Pep Guardiola ndio Kocha Bora kwa sasa Duniani

Mkuu mimi huwa nahama na Pep guardiola kila anakokwenda atanikuta nimetangulia .

Kiukweli dunia hii kwa sasa hakuna kocha bora anayefundisha amazing football kama mwamba niko naye hadi atakapoamua kupumzika kufundisha soka.
Mimi nilikua namchukia kwa ishu ya Etoo kipindi kile. Ila baadaye nikaona sawa tu watu weusi ndiyo tatizo. Toka hapo nimeamua nimpende tu kiparangoto.
 
Mkuu unaongelea UEFA as if Pep anazingua sana kwenye UEFA kitu ambacho si kweli.

Pep ana UEFA mbili sawa na mnayemuita kocha bora wa muda wote (SAF) and he's just at the mid of his career.

Pep UCL ameingia back to back UCL semis in consecutive years. Ameingia fainali mbili ndani ya miaka mitatu. Ana longest unbeaten run at home kwenye UCL kwa timu za uingereza. Cime on mkuu kama unapima uwezo wa kocha kwa cup matches na sio marathon ya ligi basi utaniambia kuwa Di mateo au Zidane ni bora kulio SAF.
 
UEFA walishawatuhumu City na hawakuambulia kitu hata hao FA hawatapata kitu. Endeleeni kuota tu mkidhani wale wote mliomaliza wa pili mtapata ushindi wa mezani kwa msaada wa FFP .City won't be found gulty hao FFP watagonga mwamba tu. Man U enzi hizo mmetawala EPL miaka na miaka na palikua hakuna FFP enzi yenu imekwisha huu ni wakati wa ufalme wa City.
 

sasa kama hutaki kipimo cha mafanikio kuwa ndio ubora unataka kipimo gani chengine? wangapi wanatimuliwa timu zao kwa kufika hizo semi finals?
 
Mou mtoe kwenye hii orodha, alishadhihirisha mara nyingi hata kwa bajeti ya kawaida anaweza kupata vikombe.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Swali unafikiri Mourinho ukimpa Hulk City anaweza shinda EPL au Espanyol anaweza shinda La Liga?. Huyo Mou kaenda Tot kafurushwa. Anaweza shinda EPL na Crystal Palace?
 
sasa kama hutaki kipimo cha mafanikio kuwa ndio ubora unataka kipimo gani chengine? wangapi wanatimuliwa timu zao kwa kufika hizo semi finals?
Pep hana UCL? kaingia fainali ngapi na nusu fainali ngapi ukilinganisha na Mou au SAF? unaongelea UCL kama vile pep anatokaga makundi vile. Unashindwa kuelewa kuwa Cup competition inahisisha pia na bahati. Mafanikio pima kotekote usiegemee kwenye UCL tu. Pepe ana UCL 2 sawa na SAF na ndio kwanza yupo katikati ya Career yake unasemaje anazingua UCL.
 
Swali unafikiri Mourinho ukimpa Hulk City anaweza shinda EPL au Espanyol anaweza shinda La Liga?. Huyo Mou kaenda Tot kafurushwa. Anaweza shinda EPL na Crystal Palace?
Umesahau Mourinho alibeba ndoo ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE akiwa na timu gani iliyo na hadhi ya Wachezaji wa kawaida sana kimasilahi lakini aliishangaza dunia ndipo akaletwa Chelsea FC na Tajiri Abrahamovich?

Pep kipara bila pesa hana ubora wowote, fatilia mafanikio yake alitembelea klabu zipi haswa na maranyingi anazikutaga ziko on [emoji91].

Kwangu Ancelloti, Klopp, Mourinho na Conte ni Makocha bora mara 10 zaidi ya Kipara.

Sent from my CPH2387 using

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Achana na huyo kichaa

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Unataka Mourinho apewe timu za kawaida mara ngapi ikiwa 2002 alibeba UEFA CHAMPIONS LEAGUE na Porto FC ambayo ilikuwa na Wachezaji wa gharama za kawaida sana?

Weka hapa sasa timu ndogo ya Pep kupata nayo mafanikio kabla hajafundisha Barcelona FC ujione unavyopumbazwa na mahaba badala ya akili sahihi [emoji16]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 

naona mda wote unafukuzia Mou na SAF hivondio vigezo vyako tu?
 
Kwa hio Porto ni timu ndogo?
 
Bruh bajeti ya man u man city hazipishani sana
Guardiola msimu wake wa kwanza City alipewa €216m. Msimu uliofuata akapewa €317m.

Solskjaer msimu wake wa kwanza United alipewa €234m. Msimu uliofuata akapewa €83m.

City wamiliki wake ndani ya misimu 2 ya Pep wali-invest €533m.

Yani budget aliyopewa Pep msimu wake wa 2 (aliobeba ubingwa) ni budget ya misimu 2 aliyopewa Solskjaer.

Msimu wa 3 na wa mwisho kwa Solskjaer kusajili akapewa €142m hata ukijumlisha bado haifikii pesa aliyopewa Pep ktk misimu 2 na ukumbuke Solskjaer alipewa kikosi kibovu zaidi post Ferguson.

Msimu wa 3 Pep alipewa €78m. Ukijumlisha ni €611m. Msimu wa 4 Pep akapewa tena €166m.

Katika misimu 4 Pep katumia €777m. Huo ni wastani wa €194.25 kila msimu, ambayo hiyo pesa inaweza kusajili wachezaji 3 wa €64.75 kwa msimu na ktk 4 seasons ni 12 players. Na baada ya miaka 7 ndiyo tumeona matokeo ya huo uwekezaji, sasa hivi wanaoanza na wanaokaa bench Man City wana uwezo sawa/unaokaribiana.

Kwenye misimu 7 Pep katumia zaidi ya €1.2B

Sasa niambie ni top manager gani Europe akiwekewa huo mzigo kwa misimu 7 mfululizo hawezi kufanya anachokifanya Pep?
 
Pep is a fraud. Na hii fainali na Inter aki-overthink yatamkuta kama yale ya Chelski ya 2021. Kocha bora fainali ya UCL hauanzi na dm!!
 
Kazi alioifanya Ferguson kwenye Soka ni kubwa sana. Guardiola hata afundishe miaka 50 inayokuja hataifikia.
Ferguson alichukua kombe la Scotland mara tatu mbele ya Old Firm, mpaka sasa Old Firm wanabadilisha hilo kombe hamna mwingine anayenusa.
Pale Manchester United ametengeneza vikosi vinne tofauti vya ushindi. Kuna timu aliyoikuta na baadaye kuwasajili akina Wilkins, baada ya hapo kuna timu ya akina Cantona, Hughes, Kanchelkis. Then kuna timu ya class of 92. Kuna timu ya akina Ruud van, baadaye wanakuja kina Rooney.
SAF aliweza kuhimili changamoto za makocha wengine kama Keegan, Wenger, Mourinho na Mancini na kuibuka mshindi.
Haya mambo Billion squad manager hawezi.
 
Hatuangalii tu kushinda treble tunaangalia ubora wa kikosi hata baada ya kushinda hiyo treble. Angalia rekodi yake mpaka anaondoka Barça ikoje.

Kwa kukusaidia Barça ya 2008-2012 chini ya Pep ilikuwa na ubora wa hali ya juu hii ni baada kukisuka kikosi chake. Hakuna timu Ulaya ingependa ikutane na Barça.

Aliipoteza RMA pale Spain kwa misimu 4 kama haitoshi 2010 RMA wakamsajili Mourinho naye Msimu wa 2010-2012 Mourinho aliipotezwa na Pep pale Spain.

Akiwa Barça kwa misimu 4 amebeba trohies 14, mpaka sasa anashika rekodi ya kocha mwenye mafanikio makubwa kuwahi kuifundisha Barça
● 2 UEFA
● 3 la liga
● 2 Copa de Rey
● 3 Spanish Super Cup
● 2 European Super Cup
● 2 World Club Cups

Achana na mtu anaitwa Pep Guardiola.

NB: Kwa uzoefu wangu mdogo mashabiki wengi wa Man U hawajawahi kumkubali Pep Guardiola
 
Kazi alioifanya Ferguson kwenye Soka ni kubwa sana. Guardiola hata afundishe miaka 50 inayokuja hataifikia
Ila cha ajabu mara 2 kwenye fainali za UEFA Pep alimfundisha mpira unachezwaje mzee Ferguson mwaka 2009 na 2011

Ile fainali ya 2011 baada ya mechi, ona maneno ya Ferguson alivyompa credit Pep: "Pep Guardiola's team is the best team I have ever faced"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…