Pesa zako zinanuka!

Pesa zako zinanuka!

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
346
Reaction score
522
Je, pesa zako ni baraka au mzigo unaobeba harufu ya maumivu ya wengine?.

IMG_6493.jpeg

NB😛icha kwa hisani ya gazeti la mwananchi mwakajana.

Katika jamii ambayo utajiri hutafsiriwa kama nguvu, pesa mara nyingine hutumika kama silaha ya kudhibiti na kudhalilisha. Lakini utu unaweza kununuliwa? Heshima inaweza kuuzwa? Na nini kinachobaki kwa wale wanaolazimishwa kukubali dhuluma kwa kisingizio cha msaada wa kifedha?
Pesa zako zinanuka ni kilio cha waliodhulumiwa, lakini je, tuna ushujaa wa kuusikia?.

Mashangazi na mafataki hutumia pesa, ushawishi, na hadhi zao kijamii kama silaha ya kunyonya tamaa ya mahitaji ya waathirika wao. Wanaolengwa mara nyingi ni vijana wanaokabili changamoto za kifamilia, kiuchumi, na kisaikolojia, na hivyo wanajikuta wakikubaliana na udhalilishaji huu kwa matumaini ya maisha bora na misaada ya muda mfupi,huku ni kuporomoka kwa maadili ya jamii zetu!.
IMG_6494.jpeg

picha kwa hisani ya mtandao!

Udhalilishaji huu una athari kubwa kwa waathirika. Kisaikolojia, wanajikuta wakitumbukia katika maumivu ya kiroho na kiakili, huku wakishindwa kujinasua kutokana na utegemezi wao wa kifedha. Mara nyingi, hofu ya kupoteza kazi au nafasi ya kiuchumi inawafanya kukubali udhalilishaji kwa sababu wanaona kama ni njia pekee ya kujikimu.

Lakini, jamii inahitaji kubadili mtazamo kuhusu matumizi ya pesa. Pesa hazipaswi kuwa chanzo cha kutawala wala kudhalilisha. Badala yake, inapaswa kuwa njia ya kuboresha maisha na kuleta maendeleo,pia tunahitaji mfumo wa kijamii unaojali na kuhakikisha kuwa kila mtu anapata haki yake bila kutishiwa au kudhulumiwa kwa sababu ya hali yake ya kifedha.

Kwa kumalizia, "Pesa zako zinanuka" si tu maneno ya onyo, bali ni wito wa kuhamasisha jamii kuzingatia maadili na haki za binadamu. Pesa inapaswa kuwa zana ya maendeleo, sio ya kudhalilisha. Kama jamii, lazima tushikamane kupinga udhalilishaji huu na kuhakikisha kuwa kila mtu, bila kujali hali yake ya kifedha, anapewa heshima na haki zake.
 
Je, pesa zako ni baraka au mzigo unaobeba harufu ya maumivu ya wengine?.

View attachment 3198754
NB😛icha kwa hisani ya gazeti la mwananchi mwakajana.

Katika jamii ambayo utajiri hutafsiriwa kama nguvu, pesa mara nyingine hutumika kama silaha ya kudhibiti na kudhalilisha. Lakini utu unaweza kununuliwa? Heshima inaweza kuuzwa? Na nini kinachobaki kwa wale wanaolazimishwa kukubali dhuluma kwa kisingizio cha msaada wa kifedha?
Pesa zako zinanuka ni kilio cha waliodhulumiwa, lakini je, tuna ushujaa wa kuusikia?.

Mashangazi na mafataki hutumia pesa, ushawishi, na hadhi zao kijamii kama silaha ya kunyonya tamaa ya mahitaji ya waathirika wao. Wanaolengwa mara nyingi ni vijana wanaokabili changamoto za kifamilia, kiuchumi, na kisaikolojia, na hivyo wanajikuta wakikubaliana na udhalilishaji huu kwa matumaini ya maisha bora na misaada ya muda mfupi,huku ni kuporomoka kwa maadili ya jamii zetu!.
View attachment 3198764
picha kwa hisani ya mtandao!

Udhalilishaji huu una athari kubwa kwa waathirika. Kisaikolojia, wanajikuta wakitumbukia katika maumivu ya kiroho na kiakili, huku wakishindwa kujinasua kutokana na utegemezi wao wa kifedha. Mara nyingi, hofu ya kupoteza kazi au nafasi ya kiuchumi inawafanya kukubali udhalilishaji kwa sababu wanaona kama ni njia pekee ya kujikimu.

Lakini, jamii inahitaji kubadili mtazamo kuhusu matumizi ya pesa. Pesa hazipaswi kuwa chanzo cha kutawala wala kudhalilisha. Badala yake, inapaswa kuwa njia ya kuboresha maisha na kuleta maendeleo,pia tunahitaji mfumo wa kijamii unaojali na kuhakikisha kuwa kila mtu anapata haki yake bila kutishiwa au kudhulumiwa kwa sababu ya hali yake ya kifedha.

Kwa kumalizia, "Pesa zako zinanuka" si tu maneno ya onyo, bali ni wito wa kuhamasisha jamii kuzingatia maadili na haki za binadamu. Pesa inapaswa kuwa zana ya maendeleo, sio ya kudhalilisha. Kama jamii, lazima tushikamane kupinga udhalilishaji huu na kuhakikisha kuwa kila mtu, bila kujali hali yake ya kifedha, anapewa heshima na haki zake.
Pesa zangu huwa zinanuka upya kila mwisho wa mwezi
 
Umenikumbusha kitabu cha BEN R MTOBWA .Kitabu kinaitwa PESA ZAKO ZINANUKA

Hicho kitabu kilikuwa na madini ya kutosha nawakumbuka baadhi ya wahusika Bon kolo aliyekuwa na sura mbaya bila kumsahau Kandili maulana . Na jumba lake akaliita kandili's villa da yule mwanamke wake wakuitwa dora .

Mtoto wao aliitwa chema .ngoja niishie hapa kitabu hiki niliwahikuunguza maharage kisa nilikuwa nakisoma huku naangalia maharage mwaka 2001
 
Umenikumbusha kitabu cha BEN R MTOBWA .Kitabu kinaitwa PESA ZAKO ZINANUKA

Hicho kitabu kilikuwa na madini ya kutosha nawakumbuka baadhi ya wahusika Bon kolo aliyekuwa na sura mbaya bila kumsahau Kandili maulana . Na jumba lake akaliita kandili's villa da yule mwanamke wake wakuitwa dor
Naam mhenga
 
Back
Top Bottom