Pepe na Bruno Fernandes wailaumu Argentina kwa kufungwa jana

Pepe na Bruno Fernandes wailaumu Argentina kwa kufungwa jana

Mpira ulikuwa hadharani.

Uraia wa refa sioni shida sababu mechi naona ilikuws fair.
 
Yaani ina maana walidhani wasingetolewa wangebeba ubingwa? Kweli wanatia huruma. Mbona hata siku moja Messi hutamsikia akionyesha kuwa na ushindani na CR7 lakini kila akiongea Rodaldo lazima directly or indirectly ataonyeshesha uhasimu wake na Messi? Argentina ichukue au isichukue Rodaldo ajue tu kuwa Messi kamzidi saaaana tu. Asitafute marefa
 
Sio kosa lao, maumivu ya kutolewa ndio yanawasumbua, wapewe pole tu.

Ubelgiji alitoka, Ujerumani alitoka, Hispania akatoka, Brazil nae akatoka, wao nani wasitoke?!

Siku zote bingwa atabaki mmoja tu, kama ikitokea wakawa Argentina basi watakuwa wamestahili, hao jamaa wasilete majungu.

Wanashangaza zaidi kumchukia Messi wakati wao walimuweka Ronaldo benchi..!!
Umemsahau Italy yeye hakwenda kabisa
 
Wapewe flash yenye game nzima waangalie halafu waseme ni wapi refa aliwaonea
 
Wapewe flash yenye game nzima waangalie halafu waseme ni wapi refa aliwaonea
Jamaa umenifanya nimecheka kifala fala sana.Mpaka jirani kakasirika hapa...hahhahaahaahaha

Buruuuno Fernandes alijikuta keki sana ile siku...wakapelekewa moto wa Casablanca.

Anafikiri ni yeye tu mwenye shida na Kombe na zile hela za nusu fainali?

Morocco wanatafuta hela waje wajenge kiwanja chetu pale Idodomya.

Historia ya Morocco na Portugal inaeleweka
11 Jun 1986 -World Cup :Morocco 3- 1 Portugal nintini kweusi huko babu zao walikula mzigo na hapo bado tulikuwa utumwani, walitakaje?

20 Jun 2018-World Cup :Morocco 0- 1 Portugal hapa angalau tuna umeme na maji ya kusua sua wakatupiga, hatukusema ila tukaambiwa Waafrica hatujiwezi World cup.


Juzi wamebinuliwa kamoja tu ...povu Kontena.

Ronaldo alicheka sana alipokuwa kule kwenye Tunnel..mana kale kadogo huwa kana roho pana sana.
 
Makasiriko tuu hayo ya kufungwa na timu waliyoidharau
 
Argentina anaenda kubeba hilo kombe habari inaishia hapo, yule Croatia anapasuliwa ndani ya dkk 90 mapema..
 
Cwezi shangaa hasa kwa huyo mapepe na christina namna walivyokuwa wakimchukia LAPUGA pale walipokutana ktk ELCLASICO
 
Wachezaji wa Ureno Pepe na Bruno Fernandes wanamlaumu Messi na Argentina kwa kufungwa jana.
Wanasema kuwa FIFA inamuandalia Messi kombe la dunia kwa lazima na ndio maana refa wao aliwekwa wa Argentina aliyekuwa anaipendelea Morocco.

My take: Hawa wametumwa na binadamu mwenye wivu mwingi kuliko kipaji aitwaye CR7View attachment 2443268View attachment 2443269

Kwahiyo wewe umelichukuliaje hilo? Umeamini kisemwacho na hao wachezaji?
 
Hawa wa portuguese ndio kawaida yao kulialia nini!, hata ndugu zao brazil walivyonyukwa na france 1998 na akina fundi zizou tulisikia malalamiko. Ni upumbavu mtupu, waache kulialia,

Safi sana Morocco, endelezeni kichapo mtuheshimishe wa-Afrika

Vamos Argentina 🇦🇷
Vamos Morocco 🇲🇦
 
Uyo refa jana kachezesha poa sana wangepewa yule refa aliyecheza Argentina na Holland wangesemaje??

Acha walalamike tushawazoea hata brazil baada ya kunyooshwa na ufaransa ya akina zinedine zidane 1998, tena goli 3 safi, tulisikia malalamishi yasiyokua na kichwa wala miguu

Morocco mmetunyooshea hao jamaa, na bado ufaransa

Vamos Argentina 🇦🇷
Vamos Morocco 🇲🇦
 
Back
Top Bottom