BatteryLow
JF-Expert Member
- Aug 14, 2011
- 446
- 149
Nilisikia kwamba Benki Kuu ndiyo hudhibiti mzunguko wa fedha katika nchi na ndiyo inayoachia kiwango maalumu cha fedha kuingia ktk mzunguko huo kwa sababu za kiuchumi. Je, inakuwaje pale pesa zinapopelekwa/zinapoingizwa kwenye nchi nyingine? Mfano Tz kuna fedha zinazohamishwa taslimu kupelekwa nje na siyo kwamba kuna bidhaa au huduma itakayoletwa/itakayopelekwa kuuzwa hapa/huko na kurejesha ile fedha? Transactions za aina hiyo siyo kwamba zinavuruga kile kiwango kilichotolewa na Benki Kuu kiwe kwenye mzunguko? Athari zake ni zipi? Naomba elimu kidogo hapo!
Ni kwamba hakuna bei ya kuchenji kwani zinasafirishwa dola taslim moja kwa moja bila kupitia Bur de Change wanaenda ku deposit nje ya nchi!Mimi naona kinacho athrika ni bei ya kuchenji hiyo shilingi kwenda kwenye hiyo hela ya kigeni. Kwa mfano kama hiyo hela inayohamishiwa nchi nyingine ( Maana si shilingi) ni dollar ya Marekani na ni watu wengi wa kiwango kikubwa kinachotaka kuhamishwa basi bei ya kuinunua hiyo US Dollar kwa hapa Tz kitapanda. Kwa maana hiyo shilingi nyingi zitatumika kuinunua US Dollar, na hapo ndio utasikia shilingi imeshuka bei. BOT wao wana regulate au kurekebisha kiwango kinachotoka kulingana na reserve au akiba ya hiyo hela ya kigeni inayolipwa nje. Sijui kama nimeeleza vizuri lkn wataalamu wataongezea.