Kwa ss tulioajiriwa mwaka jana' ilikua kama ifuatavyo:
Halmashaur za Majiji na Manispaa n Tsh 65,000 kwa siku 1 na hutolewa pesa ya siku 7 kwa maana 65,000×7. Halafu kwa halmashauri za wilaya n Tsh 45,000 kwa siku 1 vilevile hutolewa kwa siku 7 kwa maana ya 45,000×7.
Kuhusu kuingia Payroll hapo kuna tatatizo sana ila itategemea ushapu wa watendaji wa halmashauri kuingiza taarifa zenu kwenye LOWSON huu mfumo unatuma taarifa kwa mtandao mpaka Ofis ya utumishi wa umma makao makuu then wakishapitia taarifa zako wanazituma hazina kuu' zikifka hazina kuu wao wanakuingiza kweny payrol na utapata cheque no.yako.
ANGALIZO: Mfumo huu wa LOWSON kwa ss wa mwaka jana ulisababisha watu kuingia payrol kwa makundi makundi, wapo waliingia mwez April, wengne Mei, June na wengine walifika mpaka July. Kwa sasa serikali imeeanza kulipa fedha za wale waliochelewa kuingia Payroll tumejikuta tunaingiziwa mshahara double ktk mwez mmoja.