Pep Guardiola amejibu tuhuma za Thomas Tuchel

Pep Guardiola amejibu tuhuma za Thomas Tuchel

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari,

Pep Guardiola ametupilia mbali tuhuma za kocha wa timu ya Chelsea, Thomas Tuchel baada ya kusema Manchester city wana bahati ya kuwa na idadi ndogo ya wachezaji waliopata maambukizi ya COVID sambamba na idadi ndogo ya majeruhi ukilinganisha na washindani wenzao wa ubingwa EPL.

Thomas Tuchel aliulizwa kwa namna gani ambavyo kirusi cha Omicron kilivyoathiri kikosi chake maana janga hili limesababisha baadhi ya mechi kuhahirishwa, Ila ikumbukwe Manchester City ilifikia hadi wachezaji saba wa kikosi cha kwanza kukosekana mwisho wa wiki kwenye kombe la FA mzunguko wa watatu ambapo Manchester city iliondoka kwa ushindi wa mabao manne kwa moja dhidi ya Swindon Town, ambapo week hiyo hiyo pia Pep Guardiola na msaidizi wake Juanma Lillo walikosekana sababu walikutwa na maambukizi ya COVID.

Kocha huyu wa Chelsea, Thomas Tuchel amesema leo, Manchester city ambao kesho watakutana na timu yake, wana bahati au wameweza kufanya vizuri kuepuka maambukizi haya kwa wachezaji wao.

Tuchel alisema " Wamefanikiwa vizuri kutokuwa na majeruhi pamoja na maambukizi ya COVID. Inaweza kuwa bahati au wameweza kuchukua tahadhari vizuri zaidi. Na wachezaji wao wachache wamekosekana kwa kipindi kifupi na hiyo ndio tofauti kubwa na kwetu ambayo tumekuwa na wachezaji wengi wenye maambukizi na wamekosekana kwa kipindi kirefu."

Pia kwenye mechi hiyo dhidi ya Swindon Town, kombe la FA, ukiachana na wachezaji saba wa Manchester city kukosekana, Pia kulikuwa na maafisa 14 wa benchi la ufundi walikosekana sababu pia ilikuwa na maambukizi ya COVID.

Manchester City wamekuwa na sera ya kutotangaza majina ya wenye maambukizi lakini wachezaji hawa walikosekana kwenye mechi hiyo Ederson, Stone, Zinchenko, Fernandinho, Jack Grealish, Raheem Sterling na Phil Foden.

Pep Guardiola alijibu tuhuma hizo kwa kusema " Unataka kusema sisi ni welevu zaidi kuliko Omicron?
Tuna idadi kubwa ya majeruhi na maambukizi ya COVID. Na mechi yetu hivi karibuni tulikuwa na wachezaji watano wanaocheza academy wakiwa ndio wachezaji wa ziada.

Tupo kwenye hali sawa kabisa na vilabu vingine juu ya idadi ya maambukizi pia."

Idadi ndogo ya majeruhi sababu tuna idara nzuri ya matibabu, janga hili limetokea duniani kote na limekuja kwa kasi hivyo sisi sio welevu zaidi na kila mmoja anapitia katika kipindi kigumu kwa namna yake.

Guardian hajatoa taarifa yeyote juu ya wale wachezaji saba walikosekana week iliyoisha kama watalejea week hii.

Alisema " Wachache watarudi pia bado wana maambukizi, Ila tuna maambukizi kwa kiwango kidogo siwezi kusema Kwa sababu ni sera yetu kuweka usiri kwa wote wenye maambukizi."

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu
 
Pale Wingereza hakuna kocha atayemweza Pep,sana sanasana Crop ndiye anayejaribu, lakini wengine ni nyanya kwa Pep
Uingereza hakuna kocha aneyeitwa "Crop" labda Uingereza ya ile Ulaya iliyopo kule Kilosa au ya kule Igunga maanake napo kuna Ulaya.🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom