Personal Floating Device (PFD)

Personal Floating Device (PFD)

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
5,489
Reaction score
14,091
Hii ni koti la kujiokoa (Life jacket/ Life vest) ambalo mfumo wake ni tofauti na life jacket nyingine.

Hili lina umbo la kawaida na mtu akivaa huwa kama mikanda ya reflector.

Lina kuwa na vyumba vilivyojazwa hewa ya Carbon dioxide na endapo mtu ataingia au kuzama kwenye maji atavuta kamba na litajaa na ataelea kama amevaa boya la kawaida.

Pia lina mfumo wa kujifyatua endapo mtu atazama au kuingia kwenye maji ghafla kama hajavuta kama, Kutokana na presha ya maji ( Hydrostatic release) kuna kitu kina ncha huwa kinatoboa na boya hujaa haraka hivyo mvaaji uelea kwenye maji.

Faida ya PFD ni rahisi kuvaa na halimsumbui mvaaji pia usalama ni mkubwa kwa mtumiaji.
20191017_235851.jpg
IMG-20191016-WA0004.jpg

Pichani ni wanajeshi wa maji wa India wakiwa wamevaa PFD.
 
Vipi likisha jaa hewa na baada ya mtumizi linaweza kurudi kama mwanzo au ni matumizi ya mara moja tu?
 
Vipi likisha jaa hewa na baada ya mtumizi linaweza kurudi kama mwanzo au ni matumizi ya mara moja tu?
Utapeleka sehemu ambayo wanafanyia service ili ijazwe tena gesi ya Carbondioxide. Hii kama air bag ikiisha tumika lazima ifanyiwe marekebisho tena.
 
Kwa ruhusa yako, naomba nitoke kidogo nje ya mada.
1.Vipi kuhusu gharama za kupark (mahali wanapo park boat) unapo miliki boti yako binafsi?
2.Naomba utueleze kuhusu mafunzo ya uendeshaji boat ndogo binafsi/yatch. Yanachukua muda gani, vigezo, ada n.k

Bila shaka watu wengi wangependa kujua kuhusu hayo. Natanguliza shukrani
 
Utapeleka sehemu ambayo wanafanyia service ili ijazwe tena gesi ya Carbondioxide. Hii kama air bag ikiisha tumika lazima ifanyiwe marekebisho tena.
Bila shaka hizi hazipo sana kwa matumizi ya raia wa kawaida. Hata kwenye masoko sijaziona kabisa
 
Bila shaka hizi hazipo sana kwa matumizi ya raia wa kawaida. Hata kwenye masoko sijaziona kabisa
Zipo kwa ajili ya matumizi ya kawaida, hizi ni maboresho ya kisasa kwenye life jacket.

Kwenye chombo cha majini life jacket la kawaida ni lazima(Mandatory) yawepo kulingana na idadi ya abiria wanaoingia au kufanya kazi.

Kwenye meli za kisasa au baadhi ya kampuni wanatumia hizi kwa kuwa hazimpi uzia mtumiaji. Na sasa kuna PFD za kisasa ambazo unaweza ukaivaa kama saa ya mkononi endapo utaingia kwenye maji itaji activate na utaelea kama umevaa life jacket.
 
Nashukuru kwa kulifahamu hilo
 
Bila shaka hizi hazipo sana kwa matumizi ya raia wa kawaida. Hata kwenye masoko sijaziona kabisa
Kwa sasa hii ni kama luxury life jacket.

Ni sasa unapoendesha pikipiki lazima uwe na helmet ili kujilinda, lakini helmet hiyo sharti iweze kukinga kichwa. Ila kuna helmet za kisasa zenye system ya kutoka hewa,muonekano nadhifu.
 
Back
Top Bottom