Pesa za kununua mechi zipo, za kulipa deni hazipo?

Pesa za kununua mechi zipo, za kulipa deni hazipo?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
SAKATA LA MTIBWA DHIDI YA YANGA

🔋 Wakati Yanga wanakubaliana uhamisho wa Kinda Abou Msheri kutoka Mtibwa, walitaka kulipa ada ya uhamisho kwa mikupuo miwili (installments)

🔋Mtibwa walisema wazi kuwa wao wanachotaka ni pesa yote kamili kwakuwa hawana haraka nayo, Mtibwa ikaomba ipewe tarehe maalum ya kulipwa pesa yao yote

🔋Yanga wao walisema pesa yote italipwa DECEMBER 30, Mtibwa walikubaliana na hilo kwakuwa waliwaamini Wananchi na wakakamilisha paperworks zote

🔋Ule muda wa Mtibwa kuingiziwa pesa yao ulipofika haikutumwa hata senti kutoka Yanga, Mtibwa walivumilia kwa wiki mbele kisha kuwapigia kuomba feedback kuhusu malipo

🔋Majibu ya muda wote yalikuwa “tunashughulikia”, “tupo kwenye mchakato” lakini Manungu walisema wapewe tarehe nyingine sahihi ya kuingiziwa pesa yao, Yanga wakatoa tena ahadi

🔋Usiku wa deni haukukawia kukucha, ilipofika tarehe simu hazikuwa zikipokelewa na Viongozi wa Yanga, Mtibwa walituma email, texts WhatApp na simu za kawaida ila hapakuwa na majibu

🔋Katika harakati za kuhitaji mzigo upatikane, CEO alionana na Viongozi wa Yanga, February 23 pale Manungu na mbele ya Mchezaji wakahaidi kulipa siku ya Jumatatu ila ikapita hakuna pesa

🔋Danadana zimekuwa nyingi mpaka hii leo, majibu hayaridhishi kutoka kwa Viongozi wa Yanga na Mtendaji Mkuu wa Mtibwa anakiri wazi kuwa kuna uungwana unakosekana wakati wanapodai haki yao, mara hawaoni emails, mara subirini

🔋Mtibwa wanafikiria Jumatatu wapeleke malalamiko rasmi TFF kuhusu madai yao kutokana na mauzo ya Mchezaji wao

🔋Mtendaji anakiri wazi kuwa licha ya jitihada kubwa za Mtibwa kulea Vijana na kuisaidia nchi lakini kadhia kama hizi zinawaumiza sana Wawekezaji wa Mtibwa na Viongozi, kudai haki imekuwa kama Uadui

🔋Walimruhusu Kijana aende sio kwamba hawakuwa wakimuhitaji ila walikubali ili Kijana atimize ndoto yake, huo ndio uungwana, ni wakati sasa wa Yanga kuwa waungwana
 
Kama ni hivyo basi Simba ndio ilikua timu Ya kwanza kumuuzia Yanga mechi ya Ngao ya jamii.
Ile game ya Ngao ya Jamii ilikuwa fluk...Lakini hamna uwezo wowote ndo maana mnatumia bahasha kwa timu nyingine..!
 
SAKATA LA MTIBWA DHIDI YA YANGA

🔋 Wakati Yanga wanakubaliana uhamisho wa Kinda Abou Msheri kutoka Mtibwa, walitaka kulipa ada ya uhamisho kwa mikupuo miwili (installments)

🔋Mtibwa walisema wazi kuwa wao wanachotaka ni pesa yote kamili kwakuwa hawana haraka nayo, Mtibwa ikaomba ipewe tarehe maalum ya kulipwa pesa yao yote

🔋Yanga wao walisema pesa yote italipwa DECEMBER 30, Mtibwa walikubaliana na hilo kwakuwa waliwaamini Wananchi na wakakamilisha paperworks zote

🔋Ule muda wa Mtibwa kuingiziwa pesa yao ulipofika haikutumwa hata senti kutoka Yanga, Mtibwa walivumilia kwa wiki mbele kisha kuwapigia kuomba feedback kuhusu malipo

🔋Majibu ya muda wote yalikuwa “tunashughulikia”, “tupo kwenye mchakato” lakini Manungu walisema wapewe tarehe nyingine sahihi ya kuingiziwa pesa yao, Yanga wakatoa tena ahadi

🔋Usiku wa deni haukukawia kukucha, ilipofika tarehe simu hazikuwa zikipokelewa na Viongozi wa Yanga, Mtibwa walituma email, texts WhatApp na simu za kawaida ila hapakuwa na majibu

🔋Katika harakati za kuhitaji mzigo upatikane, CEO alionana na Viongozi wa Yanga, February 23 pale Manungu na mbele ya Mchezaji wakahaidi kulipa siku ya Jumatatu ila ikapita hakuna pesa

🔋Danadana zimekuwa nyingi mpaka hii leo, majibu hayaridhishi kutoka kwa Viongozi wa Yanga na Mtendaji Mkuu wa Mtibwa anakiri wazi kuwa kuna uungwana unakosekana wakati wanapodai haki yao, mara hawaoni emails, mara subirini

🔋Mtibwa wanafikiria Jumatatu wapeleke malalamiko rasmi TFF kuhusu madai yao kutokana na mauzo ya Mchezaji wao

🔋Mtendaji anakiri wazi kuwa licha ya jitihada kubwa za Mtibwa kulea Vijana na kuisaidia nchi lakini kadhia kama hizi zinawaumiza sana Wawekezaji wa Mtibwa na Viongozi, kudai haki imekuwa kama Uadui

🔋Walimruhusu Kijana aende sio kwamba hawakuwa wakimuhitaji ila walikubali ili Kijana atimize ndoto yake, huo ndio uungwana, ni wakati sasa wa Yanga kuwa waungwana
Wakati wanauziana mchezaji hawakuuzina kwenye vyombo vya habari lakini wakati wa kudai wanakwenda kwenye vyombo vya habari na kuviacha vyombo rasmi vya kudai haki yako kama TFF, CAF, FIFA na mahakamani kupata Suluhu.
 
Tuliza mshono kwanza,eti ilikuwa fluke, kama kubahatisha mbona mechi nyingine tuna clean sheets nyingi
Tuliza mshono wako wa miaka minne bila kusonwa..! Clean Sheets ya kununua hata Azam FC anaweza.

Na kuna hela ya kuwapa Mtibwa Sugar ili waachie game bado hawajalipwa, wanasubiri wamalize ya golikipa kwanza halafu waliamshe..!

Imekuuma sana, Punguani wa Akili Wee!
 
UNATESEKA SANA MTANI, POLE.. UKIAMBIWA UTOE USHAHIDI KWAMBA YANGA WAMETOA HELA ILI MTIBWA WAACHIE UTATOA FACTS AU UNABWABWAJA?
 
SAKATA LA MTIBWA DHIDI YA YANGA

[emoji367] Wakati Yanga wanakubaliana uhamisho wa Kinda Abou Msheri kutoka Mtibwa, walitaka kulipa ada ya uhamisho kwa mikupuo miwili (installments)

[emoji367]Mtibwa walisema wazi kuwa wao wanachotaka ni pesa yote kamili kwakuwa hawana haraka nayo, Mtibwa ikaomba ipewe tarehe maalum ya kulipwa pesa yao yote

[emoji367]Yanga wao walisema pesa yote italipwa DECEMBER 30, Mtibwa walikubaliana na hilo kwakuwa waliwaamini Wananchi na wakakamilisha paperworks zote

[emoji367]Ule muda wa Mtibwa kuingiziwa pesa yao ulipofika haikutumwa hata senti kutoka Yanga, Mtibwa walivumilia kwa wiki mbele kisha kuwapigia kuomba feedback kuhusu malipo

[emoji367]Majibu ya muda wote yalikuwa “tunashughulikia”, “tupo kwenye mchakato” lakini Manungu walisema wapewe tarehe nyingine sahihi ya kuingiziwa pesa yao, Yanga wakatoa tena ahadi

[emoji367]Usiku wa deni haukukawia kukucha, ilipofika tarehe simu hazikuwa zikipokelewa na Viongozi wa Yanga, Mtibwa walituma email, texts WhatApp na simu za kawaida ila hapakuwa na majibu

[emoji367]Katika harakati za kuhitaji mzigo upatikane, CEO alionana na Viongozi wa Yanga, February 23 pale Manungu na mbele ya Mchezaji wakahaidi kulipa siku ya Jumatatu ila ikapita hakuna pesa

[emoji367]Danadana zimekuwa nyingi mpaka hii leo, majibu hayaridhishi kutoka kwa Viongozi wa Yanga na Mtendaji Mkuu wa Mtibwa anakiri wazi kuwa kuna uungwana unakosekana wakati wanapodai haki yao, mara hawaoni emails, mara subirini

[emoji367]Mtibwa wanafikiria Jumatatu wapeleke malalamiko rasmi TFF kuhusu madai yao kutokana na mauzo ya Mchezaji wao

[emoji367]Mtendaji anakiri wazi kuwa licha ya jitihada kubwa za Mtibwa kulea Vijana na kuisaidia nchi lakini kadhia kama hizi zinawaumiza sana Wawekezaji wa Mtibwa na Viongozi, kudai haki imekuwa kama Uadui

[emoji367]Walimruhusu Kijana aende sio kwamba hawakuwa wakimuhitaji ila walikubali ili Kijana atimize ndoto yake, huo ndio uungwana, ni wakati sasa wa Yanga kuwa waungwana
Haya ni madai madogo kwa Yanga, mbona tusianze na utapeli wa Mo, alisema kaweka billions kwenye account ya Simba, ukimuuliza bank aliuoweka hizo pesa na ni account ipi mtagombana.
 
Tuliza mshono wako wa miaka minne bila kusonwa..! Clean Sheets ya kununua hata Azam FC anaweza.

Na kuna hela ya kuwapa Mtibwa Sugar ili waachie game bado hawajalipwa, wanasubiri wamalize ya golikipa kwanza halafu waliamshe..!

Imekuuma sana, Punguani wa Akili Wee!
Kwanza mpira na rushwa ni kosa kubwa kisheria kwanzia CAF hadi FIFA wenyewe, Juventus waliwahi kushushwa daraja kwa kosa la upangaji wa matokeo. Sasa nyie watu wa Simba mnakwama wapi kuifungulia kesi Yanga ilihali mnao uthibitisho kuwa inanunua mechi? Yaani mnaishia kuropoka humu utafikiri hakuna vyombo vinavyoshugulikia malalamiko. Acheni upumbavu kama mnaona Yanga inanunua mechi kafungueni kesi pelekeni na uthibitisho wenu laasivyo mkae kimya maana ni tuhuma msizokuwa na uhakika nazo
 
UNATESEKA SANA MTANI, POLE.. UKIAMBIWA UTOE USHAHIDI KWAMBA YANGA WAMETOA HELA ILI MTIBWA WAACHIE UTATOA FACTS AU UNABWABWAJA?
Hivi wakati golikipa Metacha Mnata anasemwa kuwa yeye ni Duka (anauza game) Nyie mlitoa shahidi na mlitoa Facts?

Haya mambo naona tuache tu kama yalivyo.
 
1. Yanga imeifunga simba (mabingwa mara 4 mfululizk wa TPL) ngao ya jamii je simba ilipokea mlungula toka kwa yanga?
2. Azam alikula 2 kavu je naye na mapesa yake alihongwa?
3. Mbeya city alisuluhu na yanga, namungo pia. Je wao hawana njaa hadi wakatae mlungula wa yanga?
4. Mtibwa wako kwenye tundu la kushuka daraja.je wanapata wapi ujasiri wa kuuza mechi ili waendelee kujiweka hatarini?
5. Yanga waifunge timu gani ili mkubali kuwa wako vizuri mwaka huu?
Acheni ushabiki maandazi
 
Namba 3...Mchezo wa Mbeya City refa alitaka chake lakini Jamaa wakasuasua kwa mujibu wa Mwanachama wa Yanga ambaye yupo karibu na Kiongozi wa juu, matokeo yake kama ilivyotokea sare, watu hawakuamini mpaka Wazee wakaomba kumuona Rais Samia Suluhu.

Namba 4...Toto African walikubali kushuka daraja ili Yanga awe bingwa, Nakukumbusha tu.

Kwahivyo kwa Ligi Kuu usibishe kila kitu.
 
Kwa mujibu wa mume wa Barbara, Simba inashika nafasi ya 10 Kwa utajiri Afrika Sasa tembezeni bahasha Ili muwe mabingwa.
Tutakuwa Mabingwa wa Nchi... Pressure ipo kwa Yanga ndo maana Sare moja walianza kuchanganyikiwa wasiamini kilichotokea.

Siku wakipoteza sijui wanakuwaje..!
 
Makolo mna shida kubwa sana vichwani

Hivi kwa akili ya kawaida kabisa, bila degree hata moja au certificate anaetumia hela ni anaepewa penalties kila mechi, anaepewa red cards kwa timu pinzani kila mechi au kila timu inayokutana nae inakataliwa magoli yake kwa kisingizio cha offside au anaeshinda kwa kupambana uwanjani na inaonekana kabisa anapambana?

Vijana wa Simba kubalini msimu huu timu yenu sio bora sasa kwanini hamtaki timu nyingine zilizopambana kwenye usajili zionekane kufanya vizuri? Yaani mnatakaje kwani, hata kama timu zingine zimefanya maandalizi mazuri lakini hazitakiwi kushinda?

Una ushahidi gani wa hela za bahasha?

Hii inathibitisha kabisha slogan ya miaka mingi ya Simba sports club kuwa shabiki wa Simba bishana hata kama huna haki!
 
Back
Top Bottom