mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Mjadala ulijitokeza miaka iliyopita kuhusu pesa za Escrow zilikuwa za umma au siyo za umma. Waliokuwa wanasema si za umma kimsingi walikuwa wanatetea upigaji wake na serikali isiingilie.
Waliokuwa wanasema ni za umma walikuwa wanatetea maslahi ya umma ikizingatiwa kuwa zilikuwa zinahifadhiwa benki kuu na wajanja wakafanya mchongo wa kuzipiga na kutetea kuwa hamna shida maana siyo pesa za umma.
Hali kama hiyo imeanza kujitokeza hasa baada ya dalili za awali kuonesha kuwa mradi huo wa filamu ya The Royal Tour utaingiza pesa nyingi licha ya kuvutia watalii wengi. Watu wameanza kuhoji hizo pesa zinazoingizwa na filamu hiyo ni za serikali au?
Maandalizi ya kutoa jibu hilo tayari yanaonesha dalili kuwa kuna ujanja unatumika pesa hiyo kuingia mikononi mwa wajanja!! Kiongozi mkubwa kabisa wa serikali amesema, " Zile pesa sh bilioni 7 zilizotumika kuandaa filamu hiyo hazikutoka seikalini, bali serikali iliyachangisha mashirika (bila shaka ya umma na ya binafsi) ili kupata pesa hizo".
Tujiulize maswali mawili:
1. Kwanini kauli hiyo itoke sasa wakati watu wameanza kuhoji mapato ya filamu hiyo yataishia wapi na nchi yetu itafaidikaje?.
2. Ina maana serikali ikipata mapato kwa njia ya harambee (kwa hapa harambee ya mashirika), mapato hayo hayatakuwa ya serikali?
Inajulikana kuwa serikali hupata mapato yake kwa kuchangisha kwa mfano kodi. Kodi ni mchango, tofauti yake tu ni kuwa ni mchango wa kisheria kwa hiyo si wa hiari.
Niishauri serikali yetu kuwa jambo hili halijakaa vizuri na linafukuta moto, litakuja kuiweka serikali katika hali ngumu mbele ya safari.
Nashauri serikali itangaze rasmi tangu mwanzo kuwa mapato yatakayotokana na mauzo hayo NI YA SERIKALI.
Isisubiri kuangalia upepo nukoje, itakuja imweke MAMA kwenye kona na wenzake WATAMRUKA kimamba!
Karibuni tujadili.