Pep Guardiola na Mapinduzi ya Soka

Pep Guardiola na Mapinduzi ya Soka

Yaan unataka Pep awatumie kina Phil Jones na wavunja kuni wengine ?

Kuhusu kutumia pesa mnamuonea ,dirisha hili man u ,Chelsea, forest wamemwaga pesa kuliko Yeye ,Cha ajabu anawaacha mbali kimbinu
Sasa jamani Nunes na Antony eti 100 million usd
 
Kwasasa mpira umebadilika sana tofauti na enzi za kina Ferguson, Arsene Wenger n.k miaka ya 2000s.

Moja ya watu walioleta mapinduzi ya soka ni Pep Guardiolaz, huyu ana wanafunzi wake wengi sana aliokaa nao na wanaoiga uchezaji wake, kina Xavi Hernandez, Mikel Arteta, Erik Ten hag, n.k

Moja ya mapinduzi aliyoleta ni progressive football kuanzia kwa GK, Overload au Outnumbered kila eneo

Leo nitazungumzia Overload, hakuna kitu nakipenda ninapoangalia mpira na kufurahia ninapoona OVERLOAD, yaani hapa kila eneo unakuta umezidiwa, hiiinakuwaje? Fatana nami uone.

Timu nyingi huwa tunaona zinaingia na mifumo kama 4-3-3,4-4-2,4-2-3-1,3-4-3, n.k.

Hii kwa kawaida ni mifumo inatumika kuzuia, au timu ikishaingia uwanjani ikazuia kwa mfumo mwingine na kushambulia kwa mfumo mwingine.

Mifumo ya kushambulia imekuwa ikitumika kama 2-3-5, 3-1-6, 2-3-3-2, n.k.

Sasa twende pamoja ukaone jinsi Overload, hasa Pep Guardiola anavyoitumia pia makocha Kama Xavi, Arteta ,Erik Tan hag , Graham Potter jinsi wanavyocheza.

Ikiwa timu pinzani watacheza na mabeki wa 5, Guardiola atacheza na wachezaji 6 mbele.

Ikiwa timu pinzani itacheza na wachezaji wawili kwenye safu yao ya mbele(e.g 4-4-2,4-2-2-2,3-5-2,n.k) basi Guardiola utamuona atacheza na walinzi 3 (hivyo 3-1-6).

Ikiwa timu hiyo itacheza 5-4-1 (hivyo mchezaji mmoja katika safu yake ya mbele) Guardiola atacheza 2-2-6.

Man City walipocheza na Bournemouth , Bournemouth walilinda kwa shepu ya 5-4-1.

Manchester City walishambulia kwa uchezaji katika umbo la 2-2-6.

DM wa 2 ili kuwazidi idadi ya CF na 6 kwenye mstari wa mbele ili kuwazidi mabeki wao wa 5.

Angalia hapa,

View attachment 2382936
View attachment 2382937

CMs na Wingers/Full Backs kazi yao ni kuwezesha OVERLOAD katika maeneo mbalimbali.

Mfano mwingine huu hapa;

Nott’m Forest ililinda kwa 5-3-2 ilipocheza na Man City, Guardiola akaseti timu yake katika mfumo wa 3-1-6. Umbo hili linafanana sana na
3-Diamond-3.
View attachment 2382947
View attachment 2382948
Unaweza kuona jinsi wachezaji wa City wa kati wanavyoweza kuwazidi wachezaji wa Forest wa 5 na viungo wao wa 3.

CM ya kati (10) anakuwa huru ku OVERLOAD na kufanya yake.

Twende mfano Mwingine;
Mech ya Manchester City vs Man United.

Manchester Utd walijilinda kwa 4-2-3-1 lakini winga mmoja au AM ndio walitumika kupress CBs za City.

City walicheza 2-3-5 wakiwa na mabeki wa pembeni ili kuzuia mashambulizi ya kukabiliana ya Man U, lakini kama umegundua cha kwanza kama mpinzani atakubonyeza na mchezaji mmoja, basi unawekewa mabeki wawili ili waweze kufanya buildup watoke nyuma (hapa ndipo Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na GK mwenye uwezo mguuni)

Shepu hii ya 2-3-5 ilimpa nafasi katika kiungo wa chini siku hiyo ambaye alikuwa Gundogan (DM) kupeleka mipira kwa Haaland pia KDB na B.Silva kushambulia au kutumia half spaces.

View attachment 2382956
View attachment 2382957

OVERLOAD EVERYWHERE

Mechi ya Arsenal vs Spurs ni mfano wangu wa mwisho.

Conte aliingia na 3-4-3, lakini akawa anacheza kwa 5-4-1.

Arteta akaiseti timu yake kwenye shepu ya 2-3-5, kwanza kuweza kutoka nyuma kwa buildup ya 2v1, halafu kwenye Midfield anaongezeka Zinchenko na kuungana na Xhaka Partey na kufanya 3v2, sababu hawa wingbacks wanatolewa au kuondolewa na winga mbili za pembeni(Saka & Martinell) ambazo watacheza kwa kutanua uwanja hivo wingbacks Emerson Loyal na Perisic inabidi wawafate, na kuacha viungo wao wawili dhidi ya watatu wa Arsenal.

OVERLOAD EVERYWHERE

View attachment 2382967

Note: HII OVERLOAD INAHITAJI WACHEZAJI MAALUM SIYO KILA MCHEZAJI ANAWEZA KUTEKELEZA MAJUKUMU HAYO.
Safi mwanawane. Ila hapo mwisho umetudanganya. Overload haitaji wachezaji maalum. Overload ni kwamba unakuwa na wachezaji wengi kuliko mpinzani wako kwenye eneo ambalo mpira upo. So that said it is not related in anyway to the quality of the player.


Haya sasa twende nddani zaidi ili uelewe somo na peps ideas. Kwanza kabisa katika suala la kushambulia tunatafuta vitu viwili vikuu:

1) quantitative superiority ambayo ndio wewe unazungumzia hapo i.e. overload.
2) qualitative superiority. Hapa nina maanisha kwamba namweka mchezaji wangu mzuri dhidi ya mchezaji dhaifu wa mpinzani. Mfano naweza muweka winger wangu mwenye speed dhidi ya fullback ambaye najua hana speed au my tall striker dhidi ya centreback ambaye hayupo gud aerialy.

Tukienda mbali zaidi ni kwamba timu inapo miliki mpira kuna vitendo vikuu vinne ambavyo watafanya:

1) passing the ball
2) protecting the ball (tulinda mpira)
3) providing support (kumpa usaidizi mchezaji mwenye mpira)
4) pinning (kuondoa usaidizi kwa beki ambaye anakaba)

Hili la 4, pinning lina uhusiano wa moja kwa moja na suala la overload unalozungumzia.
Bila kuubana mstari wa mwisho wa wapinzani inakuwa ngumu kuweza tengeneza hizi overloads. Mfano mstari wa mabeki wanne wanaweza kubanwa na washambiliaji wawili au watatu. Depends na kocha anataka vipi. Lakini tunapendekeza ubane mstari wa mabeki kwa idada pungufu ya wale mabeki. So kama mabeki wapo watano basi wee ubane huo mstari kwa wachezaji wanne. Always one less player than the number of defenders!

Matokeo yake ni kwamba tayari nakiuwa na mtu mmoja ambaye yupo huru (free player) ambaye anaweza kutumika kufanya overloads sehemu nyingine ya uwanja. Pia kumbuka pia kwamba pinning inafanywa sio tuu kwa mstari wa mwisho wa mabeki, unaweza pia fanya kwenye mstari wa midfielders.

Mwisho tunakuka katika suala uliozungumzia kuhusu builup play. Anachotafuta katika first phase ni 'clean progression' nikimaaniaha kwamba nataka kupata mchezaji huru atoke na mpira bila budha yoyote toka kwa mpinzani. Ndio hiyo umesema hapo kama nacheza na mpinzani mwenye forwards wawili basi najaribu progress the ball na mabeki watatu nikijua kuwa wakixhekecha mpira vizuri basi mmoja atatoka na mpira akiwa huru.

Sasa huyu mchezaji huru ndio atajenga overload kwenye eneo la midfield. Lakini ili tuendelee kuwa na mchezaji huru katika kila hatua kuelekea goli na upinzani ndio ile comcept ya 'pinning ' inapo kuja.

So overloads zinatemgenezwa kwa kuwa na uelewa wa namna gani naweza kuibana mistari ya wapinzani kwa mpangilio maalum wa wachezaji wangu na pia kuhakikisha napata 'clean progression' kwenye first phase ya buildup.

Nimependa hii topic, very interesting. Haya ndio mambo ya kuchambua kwa kina sio kupiga porojo za wachambuzi wetu. Let me leave u with this:

Tactics is the intelligent deployment of players and their movement within than deployment.
 
Labda wewe ni Edo ama Dk liki
Edu mchambuzi anae endana na wakati
Edu anajua sana kuchambua mpira, kutoa hints. Kukupa maoni
Edu anachambua soka ili u-enjoy

Dr lik anaujua mpira, mchambuzi mzuri hasa zile games ngumu ngumu
Ikifika half time anakupa real analysis ya game 90% perfectly

Mimi ni mkorea wa jf mkuu[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wachambuzi wengi wa kibongo wanadhani kuuadisia matukio ya kiwanjani ndio kuuchambua mpira kitu ambacho sio kwel lkn umeonyesha mfano wa kuchambua mpra inavyobidi iwe. SAFI
 
Ila kwa aina Ya Timu anazofundishaga Guardiola ni za Viwango vya juu sana (Top 5)

Ili ubora na uwezo wake uthibitike alipaswa Kupewa Timu kama Everton, Brighton au Watford zenye Budget ya kawaida kabisa ndipo ubora wake utaonekana.

Ile Barcelona ya akina Xavi, Iniesta Messi, katika ubora wa ujana wao hata Ungemuweka Mwijaku kuwa Head Coach lazima Wangebeba vikombe.

Hii Man City ya sasa iko kwenye Top 3 ya Timu zilizotumia Fedha nyingi zaidi kusajili wachezaji wakubwa.

Natamani Siku moja nimuone Guardiola akifundisha timu Kama Borrusia Dortmund, Monaco au AS Roma nione...
Mpira sio kufundisha tu kiongozi unahitaji pia watu sahh
Pep ukimpeleka everton atahitaji watu sahh na timu itaanza kubadilika
Mtu kama maguire wa man u 😆 ntaendelea kesho.......
 
Mkuu naomba mnipe mwanga wa kichambuzi kwamba kwanini Pep anapigwa mara nyingi tu na Klop.. Tactics za Pep zinafeli wapi anapokutana na Klop?
 
Back
Top Bottom