Pesa imepotea kwa mazingira ya kutatanisha

Pesa imepotea kwa mazingira ya kutatanisha

DR SANTOS

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2019
Posts
12,846
Reaction score
28,106
Habari wana jamvi

Leo katika pita pita zangu nikaingia mgahawa mmoja kwaajili ya kupata breakfast ambapo nilifika na kuagiza na nikaletewa kama nilivoagiza baada ya kula nikatoa noti ya shilingi elf kumi na kumkabidhi yule mama ambapo alinirudishia chenji ambayo ni shilingi elf 6 niliipokea na kuiweka kwenye mfuko wa shati kwani niliona uvivu kuiweka katika wallet kwakuwa nilikuwa na safari fupi ambayo lazima ningehitaji kuitumia pesa hio.

Hatua chache baadae nilipanda bodaboda ambayo ilinifikisha hadi ninapokwenda lakini ipofika saa ya kutoa nauli kwenye mfuko washati sikukuta hata senti

Shida hapa sio elfu sita em tujadili kidogo hivi hizi mambo za chuma ulete bado zipo?
Na kinga yake ni nini?

Nikawaza what if ningechanganya na pesa zangu za kwenye wallet si zingekwenda zote sasa😀
 
Duuh! Teknolojia ya Muafrika Ni Balaaa......
 
Hakuna cha chuma ulete walanini hapo hiyo pesa ilipeperushwa na upepo.
 
Uliangusha hela mkuu,

Hayo mambo yapo ila sio ktk namna ilivyokutokea wewe
 
90% hiyo pesa umeangusha. Huwa inatokea unapoingiza mkono mfukoni kuweka pesa unachomoa mkono na pesa hutoka kufata mkono.
 
mfuko wa shati huwa siuamini kbs..ukiinama tuu ela imeenda
 
Back
Top Bottom