Peter Kenyoni; Jasusi wa soka

Peter Kenyoni; Jasusi wa soka

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Julai 2003, Chelsea FC ilinunuliwa na bilionea wa kirusi, Roman Abramovich, kutoka kwa 'babu madevu', Ken Bates. Septemba mwaka huo huo, RA 'akamnunua' mtendaji mkuu wa Manchester United, Peter Kenyon aka mzee wa kazi chafu.

Moja ya kumbukumbu za Peter Kenyon pale darajani ni usajili tata wa Arjen Robben, na Petr Cech.

TUJIKUMBUSHE KIDOGO

PETR CECH

Februari, 2004 Chelsea FC ilitangaza kumalizana na klabu ya Rennes ya Ufaransa kwa ajili ya kipa wao mwenye miaka 21, Petr Cech.

Lakini hata hivyo, makubaliano baina ya vilabu hivyo yalikuwa kipa huyo ajiunge na Chelsea mwezi Julai, baada ya msimu kumalizika.

Petr Cech alijiunga na Rennes mwaka 2002 baada ya kung'aa kwenye Euro ya U-21 ya 2002 alikoisaidia nchi yake kushinda ubingwa dhidi ya Ufaransa.

Katika fainali hiyo iliyoisha kwa sare ya 0-0, Cech aliokoa penati 3 na Jamhuri ya Czech kushinda kwa penati 3-1.

Hapo ndipo dunia ikamtambua na Rennes wakawa wa kwanza kuipata saini yake kutokea klabu ya Sparta Prague.

Akiwa Rennes, aliendeleza uhodari wake na kuvivutia vilabu kadhaa lakini ni Chelsea ndiyo waliofanikiwa kumshawishi bwana mdogo...starring alikuwa Peter Kenyon.

ARJEN ROBBEN

Wakati Chelsea wakiwa 'bize' na Cech, Manchester United walikuwa bize na kinda mwingine wa kutisha kutoka PSV Eindhoven ya Uholanzi, aliyeitwa Arjen Robben.

Alex Ferguson alimchukua Robben hadi uwanja wa mazoezi, Carrington, na uwanja wa mechi, Old Trafford, na kumtembeza maeneo yote ya kihistoria ambayo huwavutia wachezaji wengi chipukizi.

Wakakubaliana kila kitu, ikabaki kusaini mkataba tu. Baba yake Arjen, Hans, akasema 'mwanangu ataichezea vilabu viwili tu, PSV na Manchester United, basi.' Peter Kenyon alipomaliza dili la Petr Cech, akahamia kwa Robben. Akamtafuta wakala wake, Pini Zahavi, na kumtengea donge nono...likamvuruga!

Akaenda PSV na kutoa dau la karibia mara mbili ya lile la Manchester United...PSV wakavurugwa.

Baba yake Robben akaitwa, akaambiwa, 'mzee, mpira ni maisha, ni biashara...muache mtoto akacheze kwenye hela.' Mzee akasema sawa. Robben akaenda Chelsea!

Cech na Robben wakatambulishwa siku moja darajani.

Aaron Arsenal

Double A
tapatalk_1569653194083.jpeg
 
kumbe masuala ya kufuata lilipo dau nono yameanza kitambo........
 
@aroon@ unapuizungumzia chelsea yang moyo wang upata gafla raha tele
Nam nakutunuku ushindi juma tatu yule ya jamaa mbovu sana.
 
Peter Kenyon yuko wapi sasa hivi
Former Manchester United and Chelsea chief executive Peter Kenyonis reported to be part of a new bid take over Newcastle United. Kenyon was linked with a move for the Magpies at the end of 2018, but no deal was struck at the time.
 
Back
Top Bottom