Hapana wakati ni sasa
Hata hiyo miradi ya Gesi itakuza uchumi
Kwa mujibu wa TPDC kwa gesi inayochimbwa tu Songosongo na Mnazi Bay haitumiki ipasavyo! Na mbaya zaidi nishati ya kuni inaiweka nchi kwenye hatari kubwa zaidi ya kugeuka jangwa!
Ukitembea maeneo mengi ya Tanzania kama ni mtu mwenye uelewa wa mambo utagundua hii nchi miaka si mingi sana tutaanza kuzalisha chakula pungufu na kukosa hata mvua za kujaza mabwawa yetu ya umeme kwa ukataji wa miti wa kutisha unaoendelea kwa sababu ya matumizi ya kuni na mkaa
Wengi hili suala la gesi hamjalijua vizuri. Tanzania tunazlisha CNG, hatuzalishi LPG(hii mitungi ya kupikia).
CNG kuigeuza kuwa LPG ni ngumu na gharama na ni hatuwezi kabisa.
Option iliyopo ni kutumia mabomba kupitisha hii CNG ili iweze kutumika direct. Mradi wa kujenga mabomba kwa nchi nzima hadi vijijini ni gharama na ni ngumu sana, nadhani unakumbuka mradi wa bomba la gesi mtwara tulitumia tril 2.4 na zilikua za mkopo ambao hadi leo haujaisha. Hii CNG yenyewe ni kitendawili maana sio yetu tunainunua kutoka kwa hao wawekezaji
Hapo ni kutoka mtwara kuja dar, vipi kutoka mtwara kwenda Bukoba, kigoma, mwanza, katavi, Tabora, geita n.k tena mabomba yafike kila Kijiji. Ni trillions ngapi hizo zitakua?? Na pia hata hii CNG yenyewe nayo tunainunua kutoka kwa wawekezaji
Ndio maana tunanunua hii LPG(mitungi) kutoka nje, na hasara yake ni Kama unavyoona kwenye mafuta, ni ngumu kucontrol bei na upatikanaji. Ambapo watu wataendelea bado kutumia mbadala kwa kuwa ni rahisi na unapatikana(mkaa na kuni).
Unasema miti inaisha? Ni kweli inaisha, Ila kwenye hili kwanza ningeishauri serikali kusitisha tena biashara ya magogo maana imeanza tena na yanasafirishwa nje ya nchi.
Lakini kwa watu wa vijijini kwa umaskini huu uliopo, na hayo niliyokueleza unafikiri watakuwa na laki 1 kila mwezi ili kutumia gesi? Ikiwa tu chakula ni shida kukipata? Wafanyakazi hawa tu wa serikali wenye mishahara huo ubavu hawana