Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Whethe mpango huo wa kitapeli utafanikiwa ama laa, lakini mwisho wa siku pesa ndio itakayo wagombanisha na kuvuana nguo hadharani uongozi mpya wa chadema. Ni suala la muda tu kwa jambo hilo kutokea.
Baada ya kuacha misingi ya kuanzishwa kwake, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kimejigeuza ni taasisi ya fedha na kujikita zaidi katika kuhakikisha inatumia njia zote kupata pesa kwaajili ya matumizi ya viongozi wake waandamizi na kuachana kabisaa na mambo ya kuchochea na kutetea haki, uhuru, usawa na Demokrasia, na kufikia hatua mpaka ya kupuuza na kususia uchaguzi ili kujiepusha na kushika dola na kuunda serikali na kuongoza nchi.
Pia soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Soma Pia: CHADEMA wazindua mkakati maalum wa kidigitali wa tone tone, Februari 27, 2025
Chadema chini ya uongozi mpya haitaki kabisa kuskia wala kujihusisha na masuala ya kushika dola, kuunda serikali wala kuongoza nchi, bali inataka kushika pesa tu kwa namna zote zile kwa manufaa ya HQ.
Sasa kwa hali ilivyo,
Ni wazi wahamasishaji na wasimamizi wa mfumo wa ukusanyaji wa pesa hizo wote ni wajanja wa mjini, hawaaminiani lakini pia hawaaminiki hata kwa wanachadema wenyewe na wanainchi kwa ujumla na ndiyo maana hata zoezi la uchangiaji linaenda kwa mwendo wa kobe. Ni kwasababu waliowekwa mstari wa mbele katika uhamasishaji hawaaminiki kulingana na historia mbovu za utapeli na upigaji walizonazo.
Matumizi ya pesa, kuzidiana kete kwenye kuzichota na kuzitafuna, ndiko hasa kutawafarakanisha na kuwasambaratisha hao wangwana, na hapo wanachadema wataanza kujua na kufahamu mambo mengi kuhusu michango hii ya pesa kwamba ilikua ni utapeli na ililenga kumnufaisha watu binafsi na sio chama.
Kuna kila dalili kwamba wapo watakao sepalea ughaibuni na mlungula wa maana wa wananchi na hapo ndipo itakua chanzo cha kujua mengi zaidi kwasasababu wataanza kuvuana nguo wao kwa wao, na kupelekea, the end of chadema in Tanzanian political scene.
Mungu Ibariki Tanzania.