Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,986
Tumezoea kuona watu wakitoa sifa nyingi mtu anapokufa, lakini ninaomba sifa nizitoe mtu akiwa hai.
Mara nyingi nimeona wakili Kibatala akipanda mahakamani kwenye kesi za viongozi wa chadema, analipwa au halipwi hio sijui na hainihusu.
Lakini kitendo tu cha kukubali kusimamia kesi za upinzani kwenye nchi kama hii ambayo inaendeshwa kibabe ni kitendo Cha kishujaa sana.
Angeweza tu kuwa wakili wa serikali au wakili wa kujitegemea na mambo yakaenda, ila Hilo amelikataa.
Yote tisa, kumi ni tukio la leo kisutu ambalo limeniacha mdomo wazi baada ya kumuona wakili Kibatala akitoka mahakamani na kwa mbele akaona gari ya polisi imembeba mmoja wa watu waliokamatwa kwa kubeba mabango.
Kibatala aliifata ile gari ya polisi bila woga na kumuambia yule mtu kuwa asiwe na wasiwasi, wapo pamoja na atamuwekea dhamana. Hivyo atulie atahakikisha anatoka kwa dhamana kwani kubena bango sio kosa.
Ipo hivi, kutokana na kuwa busy siku ya jana na leo, wakili Kibatala angeweza kupita tu kimya bila kumfuataa yule mtu na maisha yakaendelea.
Fikiria tu Kibatala hamfahamu huyo Mtu, na wala huyo Mtu hana uwezo wa kumlipa Kibatala Ila Kibatala ameamua tu kumsaidia bure kabisa.
Ni watu wachache Sana wenye huu moyo.
Kwa kitendo hiki Cha Kibatala ninaomba mnaokuwa nae karibu mtieni moyo sana kwa anayofanya, ni Mtu wa muhimu Sana.
Mtieni moyo Kibatala, mtieni moyo jamani