Fountain of Youth
JF-Expert Member
- Aug 21, 2019
- 1,026
- 2,299
Mpira wa zama hizi ni uwekezaji mzee hiyo mifano ya Ferguson na Arbedeen ni ya zamani sana mpira umebadilika hizi zama bila uwekezaji na kutengeneza structure nzuri ya timu na kuweka mpunga huwezi kubeba mataji. Hata huyo Fergie mnayemsifia angekuwepo zama hizi bila uwekezaji angelambishwa mchanga.Huyo ni manager wa Billion Pound Squad, kuchukua kombe na Leicester kama Ranieri, Blackburn kama Dalgish, Valencia kama Benitez, Arbedeen kama Ferguson, Porto kama Mourinho hawezi na hawezi hata kujaribu.
Ancelloti mnayemsifia kwamba ni bora (kabeba mataji kila ligi kubwa) si alikuwepo Everton mbona hakuifanya imalize top four tu (achilia mbali kuipa ubingwa). Huyo Mourinho si alikuwepo United timu yenye hela mbona hakuipa ubingwa.
Kubalini tu Pep ana mbinu bora za kufundisha kiasi kaweka high standard ambayo ni ngumu kushindana naye na ukachukua kikombe mbele yake.
Hiyo hoja ya kusema Pep ni billion Pound coach au hawezi kufundisha timu ndogo ni dhaifu ni sawa na kusema kama Ronaldo au Messi ili tuwaone bora basi waende Crystal Palace na waipe ubingwa.