Ni Muhimu Serikali Ituambie nini umuhimu wa Janabi kuwa Mkurugenzi wa WHO, na kama taifa tunafaidikaje?
kwasababu Tuliona Kikwete akizunguka naye na tuliona Mabalozi wakipeleka Barua maalumu kutoka kwa Rais SSH kwenda ,marais kama Museven na wengine ambao hawakufikiwa mojakwa moja lakini tulifahamu wote hao walitumwa na Ikulu, je gharama hizo zilikuwa za lazima na kama ilikuwa ni lazima nini faida ya Janabi kuwa mkurugenzi wa WHO afrika?
Je ni nafasi zote kimataifa tunagharimia kiasi hicho na kama ndiyo kwanini na tunafaidikaje, na kama siyo kwanini tunafanya haya sasa?
Je, Nikwasababu watu wetu hawawezi kujieleza kujitafutia ushawishi wenyewe mpaka serikali ihusike au kwanini hasa ni elimu yetu au serikali zote hufanya hivyo nasi tukaamua kuanza kufanya haya?
Taarifa ya CAG mwakani ije na majibu tumetumia kiasi gani na kwanini au kulikuwa na ulazima gani kufanya hivyo, na faida gani tuna pata au kama ni hasara ni kiasi gani, na je kulikuwa na ulazima wa nchi/taifa kumfanyia kampeni kiasi hicho kwa gharama hizo?