Kuna Dada yangu aliambiwa Kuna wazungu Kenya wananunua pasi za miaka ya 1930 kwa million 30 kwa pasi moja. Jamaa aliemwambia ivo akamwambia Kama anayo aseme au akiipata amuunganishe. Bahati nzuri home kwao wanayo yaani imetumika vizazi Kama vinne mpaka sasa.
Alinipigia akiomba ushauri eti aifuate hiyo pasi Mbeya aje kuiuza awe milionea. Nilimwambia atulie kwanza asome upepo, haukupita muda mtu mwingine ambae baadae ilikuja kufahamika kuwa ni timu moja na mtoa taarifa alimwendea sister na kumuuliza Kama anawajua wanaonunua vitu vya zamani amuunganishe maana yeye anapasi anaiuza kwa laki 2 tu maana anashida ya haraka.
Huyo sister kwa hesabu za haraka aliona anaenda kuwa na pesa ndefu maana angekua na pasi mbili pamoja na Ile ya familia. Bahati mbaya hakua na hiyo pesa na walishuka mpaka laki 2, aliponijulisha nilimwambia asitoe hata Mia wamtafute huyo mzungu pamoja wakiwa wote watatu yaani mleta taarifa, muuza pasi na yeye. Ndani ya masaa hakuwaona tena na walihama eneo lile.
Haya Mambo huenda kweli yapo na watu wanauza hizo pesa lakini tanguliza umakini.