Pesa uliyopata kwa jasho lako kwa mara ya kwanza uliipata ukiwa katika steji ipi ya maisha?

Pesa uliyopata kwa jasho lako kwa mara ya kwanza uliipata ukiwa katika steji ipi ya maisha?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Leo nimemkumbuka anko wangu aliyefariki kabla sijqanza hata vidudu lqkini nilikiwa najitambua.

Uncle akiwa darasa la tano, alikuwa amejijengea chumba chake cha kulala hapo nyumbani. Alikuwa na marafiki hadi wazungu alipokuwa form 1. Alikuwa anafuga kuku, bata na na anapiga pesa huku shuleni yuko vizuri hadi alipofariki kwa kuvimba tumbo ghafla ( ilisadikiwa alitiwa sumu na majirani au alipata shambulizi la kitamaduni akiwa form 1 mwishoni)


Hii iimenifanya leo nijikumbushe, hivi ni lini nilipata pesa yangu binafsi.
Binafsi ilikuwa darasa la nne, mvua kubwa ilinyesha, nikatoroka nyumbani kuingia korogoni na chepe, nilikusanya mchanga na mabro wa kita. rundo langu nilimuuzia mqma Dani kwa Tsh 2000.

Hiyo ndio pesa yangu ya kwanza kuipata kwa kujitafutia mwenyewe.
Matumizi
Tsh 100 nilienda kunyoa kwa fundi .
Tsh1900, niliagiza pipi,soda, mandazi,, vibaragara, bajia nikaarika washkaji tukavula kurudisha afya iliyopotea wakati wa utumishi ule. Pesa hiyo ilotakiwa iishe siku hiyohiyo maana nyumbani wangejua ningepigwa zaidi ya Bonge aliyenurika kutekwa kiluvya.

Ni hayo tu.

Mara yako ya kwanza kupata pesa kwa jasho yako ilikuwa ni lini na wapi na ilikuwaje mkuu.

Karibu
 
Ilikuwa 6000 ya kung'oa kisiki kikubwa sana cha muwembe.. Nilifanya hiyo kazi kwa siku tatu

Nilikuwa bado nahemea kwa bro

Mia saba nilijipongeza na chipsi yai na kifurushi cha kuku (kichwa, makanyagio vimeviringwa na utumbo)
Mia ya tatu nikajipongeza na viroba vitatu vya Power no.1

Buku mchumba

Elfu nne nikasunda
 
Back
Top Bottom