Pesa za mitaji hizo vijana kachukueni

Pawaga

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2011
Posts
1,349
Reaction score
1,011
Habari ya majukumu watanzania wenzangu?

Kuna siku niliuliza taratibu za kufuatwa ili kumuona DC wadau humu walinielekeza na leo nimefanikiwa kuonana nae.

Lengo la uzi huu ni kutaka kushare nini kilinipeleka kwa DC na matokeo yake. Ukwel mi ni mhitim wa shahada ya uhasibu lakin nimekuwa najihusisha na ufugaji wa kuku wa asili na kilimo,kama kawaida kilio cha wengi ni mitaji ya kuanza biashara hivyo mimi nilienda kwa DC kupata taarifa ya namna gan yeye mkuu wa wilaya na idara zake za maendeleo wanaweza kuwasaidia vijana kupata mitaji.

Baada ya kumweleza sababu ya mimi kuwa pale ofisin kwake alinipa kimemo nikampe AFISA VIJANA WA WILAYA. Afisa vijana akanitaka nimweleze tena maelezo nliyotoa kwa mkuu wa wilaya na baada ya kumweleza akasema:

"Ni kwel kuna fungu la pesa la kuwawezesha vijana na wanapewa kwa riba ya 10% kwa mwaka".

1. Lazima muwe kundi la vijana 5 - 15.
2. Msajili kikundi chenu
3. Mjishughulishe na kaz yoyote halali ya kimaendeleo.
4. Mpeleke katiba ya kikundi, muhtasi wa kikao, mpango biashara, barua ya kuwatambulisha toka kwa mtendaji wa kijiji/mtaa na sh 5000 ya usajili.
6. mikopo hii haihitaji dhaman yoyote yaan ni free kabisa mambo ya hati ya nyumba/kiwanja,sijui kadi ya gar mara salary slip huku hakuna

Vijana wenzangu TAARIFA NI SILAHA KALI SANA KTK MAPAMBANO KULIKO HATA AK47 hivyo nawashauri nendeni ktk ofisi za maDC mkapate taarifa zaidi.

OMBI LANGU: Nisaidieni katiba yeyote ya kikundi inisaidie kuandaa yetu au jinsi ya kuandika katiba. Pls tuache kulalamika tupambane aiseee.
 
Jambo jema sana, I'm inspired.

Wacha waje kutupa sample ya katiba.
 
mkuu umenena vyema na mimi ngoja nilifanyie kazi hili jambo
 
mkuu umenena vyema na mimi ngoja nilifanyie kazi hili jambo
vijana tunakosa tu taarifa lkn fursa zipo sana muhim ni kupeana hzo taarifa kupitia mtandao wetu pendwa jf
 
vijana tunakosa tu taarifa lkn fursa zipo sana muhim ni kupeana hzo taarifa kupitia mtandao wetu pendwa jf
ni kweli mkuu yani muda wote huu tungelikuwa tumeshafanya kitu lakini hatuna taarifa mdau ubarikiwe sawa kwa taarifa
 
Asante kwa taarifa naitendea kazi mapema jaman mwenye sample ya katiba atusaidie plzzz
 
Nimekuja mbioo nikujua zile million 50 kila kijiji zimetolewa


Lakini asante kwa taarifa
 
Nitupie na mm kwenye hicho kikundi mkuu kama kipo ili tufahamiane
mtendaji atakutambua kwel?,wanakikundi lazima wawe wa kijiji kimoja ambao mtendaji atasaini kuwa anawafaham
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…