PesaX / CashX (Singularity) wanatumia taarifa binafsi za watu na wanakiuka mamia ya sheria Tanzania

Joined
May 6, 2024
Posts
77
Reaction score
103
Ndugu zangu wa Tanzania,

Kuna kampuni inayotoa huduma za kukopesha pesa mtandaoni ambayo inajulikana kwa majina kadhaa katika aplikesheni zake, ambayo kwa ujumla hutumia jina la "Singularity". Sijawahi kukutana na kampuni inayoendeshwa hovyo kama hii! Nimekuwa nikikopa pesa mara kwa mara kutoka kwao na kurudisha bila kuchelewa wala kuchenga. Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kwamba, unapokopa pesa, unakuwa na makubaliano ya kuchagua muda wa kurejesha pesa. Kwa mfano, ukichagua siku 7, huduma ya wateja yao huanza kukusumbua siku ya 6 ili urudishe pesa kabla ya "due date" kufika. Wanatuma meseji za hovyo bila mpangilio, na kupiga simu mara kwa mara, hata kufikia kiwango cha kero. Meseji zao za vitisho na kauli zao za kukera na dharau huathiri sana.

Haya yote yanakiuka sheria, miongozo, kanuni, na sera zilizowekwa na TCRA: Kuna muda maalumu wa kufanya mawasiliano na mteja, na si nje ya muda huo. Kuna lugha maalumu na namna ya kumfikia mteja, sio kiholela na kutumia namba mpya kila siku na huduma ya wateja au watoa huduma za kukusanya madeni kutuma meseji kwa namna wasiyojali.

Kampuni hizi zinakiuka haki ya raia kwa kuchukua taarifa binafsi na kuzitumia kwa njia isiyofaa. PDPC (Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi) inapaswa kuchukua hatua. Aidha, kampuni hizi zinaenda kinyume na miongozo ya BOT. Mtu akichukua mkopo, hatakiwi kusumbuliwa kulipa kabla ya tarehe ya mwisho ya urejeshaji wa mkopo tena kwa vitisho.

kwa uchache hayo ni baadhi tu ya mambo yanayofanywa na kampuni hii.
images.png

Je ni yapi mengine umekutana nayo ama kuskia kuhusu kampuni hii?
 
Lipa madeni acha kutafuta huruma, pesa za watu hizo.
 
Ila wee jamaa unachekesha kweli,yaani unasema unakopa mara kwa mara alafu unasema kampuni ya hovyoo..kwani wanakulazimisha uendelee kukopa au mwenyewe unapenda kukopa ukitegemea huruma ya watu
 
Ndugu zangu wa Tanzania,

Kuna kampuni inayotoa huduma za kukopesha pesa mtandaoni ambayo inajulikana kwa majina kadhaa katika aplikesheni zake, ambayo kwa ujumla hutumia jina la "Singularity". Sijawahi kukutana na kampuni inayoendeshwa hovyo kama hii! Nimekuwa nikikopa pesa mara kwa mara kutoka kwao na kurudisha bila kuchelewa wala kuchenga. Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kwamba, unapokopa pesa, unakuwa na makubaliano ya kuchagua muda wa kurejesha pesa. Kwa mfano, ukichagua siku 7, huduma ya wateja yao huanza kukusumbua siku ya 6 ili urudishe pesa kabla ya "due date" kufika. Wanatuma meseji za hovyo bila mpangilio, na kupiga simu mara kwa mara, hata kufikia kiwango cha kero. Meseji zao za vitisho na kauli zao za kukera na dharau huathiri sana.

Haya yote yanakiuka sheria, miongozo, kanuni, na sera zilizowekwa na TCRA: Kuna muda maalumu wa kufanya mawasiliano na mteja, na si nje ya muda huo. Kuna lugha maalumu na namna ya kumfikia mteja, sio kiholela na kutumia namba mpya kila siku na huduma ya wateja au watoa huduma za kukusanya madeni kutuma meseji kwa namna wasiyojali.

Kampuni hizi zinakiuka haki ya raia kwa kuchukua taarifa binafsi na kuzitumia kwa njia isiyofaa. PDPC (Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi) inapaswa kuchukua hatua. Aidha, kampuni hizi zinaenda kinyume na miongozo ya BOT. Mtu akichukua mkopo, hatakiwi kusumbuliwa kulipa kabla ya tarehe ya mwisho ya urejeshaji wa mkopo tena kwa vitisho.

kwa uchache hayo ni baadhi tu ya mambo yanayofanywa na kampuni hii.
View attachment 2985449
Je ni yapi mengine umekutana nayo ama kuskia kuhusu kampuni hii?
Kama umechukua pesa yao warudishie
 
Hawa jamaa sitaki hata kuwasikia, nilijiunga nao baada ya kuwa na shida flani hivi, wakanitumia kiasi kidogo tofauti na walichojipambanua nacho mpaka kunivutia ila nikaona powa tu. Baada ya muda dau langu likapanda mpaka 320,000/=. Sasa walichonikera ni kuanza usumbufu siku ya 4 kabla ya due date, mbaya zaidi nilimuweka mama kama mdhamini, walimtumia SMS mbaya sana kuhusu mimi kuwa nimekuwa mkaidi kulipa pesa na wataniripoti kwenye vyombo vya ulinzi na huduma zingine za kifedha kama mimi ni tapeli niliyekubuhu ili nisipate huduma zingine za kifedha.
Aisee mama alinijia juu balaa, nikamwambia naomba unifowardie hizo sms, hee kuja kuangalia ni sms kutoka kwa hawa jamaa. Nlipata muda mgumu sana kumuelewesha mama tena kwa vielelezo vya jinsi ninavyowakopa pesa na kurudisha on time. Swali la mama juu yangu "Una shida gani mpaka unakopa? Umeshindwa hata kuniomba mimi mama ako mpaka unakopa kopa huko huoni unajitia aibu na kazi yako hiyo?" Niligadhibika sana, nikaanza kuwatafuta hawapokei simu zangu. Nikatuma complaints kwa number zote walizokuwa wakanitumia matangazo yao inakuwaje wamemtumia sms mdhamini wangu sms kama zile na si mimi mhusika na sijawahi chelewa hata maramoja kulipa pesa zao zaidi nilikuwa nalipa mapema ili nipande madaraja zaidi na zaidi? Mwisho nikamwambia nitawashtaki kwa walichokifanya na kwa hasira muda huo huo nikalipa hiko kiasi walichokuwa wananidai while nilikuwa nimebakiwa na siku 3 kabla ya muda kuisha. Nikadelete application yao nikabaki na zile conversations za WhatsApp tu kama ushahidi.
Baada ya siku kama mbili manager wao akanipigia simu na kujitambulisha na kuniomba msamaha sana kuwa loan officer aliyekuwa ananisimamia alijichanganya na kutuma hizo sms kwa bahati mbaya kwangu na si kwa mhusika aliyekuwa amelengwa. Kwakweli niliwaponda sana kwakutoa huduma kwa kubahatisha na kuwa na loan officers wasiojua a good customer care. Nikamwambia wana bahati wameniwahi vinginevyo I was about to sue them. Akaniomba niendelee na huduma zao na wataniboresha huduma kwangu maana nimekuwa a very good client kwa kulipa mapema mara zote ninazochukua pesa ndani ya wiki 3 nimepanda daraja zaidi ya mara 5. Kwakweli sikumficha nikamwambia msamaha wangu kwenu ni kuacha kwenda Mahakamani ila naachana na huduma zenu nikakata simu.
Wamekuwa wakinitumia sms mara kwa mara lakini it's a big NO continuing with their service
 
Back
Top Bottom