teh teh teh teh teh teh
 
dah! Yaukwel na ni nzur umetumia muda gan kutunga au kwanini usiende RADIO FREE AFRICA UKASIMULIE MZAZI mana unajua kutengeneza picha kha!
 
Hakuna sehemu inayoonyesha mlipata wasaa wa kuvaa zana.

sasa mtoto angetokea wapi jameni!?afu kama ni kosa alishakosea mwanzoni so kuvaa tena angekuwa anajidanganya tuu.pia since anasema it's based on a true story,basi manake anatuambia kiuhalisi kabisa kilichotokea kikiwa tu na mguso wa ki-sanii(artistic touch) ndo maana kamanda ana ka-fotokopi ka marehemu zuwena!!
 
sasa mtoto angetokea wapi jameni!?afu kama ni kosa alishakosea mwanzoni so kuvaa tena angekuwa anajidanganya tuu.pia since anasema it's based on a true story,basi manake anatuambia kiuhalisi kabisa kilichotokea kikiwa tu na mguso wa ki-sanii(artistic touch) ndo maana kamanda ana ka-fotokopi ka marehemu zuwena!!

Wakati mwingine watu wanashindwa kuelewa kuwa stori huwa zinaandikwa kwa ajili ya burudani tu; hivi kwenye movie ngapi umeona watu wanaanza kuvaa zana kwanza? Mara nyingi stori hizi ni za kuburudisha, msomaji anatakiwa kujua wajibu wake maana mwisho itakuwa mbona "baada ya kula hawakushirikiana kuosha vyombo".. au mbona "hawakujifunika shuka, ingekuwaje kama mtu anawalia chabo na kuwaweka kwenye youtube"...
 
Mhhh Aksante kuna mistari na mbinu nitajaribu kuzitumia . Yaani tushindwe kuendelea kicuchumi, kiafya kielimu Hata kimapenzi na mahusiano.
 
Mhhh Aksante kuna mistari na mbinu nitajaribu kuzitumia . Yaani tushindwe kuendelea kicuchumi, kiafya kielimu Hata kimapenzi na mahusiano.

Yaani unasema "angalau" katika huku tuoneshe na sisi wamo eh? Well.. tuombe uzime mnaweza kukuta kastori kangu fulani kwenye Lifetime Channel au Hallmark channel.. one of these days.
 
Oooh mwana kijiji nimechemsha, nimesoma weeee si malizi ghafla face book hiyoo eeeh nika sepa aiseee, ntamalizia badae.
 
Back
Top Bottom