PERLUIGI COLLINA: HANA MFANOWE

PERLUIGI COLLINA: HANA MFANOWE

Nihzrath

Member
Joined
Jan 15, 2013
Posts
51
Reaction score
116
NA
NIHZRATH NTANI

Jioni moja ya mwaka 1977 ndani ya mji wa Bologna nchini Italia. Vijana wadogo wenye umri kati ya miaka 15-18, walikuwa na mechi kati yao. Mechi yao iliwakutanisha watoto wa kutoka sehemu ya Tuscany na wale kutoka eneo la Forte du Marmi.

Ni mechi iliyojaa upinzani mkubwa kwa vijana hao jioni hiyo. Hata hivyo , mechi hiyo haikumalizika katika muda sahihi, baada ya kujaa maamuzi mengi yenye utata. Mwamuzi alionekana kuwabeba mno vijana kutoka katika eneo la Forte du Marmi.

Ndani ya timu ya wavulana kutoka eneo la Tuscany. Mvulana mwenye umri wa miaka 17 wakati huo ,alionekana kuchukizwa mno na maamuzi mabaya kutoka kwa mwamuzi dhidi ya timu yake.

Kijana huyu alicheza nafasi ya kiungo ndani ya timu hiyo. Hasira za kijana huyu zilimfanya aanze kuuchukia mchezo wa soka. Aliamini kuwa mchezo wa soka hauna haki.

Chuki dhidi ya mwamuzi yule zikamfanya aukache mchezo wa soka na badala yake akaelekeza nguvu kucheza mchezo wa Basketball.

Marafiki zake walijaribu kumshawishi kurejea katika soka. Ushawishi wao haukuleta maana kubwa ndani ya akili ya mvulana yule. Alisimamia alichokiamini.

Miezi michache ndani ya mwaka 1977. Marafiki zake wale wale wakajaribu tena kumshawishi kwa mara nyingine angalau ajifunze kuwa mwamuzi ili aweze kutenda haki kama anavyoazimia.

Ombi hili lilipokelewa kwa tabasamu lenye kumaanisha ndani ya akili ya kijana yule. Ndipo alipoamua kuanza kuhudhuria kozi ndogo ndogo za uamuzi wa soka ndani ya mji wa Bologna.

Miaka 27 baadae ,tangu ombi la kuanza mafunzo ya uamuzi wa soka kulikubali. Kijana yule alikuwa anastaafu kazi ya uamuzi katika soka. Ajabu ilioje!

Pamoja na kustaafu kwake kwa mujibu wa sheria lakini uamuzi huo ulileta simanzi na huzuni kuu kwa wadau na mashabiki wengi wa soka Duniani.

Akiwa na miaka 45 hadi kufikia mwaka 2005 alipostaafu. Huku akiwa na miaka 58 hivi leo. Kijana yule ndio huyu anayeitwa Pierluigi Collina. Hauhitaji kufungua vitabu vingi vya historia kujua mtu huyu alikuwa nani?

KWANINI NIMEAMUA KUMZUNGUMZIA PIERLUIGI COLLINA?

Unahitaji mistari miwili au mitatu kujaza makosa yake dimbani. Lakini unaweza kuhitaji kurasa zenye kujaza kitabu kizima kuweza kuuandika umakini na ukamilifu wake dimbani.

Ni kwamba ,alikuwa na makosa machache zaidi wakati alipokuwa akichezesha soka. Bila shaka,Pierluig Collina aliishi katika mtazamo na ndoto aliyoiota angali kijana mdogo zaidi.Ndoto ya kuona haki ikitendeka uwanjani. Kizazi cha sasa hakikuweza kumshuhudia mtu huyu. Huzuni ilioje!

Wakati huu. Waamuzi wengi wamekuwa wana makosa mengi lenye kuleta utata. Utata wenye kuumiza. Malalamiko dhidi ya waamuzi ni kama jambo lenye kuzoeleka machoni na masikioni mwetu kwa sisi wapenda soka Duniani.

Lakini ilikuwa nadra kuyaona makosa wakati filimbi ikiwa mdomoni mwa Pierluigi Collina dimbani.Iwe ndani ya viwanja vya Nou Camp, Santiago Bernabeu, San Siro, Olympic kule Rome ,Estadio Da Luz kule Lisbon ama Old Trafford .Mioyo yetu ilikuwa ikiridhika na uamuzi wake.

TUNAZO KUMBUKUMBU NYINGI DHIDI YAKE.

Pierluig Collina hapana shaka ndiye Pele au Maradona wa waamuzi katika historia ya soka Duniani. Ndiye, anayetajwa kuwa mwamuzi bora wa miaka yote. Jina lake linatukumbusha.

Achana na usiku wa September 1,2001 ,wakati timu ya Taifa ya England ikiwachakaza wajerumani katika mechi ya kugombea kufuzu michuano ya kombe la Dunia ndani ya ardhi ya wajerumani.

Sahau usiku wa Juni 30,2002 kule ndani ya dimba la kimataifa la Yokohoma nchini Japan, kwenye ile fainali ya kombe la Dunia kati ya Brazili na Ujerumani.

Ni usiku wa Mei 26,1999 kunako dimba la Nou Camp jijini Barcelona. Ni usiku wenye furaha na huzuni kwa wakati mmoja . Usiku utakaoendelea kukumbukwa kwa miaka mingi ijayo kwa sisi tulioushuhudia.

Ni fainali kati ya Bayern Munich na Manchester United. Magoli mawili ya Manchester United katika dakika za lala salama yakifuta goli la mapema la Bayern Munich. Magoli hayo ya kusisimua yalileta mtikisiko mkubwa usiku huo. Hakuna aliyeamini ukweli huo.

Ni tukio ambalo litachukua miaka mingi kutokea tena. Kwangu mimi mechi hiyo naichukulia kuwa mechi bora zaidi ambayo macho yangu yaliwahi shuhudia maishani.

Mwamuzi wa mechi hiyo alikuwa Pierluigi Collina. Achana na uamuzi wake. Collina alionesha yeye ni binadamu kati ya binadamu wenye huruma na utu. Filimbi ya mwisho alipohitimisha.

Ilimuacha akibakia uwanjani huku wachezaji wa Manchster United na mashabiki wao wakizunguka kama vichaa kwa furaha uwanjani hapo.

Macho ya Collina yalibakia yenye huzuni alipokuwa akiwatazama wachezaji wa Bayern Munich walipokuwa wakilia huku wengine wakiwa wamejiangusha chini kwa majonzi.

Collina alifanya kazi ya kuwabembeleza na kuwanyanyua miongoni mwao akiwemo Stefan Effenberg na Lothar Mathaus. Kitendo hichi kilichukuliwa kwa namna ya kupekee sana usiku huo.

NYAKATI HAZIWEZI RUDI TENA NA KUMSHUHUDIA MTU HUYU.

Inaumiza ukifikiria.Inatia hasira unapoyaona makosa ya wazi ya waamuzi hivi leo. Mtu huyu alikuwa mfano bora wa wapenda haki pamoja na makosa yake machache aliowahi kuyafanya.

Golikipa wa zamani wa Ujerumani Oliver Khan anamtaja Collina kama mwamuzi wa aina yake lakini mwenye laana kwa upande wake. Hakuwahi kuibuka na furaha baada ya filimbi ya mwisho ya Collina akiwa golini. Ajabu nchini Uturuki jina la Collina linatukuzwa mno kama mtu mwenye bahati na nchi hiyo.

Timu ya Taifa ya Uturuki pamoja na klabu za nchini humo hazikuwahi kupoteza mechi hata moja wakati mwamuzi alipokuwa Collina akichezesha. Imani ilioje!

Alitambulika kwa kipara chake kichwani. Kipara kilichosababishwa na ugonjwa wa kunyonyoka nywele wa Alopecia. Macho yake makali yenye umakini. Tungali tukikumbuka pia lile tabasamu lake liliowafanya wachezaji wengi wakiziachia hasira zao na kumtii.

Namna alivyokuwa makini na maamuzi yake. Alivyokuwa akikimbia kwa kufuata uelekeo wa mpira .Hakika ilikuwa burudani kubwa kwa Pierluigi Collina kumtazama.

Mwamuzi huyu aliyekuwa na elimu ya degree ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Bologna. Mwaka mmoja kabla ya kustaafu kuchezesha soka yaani mnamo mwaka 2004.

Chuo kikuu cha Hull cha nchini Uingereza kilimtunuku shahada ya PHD katika sayansi. Kwa mchango wake wa kuendeleza michezo Duniani.

Kwa kipindi cha miaka 27 ya kazi yake. Aliweza kuchezesha jumla ya mechi 464 huku akitoa kadi nyekundu za moja kwa moja 131.

Na akitoa kadi nyekundu zilizotanguliwa na kadi ya njano jumla 48.Huku pia akitoa kadi za njano jumla 1437. Alifanikiwa kubeba tuzo ya mwamuzi bora wa soka Duniani kwa miaka 6 mfululizo. Ni rekodi hadi hivi leo.

Pia ,nchini Italia akifanikiwa kubeba tuzo ya mwamuzi bora wa Italia mara saba. Hakuna kama yeye. Mpaka sasa hajatokea kama mtu huyu katika soka. TUNAMKUMBUKA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba picha yake iwekwe hapa.

Naomba nijulishwe kama picha hiyo inahitaji kulipiwa.
 
Collina
images%20(3).jpeg
images%20(2).jpeg
 
Alitenda haki ila.sasa refarii wametingwa na teknklojia kila sehemu inawabana kutitenda haki.
Web alikua bonge la.boya kati ya marefarii ninaowafahamu
 
Aisee tuachie Web wetu bhana!
 
Alikua na macho makali, wale wachezaji wakorofi wote walinywea, nakumbuka alisema kama Italy itaingia final WC 2002 basi atakosa kuchezesha final, mwisho wa siku Italy hakuingia na kipenga kilipulizwa nae
 
Back
Top Bottom