Pesa za Mashabiki Simba vs Yanga zilizolipwa machi ya leo,Serikali izichukue

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Posts
24,314
Reaction score
38,919
Kufuatia sintofahamu ya mechi ya Simba kuahirishwa na Bodi ya Ligi, nashauri hela zote zilizokusanywa zichukuliwe na Serikali na ziwekwe kwenye budget ya huduma za kijamii. Kuwaachia hela hizo TFF na matapeli wenzao ni wizi wa waziwazi kabisa.

Karia juzi tu ulisisitiza kanuni hazifuatwi, ndiyo maana unawafungia baadhi ya Viongozi, ingependeza nawewe ukajiuzulu maana taasisi yako imeshindwa kufuata kanuni, pia waziri Bashungwa ingekupendeza ukapumzika

Meck Mexime apewe ulinzi, maana alisema juzi tu wakati anatambulishwa na viongozi wa Cambiaso sports kuwa viongozi wengi wa mpira ni WAJINGA WAJINGA TU......Hata week haijPita imedhihirika.

Mpira wetu haupo serious kabisa, ndiyo maana sponsor's wamekuwa wachache, unaahirisha mechi kienyeji tu, hata walio na haki ya kurusha matangazo, Azam Tv 📺 ,sijui mikataba yao ipoje, maana wanapelekeshwa pelekeshwa tu......

Tukiacha ujinga aliousema Mecky tutasonga mbele
 
Ila wametukosea sana, basi tu watanzania ni wapole...vinginevyo TFF,Bodi ya ligi na Waziri wao wangeondoka watake wasitake
 
Serikali wazichukue??

Pesa zirudishwe

Yaan haya CCM ndo yamebebe hela?? Majizi.,zitaingia mikonon mwa watu.
Kuna maeneo mengi serikali inaweza kuzipeleka kuliko kupotelea kwa wachache wakati mchezo haujachezwa
 
Ila wametukosea sana, basi tu watanzania ni wapole...vinginevyo TFF,Bodi ya ligi na Waziri wao wangeondoka watake wasitake
Sure, then na mashabiki wamepigwa mabomu
 
Mashabiki wa timu zote susieni kwenda viwanjani huu ni upumbavu.
 
Mashabiki wa timu zote susieni kwenda viwanjani huu ni upumbavu.
Labda kwa Uto kama ikiwapendeza,lakini kwa Simba ambae ubingwa unamnukia sidhani swala la kususia kama mashabiki wa Simba watakubali,ingawa baadhi ya mashabiki wa Simba nao wamechukizwa na haya mabadiliko ya muda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…