Pesa kuingizwa nchi moja toka nchi nyingine

BatteryLow

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2011
Posts
446
Reaction score
149
Nilisikia kwamba Benki Kuu ndiyo hudhibiti mzunguko wa fedha katika nchi na ndiyo inayoachia kiwango maalumu cha fedha kuingia ktk mzunguko huo kwa sababu za kiuchumi. Je, inakuwaje pale pesa zinapopelekwa/zinapoingizwa kwenye nchi nyingine? Mfano Tz kuna fedha zinazohamishwa taslimu kupelekwa nje na siyo kwamba kuna bidhaa au huduma itakayoletwa/itakayopelekwa kuuzwa hapa/huko na kurejesha ile fedha? Transactions za aina hiyo siyo kwamba zinavuruga kile kiwango kilichotolewa na Benki Kuu kiwe kwenye mzunguko? Athari zake ni zipi? Naomba elimu kidogo hapo!
 
Nenda Monday pale BOT ukaulize swali ukiwabana sana wanaweza kukupa kibarua pale.
 
Kuna wafanyabiashara wengi wa nje wanahamisha dola taslimu kupeleka nje, wanaogopa wakiweka benki kuna watu wanadodosa akaunti zao na watagundulika wana pesa nyingi na hawalipi kodi. Kuna mmoja alishapigwa cha moto njia ya Namanga akanyang'anywa boksi 3 zimejaa $!
 
Mimi naona kinacho athrika ni bei ya kuchenji hiyo shilingi kwenda kwenye hiyo hela ya kigeni. Kwa mfano kama hiyo hela inayohamishiwa nchi nyingine ( Maana si shilingi) ni dollar ya Marekani na ni watu wengi wa kiwango kikubwa kinachotaka kuhamishwa basi bei ya kuinunua hiyo US Dollar kwa hapa Tz kitapanda. Kwa maana hiyo shilingi nyingi zitatumika kuinunua US Dollar, na hapo ndio utasikia shilingi imeshuka bei. BOT wao wana regulate au kurekebisha kiwango kinachotoka kulingana na reserve au akiba ya hiyo hela ya kigeni inayolipwa nje. Sijui kama nimeeleza vizuri lkn wataalamu wataongezea.
 
Nilisikia kwamba Benki Kuu ndiyo hudhibiti mzunguko wa fedha katika nchi na ndiyo inayoachia kiwango maalumu cha fedha kuingia ktk mzunguko huo kwa sababu za kiuchumi. Je, inakuwaje pale pesa zinapopelekwa/zinapoingizwa kwenye nchi nyingine? Mfano Tz kuna fedha zinazohamishwa taslimu kupelekwa nje na siyo kwamba kuna bidhaa au huduma itakayoletwa/itakayopelekwa kuuzwa hapa/huko na kurejesha ile fedha? Transactions za aina hiyo siyo kwamba zinavuruga kile kiwango kilichotolewa na Benki Kuu kiwe kwenye mzunguko? Athari zake ni zipi? Naomba elimu kidogo hapo!

According to the financial act 2006/2010 hairuhusiwi kusafirisha pesa nje zaidi ya usd 10,000 zaidi ya hapo ni hadi upate kibali BOT kwanza
 
Mimi naona kinacho athrika ni bei ya kuchenji hiyo shilingi kwenda kwenye hiyo hela ya kigeni. Kwa mfano kama hiyo hela inayohamishiwa nchi nyingine ( Maana si shilingi) ni dollar ya Marekani na ni watu wengi wa kiwango kikubwa kinachotaka kuhamishwa basi bei ya kuinunua hiyo US Dollar kwa hapa Tz kitapanda. Kwa maana hiyo shilingi nyingi zitatumika kuinunua US Dollar, na hapo ndio utasikia shilingi imeshuka bei. BOT wao wana regulate au kurekebisha kiwango kinachotoka kulingana na reserve au akiba ya hiyo hela ya kigeni inayolipwa nje. Sijui kama nimeeleza vizuri lkn wataalamu wataongezea.
Ni kwamba hakuna bei ya kuchenji kwani zinasafirishwa dola taslim moja kwa moja bila kupitia Bur de Change wanaenda ku deposit nje ya nchi!
 
Back
Top Bottom