Pesa Mtandao

LessKnown

Member
Joined
Oct 24, 2024
Posts
81
Reaction score
104
Kwa wale tuliozoea neno 'Tigopesa' na uhusiano wake na huduma inayopatikana ya 'Pesa' kwa njia ya mtaandao wa TIGO, mnaonaje matumizi ya neno jipya la 'Mixx by Yas' lisivyo na uhalisia/ufanani na huduma inayotolewa ya 'Pesa'!

Inawezekana wahusika na kubadilika kwa jina hilo wana maana nzuri tu kwa upande wao, lakini kwa mimi mlaji/ninayetumia huduma hii, labda na wengine kama imewakwaza, tukiwa maeneo mbali mbali ya nchi ni kama wametutoa kwenye uelewa na mazoea tuliyodumu nayo kwa muda mrefu ya uwepo wa neno 'Pesa' kwenye huduma za aina hii.

Labda wangetuwekea neno angalau hata 'Mixx Pesa' ili kuleta uhalisia wa huduma inayotolewa ikimaanisha kutuma na kupokea pesa kwa njia ya mtadao wa 'Mixx' kama walivyoita. Wadau nini maoni yenu juu ya hili?
 
YAS PESA AMA YAS MONEY haya mawili ndio rahisi kwa watanzania nje na hapo watatusumbua!
 
Neno Tigopesa litaendelea kudumu midomoni mwa watu kwa muda mrefu sana kama ilivyo kwenye vituo vya kujazia mafuta vyote kuitwa "Shell" japo kampuni hiyo imeondoka Tanzania miaka mingi iliyopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…