Pete katika ndoa


Kwa hiyo ya Blue hapo...........sina la kuongeza!
 
Reactions: Mbu
Ni ishara ya ndoa halali ya wawili walioamua kupendana maisha yao yote hapa duniani na kwamba hawatoachana japo ni kinyume kwa wanandoa wengi hususani wabongo wanaooa ucku na kuacha mchana. Ni vema tukazitumia kama zinavyomaanisha na sio kuchakachua.
...kwakweli bora tungekuwa tunafungishwa pingu ya ukweli tu jamani na [funguo unatupwa baharini],...!



 
Usicheke Mbu,watu tumefanana na mayai viza ni basi tu pa kupasuliwa hakupo miji ingenuka nakwambia tuonanage tukiwa tumejipigilia visuti vyetu wenyewe eti watu wa heshima na familia zao.Acha tuendelee kuamini yale tunayoamini maisha yawe na amani angalau kwa sekunde chache.

 

...mmnnh, laaziz jiaminishe without apostrophes bana...BTW, siku hizi kwenye kadamnasi utakuta Groom na brides wenyewe macho juu juu,...vows zinatamkwa kama Obligation tu, moyoni walaa... Nita share nanyi jamaa ambaye kweli vows zilimuingia moyoni, stay tuned


...Mwj1 wangu wee,...Zipuwawa ushamsoma hapo juu? Imani 'potofu' za watu wa kisasa...


Kwa hiyo ya Blue hapo...........sina la kuongeza!
 
Last edited by a moderator:

Chauro......huu msitari mwekundu huu una ujumbe mzito sana dada yangu na kwa kuwua nimekuwa nikiusoma kutoka kwako mara nyingi.nimejikuta nimekuwa mfuasi wako tafadhali nipokee!. I salute
 

Hah Ziipuwawa mydia ndo umenimaliza nguvu kabisa...usijenfanya nikavua hutu tupete twangu nikaambulia kipigo kisa JF mwe!! mnasema ukweli sana bana hebu funikeni kidogo ili niwezemfuata vizuri mwalimu wangu Chauro.kuamini tunavyoamini tu!

Darl Mbu we ...........hizi vows hizi we acheni tu, nilishawahishuhudia mkaka anaongea peke yake na Kideo..alikuwa anaangalia mkanda wa arusi yake, sehemu ya kiapo wakati mkewe anaapa kaka akaanza kutukana...muongo mkubwa.huna haya aibu!!!. kipindi kile sikumwelewa!
 
Last edited by a moderator:

...lol...jamani iweje mnaishi kama roho ipo kooni, mkipaliwa tu inaacha mwili?
Kuna haja ya kuishi kwa matumaini.
 
Karibu rafiki Mpenzi hako kamstari kamenisaidia sana maana sekunde zinazaa dakika,masaa ,siku ,miezi ,mwaka,miaka.
Chauro......huu msitari mwekundu huu una ujumbe mzito sana dada yangu na kwa kuwua nimekuwa nikiusoma kutoka kwako mara nyingi.nimejikuta nimekuwa mfuasi wako tafadhali nipokee!. I salute
 
Reactions: Mbu

...LOL...hhhhaahhhahh! Mwj1 daaahhh,...huyo mkaka ni yapi yaliyomkumba yarabi?
hhhaaahha...maisha haya!

Halafu hapo penye kuvua pete hapo mnnnnn?, halahala mti na jicho, ukitaka kuzivua, alika tena ndugu jamaa na marafiki pale madhahabuni...mbele ya kasisi na utamke "Menzangu nimeamua kuvua pete hizi!"
 

LOL...Baba_Enock,..ulipoivua hiyo pete na uaminifu uliuvua hapo, au uliivua kwakuwa ilikuwa inakusuta?
Timbwili lake lilikuwaje nyumbani Mama_Enock alipokuuliza pete iwapi?

Enzi zangu za kwenda Guest nilikuwa nalala huko huko! Kwahiyo asubuhi yake nilaimakia Kariakoo (Kitumbini) nikarekebisha mambo and the life went on! Ndoa yetu though haitegemei sana uvaaji wa pete lakini jamii inayotuzunguuka inaamini hivyo na waswahili walisema "wengi wape"!
 
Reactions: Mbu
Kuna mtu alimuhifadhia mahali salama....

...Kiongozi, are you proud to wear your ring?...ni swali la kizushi tu.
Unajiskiaje ukiwa umeivaa...

Unajua kuna hisia fulani hunipata kila nikivaa ring yangu, hebu nisikie na wenzangu mnasemaje.
 

Hahahaha Mbu we acha tu.........kipindi hicho nilikuwa bado kigori, mwari nang'ara nikabaki tu kumcheka na kumwona chizi mwe!! laiti ningalijua, ningeingia na bullet proof!!

LOL hapo kwenye kuvua mbele ya kadamnasi tena mbona itakuwa process ndefu?
 
Reactions: Mbu
hii topic inaweza ikabadilisha wengi.

pete imekuwa ni fasheni tu, hazitumiwi kama maneno yanavyonenwa mtu anapovalishwa/valisha,

ni vema pete zivaliwe moyoni/rohoni na wala si vidoleni
 
Reactions: Mbu
hii topic inaweza ikabadilisha wengi.

pete imekuwa ni fasheni tu, hazitumiwi kama maneno yanavyonenwa mtu anapovalishwa/valisha,

ni vema pete zivaliwe moyoni/rohoni na wala si vidoleni

Umenena vyema Ikunda,...ila kuna hali fulani mie hujihisi kila nikiwa na pete.
Nikiwa nayo, najihisi nampa thamani mwenzangu, sana tu...
Najihisi proud watu wanaponiuliza kumbe umeoa?...
na wengine hufikia kusema "waonyesha wampenda sana mkeo!"

Kimbembe ni baada ya kuachana, Natamani niendelee kuivaa lakini jinsi ya kubadilisha mawazo
tokea thamani ya ndoa yangu, ibakie ni urembo wa kidole na kujistahi inakuwa ngumu.

Kila nikiivaa najiona kama nampa bichwa tu, as if bado sija move on...aarrgghh!
Sijui wenzangu hujiskiaje, ndio nataka ufahamu hapa...
 
Wengi huzitia mfukoni ili jamii inayomzunguka mara afanyapo maasi isijiulize si huyu kaoa/kaolewa?
 
Reactions: Mbu

Mbu hapo kwenye bold, unasema?????? tafadhali bana, unajua unaweza ukamtadhimini mtu kutokana na comment zake hapa sasa wewe kutokana na hapo nilipobold unanichanginyi kbs, sikutegemea hillo kutoka kwako bro!

naomba unapoivaa chukulie hakuna ishu iliyotokea baina yako na mweza wako,

mie nikivaa najiona poa tu, ila inapotokea kutokuelewana na mwenzangu natamani kuivua.
 
Reactions: Mbu

...hhahha,...Ikunda usishtuke bana, ndio hali ya dunia na mapito yake,
ila hapo kwenye ubuluu, umenichekesha sana...wengi hujifanya wameisahau juu ya dressing table
Halafu upo kazini unashtukia simu/sms ..."umeiachia nini pete nyumbani?"---Problem Solved.

Dawa tosha hiyo saa ingine.
 
Hah hapo ameondoka nyumbani kanuniwa....hahah maisha ya ndoa mwe acheni tu!

Mie nilikuwa nikitoka nje ya nyumba bila nayo yaani nakosa amani sasa najiuliza kwa nini nakosa amani sipati jibu!! maana kama kusahau si nimesahau na hakuna kitu kibaya unafanya........mwe vifungo vingine ni kujipa jakamoyo tu!

Hapo kwenye Blue.............Naomba nitume application LOL.
Waiting na kikombe changu cha kahawa naangalia Coming to America LOL
 
Reactions: Mbu
pete halisi iko ndan ya moyo wa mtu..............hizo za mkononi ni mapambo tu ya siku ya harusi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…