BatteryLow
JF-Expert Member
- Aug 14, 2011
- 446
- 149
Nilisikia kwamba Benki Kuu ndiyo hudhibiti mzunguko wa fedha katika nchi na ndiyo inayoachia kiwango maalumu cha fedha kuingia ktk mzunguko huo kwa sababu za kiuchumi. Je, inakuwaje pale pesa zinapopelekwa/zinapoingizwa kwenye nchi nyingine? Mfano Tz kuna fedha zinazohamishwa taslimu kupelekwa nje na siyo kwamba kuna bidhaa au huduma itakayoletwa/itakayopelekwa kuuzwa hapa/huko na kurejesha ile fedha? Transactions za aina hiyo siyo kwamba zinavuruga kile kiwango kilichotolewa na Benki Kuu kiwe kwenye mzunguko? Athari zake ni zipi? Naomba elimu kidogo hapo!