Pep Guardiola ndio Kocha Bora kwa sasa Duniani

Pep Guardiola ndio Kocha Bora kwa sasa Duniani

Baada ya Arsenal kuchezea kichapo cha goli moja kwa bila dhidi ya Nottingham forest ni rasmi ubingwa wa ligi kuu uingereza msimu wa 2022/2023 unakwenda kwa manchester city ambaye anajumla ya point 85 huku anaemfuata Arsenal akiwa na point 81 na amebakiwa na mchezo mmoja mkononi ili kumaliza ligi wakati man city yeye akibakiza michezo miwili.

Ubingwa huu aliochukuwa man city chini ya kocha Pep Guardiola utakuwa ni ubingwa wao wa tatu mfululizo kuchukua chini na Kocha Pep Guardiola akifanya ivyo msimu wa 2019/2020, 2021/2022, 2022/ 2023 Wakati huo huo man city bado yupo kwenye mbio za kugombania makombe mengine fainali kombe la FA Ambayo atamenyana na Manchester United, fainali ya Uefa champion league dhidi ya Inter Milan, Kiufupi Guardiola ameshindikanika.

Licha ya makombe anayozidi kuyakusanya katika club mbalimbali pia guardiola ni kocha anayesifika kwa kufundisha mpira unaovutia kwa watazamaji mpira wa pasi nyingi, ikumbuke ile Barcelona ya akina Iniesta, Xavi na Lionel Messi, ilikuwa ni hatari mpaka Furgeson anatetemeka mikono [emoji1787][emoji1787]. Kumbuka jinsi alivyoweza kuibadilisha Beyern Munich kutoka kwenye piga tukimbizane mpaka mpira wa pasi nyingi.

Haya ni baadhi ya makombe makubwa aliyowahi kuyachukua Mtaalam Pep Guardiola.

1. Uefa champion league..... ×2
2. Uefa Supercup....×3
3. Spanish (Laliga)......×3
4. England premier league.......×5
5. Bundersliga..........×3
6. Fifa club world cup......×3

View attachment 2629308
Fifa club world cup alibeba akiwa na klabu zipi na miaka gani?

Una mahaba hadi unaongeza chumvi [emoji16]

Kabeba mara 2 tu akiwa na Barcelona aliyoikuta ilitoka kubeba UEFA CHAMPIONS LEAGUE chini ya Rijkard.

Mahaba yatakuua wewe Mwa-City [emoji4]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Pep hawezi kama walivyo Makocha wengine pia. Mpira ni uwekezaji huwezi kubeba ubingwa kwa kushindana na timu zenye budget kubwa ndio maana kila siku timu zenye mfuko uliotuna ndizo zinadominate.

Kwa maana hio kama unamuita Pep si kocha bora sababu ni billion pound coach na anafundisha timu kubwa tu nikakuuliza Ancelloti/Mourinho/Fergie ukawapa Crystal palace wanaweza ipa ubingwa?

kitu ambacho unajaribu kukifumbia macho ni kuwa, PEP amespend millions kuwa na timu aliyonayo sasa, anakwenda mwaka msimu wa 7 bado anaitafuta Champion League, Sasa tizama spending ya Carlo toka awe kocha wa Real Madrid na mafanikio aliyoyapata ndio utaona utafauti wao.
 
Kuwa kocha bora haina maana upewe timu yoyote ile
Pep kajitahidi sana kwa bajeti anayopewa kupata wachezaji sahh
Kuna kocha mmoja katumia 100mill kwa kibaka mmoja asiye na msaada kwenye timu 🍻
 
Budget ya clubs anazofundisha huwa unaipitia? Ji kweli ni kocha bora sana, ila nae anakuwa na budget kubwa sana. Hata jana Mourinho alisema, una bench lenye 200m, wakati huo upo na quality ya hali ya juu ndani ya uwanja. Huwezi kulinganisha na hawa wanaopewa limited budget.
Uyo morinyo akae kimya TU mpira ushamshinda,yeye mbona pia kafundisha club kubwa zenye bajeti kubwa ila kimafanikio hamfikii pep hata nusu
 
Kwa hiyo unataka kuniambia Ancelloti/Mourinho/Fergie wakipewa Southampton kwa bajeti kiduchu kama hii walionayo na wakapewa muda wanaweza beba kikombe cha EPL?
Mou mtoe kwenye hii orodha, alishadhihirisha mara nyingi hata kwa bajeti ya kawaida anaweza kupata vikombe.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Ancelloti alipokuwa Everton alikuwa anapigwa na Guardiola nje ndani, sema jamaa aliweza fanya Everton kuwa katimu ka ushindani ila mfumo wa Carlo ule ni WA darasani, ila wa Pep sio wa darasani, ile ni alien level .
Naunga mkono hoja[emoji4]
 
ivi swali nililo uliza na ulicho andika mbona ni IPP
Nimekutafunia jibu kuwa pesa za Chelsea FC zimezingatia FFP ndiyomaana husikii akihusishwa na malalamiko wala mashtaka yoyote maana asilimia kubwa ya Wachezaji waliosajiliwa wamepewa mikataba mirefu sana.

Sasa hilo Kipara lenu mara ngapi lililalamikiwa na FIFA hadi lilishitakiwa kwa ubadhirifu wa pesa kupita kiasi hadi lilikata rufaa?

Je mwaka huu March halikulalamikiwa na kuwekwa chini ya uchunguzi na FA kwa kutofata na kukidhi vigezo vya sheria za FFP kwa makosa makosa zaidi ya 100?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Huyo ni manager wa Billion Pound Squad, kuchukua kombe na Leicester kama Ranieri, Blackburn kama Dalgish, Valencia kama Benitez, Arbedeen kama Ferguson, Porto kama Mourinho hawezi na hawezi hata kujaribu.
Tangu fergi amestaafu mbona man UTD imetumia mabilioni kibao ila hamna kitu[emoji4]
 
Kuwa kocha bora haina maana upewe timu yoyote ile
Pep kajitahidi sana kwa bajeti anayopewa kupata wachezaji sahh
Kuna kocha mmoja katumia 100mill kwa kibaka mmoja asiye na msaada kwenye timu 🍻
Amekaa misimu saba pale man City ndio anainusa CL, hype kubwa tu mnampa ila kwa budget anayopewa hana uspesho kivile.
 
Back
Top Bottom