Pesa za tanzania ajabu lingine

FELIPE

Senior Member
Joined
Aug 4, 2011
Posts
107
Reaction score
45
Bandugu kuna hili tatizo la noti zetu mpya za shilingi 500, 1000 na 2000 kutokuwa durable, hili tatizo ni kubwa sana hasa kwenye maeneo yenye transactions nyingi. hizi noti zinachakaa mapema sana na watu wanaanza kuzikataa tena angalau kwa Dar nimeona watu sio wabishi sana kuzipokea hizo noti kama zimechakaa, lakini mikoani tatizo ni kubwa mno. BOT wanaliona hili au ulikuwa mradi wa fisadi kuzitengeneza hivo analindwa? Au zilitengenezwa China kama ilivosemekana?
 
Thamani yake inashuka kila siku..ubora wake pia unashuka kila siku..shillingi 80 za kenya ni dola moja...shillingi 1650 za tanzana ni usd 1..mabigwa wa kutoa hotuba majukwaani..uchumi umepanda kwa kasiiiiiiii!!!!
 
Noti hizo ubora wake ulianza kuchakachuliwa tangia mchakato wa kuzitengeneza. Ilitumika gharama kubwa kuzitengeneza kwa ushawishi mkubwa ili zikubalike lakini kwa lengo la kuchakaa haraka zaidi ili ng'ombe aendelee kukamuliwa zaidi na zaidi na zaidi. Sasa tunakaribia 2015 inapotakiwa hela ya uchaguzi, unadhani wapate wapi? Hata zilipokuwa zinatengenezwa ilikuwa tunajiandaa kwa uchaguzi na ilibidi mpango mzima ufanyike pesa ipatikane ndo maana miradi hewa mingi sana ikabuniwa kama EPA, MEREMETA nk. Kaa mkao wa kusikiliza mipango mingi mingine kwa sasa, maana bila hela TZ siku hizi mtu hachaguliki kuwa kiongozi. Imekuwa kama sheria vile.
 
Mkuu wa kaya kapitishwa na tbs? Kama hana tbs, unategemea nini kwenye noti za jero jero?
 
pia kuonesha kama hawa jamaa ni wa ajabu nchi moja tunatumia noti tofauti kwa wakati mmoja, toleo la zamani na jipya vinatumika kwa wakati mmoja alafu eti kuna wachumi daraja la kwanza, hii nchi!!!
 
Ukisikia majibu yao ndiyo balaaa,hawataki kukubali kwamba ubora wake mdogo.

watakwambia oooh ziko sana katika mzunguko,pia hamuweki pesa kwenye walet.

khaaaaa,wakati mnatengeneza mlitengeneza hamjui zinatumikaje?..mzunguko wake ukoje?..

yaani tz tunakoelekea ni pabaya sana!..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…